CCM kumtwisha mzigo Lowassa Arumeru Mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kumtwisha mzigo Lowassa Arumeru Mashariki

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Ritz, Feb 18, 2012.

 1. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,172
  Likes Received: 4,505
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Chama cha Mapinduzi (CCM) kina mpango wa kumbebesha mzigo mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, kwenye mapambano ya kuchukuwa Jimbo la Arumeru Mashariki..

  Sababu zinazotolewa na baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM pamoja uongozi wa CCM Arusha, ni kwamba Lowassa ni mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za Arusha.

  Machi 9 mwaka huu kampeni zinaanza na Aprili Mosi upigaji kura utafanyika.

  Wananchi kadhaa wa Arumeru, wanaozungumzia uchaguzi huo mdogo wa Arumeru wanasema wazi Lowassa, ndio pekee anayeweza kujibu na kusikilizwa na jamii inayoishi katika jimbo hilo.

  Ikielezwa kwamba Slaa, ana ushawishi mkubwa kwa wakazi wa Arusha, ushawishi ambao unaweza kupanguliwa na Lowassa pekee miongoni mwa makada wa chama tawala.

  Arumeru kuna makabila makubwa mawili Wameru 66% na Wamasai, ambao wengi wanamkubali sana Lowassa.
   
 2. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,846
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na hoja yako, HIYO ni sababu tosha Dr. Slaa kachomooa Kugombea Arumeru alijuwa hataweza kupangua makombora ya Lowasa wakati wa kampeni. POLENI CDM huu utakuwa uchaguzi mdogo wa tatu kulalia pua; kumbukeni IGUNGA, UZINI
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 19,449
  Likes Received: 269
  Trophy Points: 180
  we kweli mafilifili
   
 4. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 9,792
  Likes Received: 1,185
  Trophy Points: 280
  Ila wanapenda cchadema japo Lowassa anakubalika ila mapenzi ya wameru nakumpenda Lowassa hawatambui chama zaidi ya CHADEMA!!
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,240
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Time will tell!
   
 6. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,440
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Kama lowasa akiachiwa meru ,hakika ccm itashinda hili halina ubishi hata kidogo ( iwapo tu sioi sumari atakuwa mgombea ) . Wameru siku zote wanaomba kwa Mungu nawao watoe rais wa hii nchi na karata yao ni kwa lowassa . Wanaamini kama sioi atakuwa mbunge na lowassa rais watapata maendeleo kwa haraka jimboni kwao ,hili halina ubishi hata kidogo . Kwa upande wa chadema wanahitaji kazi ya ziada ili waweze kuwashawishi wameru .

  NB . LOWASSA NI MKWE WA SIO SUMARY.
   
 7. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,663
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Kwanza naomba source ya takwimu zako ili tuweze kuzihakiki. Pili sidhani kama Lowassa ana huo ushawishi unaousema mjini Arusha labda kama ukisema Arusha unamaanisha Monduli.

  Tatu kama Lowassa ndo atashika mikoba ya Magamba basi ntaamin sasa CCM imeishiwa mana ni kati ya watu mnaowatuhumu kwa Ufisadi, leo hii huyo huyo anaonekana tena anafaa??au kuna MaLowassa wangapi huko kenu??Au kila mwenye mvi mnamuita Lowassa??? Sidhan kama wa arumeru watakuwa wamepoteza kumbukumbu ya mambo aliyoyafanya Lowassa. Nakubali kuwa CCM wameisha kisiasa na kifikra ila siamin kama watafikia level ya kumshikisha Lowassa Mikoba.
   
 8. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2012
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Lowasa Ikulu hiyoooo,kila la heri, ila usitusahau kwenye ufalme wako.Matumaini yetu ni kwamba baada ya madongo mengi ya wananchi huhusu ufisadi wako,sasa utakuwa umejifunza na utawatumikia wananchi kama ipasavyo,na ufisadi kwako utakuwa mwiko.
   
 9. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,720
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Mkuu inaelekea upo kiccm zaidi,na unapga kampeni live! Kwa Joshua Nassary wa CHADEMA ni kabila gani? Kwanini usiseme wameru wanatamani Joshua awe mbunge wao na Lowassa awe rais ?
   
 10. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,407
  Likes Received: 692
  Trophy Points: 280
  Ufisadi uko ndani ya damu yake hawezi kuacha; toka lini nyani akaacha kula mahindi?
   
 11. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 9,160
  Likes Received: 1,365
  Trophy Points: 280
  Kumbe kule hawajui kama ni fisadi?
   
 12. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,720
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Ndio maana nchi inaendelea kuliwa na wachache mnaozingatia Ushemeji,ukwe,ukabila,udini nk. Huu ndio upumbavu wa watanzania wengi,tuache siasa za kijinga hvyo!
   
 13. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #13
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,965
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  mkuu ritz aka sura mbaya (as per ur avatar) el anakubalika kwao monduli. yaani akiongoza kampeni ya magamba,cdm watapeta sana kwenye kampeni.
   
 14. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #14
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,663
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Wazo lolote la mtanzania linaloonyesha kuwa Lowassa anafaa kuwa Rais wa Nchi hii mimi huwa nalipuuza vikali na kulitupilia mbali sana. Hii dhana ya sehemu/jimbo flani kupelekewa maendeleo kwakuwa Rais/Waziri Mkuu ni Mkwe wa Mbunge flani limetokea wapi???Hii ni dhana ya zamani sana na inayoleta hasira sana hasa kama kauli hiyo inatolewa na Mzalendo. Lowassa alikuwa waziri mkuu alilifanyia nini Jimbo la Arumeru???Au huko nyuma Arumeru haikuwepo???

  Hivi FEDHA zinazotumika kwa maendeleo ya nchi sio Kodi za wananchi wote wa Tanzania??iweje mtu mzima useme kuwa flan akiwa rais na flan akiwa mbunge jimbo flan litaendelea??Unamaana watapewa nafasi ya upendeleo kwa gharama za wananchi wengine??? Kama hizo hela ni kutoka mfukon kwake kwanini asitoe sasa hivi had asubiri awe Rais??? Mtazamo huu ni wa mtu asiyejua nchi inafanyaje kazi zake. Kama ingekuwa hivyo Jimbo linaloongoza kwa umaskini lisingekuwa chini ya Mbunge wa CCM.
   
 15. m

  msnajo JF-Expert Member

  #15
  Feb 18, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,129
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Imekaa kishabiki zaidi!!
   
 16. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #16
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,440
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  mkuu mimi nasema ukweli wa hali jinsi ilivo sihitaji kumpigia mtu yoyote kampeni maana hakuna mwanasiasa ananisaidia kitu naongea kama mwananchi wa kawaida .
   
 17. muwaha

  muwaha JF-Expert Member

  #17
  Feb 18, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Let's wait tuone jinsi masanduku yatakavyopotea na kuchelewa kufika vituoni au wasimamizi kusahau wino, daftari n.k Bongo hakuna kisichowezekana!
   
 18. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #18
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,663
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mbona sisi wananchi wa kawaida hatuna mawazo kama yako???wewe sio mwananchi wa kawaida wewe utakuwa gamba tu.
   
 19. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #19
  Feb 18, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,720
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Ndio maana nchi
  inaendelea kuliwa na
  wachache mnaozingatia
  Ushemeji,ukwe,ukabila,udini
  nk. Huu ndio upungufu
  wa watanzania wengi,tuache siasa za
  kindugundugu na kirafiki hvyo!
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #20
  Feb 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,172
  Likes Received: 4,505
  Trophy Points: 280
  Kwa mujibu wa utafiti wetu huo idadi kubwa ya wakazi wa jimbo hilo ni kabila la Wameru, idadi yao ni 66% Wamasai 15% asilimia iliyobaki ni mchanganyiko wa makabili mbalimbali yaliyohamia kutoka maeneo mbali mbali ya nchi yetu.

  Utafiti huo unaonyesha kwamba Wameru wametapakaa eneo lote la Akari hadi maeneo yote yanayozunguka Mlima Meru.

  Wakati Wamasai wametapakaa katika maeneo ya Nangaranyuki hadi Maroroni.

  Kubwa zaidi kwa mgeni anayaona kama makabila mawili tofauti, lakini mila na desturi zao karibu zote zinafanana, na upo mwingiliano mkubwa wa vizazi baina ya koo za makabila ya mawili ya jimbo la Arumeru.

  Source: Ritz wa JF
   
Loading...