CCM kumtwisha mzigo Lowassa Arumeru Mashariki

CCM kumtwisha mzigo Lowassa Arumeru Mashariki

Huenda lengo kuu la CCM kumkabidhi Lowasa Arumeru ni kumfunga Gavana katika urais 2015. Lowassa kama ana akili ni bora hiki kikombe akiepuke kama kweli ni contender wa 2015. Ajue wazi kuwa katika kampeni Richmond na madudu yote yatakuwa fair game. Na ikitokea CCM wakashindwa Arumeru hiyo itakuwa ni kudhihirisha kuwa Lowassa hawezi kushika bendera ya CCM 2015 maana hata mkoa ambao ana ushawishi hawakumsikiliza.

Arumeru si Igunga, Nina hakika kuwa umafia wa Igunga ukitumika Arumeru basi itakuwa ni mwanzo wa mwisho wa CCM.
 
Kwa mujibu wa utafiti wetu huo idadi kubwa ya wakazi wa jimbo hilo ni kabila la Wameru, idadi yao ni 66% Wamasai 15% asilimia iliyobaki ni mchanganyiko wa makabili mbalimbali yaliyohamia kutoka maeneo mbali mbali ya nchi yetu.

Utafiti huo unaonyesha kwamba Wameru wametapakaa eneo lote la Akari hadi maeneo yote yanayozunguka Mlima Meru.

Wakati Wamasai wametapakaa katika maeneo ya Nangaranyuki hadi Maroroni.

Kubwa zaidi kwa mgeni anayaona kama makabila mawili tofauti, lakini mila na desturi zao karibu zote zinafanana, na upo mwingiliano mkubwa wa vizazi baina ya koo za makabila ya mawili ya jimbo la Arumeru.

Source: Ritz wa JF
Ahsante sana sana NDG. Mtafiti sina swali.
 
Mbona sisi wananchi wa kawaida hatuna mawazo kama yako???wewe sio mwananchi wa kawaida wewe utakuwa gamba tu.

naona ulitaka niseme upinzani utachukua jimbo kirahisi ? Kama ni hivo unahitaji dawa ya minyoo . Siwezi kubishana na mtu kama wewe ni kujipotezea muda . Hukai meru na wala hujui siasa za huku . We tulia subiria matokeo maana kura hazipigwi huku jamvini .
 
Hapana ungekuwa neutral, ila kwa kulalia upande mmoja wowote uwe ccm au cdm, unakuwa umepoteza sifa ya kuongea kama mwananchi wa kawaida. Hakuna anayetaka kubishana hapa, hapa unaelimishwa tu, kama utaki unaacha uendelee na unayoyaamini. Hakuna mwenye muda wa kubishana kiongozi.
 
Mmejipanga vizuri ila hamna facts to back you up. Chukue hii mchango mkaifanyie kazi Lumumba. Mungu halali
 
Lowasa akiongoza kampen ccm itakuwa nawakati mgumu kisiasa ikishinda kuliko ikishindwa kutokana na makundi yaliyopo. Ccm ikishinda (rahisi kama watacheza mchezo mchafu) kundi la sita litakua pagumu na sera za gamba zitazoofu zaid ccm itapoteza mvuto zaid kwa wananchi wanaoumia kutokana na ufisa. Ikishindwa we all know that itakua shangwe kwa sita na kundilake ambalo litapata chakusema.
 
Mpira ndo umeanza tusubiri mshindi . Naomba baada ya uchaguzi turudi hapa tupeane matokeo .
 
Kwanza naomba source ya takwimu zako ili tuweze kuzihakiki. Pili sidhani kama Lowassa ana huo ushawishi unaousema mjini Arusha labda kama ukisema Arusha unamaanisha Monduli.

Tatu kama Lowassa ndo atashika mikoba ya Magamba basi ntaamin sasa CCM imeishiwa mana ni kati ya watu mnaowatuhumu kwa Ufisadi, leo hii huyo huyo anaonekana tena anafaa??au kuna MaLowassa wangapi huko kenu??Au kila mwenye mvi mnamuita Lowassa??? Sidhan kama wa arumeru watakuwa wamepoteza kumbukumbu ya mambo aliyoyafanya Lowassa. Nakubali kuwa CCM wameisha kisiasa na kifikra ila siamin kama watafikia level ya kumshikisha Lowassa Mikoba.

CCM bana !! Kwani mmesahau walivyomuomba fisadi Rostam akawapigie kampeni Igunga? Hawa watu wamepoteza muelekeo kabisa. Huyo huyo Lowassa wanamwita gamba fisadi sasa wanataka kumtumia tena kwenye kampeni, si wamsafishe basi waseme sio fisadi ni mtu safi.
 
Mpira ndo umeanza tusubiri mshindi . Naomba baada ya uchaguzi turudi hapa tupeane matokeo .
Huwa hatutoki humu, JF ndio jukwaa letu so usihofu utatukuta tu sisi ni wa hapahapa.
 
Lowassa ana ushawishi mkubwa sana kwa jamii. CCM wamtumie.
 
Lowassa ana ushawishi mkubwa sana kwa jamii. CCM wamtumie.

Ingekuwa vyema ukaqualify your sentence, Lowassa anaushawishi mkubwa sana kwa jamii gani na kuhusu nini???Kwa jinsi ulivyoiweka unaweza shindwa kueleweka unamaana gani. Maana anaonekana anaushawishi kwa mafisadi, ccm-mafisadi na wa monduli sasa cjui unalenga jamii gan hapa.
 
Ni bora tupoteze jimbo kuliko kupigiwa kampeni na Lowassa.
OTIS
 
Nakubaliana na hoja yako, HIYO ni sababu tosha Dr. Slaa kachomooa Kugombea Arumeru alijuwa hataweza kupangua makombora ya Lowasa wakati wa kampeni. POLENI CDM huu utakuwa uchaguzi mdogo wa tatu kulalia pua; kumbukeni IGUNGA, UZINI

Wamlete tu waona anguko lake, sisi ndio wameru na kama hawajajua , tunafurahi sana kumleta Lowassa, wangeleta akina Sitta na kundi lake labda wangetupa wakati mgumu kidogo
 
Nakubaliana na hoja yako, HIYO ni sababu tosha Dr. Slaa kachomooa Kugombea Arumeru alijuwa hataweza kupangua makombora ya Lowasa wakati wa kampeni. POLENI CDM huu utakuwa uchaguzi mdogo wa tatu kulalia pua; kumbukeni IGUNGA, UZINI

Unajua maana ya kuchomoa. Kwani alikua ameingiza team. au alikuingiza wewe
 
Akipitishwa mtoto wa marehemu ataongoza mapambano lakini wengine ?????????????????
 
Baasi, kama Edward Ngoyai Lowassa Ndosi ataongoza team ya kampeni CCM lazima washinde
 
Mkuu binafsi sio shabiki wa chama chao ila kwa watu tunaotoka pande za kaskazini lowasa ni kitu kingine kabisa licha ya kukubarika vile vile ana heshimika.Cha muhimu tusubiri tujionee yatakayojitokeza manake upepo wa kisiasa huwa unabadilika.

Back
Top Bottom