Nilipotoa tamko kuwa CCM ni adui wa Maendeleo ya Tanzania na Watanzania, sikuwa nimekosea wala kupungukiwa kitu. Huo ni ukweli muutake au musiutake!
Kama kuna kitu ambacho Mwanakijiji kakieleza vizuri ni hiki hapa
Hilo ndilo linalohitajika kutoka ndani ya Chama cha Mapinduzi. Hata hivyo haliwezi kutokea hadi pale baadhia ya "vigogo" wa chama hicho hasa wakongwe au wale ambao wamejikuta wakiwekwa pembeni kutokana na misimamo yao watakapoamua kujitoa ndani ya chama hicho na kuanzisha chama kingine. Hili litawezekana tu pale ambapo wakongwe walioko CCM watakapotambua mioyoni mwao kuwa CCM siyo mama yao. Pale watakapotambua kuwa wanaweza wasife wana CCM lakini watakufa wakiwa ni Watanzania!
Sasa hivi heshima kubwa ambayo baadhi yao wanayo (kama alivyosema Mzee Kawawa miaka ile) ni kuhakikisha kuwa wanakufa wakiwa wana CCM pia. Wengine kati yao wameapa kabisa kuwa liwalo na liwe wao ni "wana CCM mpaka kufa". Nakumbuka wengine wetu tuliimba nyimbo za "naapa naahidi mbele ya Chama, Mapinduzi nitakulinda mpaka kufa". Lakini ahadi hiyo ni ya uongo kwani utii na mapenzi yetu kama raia wa taifa letu hayawezi kamwe kuwa kwa mtu, idara, taasisi au chama cha kisiasa. Mapenzi na utii wetu wa kwanza na wajuu zaidi ukiondoa ule ulioko kwa muumba wetu ni kwa nchi yetu.
Wazo hili litakapoingia ndani ya viongozi wa CCM hasa wale ambao kweli wanaamini mabadiliko yanahitajika haitawachukua muda kuamua kujitoa ndani ya CCM na kuanza harakati za kuleta mabadiliko ya kweli.
Hapa tunarudi tena kwenye ile ibara maarufi ya CCM, ibara ya 15.1 ambayo inatamka wazi kuwa wajibu wa mwanaCCM ni kwa CCM kwanza na wala si kwa Taifa.
Sasa nikimsoma FMES na kauli yake kuwa kamwe ndani ya CCM hakutatokea mvutano au kumeguka kama Madela alivyotupa tafsiri sanifu ya kumeguka na kumegwa, natatizwa na hoja ya FMES kusema kuwa msukumo pekee wa kuleta mabadiliko ya Katiba utatoka kwa Wananchi ambao wengi wao kwa ridhaa, unyonge au mazoea wamejisalimisha haki zao kwa kuipa nguvu CCM.
Labda nimkumbushe FMES mambo mawili matatu ili atambue kuwa msukumo kutoka nje ya CCM pekee kudai katiba hautoshi.
Mchungaji Mtikila katika kesi yake ya kutaka kuwepo kwa mgombea huru, alipata ushindi mahakamani ambao umesema kuwa mgombea binafsi na huru wa chama ni haki ya kila Mtanzania. Sasa ili kauli ya mahakama iwe sheria kwa jinsi katiba ya Tanzania ilivyojengwa, ni lazima Bunge lipitishe muswaada wa kubadilisha katiba na kuweka kifungu hicho. Ni nani mwenye kura nyingi ndani ya Bunge? ni CCM. Na pale wana CCM wengine watakapojifanya a Joe Lieberman, kuvuka mstari na kwenda upande mwingine, vikao maalumu vya kichama hufanyika na vitisho hufanywa hapo kwa papo kisha kura zote kwa sauti moja husema CCM!
Lakini bahati mbaya ya Watanzania ni kunukuu kauli za viongozi kadhaa wa Tanzania ambao si mara moja au mbili wametoa kauli kusema kuwa CCM ina dhamana na uamuzi wa mwisho. Kama hilo halijatosha ni kauli zinazosema kuwa kama CCM haioni jambo lolote kuwa ni tatizo na hasa kuhusiana na katiba, basi CCM kama chama tawala hakioni ulazima au umuhimu wa Katiba kubadilishwa kwa kuwa kina madaraka na Katiba ni safi kabisa kwa Tanzania kwa mujibu wa CCM.
Kauli hii ya Serikali ambayo ilitolewa ndani ya Bunge kwenye bunge mwaka jana ilitolewa na Mama Mary Nagu ambaye alisema kuwa katiba ni safi kabisa.
Labda nijinukuu mazungumzo ambayo nimeyafanya pembeni ya JF baada ya kuandika ile thread ya Azimio Jipya. Nimekukwa na mawasiliano na ndugu kadhaa (Yohana wa Mnyika akiwamo) kulizungumzia suala hili la kudai katiba mpya na ukweli ni kuwa nimekuja kugundua kwa sikuwa pekee yangu.
Peter Maina, Issa Shivji, Robert Kisanga, Joseph Warioba, Barnabas Samatta, Francis Nyalali, Sefu Hamad, Ibrahim Lipumba, Tanganyika Law Society, Law Reform of Tanzania na watu wengine wengi wamekuwa kwenye huu mchakato wa kuzungumzia Katiba mpya, lakini kizingiti kimekuwa ni CCM na ugumu wa CCM kukubali kuwa kuna haja ya kuunda katiba mpya kwa ajili ya manufaa ya Tanzania na Watanzania na si CCM na Wana CCM.
Najinukuu nilichoandika mwezi wa March 2008
Sun, Mar 2, 2008 at 7:58 PM
subjectKatiba Project
mailed-bygmail.com
hide details Mar 2 Reply
Wapendwa,
Miezi miwili na nusu iliyopita, nilikuwa na mazungumzo marefu na XXXXX kuhusiana na Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Mazungumzo yetu yalikuwa ni kufuatilia mchakato wa gumzo la pale kijiweni na ombi rasmi la XXXX kuwa pamoja na kuwa yupo siriasi na kazi yake, lakini suala la Katiba tumuite.
XXXXX na mimi tulipitia majina ya wachache ambao tulionelea kuwa wanaweza kuwa "siriasi" kwenye huu mradi na hivyo tukakubaliana tufanye mawasiliano na kuanza gumzo.
Naomba mniwie radhi kwa kuchelewa kuandika na kukutanisha kama nilivyoombwa na XXXXX kufuatilia ujenzi wa kikundi hiki ambacho ni huru wa kufungamana na vyama vya siasa na lengo lake kuu ni kuujenga Utaifa na kumpa mwananchi wa Tanzania haki na uhuru wa kweli.
XXXXX utaniwia radhi kwa kujivutavuta kwangu kutuma waraka huu kwa hawa ndugu kuhusiana na hili. Lakini nafikiri kujivutavuta kwangu kumesadia kutupa picha na msukumo mpya au wa ziada katika kuanza harakati hizi za kutafiti ni njia gani zinabidi kufanyika na ni ushirikiano wa namna gani tutafute ili kuleta msukumo wa kuleta mabadiliko ya Katiba yetu ambayo hayajafanyika tangu vipengele vya mwisho kubadilishwa mwaka 1984 na kufuatiliwa na viraka mara kwa mara.
Najua tumekuwa na mazungumzo hapa na pale miaka nenda rudi kuhusiana na Katiba ya Tanzania . Nafikiri ni wakati muafaka kuanza kuweka mawazo yetu na kutafuta wataalamu wa kisheria ili kuleta msukumo huru usio ambatana na chama cha siasa kuhakikisha kuwa Katiba ya Taifa letu la Tanzania ni kwa faida ya mtanzania na si chama chenye madaraka au kikundi kidogo ambacho hiushia kujitwalia nguvu na mamlaka ya dola na kiserikali.
Aidha dhumuni lingine ni kuhakikisha kuwa Katiba ya Tanzania inabainisha kwa dhati mihimili mikuu ya Serikali (Executive, Legislative and Judicial) kwa kuzipa nguvu za kisheria kuwajibishana na kutoa haki na usawa.
Matukio makubwa mawili ambayo ni ya ziada kutoa nguvu ya kudai Katiba mpya ni yale ya kuanguka na kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa na Muafaka wa Kenya uliofikiwa majuzi.
Mtagundua kuwa katika suala la Waziri Mkuu na kuvunjwa kwa baraza la mawaziri, uundwaji mpya umetumia watu ambao ni wabunge na hivyo kuondoa fursa ya watu ambao si Wabunge ambao ni wataalamu wa mambo mbali mbali kama uchumi, fedha, biashara na menginewe kukosa kuwekwa katika nafasi hizo nyeti kutokana na mapungufu ya Katiba.
Yaliyotokea Kenya ni somo. Mkumbuke kuwa kutokana na tafurani na vurugu zilizotokea, kumesukuma kufanyika mabadiliko ya lazima ya Kikatiba ambayo yamehitimika kwa Raila na Kibaki kutia sahihi makubaliano ya Muafaka kuunda Serikali ya Mseto.
Hivyo basi naomba wote mpokee waraka huu kama kianzio cha mazungumzo na wale ambao watakuwa tayari kuendelea na harakati nawaseme hivyo. Wale ambao hawatakuwa na muda au nia ya kushiriki, pia tutaomba mseme hivyo ili kazi ya kubadilishana mawazo na harakati zianze.
Matumaini yetu mimi na XXXXX ni kutumia msukumo katika jamii yetu kudai Katiba mpya. Kazi hii si ndogo au nyepesi na katika kujivutavuta kwangu nimebaini kuwa wengi wamejaribu kufanya hivyo kuanzia vyama vya upinzani, taasisi za haki na sheria na wananchi wa kawaida.
CCM kupitia Serikali yake, imetangaza rasmi kuwa Katiba ni safi kabisa, lakini hata aliyekuwa Waziri Mkuu na Mwanasheria Mkuu Joseph Warioba ametamka hivi kaibuni kuwa kuna haja ya kuundwa kwa Katiba mpya na si kuendelea kuweka viraka.
Basi naomba tukae tutafakari na tuanze mdahalo na mchakato wa kuweza kufanya kazi hii.
Sasa utaona kuwa katika harakati zetu, nasi tumekumbana nahali halisi na tumekuwa kama fisi tukiotea mkono uanguke maana kuunyofoa pekee ni mgumu, hivyo kurudia maneno ya Madela wa Madilu ni kuwa kazi ya kuibomoa CCM na hata kuleta katiba mpya haitatokana na nguvu za nje pekee bali ni hata mfukuto wa ndani mithili ya Volcano.
Upinzani na hata sisi wananchi, tulichokosea awali ni kuamini kuwa CCM wangekuwa ni watu wenye Utu na kufuata Haki na hivyo kujenga mandhari sawa ya kuleta maendeleo ya Taifa. Ulipoanza Upinzani, iwe ni kwa hiyari yetu wenyewe au kwa mashinikizo, hakuna aliyetegemea kuwa CCM ingekuwa na undumilakuwili wa hali ya juu kiasi hicho. Labda tulichosahau ni ile tabia ya kuwa kigeugeu tuliyoiona kwa lile kundi la G-55 ambalo lilipewa baraka na Mzee Malecela na kisha wakaja mgeuka baada ya kutikiswa na maswali kutoka kwa Mwalimu Nyerere na hivyo kumuachia Mzee Malecela na Kolimba laana ya kuandikiwa kitabu.
Sasa kujua kuwa CCM inafanya mambo kwa manufaa yake na uimara wake pekee ni jinsi gani kila jambo linaloihusu CCM linavyofanyiwa kazi kupatiwa ufumbuzi. Jiulize ni vipi Somaiya anatoa pesa mfukoni kugharamia kamkutano ka UVCCM kufanya uchaguzi kama si kuwa CCM ina wenyewe na ina lindwa na Ufisadi na Uharamia?
Lakini Wanafunzi kuomba mikopo inakuwa nongwa, wastaafu kudai haki yao wanafanywa wehu na wahaini, wagonjwa kuhitaji dawa wanaachwa wanaangamia, wafanyakazi na waalimu wanadai mishahara ili kukidhi ukali wa maisha wanapewa vitisho na kukebehiwa.
Mkandara kadai kuwa wengine wanaogopa kuisakama CCM kwa kupoteza pensheni, kwani penshini si inatoka Serikalini na si CCM, hivyo kikija chama Kingine hiyo Pensheni bado ipo na hata kama ndani ya CCM kutameguka, mafao na pensheni bado yapo!
Ni uoga, unyonge na mara nyingine uzandiki kama si unyenyekevu wa kitumwa ambao baadhi ya Wana CCM wanaogopa kusimama kidete na kuvuruga chama na mshikamano wake wa kinafiki. Hivi vijikauli vya Kingunge kutishia watu au ule woga eti watakwisha kisiasa una maana gani na nguvu gani kwa watu kama Mzee Msuya, Salim, Billali, Malecela, Kafanabo, Mang'ula, Warioba, Seleli, Mwakyembe, Killango, Manyanya, na wengine wengi ambao tunajua kwa kweli wamechoka kudhihakiwa na kunyanyaswa na chama walichokitolea kiapo cha maisha?
Hivi leo unataka niambia na ni kweli unathibitisha kuwa CCM ina nguvu na wana CCM ambao wanajiita wanamageuzi, wanashindwa kuweka kiapo chao na utii wao kwanza kwa Taifa na katiba na kukimbilia kuinyenyekea CCM, imani, ahadi na upuuzi wake?
Sisi wote tumetoka na kuchipuliwa kisiasa na CCM. Wengine wetu pamoja na kuipenda kwa yale iliyoyafanya kale, imefika wakati imetubidi tuwe wakweli na tuweke maslahi ya Taifa mbele na si ya CCM au marafiki wa CCM.
Tunachotaka ni wale ambao wako ndani ya CCM kuanza kukimegua chama huku sisi nasi tukiweka nguvu kukimega na kukimomonyoa bila kuogopa nguvu za madaraka ya Rais ambaye sasa hata kama ndani ya Chama watasema hatumtaki, kuna uwezekano akatumia mabavu.
Labda kilichotokea Zanzibar 2000, Rwanda 1994 na kinachoendelea Congo kwa miaka 10 kinabidi kitokee Tanzania ili tuweze kusonga mbele maana sikio la kufa CCM halisikii dawa na njia pekee ni kulikatilia mbali.
Uchungu na damu ya Wananchi itakapomwagika, ndipo pale Watanzania kwa ujumla tutakapoamka na kukitokomeza CCM. Sawa na yale mawe ya kule Chunya au Wazee Wastaafu waliolala barabarani kudai hakio zao, tunawataka wale wanaojiita CCM mageuzi, waanze kurusha mawe bila woga au aibu na wagalegale barabarani.