Uchaguzi 2020 CCM Korogwe mlikuwa mnamdanganya nani? Kwanini mlijaza wanafunzi mkutanoni?

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,407
CCM mmetia aibu ya mwaka huko Bagamoyo, Pwani jana na leo huko Korogwe, Tanga.

Shule zilifungwa na kuamuru wanafunzi na walimu wao kuhudhuria mikutano ya kampeni ya Magufuli.

Nawaulizeni CCM, lengo la kufanya ujinga huu ni nini hasa? Mnamdanganya nani?

20201020_231219.jpg
 
Mkuu lazima muheshimiwa aone umati kwamba ni wanafunzi au raia hatujui hilo tumewatoa wapi haiwahusu, wameacha masomo! ni sehemu ya elimu bure hawa inawahusu kwanza waalimu wanachoka sana tunataka wapumzike na tukiamua tutawaleta hata wafungwa waote jua
in buku saba voice.

Hii vita ni kubwa sana walioletwa na waliokuja.
 
Mkuu lazima muheshimiwa aone umati kwamba ni wanafunzi au raia hatujui hilo tumewatoa wapi hiwahusu, wameacha masomo! ni sehemu ya elimu bure hawa inawahusu kwanza waalimu wanachoka sana tunataka wapumzike in buku saba voice.
Hii vita ni kubwa sana walioletwa na waliokuja.
Spana inazidi kubana, mwishowe magereza yote yanaweza kufungwa na wafungwa wote kusombwa kujaza hii mikutano. Kama na wao hawatatosha wagonjwa, wauguzi na madaktari nao wote wanaweza kubebwa wakahudhurie kuongeza vichwa. Si ajabu siku hiyo hata hospitali zikafungwa.
 
CCM mmetia aibu ya mwaka huko Bagamoyo, Pwani jana na leo huko Korogwe, Tanga.

Shule zilifungwa na kuamuru wanafunzi na walimu wao kuhudhuria mikutano ya kampeni ya Magufuli.

Nawaulizeni CCM, lengo la kufanya ujinga huu ni nini hasa? Mnamdanganya nani?

Ajaze wanafunzi, asijaze kushinda kupo palepale. Chama cha Mbowe, hakiwezi shinda milele. Wanapoteza rasilimali muda. Kama ruzuku tu mwala, je kodi zetu zitakuwa salama kweli?.
IMG_20201020_161500_327.jpg
IMG_20201020_161535_520.jpg
IMG_20201020_161600_472.jpg
IMG_20201020_161634_543.jpg
 
CCM mmetia aibu ya mwaka huko Bagamoyo, Pwani jana na leo huko Korogwe, Tanga...
Hapo ndio ujue mikakati ya ccm sio ya muda mfupi haifikirii uchaguzi huu maana imeshinda tayar kwa sasa hivi ni sherehe sio kampeni maana mgombea wetu karelax na anajua watanzania sio wajinga wameona yaliyofanyika,hao unaowasema wanafunzi ndio wapiga kura wa baadae.

Na hapo wengi wana kadi ya mpiga kura sasa wewe dhania wapiga kura ni wazee na akina mama ila vijana ni Chadema tu na wanafunzi iwe ni Ccm utashangaa 28oct mbona siku sio mbali tutaelewana tu mdogo mdogo utajua kuwa wale ni wananchi kama wewe.
 
Spana inazidi kubana, mwishowe magereza yote yanaweza kufungwa na wafungwa wote kusombwa kujaza hii mikutano. Kama na wao hawatatosha wagonjwa, wauguzi na madaktari nao wote wanaweza kubebwa wakahudhurie kuongeza vichwa. Si ajabu siku hiyo hata hospitali zikafungwa.
Ccm hawana hata aibu! Walimsomba hata mama Maria kule Musoma na kama alivyo mkweli, akawashushua.
 
Aibu gani hii jamani
Hebu tazameni jamani watoto wetu wanavyoteswa juani, kwa nini lakini?

CCM wanafunzi.jpg

Tafadhali sana CCM, kwa nini mnawahangaisha hivi watoto wetu? Waacheni hawa watoto wasome, tunawapeleka shule wasome na si kutumika kuongeza vichwa katika mikutano yenu. Kama watu wazima wamewasusia, msiwaadhibu watoto wetu. Sisi wazazi wao tuko na Mh. Tundu Antiphas Lissu!
 
CCM mmetia aibu ya mwaka huko Bagamoyo, Pwani jana na leo huko Korogwe, Tanga.

Shule zilifungwa na kuamuru wanafunzi na walimu wao kuhudhuria mikutano ya kampeni ya Magufuli.

Nawaulizeni CCM, lengo la kufanya ujinga huu ni nini hasa? Mnamdanganya nani?

Sasa hivi hela za kuhonga watu au kumobilize zimeisha hiyo ndio options pekee waliyonayo, hapo wanatafuta kuhalalisha wizi wao wa kura kwa msaada wa tiss na police na NEC bila kusahau jwtz.
 
Back
Top Bottom