Chrismoris
JF-Expert Member
- Oct 27, 2017
- 14,234
- 17,826
Uoga na ujinga wa watazamia nia ni mtaji kwa chama cha mwalimu magufuli et al
Baadhi ya watu, nikiwemo mimi, tumekuwa tukiamini kuwa mtaji mkubwa wa CCM katika ushindani wa kisiasa nchini ni ujinga wa wananchi.
Kwamba, kuna sehemu kubwa ya wananchi ambao ni wajinga ama kwa kutokutaka au kupenda kufuatilia mambo vizuri au kwa kuwa na uwezo mdogo wa kuchanganua mambo na hivyo kupelekea kurubuniwa na CCM pindi msimu wa uchaguzi unapokaribia ili wakipe kura chama hicho.
Tumekuwa tukiiamini sana nadharia hiyo kwa sababu tunaamini kuwa ni vigumu sana kwa mtu na akili zake timamu kuendelea kuiunga mkono CCM licha ya uborongaji wake.
Lakini, mimi binafsi nadhani mtaji wa kisiasa wa CCM si ujinga peke yake. Naamini pia uoga wa Watanzania nao ni bonge la mtaji kwao.
Sisi Watanzania ni waoga sana. Tunaogopa mno dola. Tukisikia tu polisi au jeshi, basi tunaanza kutetemeka.
Nyakati zingine huwa nikiangalia jinsi ambavyo watu wa mataifa mengine wanavyopambana na polisi huwa nabaki mdomo wazi.
Unakuta waandamanaji wanazipiga na polisi katikati ya barabara. Tena hawaogopi kabisa. Sasa mambo kama hayo hapa kwetu sidhani kama yanaweza kutokea. Na ndo maana huwa tukitishwa kidogo tu tunaogopa.
Hatuna kabisa ujasiri wa kuidindia serikali. Hatuna ujasiri wa kupigana na ma askari polisi kama wafanyavyo watu wa mataifa mengine.
Uoga wetu huu ndo unanifanya niamini kuwa CCM inaweza kutawala nchi hata kwa zaidi ya karne nzima.
Je, uoga tulionao nao ni sehemu ya ndivyo tulivyo ama?
Id yako inasawiri ulivyoChadema ilipopata fursa ya kukamata dola ikatuletea fisadi na hivyo watu wakaamua kwa dhati na kiakili mno kuwa ni lazima waibakishe CCM.
Kwa mantiki hii CCM lazima itawale milele !
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
suala la uoga Mimi nakataa.Hoja ya mleta hoja inasimama, na ni kweli sisi ni waoga, pengine kwa kujiuliza unachopigania ni nini!!??
Lakini pia haya mataifa yaliyopitia mfumo wa Ujamaa ni kandamizi, na ni wajanja hawarusu katiba ya wananchi dhidi ya serikali, bali wana hakikisha katiba ni serikali dhidi ya wananchi.
Ujinga mwingine huuBinafsi sidhani nitakuja kupanga mstari kupiga kura tena, 2015 ilikuwa mara ya kwanza na ya mwisho.
ujinga mkuu ..ukiwa mjinga nirahisi kutawaliwa na hofu kwa sbabu unakuwa upo upon tu hutambui umuhimu wakuipigania haki yko pindi unapo pokonywa ..wazee wetu walikuwa wnakamatwa na kwenda kuuzwa kama watumwa na mabepari walioshika mtutu mmoja wa bunduki huku wao wakiw wamekusanywa kwa wingi kama kuku huku wakiwa hawana maamuzi yyote Yale kwaajili ya ukombozi wao ...na ccm wanajua kabisa kuwa watanzania niwaoga na wajinga ndio maana inapofika nyakati za uchaguzi mkuu huwa wanaitumia TV ya taifa kuonyesha vita ya kagera kwa mantik yakuwatia hofu watanzania..na kwa hilo wamefauluYes! Woga pia ni tatizo kubwa linalochangia CCm kuwepo madarakani hadi leo. Sijui chanzo cha huu woga ni nini. Naamini hakuna nchi yenye raia waoga kama Tanzania. Ni kama laana.
sijawahi kufnya hcho kitendo mkuu..cjawahi kuwa mjinga wa kiasi hcho ..Binafsi sidhani nitakuja kupanga mstari kupiga kura tena, 2015 ilikuwa mara ya kwanza na ya mwisho.
watanzania niwaoga mkuu ..tena waoga haswaa njia yakukitoa chama tawala madarakani sio hiyo moja tu ykukitegemea chama pinzani ..kwa haya yaendeleayo sasa ktk nchi hii ingekuwa ni nchi nyingine sasa hvi tungeshaskia waasi wapo msituni ...hiii nchi RAIA wake sis ni mazoba kabisaWa
Watanzania sio waoga km unavyojiaminisha. Tatizo lipo kwa upinzani hauleweki pia hauaminiki. Huwezi kupigania kitu ambacho hakieleweki. Labda km haupo timamu.
Mwaka 2015 ukawa ilipata kura 52000 Kinondoni uchaguzi wamarudio imepata kura 12000. Hadi hapo unaona kuna haja ya raia kupigana na polisi? Tatizo kuu ni gia ya angani na kuanza kutakasa mafisadi. Raia wamekata tamaa wanaona ni heri zimwi likujualo.
Ndiyo,fear of unknown hupelekea mtu kuwa mjinga!!Hivi ujinga nao unaweza kupelekea mtu akawa muoga pia?
Wewe binafsi unaweza kuzipiga na polisi katikati ya bara bara? Acha ujinga wa kuhamasisha na kuchochea vurugu. Mnachochea vurugu halafu watu wakipigwa risasi mnaanza kuwalaumu polisi.Unakuta waandamanaji wanazipiga na polisi katikati ya barabara. Tena hawaogopi kabisa. Sasa mambo kama hayo hapa kwetu sidhani kama yanaweza kutokea. Na ndo maana huwa tukitishwa kidogo tu tunaogopa.
Kwani Ccm imeweza? Miaka karibu 60 ya kuongoza nchi bado mnambwela tu!Tupambane na polisi kwa sababu gani kwa mfano?
Tukiitoa ccm madarakani ni chama gani kinaweza kuongoza nchi?
Nina mashaka na IQ yako. Unakijua unachoongea au?Kwanini unataka kupigana na Polisi?
Polisi wanapiga kura?
Tatizo lako lipo ktk box la kura
Wapo wanaoipigia kura CCM na ni wengi.
Huwezi kushinda uchaguzi kwa kupigana na Polisi.
Kwa kiasi uko sawa lakini utaipataje tume huru?! Amini usiamini ni mpaka damu tena ya kutosha!! CCM hawawezi kukubalia tume huru wanajuwa watakuwa wameisha!!suala la uoga Mimi nakataa.
vita sio suluhisho mzee.tumeona nchi nyingi zilizotaka kujikomboa kwa vita mpaka Leo hakuna amani.
kikubwa NI NEC.huru.wansnchi waamue wanamtaka nani kihalali.demokrasia ichukue nafasi .tatizo CCM wanataka kufanya kwamba Wao ndo wana haki peke yao ya kuongoza.
hawakumbuki kama nchi hii NI ya demokrasia.mabavu uonevu hila.si mahala pake.
unakubalika tuonyeshe kweli unakubalika.sio KWA njia ya wizi na vitisho na umwagaji damu.