CCM itatawala nchi kwa karne nzima

CCM itatawala nchi kwa karne nzima

Ujinga mmoja tu umeona wewe huangalii ujinga mwingine kama vyama vyenyewe kutokua na msimamo wa yale wanayopigania, na kufarakana wao kwa wao na kutimuana kwa tofauti ya kimsimamo.hiyo utasemaje kama sio ujinga kwa upande wa mmoja.
Hawa jamaa ni wabinafsi sana na sasa wameanza kujivika mwavuli wa UTANZANIA nashindwa kuwaelewa usipokubaliana nao unakuwa Muhutu au Mtutsi?.
 
Hata hizo nchi unazozisifia kwamba sio waoga, walianza taratibu, na kuna vitu vilipelekea wakafikia hiyo hatua.
Naamini hata hapa kwetu kama hivyo vitu viliyopelekea watu wakapoteza uoga vikiendelea, woga utaisha na usishangae yakatokea kama yanayoendelea mataifa mengine.

Lakini kwanini uoga uangaliwe kwenye eneo moja tu la kupambana hasa kupigana na polisi au vyombo vya dola? CCM inaweza kutolewa madarakani kwa njia nyingi tu bila hata kupambana na polisi kwa mabavu.
Njia ipi mkuu?! Kinga yao wakati wa kuiba kura ni police na vyombo vingine vya dola .

Kwingine wameegemea kwenye udhaifu wa katiba yetu, ambayo imelimbikiza madaraka yote kwa mtu moja (Rais), ambaye naye anakasimu madaraka hayo kwa wateule wake dhidi ya chaguo la wananchi.
 
Mkuu Nyani kwa Mtazamo Wangu nadhani Nchi nyingi Zilizopata Uhuru Bila kumwaga Damu ikiwemo Tanganyika RAIA Wake ni waoga Mno..Na Wengi hawana Uchungu wa Kweli..Hata Zanzibar tu Wanapamba na Polisi Kudai Haki..
 
WIZI WA KURA.
NDO MTAJI WAO NAMBA 1.WALA USIZUNGUKE ZUNGUKE.
SIO CHA UJINGA WALA NINI.
 
Uwizi huo unawezeshwa na vyombo vya dola. Na ubovu wa katiba ulioifanya ccm kuwa sehemu ya vyombo vya dola
na NEC yao.
wanatumia nguvu nyingi kutuambia wanakubalika na RAIA.
cha ajabu wao ndo wanaongoza kwa udanganyifu kwenye chaguzi.
hila za kuwabugudhi mawakala Wa upinzani wao wanaongoza.
sasa mnakubalika vipi?
 
Ili uiangushe cccm ni kwa kuchochea fitina kwa ndani yameguke mapande matatu, wafia chama, wazalendo na wachumia tumbo.

Kwa sasa wote waoga joto bado halijakolea kukichemsha chungu. Ile ya nywele nyeupe lilikuwa povu tu la muda.

Hii episode ya Kizonje itakolea atakapoanza kuwatandika walioko ndani ya nyumba yake akimaliza hawa wa nje.

Wafia chama bado wanatafakari, wazalendo bado wako kwenye benefit of doubt njia ipi wachukue.

Wapinzani wala usiwahesabie walishapotezwa. Wananchi wanasubiri masihi wao wa kisiasa, ubuyu wa kuwasahaulisha hapa na pale na kudra za maulana.
 
Nakubaliana nawewe cc ni waoga na hatujui sheria hatakama haki niyakwako unadhurumiwa nahuwezi kuitetea tofauti na mataifa ya ASIA.
 
Hapo sasa wachaga na chama chenu ndo mnakosea kutuona wengine ni wajinga na kujiona nyie ni wajanja kumbe ni manyumbu. Ndio maana hatuwachagui ng`ooo.
 
Baadhi ya watu, nikiwemo mimi, tumekuwa tukiamini kuwa mtaji mkubwa wa CCM katika ushindani wa kisiasa nchini ni ujinga wa wananchi.

Kwamba, kuna sehemu kubwa ya wananchi ambao ni wajinga ama kwa kutokutaka au kupenda kufuatilia mambo vizuri au kwa kuwa na uwezo mdogo wa kuchanganua mambo na hivyo kupelekea kurubuniwa na CCM pindi msimu wa uchaguzi unapokaribia ili wakipe kura chama hicho.

Tumekuwa tukiiamini sana nadharia hiyo kwa sababu tunaamini kuwa ni vigumu sana kwa mtu na akili zake timamu kuendelea kuiunga mkono CCM licha ya uborongaji wake.

Lakini, mimi binafsi nadhani mtaji wa kisiasa wa CCM si ujinga peke yake. Naamini pia uoga wa Watanzania nao ni bonge la mtaji kwao.

Sisi Watanzania ni waoga sana. Tunaogopa mno dola. Tukisikia tu polisi au jeshi, basi tunaanza kutetemeka.

Nyakati zingine huwa nikiangalia jinsi ambavyo watu wa mataifa mengine wanavyopambana na polisi huwa nabaki mdomo wazi.

Unakuta waandamanaji wanazipiga na polisi katikati ya barabara. Tena hawaogopi kabisa. Sasa mambo kama hayo hapa kwetu sidhani kama yanaweza kutokea. Na ndo maana huwa tukitishwa kidogo tu tunaogopa.

Hatuna kabisa ujasiri wa kuidindia serikali. Hatuna ujasiri wa kupigana na ma askari polisi kama wafanyavyo watu wa mataifa mengine.

Uoga wetu huu ndo unanifanya niamini kuwa CCM inaweza kutawala nchi hata kwa zaidi ya karne nzima.

Je, uoga tulionao nao ni sehemu ya ndivyo tulivyo ama?

Miafrika ndivyo tulivyo....
 
na NEC yao.
wanatumia nguvu nyingi kutuambia wanakubalika na RAIA.
cha ajabu wao ndo wanaongoza kwa udanganyifu kwenye chaguzi.
hila za kuwabugudhi mawakala Wa upinzani wao wanaongoza.
sasa mnakubalika vipi?
Hoja ya mleta hoja inasimama, na ni kweli sisi ni waoga, pengine kwa kujiuliza unachopigania ni nini!!??

Lakini pia haya mataifa yaliyopitia mfumo wa Ujamaa ni kandamizi, na ni wajanja hawarusu katiba ya wananchi dhidi ya serikali, bali wana hakikisha katiba ni serikali dhidi ya wananchi.
 
..watanzania ni waoga ambao wamefikia hata kubaki kumwachia Mungu mambo ambayo yako ndani ya uwezo wao....mfano ..yani mtu anapigaje kura alafu anamwachia mwingine kuziiba tu huku anashuhudia!!!...hivi watu wanapokua wanaandamana kwa amani kinachowafanya wakimbie hivyo ni nini ingali hawatumii nguvu kupigana na polisi?..hivi watu wanafikiri polisi watawapiga risasi tu kama wakikomaa na kuendelea na maandamano???nina hakika Ikifika watu wakakomaaa na maandamano ya amani hata wakitishiwa kupigwa risasi hamna polisi atanyanyua risasi....huku kukosa ujasiri ndio mwanzo wa shida zote tz...nimekaa Ghana ...kule RAIA wanatembea vifua mbele maana serikali inawaogopa kiyama....maana ndio wanaoweka serikali madarakani.....yani wamekomaa hadi serikali imawahwshimu.....tz tuko na shida kubwa.....ujinga ..uoga Na ukondoo wa ajabu unaiangamiza nchi.. Hata Zanzibar wanatuzidi kwa ujasiri...
 
CCM itatolewa madarakani na jeshi Tatizo watu hawajui history ya nchi za kikomunisti, Tanzania ilikua kiini cha communism kwa Africa huwezi kuiondoa CCM madarakani ni sawa na communist party ya China iondoke madarakani, sio leo.
 
Mkuu upo sawa, lakini tatizo linapokuja ni pale mafiemu wanapo rusha risasi hadi ndani ya daladala.....
 
You are very right Mr Nyani because Mr God is your cousin
 
hatuna kitu kinachotuunganisha, mataifa mengine yana vitu vinavyowaunganisha mfano dini au kabila, those days kipindi tunasoma Milambo High School tulikuwa na uwezo wa kukabiliana na defenda nyingi za polisi na polisi walikuwa wakikimbia kwa sababu pale Milambo kulikuwa na spirit ya kuitana WANAUME
 
Cheki Korea huko uone jinsi raia wasivyo na uoga.
Mkuu una hoja katika bandiko lako ila nadhani umeangalia upande mmoja tu, Ukiangali hiyo Video na kufanya ulinganifu na Tanzania inabid umakini wa kuangali Pande zote kwa usahihi wake.
Ikumbukwe kuwa unaposema watanzania ni waoga ni Kweli, ila ukitumia hiyo Video unatupia lawama upande mmoja tu kuwa watanzania ni waoga, ila upande wa askari hujasema wako kundi gani.

Labda niseme ivi, Kwa video ya Korea uliyoweka, inawezekana hata hao Raia wake ni waoga isipokuwa tu kwakuwa Askari walitumia Weledi wao (au wamefuata Utaratibu/Sheria) ndio maana unaona hao raia Sio waoga. Kama ndivyo Je Askari watanzania ni Mashujaa?? Ukweli ni Kwamba kama hao polisi wangefanya kama wafanyavyo polisi wakwetu hapa nadhani bandiko lako lingekuja kwa style nyingine.

Tuwe tunaangalia pande mbili, Mara zote Askari wa Tanzania wamekuwa hawafuati Taratibu/Sheria au kutumia weledi kwenye kazi zao achilia mbali kwenye kuzui maandamano; mambo kama hayo ukiyaangalia kwa undani ni Rahisi sana kuja na Conclusion ya moja kwa moja kuwa Watanzania ni Waoga.

NB: Inawezekana watanzania ni waoga, ila usitumie justification ya Video ya Korea.
 
Baadhi ya watu, nikiwemo mimi, tumekuwa tukiamini kuwa mtaji mkubwa wa CCM katika ushindani wa kisiasa nchini ni ujinga wa wananchi.

Kwamba, kuna sehemu kubwa ya wananchi ambao ni wajinga ama kwa kutokutaka au kupenda kufuatilia mambo vizuri au kwa kuwa na uwezo mdogo wa kuchanganua mambo na hivyo kupelekea kurubuniwa na CCM pindi msimu wa uchaguzi unapokaribia ili wakipe kura chama hicho.

Tumekuwa tukiiamini sana nadharia hiyo kwa sababu tunaamini kuwa ni vigumu sana kwa mtu na akili zake timamu kuendelea kuiunga mkono CCM licha ya uborongaji wake.

Lakini, mimi binafsi nadhani mtaji wa kisiasa wa CCM si ujinga peke yake. Naamini pia uoga wa Watanzania nao ni bonge la mtaji kwao.

Sisi Watanzania ni waoga sana. Tunaogopa mno dola. Tukisikia tu polisi au jeshi, basi tunaanza kutetemeka.

Nyakati zingine huwa nikiangalia jinsi ambavyo watu wa mataifa mengine wanavyopambana na polisi huwa nabaki mdomo wazi.

Unakuta waandamanaji wanazipiga na polisi katikati ya barabara. Tena hawaogopi kabisa. Sasa mambo kama hayo hapa kwetu sidhani kama yanaweza kutokea. Na ndo maana huwa tukitishwa kidogo tu tunaogopa.

Hatuna kabisa ujasiri wa kuidindia serikali. Hatuna ujasiri wa kupigana na ma askari polisi kama wafanyavyo watu wa mataifa mengine.

Uoga wetu huu ndo unanifanya niamini kuwa CCM inaweza kutawala nchi hata kwa zaidi ya karne nzima.

Je, uoga tulionao nao ni sehemu ya ndivyo tulivyo ama?
Ujinga unazalisha uoga. Lakini usifikirie hali hii itaendelea kuwa hivi. Mara nyingi watu wa jinsi hii wakiamka na kuchoka hali uwa mbaya kuliko. Ni vizuri tukatatua mapema kwa kuweka mifumo sahihi.
 
Back
Top Bottom