CCM itatawala nchi kwa karne nzima

CCM itatawala nchi kwa karne nzima

Baadhi ya watu, nikiwemo mimi, tumekuwa tukiamini kuwa mtaji mkubwa wa CCM katika ushindani wa kisiasa nchini ni ujinga wa wananchi.

Kwamba, kuna sehemu kubwa ya wananchi ambao ni wajinga ama kwa kutokutaka au kupenda kufuatilia mambo vizuri au kwa kuwa na uwezo mdogo wa kuchanganua mambo na hivyo kupelekea kurubuniwa na CCM pindi msimu wa uchaguzi unapokaribia ili wakipe kura chama hicho.

Tumekuwa tukiiamini sana nadharia hiyo kwa sababu tunaamini kuwa ni vigumu sana kwa mtu na akili zake timamu kuendelea kuiunga mkono CCM licha ya uborongaji wake.

Lakini, mimi binafsi nadhani mtaji wa kisiasa wa CCM si ujinga peke yake. Naamini pia uoga wa Watanzania nao ni bonge la mtaji kwao.

Sisi Watanzania ni waoga sana. Tunaogopa mno dola. Tukisikia tu polisi au jeshi, basi tunaanza kutetemeka.

Nyakati zingine huwa nikiangalia jinsi ambavyo watu wa mataifa mengine wanavyopambana na polisi huwa nabaki mdomo wazi.

Unakuta waandamanaji wanazipiga na polisi katikati ya barabara. Tena hawaogopi kabisa. Sasa mambo kama hayo hapa kwetu sidhani kama yanaweza kutokea. Na ndo maana huwa tukitishwa kidogo tu tunaogopa.

Hatuna kabisa ujasiri wa kuidindia serikali. Hatuna ujasiri wa kupigana na ma askari polisi kama wafanyavyo watu wa mataifa mengine.

Uoga wetu huu ndo unanifanya niamini kuwa CCM inaweza kutawala nchi hata kwa zaidi ya karne nzima.

Je, uoga tulionao nao ni sehemu ya ndivyo tulivyo ama?
Ya ZANU PF na ANC yaweza tokea CCM. Iko wapi KANU,UNIP na MCP? Wana CCM wenyewe wakichoka mfumo wao wa kutawala wataji transform na kuji transfigure wenyewe.
 
Viongozi wengi wa siasa wajinga sana hasa Chadema,
haiwezekani mtu umuite fisadi arafu baade uje kumpa nafasi ya kupeperusha bendera tena kwenye nafasi ya Uraisi.

Huu ujinga ulivunja record.
 
NDUGU MEXENE MELLO et al.,
Naomba mnipige ban ya miaka miwili mpaka 2020.siwezi kuendelea kusoma maoni ya / comment ya wana Lumumba wapumbafu na machoko.
Ila endeleeni kushangilia, wakati bado unakuja .Magufuri kaweka vyombo vya habari kwapani, mahakama kwapani, jeshi la polisi kwani, bunge kwapani,shughuli za kisiasa na democrasia kwapani, taasisi za kidini kwapani nadhani uchunguzi kakobe mmeusikia. Shangilieni ,imbeni mtakavyo weza, tukaneni vyama pinzani mtakavyo weza, nunueni madiwani na wabunge mtakavyo weza ,ueni upinzani kadiri nguvu zenu zitakavyo weza.Ule mwisho badoo, Magufuri akianza kuuwa watu wake ndani ya ccm akihisi wanamuhujumu na wengine ndani ya chama chake , ndipo ule wakati uliotabiriwa utakuwa umewadia. Mtatafuta pa kukimbilia mtakosa, mtalia na kusaga meno ,mtaomboleza lakini hamtaona msaada wala hakuta kuwa na kimbilio. Endeleeni kushangilia, endeleeni kusifia.....siku zaja.
 
Viongozi wengi wa siasa wajinga sana hasa Chadema,
haiwezekani mtu umuite fisadi arafu baade uje kumpa nafasi ya kupeperusha bendera tena kwenye nafasi ya Uraisi.

Huu ujinga ulivunja record.
Umenena kweli mkuu. Halafu mtu huyohuyo anakuja mtandaoni kuwalalamikia watanzania eti hawajitambui. Siwezi kukubali kugeuzwa Msukule wa kukubalili kila kinachotoka kwenye vinywa vya watu hawa.
 
CCM si chama cha siasa, na kama kuna mtu ana amini hivyo atakuwa hajielewi... CCM is more of a state apparatus just like the rest..Police , etc...
Kupigana si hoja, hoja mtapigana hadi iweje... Mapinduzi?
Maana consequences za kupigana na dola ujiandae kisaikolojia kutupwa mabwepande, risasi za mchana kweupe na mengine mengi..
Siasa za CCM na za Urusi (United Russia) zinafanana sana....
KGB=TISS.

Mwalimu alikuwa muoga sana, akaishikamanisha CCM na Dolla(Japo alikuja gundua kosa hilo badae), im afraid kuitoa CCM madarakani itagharimu maisha ya wengi....

BTW hakuna haja ya kupigana na police kwa malengo mafupi ya ubunge au udiwani....(It must be something bigger and better than that)
Huo ndio ukweli.
 
Ujinga ni "package" mkuu, unajumuisha au kuambatana na matakataka mengi sana ndani yake ukiwamo huo uoga, umasikini, maradhi na mengineyo
Ukosawa mkuu! Nimekuelewa vizuri sana. Ujinga ni package
 
Back
Top Bottom