CCM itamke wazi kuwa kumsifia Rais ni sera yao mpya

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
6,376
6,720
Wapo watu ambao hufurahi wanaposifiwa kwa kila jema na zuri watendalo. Hili ni jambo zuri tu. Pia, wapo ambao huwa hawapendi sifa hata kama wakifanya mambo makubwa na mazuri. Hawa ni wachache. Kwa wenye busara, unaposifiwa sana lazima ujiulize. Ya kweli haya? Maana, ngoma ikivuma sana hupasuka.

Unaposifiwa, lazima uangalie anayekusifia na kwa lipi? Nitatoa mfano, wanasiasa kama Yusuf Makamba, Abdulrahman Kinana, Lusinde Kibajaji, Joseph Msukuma, Lameck Madilu Nchemba, na wengine wanaotetea matumbo yao wanapokusifia ujue unapaswa kulaumiwa.

Imekuwa jambo ambalo sasa linakera sina mfano kila mwana CCM kumsifia mama hata pale asipostahili. Nashangaa ni kwanini mama anakubali kusifiwa hata bila kustahiki. Tujikumbushe usifiaji ulipovuka mipaka pale Profedheha Kabundi alipomuita Mwendazake Magufuli akimsifu kwa kumtoa kwenye jalala wakati alikuwa kwenye nafasi nzuri na ya heshima chuo kikuu alichokigeuza kuwa choo kikuu kwa upofu na uroho wake.
Kwa wanaofuatilia mijdala bungeni na kwenye maeneo mengine, wabunge, karibia wote wa CCM humsifu na kumshukuru mama baada ya Mungu na wengine kusahau hata kumshukuru Mungu.

Je hii inatufundisha nini? Inaweza kufundisha yafuatayo:
Mosi, kuwa kuna viongozi wanaopenda kusifiwa hata wasipostahiki,

Pili, kuwa wanasiasa wengi ni wababaishaji na wachumia tumbo,

Tatu, kuwa sifa hizi si za kweli na stahiki bali wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa ili wamtumie.

Nne, kuwa kusifiwa ni jambo la hatari na hovyo. Nani alitegemea kuwa Mwendazake angegeukwa tena hata kabla ya mwili wake kuoza. Laiti angefufuka leo, huenda angebakia na Bashiru Ally peke yake kati ya wale wengi waliozoea kumtukuza na kumsifia naye akaridhika asijue ni umalayaa wa kisiasa.

Tano, kuwa ni wachache wenye hekima wanaopenda kukosolewa na kuchukia kusifiwa upuuuuzi. Rejea maneno ya Job Ndugai. Alisema bila kumung'unya kuwa Tanzania itakuja pigwa mnada. Je sasa tunafanya nini? Nani anamsifia hata kumshukuru Ndugai kwa kuliona hili?

Sita, kuwa wapo viongozi wanaopenda kusikia wanachotaka kusikia ila si kile wanachopaswa kusikia. Wako vizuri na kusikiliza uongo na mapambio ya kijinga badala ya ukweli na busara vinavyouma na kuwasuta ili wajirekebishe.

Je ni vibaya kuwashauri CCM watangaze rasmi kuwa kusifia nayo ni sera yao mpya ambayo italindeleza taifa japo kwenye sintofahamu hasa kutokana na kuchukia ushauri?

Wapo watu ambao hufurahi wanaposifiwa kwa kila jema na zuri watendalo. Hili ni jambo zuri tu. Pia, wapo ambao huwa hawapendi sifa hata kama wakifanya mambo makubwa na mazuri. Hawa ni wachache. Kwa wenye busara, unaposifiwa sana lazima ujiulize. Ya kweli haya? Maana, ngoma ikivuma sana hupasuka. Unaposifiwa, lazima uangalie anayekusifia na kwa lipi? Nitatoa mfano, wanasiasa kama Yusuf Makamba, Abdulrahman Kinana, Lusinde Kibajaji, Joseph Msukuma, Lameck Madilu Nchemba, na wengine wanaotetea matumbo yao wanapokusifia ujue unapaswa kulaumiwa. Imekuwa jambo ambalo sasa linakera sina mfano kila mwana CCM kumsifia mama hata pale asipostahili. Nashangaa ni kwanini mama anakubali kusifiwa hata bila kustahiki. Tujikumbushe usifiaji ulipovuka mipaka pale Profedheha Kabundi alipomuita Mwendazake Magufuli akimsifu kwa kumtoa kwenye jalala wakati alikuwa kwenye nafasi nzuri na ya heshima chuo kikuu alichokigeuza kuwa choo kikuu kwa upofu na uroho wake.
Kwa wanaofuatilia mijdala bungeni na kwenye maeneo mengine, wabunge, karibia wote wa CCM humsifu na kumshukuru mama baada ya Mungu na wengine kusahau hata kumshukuru Mungu. Je hii inatufundisha nini?
Inaweza kufundisha yafuatayo:
Mosi, kuwa kuna viongozi wanaopenda kusifiwa hata wasipostahiki,
Pili, kuwa wanasiasa wengi ni wababaishaji na wachumia tumbo,
Tatu, kuwa sifa hizi si za kweli na stahiki bali wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa ili wamtumie.
Nne, kuwa kusifiwa ni jambo la hatari na hovyo. Nani alitegemea kuwa Mwendazake angegeukwa tena hata kabla ya mwili wake kuoza. Laiti angefufuka leo, huenda angebakia na Bashiru Ally peke yake kati ya wale wengi waliozoea kumtukuza na kumsifia naye akaridhika asijue ni umalayaa wa kisiasa.
Tano, kuwa ni wachache wenye hekima wanaopenda kukosolewa na kuchukia kusifiwa upuuuuzi. Rejea maneno ya Job Ndugai. Alisema bila kumung'unya kuwa Tanzania itakuja pigwa mnada. Je sasa tunafanya nini? Nani anamsifia hata kumshukuru Ndugai kwa kuliona hili?
Sita, kuwa wapo viongozi wanaopenda kusikia wanachotaka kusikia ila si kile wanachopaswa kusikia. Wako vizuri na kusikiliza uongo na mapambio ya kijinga badala ya ukweli na busara vinavyouma na kuwasuta ili wajirekebishe.
Je ni vibaya kuwashauri CCM watangaze rasmi kuwa kusifia nayo ni sera yao mpya ambayo italindeleza taifa japo kwenye sintofahamu hasa kutokana na kuchukia ushauri?

Tangulini ulimzodoa mwenyekiti wako wa cdm
 
Last week alipokuwa Mwanza sijui ni ccm au nani wakawaandaa baadhi ya machinga wakampamba mama na kumpatia mbuzi kama zawadi wakimsifu kwa kuwajengea soko lao eneo la dampo kule Buhongwa.
Cha ajabu mwenyeki wa machinga wilaya asubuhi yake anaulizwa na wenzake anaruka kuwa hakutuma watu kwenda kumsifu mama na sasa wameanza kurudi mjini kwa fujo huku wakisema viongozi wanawasaliti

N:B Huu utaratibu wa kusifia kinafiki ccm ndo waasisi wa hilo jambo na Magufuli sasa ndo alikuja kubariki hilo jambo, yaani mtu akisogezewa mic sijui kusifia kunatoka wapi kwa huo muda
Mama nae sijui hajui namna apanakwa mafuta kwa …
 
Mambo ya CCM waachie wanaCCM kwasababu hakuna sheria ya nchi waliyovunja. Na nyie CHADEMA mseme kama ni sera yenu kutetea kila atakachosema Mbowe hata kama ni pumba. Majuzi Mbowe kaongea kauli za kibaguzi ila nyumbu wote wako bize kumtetea mmiliki wa chama chao.
 
Hujui usemalo na unatetea utopolo wewe mtopolo nyambuff
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom