...CCM is stabilising, CHADEMA is shrinking and CUF is disappearing!

Kichuguu

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Messages
7,438
Likes
1,326
Points
280
Kichuguu

Kichuguu

Platinum Member
Joined Oct 11, 2006
7,438 1,326 280
(1) Dynamic systems zina impulse response za aina hii hapa ambayo kukitokea mshtuko basi kutakuwa na overshoots na undershoots kabla ya kustabilize tena. Msuguano uliokuapo ndani ya chadema ni lazima ulileta impulsive response ya namna hii ndani ya chama.

(2) Halafu conservative systems zina asili ya kubadilishana kinetic na potential energy kiasi kuwa total energy ni constant. Uchaguzi ni conservative system, chama kimoja kikipata kura ni lazima chama lazima kingine kipoteze.

(3) Ukichukulia mambo hayo mawili hapo juu inakuwa si vizuri kutoa conclusion yoyote kutokana na matokeo ya uchaguzi wa madiwani uliofanyika kipindi ambacho Kitila na wenzake kwa Upande mmoja walikuwa wakiishambulia Chadema na CCM kwa upande mwingine nayo ikiishambulia Chadema ili kupata kura wakati upande wa chadema viongozi wake wakihangaika kushughulikiana na akina Kitila na wakati huo huo kuhangaika na kampeini. Magazetini habari za chadema zilikuwa mara zote ni sura mbili wakati habari za CCM zilikuwa na sura moja tu. Kwa vyovyote combination hiyo inasabaisha impuslive response kwa chadema, na ni wazi kuwa uchaguzi ulifanyika wakati ikiwa bado kwenye undershoot.

(4) Kutokana na conservative nature za uchaguzi, iwapo CHADEMA ilikuwa kwenye undershoot, basi si ajabu kwa CCM au chama kingine kupata advantage.

(5) Halafu analysis ya Dr Kitila ni shallow kidogo safari hii ukiilinganisha na ile aliyotoa mwaka huo 2012, kwa sababu safari hii amejikita katika generalization ya namba kuliko kuchambua namba hizo zina maana gani. Mwishoni anatumia results hizi kutuma ujumbe wake binafsi dhidi ya viongozi wenzake aliokorofishana nao huko chadema bila kuangalia effect ya impulsive response aliyosababisha kwenye chama chao. Matokeo ya uchaguzi yana parameters nyingi za kuangalia, na mojawapo incumbency. Mambo ambayo ningetegemea aonyeshe ni kata ngapi ambazo Chadema imepoteza na kati ya hizo ni ngapi zimechukuliwa na CCM. Iwapo uchaguzi ulihusu kata zilizokuwa zinasimamiwa na CCM zote halafu chadema ikachukua mbili au moja kati ya hizo huwezi kusema ina shrink hata kama percentage waliopata mwaka huu ni ndogo kulingana na mwaka uliopita. Kuna ile ya CHADEMA kupoteza kata moja au mbili huko Kigoma, hiyo alitakiwa aichukulie kuwa ni outlier kwa sababu Kigoma inahusiana na Zito ambaye naye alikuwa na mgogoro na CHADEMA na wala haitoi long term reflection ya performance ya CHADEMA; ni kati ya matokeo ya impulsive responses niliyozungumza hapo juu.
 
Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined
Dec 22, 2010
Messages
16,592
Likes
5,288
Points
280
Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined Dec 22, 2010
16,592 5,288 280
Inawezekana kauli yangu isiwaingie watu masikioni mwao kabisa, lakini nitawaeleza japo kwa kifupi.

Katika siasa kuna kitu kinaitwa siasa za jumla (general politics) na siasa za kijiografia (geography politics)

General politics inahusu mambo yanayohusu siasa za kitaifa bila kuchagua chama au itikadi na hizi mara nyingi husimamiwa kwa katiba, kanuni na sheria za nchi, hapa inahusiana pia na daftari la wapiga kura na tume ya uchaguzi,

Geography politics inahusu siasa za eneo husuka, kuna international gp, na domestic gp,

Katika hayo Chadema ime win kwenye Gp-D kwa asilimia zaidi ya 90%, hili linatokana na chama kushiriki uchaguzi kwa miaka yote huku mambo muhimu yanayopaswa kufanywa kwenye General Politics yakiwa doro kabisa, mambo hayo ni kama tume kuwa huru, daftari la wapigakura kuboreshwa, na dola kuvuruga chagizi nyingi kwa maslahi ya ccm.

Takwimu za chaguzi hizi zinatoa sura stahiki ya ubora wa domestic political ya Chadema,

Mathalani uchaguzi huu Chadema ilikuwa ikitetea kata 3, za Nyaisura, Kiborloni na Mikol.. Kigoma.

Tumepoteza Nyaisura, na Kigoma, na Tumeipoka ccm kata za Sombetini na Njombe.

Thamani ya kata ilizoshinda chadema nikubwa kuliko ccm, kubeba kata ya njombe ni turufu kubwa, vivyo hivyo kata ya sombetini Arusha ambapo sasa rasmi ccm inakuwa chama cha upinzani Arusha, CCM hawajaongeza thamani yoyote ya kata,

Kwa lugha nyingine nikuwa CHADEMA 0-0 CCM, lakini CHADEMA wananafasi ya golden goal kwakubeba kata ya Njombe ambayo kwanza inafuta propaganda za ccm yakuwa chadema ni chama cha ukanda, sasa tunashuhudia Chadema sio chama cha ukanda tena bali chama cha kitaifa na kila pembe ya jamhuri hii kipo.

Izingatiwe kuwa oparesheni M4C Pamoja Daima haikuwa maalumu kwaajili ya uchaguzi huu bali sehemu ya ratiba ya chama katika kutoa elimu ya umma kudai/kuhimiza uboreshaji wa daftari la wapiga kura.

Kuna wanaoamini kuwa Chadema kuwaadhibu wanachama wake waliovunja katiba ya Chama akina Zitto, Killa, Mwigamba eti ni "Mgogoro" uliochangia kwa 100% kutopata kata nyingi zaidi katika uchaguzi huu.

Nikubaliane nao wale wafikirio hivyo lakini tupeane shule ya falsa ya siasa kidemorasia kwa ufupi ambayo ndio hutawala siasa za uwanda wa chama kinachojiandaa kushika dola.

Niseme kuwa Chama cha siasa kilichokomaa na chenye wanachama wenye nguvu ya kitaifa kinapoamua kumuwajibisha mwanachama yeyote mwenye nguvu ya kitaifa aliyevunja katiba,itikadi,itifaki na falsafa ya chama hicho, kovu lake huwa halizibwi kwa miezi mitatu au sita tu, kisayansi itachukua hata mwaka kuirejesha nguvu ya chama katika mizani stahiki ya kisiasa.

Hivyo Mwanachadema yeyote na mwanamageuzi ni lazima atambue kuwa uchaguzi wa Udiwani huu kwa kata 27 nchini, sio kipimo stahiki cha kufuta pengo la akina Zitto. Labda kwa mchambuzi wa siasa asiejua sayansi ya siasa tu na mwenye agenda ya kipropaganda ndie ataamini kufukuzwa akina Zitto ni chanzo cha kupata kushindwa kupata kura nyingi zaidi katika uchaguzi huu.

Athari za kufukuzwa kwa Zitto na wenzie ndani ya chama zitapimwa baada ya miezi sita hadi mwaka mmoja kutoka sasa hii ikiwa na maana uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao ndivyo vitakuwa vipimo vyake, kwa sasa yanayotokea yalitarajiwa kwa 100% na yalipita kwenye chekecho la kimkakati la chama na kisha yakaamuliwa iwe hivyo.

Kosa kubwa kwa Chadema ni kosa la kimkakati na hili ni lazima lifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo,

Kwanza ieleweke kuwa daftari la wapiga kura ndio rungu lililoibeba ccm, ni lazima liboreshwe ikiwa ni pamoja na uingizaji wawapiga kura wapya ambao utafiti unaonyesha ni kundi kubwa la vijana wenye umri kati ya miaka 18-26 ambao hawakuwa na sifa ya kupiga kura 2010. Lakini hata hawa waliojiandikisha yaani wenye kupiga kura sasa, idadi kubwa ya wapiga kura hao hawakupiga kura kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuuza shahada zao.

Pili Tume ya Uchaguzi, hii ni lazima juhudi za msksudi zitumike kuitoa mikononi mwa chama tawala, ni hatari kuiacha iendelee kuwa wakala wa ccm badala yakuwa tume huru.

Tatu Vyombo vya dola, hapa ndipo panahitaji mkakati mkuu wa kisiasa, jeshi la polisi ni lazima tukabiliane nalo na ieleweke vema kuwa ccm haitakoma kulitumia jeshi la polisi ama vyombo vya dola kwa ujumla mpaka siku inakata roho kabisa, hivyo njia mbadala ni muhimu sana tunapoelekea kushika dola hili la Tanzania mnamo octobar 25, 2015.

Kwanza uundwe mkakati wa uhusiano mwema na vyombo vyote vya dola nchini, hili linaweza kuwa gumu kidogo na linaweza kuifanya serikali ianze kupata mafua ya msimu na kujikuta tunaingia kwenye mgogoro unaoweza kutumiwa na wakware wa akili wa ccm kama akina Mwigulu na kufikiria uhaini, jambo la muhimu ni kuziangalia sheria za nchi hasa zinazoratibu vyama vya siasa na mienendo yake,

Mathalani kiongozi wa kisiasa kuzuru makao makuu ya Jeshi la Polisi Tanzania na kusikiliza changamoto zinazowakabilli, hili halina zuio kisheria, ilimradi haendi kugawa kadi za chama hapo,

Ni lazima tuitazame upya sheria inayosema mtumishi wa umma asijihusihe na siasa, hii ni nzuru lakini iboreshwe ili iwe na tafsiri ya maslahi kwa nchi na hatimae taifa kuzaa siasa za kisasa na za kimaendeleo.

Wanamikakati warejee chini wawafanyie utafiti wa kisayansi viongozi wa majimbo, mikoa na kanda, nilazima tuwapime kwa nyuzi 360 kiutendaji kwakuwa hizi chaguzi ndogo za kata na serikali za mitaa zinatakiwa wao wasimamie na kuonyesha uwezo wao na sio hivyo tu bali lipo ndani ya uwezo wao kikatiba, Chama lazima sasa kijikite kwa nguvu zote kwenye msingi (chadema ni msingi).

Ni lazima tufanye utafiti wa kimkakati usio na unafiki wala haya,

Tukiyatekeleza haya yote, uchaguzi wa serikali za mitaa utaanza kutupa majibu ya mkakati huu na uchaguzi mkuu ujao tutashinda!

Yote kwa yote Chadema haijapoteza uchaguzi huu bali imeng'ara, kimkakati ni ccm ndio imepoteza.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
(1) Dynamic systems zina impulse response za aina hii hapa ambayo kukitokea mshtuko basi kutakuwa na overshoots na undershoots kabla ya kustabilize tena. Msuguano uliokuapo ndani ya chadema ni lazima ulileta impulsive response ya namna hii ndani ya chama.

(2) Halafu conservative systems zina asili ya kubadilishana kinetic na potential energy kiasi kuwa total energy ni constant. Uchaguzi ni conservative system, chama kimoja kikipata kura ni lazima chama lazima kingine kipoteze.

(3) Ukichukulia mambo hayo mawili hapo juu inakuwa si vizuri kutoa conclusions yoyote kutokana na matokeo ya uchaguzi wa madiwani uliofanyika kipindi ambacho Kitila na wenzake kwa Upande mmoja walikuwa wakiishambulia Chadema na CCM kwa upande mwingine nayo ikiishambulia Chadema ili kuapata kura wakati upande wa chadema viongozi wake wakihangaika kushughulikiana na akina Kitila na wakati huo huo kuhangaika na kampeini. Magazetini habari za chadema zilikuwa mara zote ni sura mbili wakati habari za CCM zilikuwa na sura moja tu. Kwa vyovyote combination hiyo inasabaisha impuslive response kwa chadema, na ni wazi kuwa uchaguzi ulifanyika wakati ikiwa bado kwenye undershoot.

(4) Kutokana na conservative nature za uchaguzi, iwapo CHADEMA ilikuwa kwenye undershoot, basi si ajabu kwa CCM au chama kingine kupata overshoot.

(5) Halafu analysis ya Dr Kitila ni shallow kidogo safari hii ukulinganisha na ile aliyotoa mwaka huo 2012, kwa sababu safari hii amejikita katika generalization ya namba kuliko kuchambua namba hizo zina maana gani.

Mwishoni anatumia results hizi kutuma ujumbe wake binafsi dhidi ya viongozi wenzake aliokorofishana nao huko chadem bila kuangalia effect ya impulsive response aliyosababisha kwenye chama chao.

Matokeo ya uchaguzi yana parameters nyingi za kuangalia, mojawapo ni ya mambo ambayo ningetegemea aonyeshe ni kata ngapi ambazo Chadema imepoteza na kati ya hizo ni ngapi zimechukuliwa na CCM.

Iwapo uchaguzi ulihusu kata zilizokuwa zinasimamiwa na CCM zote halafu chadema ikachukua mbili au moja kati ya hizo huwezi kusema ina shrink hata kama percentage waliopata mwaka huu ni ndogo kulingana na mwaka uliopita.

Kuna ile ya CHADEMA kupoteza kata moja huko la Kigoma, hiyo alitakiwa aichukulie kuwa ni outlier kwa sababu Kigoma inahusiana na Zito ambaye naye alikuwa na mgogoro na CHADEMA na wala halitoi long term reflection ya performance ya CHADEMA; ni kati ya matokeo ya impulsive responses niliyozungumza hapo juu.
Thank you sir!
 
Myakubanga

Myakubanga

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Messages
5,822
Likes
403
Points
180
Myakubanga

Myakubanga

JF-Expert Member
Joined Oct 3, 2011
5,822 403 180
(1) Dynamic systems zina impulse response za aina hii hapa ambayo kukitokea mshtuko basi kutakuwa na overshoots na undershoots kabla ya kustabilize tena. Msuguano uliokuapo ndani ya chadema ni lazima ulileta impulsive response ya namna hii ndani ya chama.

(2) Halafu conservative systems zina asili ya kubadilishana kinetic na potential energy kiasi kuwa total energy ni constant. Uchaguzi ni conservative system, chama kimoja kikipata kura ni lazima chama lazima kingine kipoteze.

(3) Ukichukulia mambo hayo mawili hapo juu inakuwa si vizuri kutoa conclusion yoyote kutokana na matokeo ya uchaguzi wa madiwani uliofanyika kipindi ambacho Kitila na wenzake kwa Upande mmoja walikuwa wakiishambulia Chadema na CCM kwa upande mwingine nayo ikiishambulia Chadema ili kupata kura wakati upande wa chadema viongozi wake wakihangaika kushughulikiana na akina Kitila na wakati huo huo kuhangaika na kampeini. Magazetini habari za chadema zilikuwa mara zote ni sura mbili wakati habari za CCM zilikuwa na sura moja tu. Kwa vyovyote combination hiyo inasabaisha impuslive response kwa chadema, na ni wazi kuwa uchaguzi ulifanyika wakati ikiwa bado kwenye undershoot.

(4) Kutokana na conservative nature za uchaguzi, iwapo CHADEMA ilikuwa kwenye undershoot, basi si ajabu kwa CCM au chama kingine kupata advantage.

(5) Halafu analysis ya Dr Kitila ni shallow kidogo safari hii ukiilinganisha na ile aliyotoa mwaka huo 2012, kwa sababu safari hii amejikita katika generalization ya namba kuliko kuchambua namba hizo zina maana gani. Mwishoni anatumia results hizi kutuma ujumbe wake binafsi dhidi ya viongozi wenzake aliokorofishana nao huko chadema bila kuangalia effect ya impulsive response aliyosababisha kwenye chama chao. Matokeo ya uchaguzi yana parameters nyingi za kuangalia, na mojawapo incumbency. Mambo ambayo ningetegemea aonyeshe ni kata ngapi ambazo Chadema imepoteza na kati ya hizo ni ngapi zimechukuliwa na CCM. Iwapo uchaguzi ulihusu kata zilizokuwa zinasimamiwa na CCM zote halafu chadema ikachukua mbili au moja kati ya hizo huwezi kusema ina shrink hata kama percentage waliopata mwaka huu ni ndogo kulingana na mwaka uliopita. Kuna ile ya CHADEMA kupoteza kata moja au mbili huko Kigoma, hiyo alitakiwa aichukulie kuwa ni outlier kwa sababu Kigoma inahusiana na Zito ambaye naye alikuwa na mgogoro na CHADEMA na wala haitoi long term reflection ya performance ya CHADEMA; ni kati ya matokeo ya impulsive responses niliyozungumza hapo juu.
Great!
Application of natural science in politics field!
Kwa kweli mkuu umenifumbua macho,sikuwahi kuwaza in those dimensions.
In long run,nadhani equilibrium will shift towards CHADEMA,kwani,pamoja na machafuko wamefanikiwa kubakiza idadi ile ile ya kata.
 
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
43,029
Likes
18,087
Points
280
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
43,029 18,087 280
Halafu utasikia watu wanapiga kelele CHADEMA lazima iingie Ikulu 2015.

Don't get me wrong, Dr. Mkumbo is not beyond questioning, especially because he is admitting that he was holding back on us facts regarding matters of national importance for partisan reasons while he was a CHADEMA cadre, but at the same time I resonate so much with his analysis, especially because I am part of the segment of the Tanzanians who are appalled by CCM but yet cannot see credible leadership in CHADEMA.

I am dying to see the opposition/ CHADEMA do better so I could give it my full support in ousting CCM, but it just doesn't.

And I do not want Tanzania to have another Chiluba moment and become a laughingstock of the democrartic process.
 
Mkuu Kiranga naomba nichangie kidogo bandiko lako

1. Kama alivyosema Kichuguu , nilikuwa miongoni mwa watu walio doubt sana credibility ya Dr Mkumbo miaka 5 au zaidi huko nyuma. Sina shaka nilikuwa sahihi kwa kumuangalia leo hii

2. Kunapotokea tatizo mara nyingi zinakuwepo 'factors' Internal or external or both
Kwa hali ya upinzani kwasasa kuna internal and external factors kwa pamoja. Nitafafanua

i)Internal factors; Miaka mingi tuliwaeleza wapinzani lengo lisiwe kwenda Ikulu bali njia za kwenda Ikulu. Kauli rahisi ilikuwa 'lengo la chama cha upinzani ni kushika dola'
Kushika dola ni hatua ya mwisho, hatua ya kwanza ni 'means' za kushika dola

Kule UK, Nigel Farage (UKIP) kilifahamu hakiwezi kushindana na Labor au conservative. Kilichofanyika ilikuwa ku ''tilt balance of power'' kati ya liberal na Tories
Farage aliweza kupata support iliyoleta Brexit na kubadilisha siasa za ndani

Ndivyo ilivyokuwa kwa Tea Party ambayo baadaye iliji filtrate kuwa Republicans.
Influence ya Tea party ndiyo iliyozaa siasa za US. Tea party hawakuwa na lengo la kushika dola

Lengo la wapinzani Tanzania ilikuwa kwanza kujitanua, pili kushika mhimili wa Bunge ambao leo ungewapa leverage katika mambo mengi. CCM wangewahitaji ku compromise

Hawakutilia maanani wakajikita katika kuendekeza 'defections' za wanachama.

ii) Tukawaeleza kwa mwendo wa katiba ya sasa ambayo CCM walitumia nguvu kuzuia mpya, it's unlikely watafanikiwa. Kwamba, katiba ya sasa hata kile kidogo kitaondolewa.
Lengo la kushika dola si priority, kujenga ''level playing field'' ni muhimu kuliko jambo jingine. Hawakuzingatia

b) External factor; Katika mazingira ya sasa ya siasa, mapungufu ya upinzani hayaonekani au yanafunikwa na nyakati. Hili ni pamoja na CCM kubadilika kutoka chama cha siasa na kuwa serikali inayomiliki taasisi zote zikiwemo zile zinazotakiwa kuwa neutral

Marufuku ya mikutano ilikuwa hatua ya awali. Kuandamana vyombo vya habari ilikuwa kujenga mazingira ya kazi za baadaye. Kazi sasa inafanywa na CCM na vyombo vyake bila kelele

Kwa haraka upinzani hauja 'shrink' . Wabunge na madiwani wanaohama si kigezo cha 'shrink

Mazingira yanalazimisha hivyo na hata wanaohama wanajua hilo
Hivyo upinzani hauja shrink bali umewekewa mazingira ya kutoendelea kwa maana umedumaa

CCM haija stabilize hata kidogo bali imejengewa mazingira ya kustawi kwa nguvu za dola
Ndani ya CCM kuna resentment , wenye reservation wana katika wakati mgumu kama ule wanaopitia wapinzani. Ndani ya CCM hali si Shwari. Unakumbuka ya mkutano mkuu wanachama kukamatwa na vyombo vya dola?

Wapinzani waanzie wapi? Wasahihishe kosa la katiba mpya walilokubali bila kujua namna ya kukabiliana na hujuma. Watafute njia za kuwa na uwanja huru wa kisiasa ikiwemo tume huru ya uchaguzi. Wafanye recalculations kwamba kushika dola ni process siyo short cut na isiwe priority

Wajikite kujiimarisha katika kuwa na upper hand ndani ya Bunge na kwingineko
Hilo nalo litategemea jitihada zao za kutafuta uwanja sawa wa siasa kisheria kupitia katiba mpya
 
Umechambua vizuri.

Mkuu, mimi nafanya kazi za kuangalia matatizo kwa kuyaweka katika layers na kutenganisha hizi layers.

Kwa sasa naona dhahama katika vyama vya siasa si matatizo halisi, huu si ugonjwa.

Hizi ni dalili tu, ugonjwa wenyewe upo katika a deeper layer.

Layer ya utamaduni, malezi, familia.

Familia ambazo zimehalalisha baba kuwa na nyumba ndogo na mama na dada kudanga, haziwezi ku produce viongozi wa kisiasa wenye integrity.

I am sure ukiangalia mtu kama Magufuli ana hang ups za familia.

Jamii inayosisitiza utamaduni wa ukondoo na hewala hewala, haiwezi ku produce viongozi wenye integrity. Hata wasomi wetu wanakuwa watu waoga waoga tu, kwa sababu formative years zao zimekuwa informed na utamaduni wa hewala hewala, ukondoo kondoo, woga woga.

Malezi ya kubwengana bwengana, kukomoana komoana, kuzibiana zibiana ndiyo yana produce viongozi walio shortsighted kama Magufuli wanafikiria kufunga funga tu vitu willy-nilly kama jina lake. Granted nchi ilioza na kuna reforms nyingi zilitakiwa, but don't throw the baby with the bathwater for gods sake.

Matatizo yetu yapo katika familia, malezi, utamaduni.

Kiongozi aliyelelewa kwa kuinewa anaona kuonea ni haki ya mkubwa. Akipata uongozi anaona na yeye zamu yake ya kuonea imefika, mshamuonea sana.

Ndiyo maana hata sioni tofauti kubwa kati ya CCM na wapinzani, ndiyo maana wapinzani wanahamahama kwenda CCM iliyominya demokrasia, kwa kisingizio wanafuata demokrasia.

Familia, malezi, utamaduni, ndiyo mizizi ya matatizo yetu. huko kwenye vyama ni matawi tu, hata tukijitahidi kutengeneza siasa za vyama, kama hatujatengeneza familia, malezi, utamaduni, tutakuja kupata matatizo mengi sana.

Siku hizi watoto wasiolelewa na wazazi wote wanakuwa kama fashion, hawa wakija kuwa wakubwa litalipuka bomu kubwa sana ambalo mabadiliko ya vyama vya siasa hayawezi kulituliza.

Viongozi wa caliber ya Nyerere tuliwapata kwa mchanganyiko wa malezi ya utamaduni wa Kiafrika pamoja na elimu ya magharibi, siku hizi tunakosa vyote viwili. Hili kwangu ni tatizo la msingi kuliko matatizo ya siasa za vyama sasa, kwa sababu haya ksho yataleta matatizo makubwa zaidi.

To be fair, sitaki ku minimize matatizo ya siasa za vyama sasa, kwa sababu katika nchi iliyo top down kama yetu, mtu wa juu akiamua kufanya reforms nzuri anaweza sana, tuna tabia ya ku idolize marais wetu kwa mfano.Lakini, my sense is, rais anahalalisha kumomonyoka maadili, na anatengeneza vi Magufuli vingine huko kwa kina Makonda, Jerry Muro, Gambo etc

Katika nchi yenye matatizo ya kiutamaduni kama yetu, hata wazee wa CCM kama marais wastaafu wanaonekana kushindwa kumuasa Magufuli aache kauli zisizo na staha za kirais, kwa sababu hiyo ni distraction hata kama anataka kufanya mageuzi, hatuna a coherent direction.

Sasa katika nchi ambayo hatuwezi kuwa na common decorum tu, habari za political ideology ni kumfundisha calculus sisimizi.

My main concern kwa sasa si kwamba siasa za vyama zinaendaje.

I am more concerned kuona rais anasema atawapiga shangazi wa wapinzani wake wa kisiasa, vijana wanaokua sasa wanaona kumbe mwanamme kumpiga mwanamke ni kitu cha kawaida tu, regardless wanakuwa chama gani.

Rais anasema wazi kabisa kwamba vyombo vya dola vikipe upendeleo CCM katika chaguzi. Yani mambo ya aibu yanasemwa wazi kama kawaida tu, na hakuna anayesema sana, inazoeleka.

Common decorum imetoweka.

Hapo maana yake, atakayeshika madaraka baada ya huyu atakuwa anatoka katika mazingira mabaya na anaweza kutupeleka pabaya zaidi
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
Mkuu Kiranga , naomba nipitie hoja zako kadhaa zilizonigusa kwa matiki zake
"Kiranga, post: 28457078, member: 13377"]
Kwa sasa naona dhahama katika vyama vya siasa si matatizo halisi, huu si ugonjwa.
Hizi ni dalili tu, ugonjwa wenyewe upo katika a deeper layer.Layer ya utamaduni, malezi, familia.
Nakubaliana nawe kwa sababu nitakazozieleza mbeleni
Jamii inayosisitiza utamaduni wa ukondoo na hewala hewala, haiwezi ku produce viongozi wenye integrity.
Nakubaliana jamii isiyo na 'curiosity' au isiyohoji, isiyo na mitazamo tofauti na isiyoweza kujifunza kutoka kwingine ni 'mfu' (dormant). Jamii zilizopiga hatua popote dunia ni zile 'vibrant'.
Hata wasomi wetu wanakuwa watu waoga waoga tu, kwa sababu formative years zao zimekuwa informed na utamaduni wa hewala hewala, ukondoo kondoo, woga woga.
Hili linatisha zaidi kuliko jingine katika jamii yetu. Wasomi wamesahau au hawajui au wametelekeza wajibu wao kwa jamii. Wasomi ndio 'architects' ya jamii yoyote. Kazi yao ni ku-map mustakabali wa Taifa. Mwalim Nyerere alielewa hili, siku zote alitoa fursa kwa wasomi kutumia 'zana' zao za akili kulisaidia Taifa.

Zama za Mwalimu Chuo kikuu kilikuwa UDSM. Historia inaonyesha chuo kilikuwa chem chem ya fikra hata kuwa kitovu cha 'intellectuals' kwa Raia, wanaharakati na waigania uhuru

Pamoja na ukali wa Mwl siku zote hakusita kuwasikiliza au kujibu hoja zao kwa hoja
Kwasasa jamii ya wasomi ni kama imetoweka.

Mfano, Wasomi hawawezi kuchambua mswada wa takwimu ambao kimsingi unaathiri shughuli zao kuliko wanasiasa au wananchi wa kawaida. Hawaoni hatari ya kujifungia katika takwimu za kuambiwa, hatari ya kutokuwa na curiosity ya takwimu n.l.

Kwamba kuna ''marufuku' ya kujadili takwimu, sasa unajiuliza wasomi wetu watajadili nini
Kwanini hawakuchukua usukani kueleza tatizo na kulitafutia ufumbuzi ?
Ndiyo maana hata sioni tofauti kubwa kati ya CCM na wapinzani, ndiyo maana wapinzani wanahamahama kwenda CCM iliyominya demokrasia, kwa kisingizio wanafuata demokrasia.
Hili linachagizwa na mambo mawili uliyosema.

Kwanza, malezi, makuzi na tamaduni. Siku hizi uongo umekuwa sehemu za maisha yetu. Huko nyuma mtu asiye na msimamo alionekana mwendawazimu tu.
Watu walisimamia walichoamini katika dhamira zao

Watu kama mwalimu walilelewa katika kuamini heshima, utu na nafasi yao katika jamii
Mwl aliweza kuunganisha nchi katika jitihada za kutafuta uhuru.

Alithamini tamaduni kila alipokwenda. Aliheshimu watu kwa marika yao na alikuwa anasimamia alichoamini. Mwl alielewa kazi ya uongozi ina changamoto zake. Hata alipobezwa aliwasikiliza waliombeza na kuwajibu kwa hoja.
Hiyo ndiyo ilikuwa nguvu ya Mwl si nchini bali duniani alikotambuliwa

Pili, wasomi wetu wanachangia sana katika hoja hii. Wasomi wetu wanaoongoza katika kuyumba kimisimamo kiasi cha kuwaacha wananchi wakihoji tofauti yao na wao

Wasomi hao ndio wanaoongoza vyama vya siasa. Ikiwa wamepoteza dira na maana ya usomi kwao kuhama hama vyama kubadili misimamo ,kukubali kazi hata chini ya viwango imekuwa sehemu ya maisha. Ni utamaduni mpya tofauti na ule wa zamani uliojengwa katika malezi, makuzi na tamaduni. Hili ni kundi linaloyumbisha taifa kuliko makundi mengine yoyote
Siku hizi watoto wasiolelewa na wazazi wote wanakuwa kama fashion, hawa wakija kuwa wakubwa litalipuka bomu kubwa sana ambalo mabadiliko ya vyama vya siasa hayawezi kulituliza.
Bomu la wasomi tayari linalipuka. Hawa half-baked wamelelewa katika fashion unayosema. Tunachokiona katika jamii ni ''mlipuko'' wa bomu la wasomi
Sitegemei kama kuna kijana anajifunza tofauti na wao zaidi ya kufikiria katika ubovu kuliko uliopo
Viongozi wa caliber ya Nyerere tuliwapata kwa mchanganyiko wa malezi ya utamaduni wa Kiafrika pamoja na elimu ya magharibi, siku hizi tunakosa vyote viwili. Hili kwangu ni tatizo la msingi kuliko matatizo ya siasa za vyama sasa, kwa sababu haya ksho yataleta matatizo makubwa zaidi.
kama nilivyoeleza kuhusu mwalimu.
Ninachokiona ni kutokuwa na uwezekano wa kupata watu wa caliber hiyo kwa muda mrefu. Utamaduni uliowajenga akina Mwalimu umetoweka, sasa tuna utamaduni mwingine kabisa
Sasa katika nchi ambayo hatuwezi kuwa na common decorum tu, habari za political ideology ni kumfundisha calculus sisimizi.
Hili la common decorum ni tatizo kubwa sana. Tunarudi kule kule, hatuna watu wa kuturudisha katika mstari, si wazee si wasomi.
Tumekuwa 'zoo' lenye wanyama wasioweza kusikilizana, hatuna common decorum

Concern yangu siyo political landscape. Politics hazina gravity zinakuwa shaped na mwenendo wa jamii. Concern niliyo nayo ;

1. Lack of common decorum ambayo ni vicious circle kama haitakuwa checked
2. Hatuna consensus katika masuala yanayohusu jamii yetu
3. Tume abandon utamaduni wetu wa kujadilina 'chini ya miti' hata kama hatukubaliani
4. Tumeanza kugawanyika kwa kukosekana common decorum, consensus and unity
 
Mwalimu

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
1,492
Likes
285
Points
180
Mwalimu

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
1,492 285 180
Umechambua vizuri.

Mkuu, mimi nafanya kazi za kuangalia matatizo kwa kuyaweka katika layers na kutenganisha hizi layers.

Kwa sasa naona dhahama katika vyama vya siasa si matatizo halisi, huu si ugonjwa.

Hizi ni dalili tu, ugonjwa wenyewe upo katika a deeper layer.

Layer ya utamaduni, malezi, familia.

Familia ambazo zimehalalisha baba kuwa na nyumba ndogo na mama na dada kudanga, haziwezi ku produce viongozi wa kisiasa wenye integrity.

I am sure ukiangalia mtu kama Magufuli ana hang ups za familia.

Jamii inayosisitiza utamaduni wa ukondoo na hewala hewala, haiwezi ku produce viongozi wenye integrity. Hata wasomi wetu wanakuwa watu waoga waoga tu, kwa sababu formative years zao zimekuwa informed na utamaduni wa hewala hewala, ukondoo kondoo, woga woga.

Malezi ya kubwengana bwengana, kukomoana komoana, kuzibiana zibiana ndiyo yana produce viongozi walio shortsighted kama Magufuli wanafikiria kufunga funga tu vitu willy-nilly kama jina lake. Granted nchi ilioza na kuna reforms nyingi zilitakiwa, but don't throw the baby with the bathwater for gods sake.

Matatizo yetu yapo katika familia, malezi, utamaduni.

Kiongozi aliyelelewa kwa kuinewa anaona kuonea ni haki ya mkubwa. Akipata uongozi anaona na yeye zamu yake ya kuonea imefika, mshamuonea sana.

Ndiyo maana hata sioni tofauti kubwa kati ya CCM na wapinzani, ndiyo maana wapinzani wanahamahama kwenda CCM iliyominya demokrasia, kwa kisingizio wanafuata demokrasia.

Familia, malezi, utamaduni, ndiyo mizizi ya matatizo yetu. huko kwenye vyama ni matawi tu, hata tukijitahidi kutengeneza siasa za vyama, kama hatujatengeneza familia, malezi, utamaduni, tutakuja kupata matatizo mengi sana.

Siku hizi watoto wasiolelewa na wazazi wote wanakuwa kama fashion, hawa wakija kuwa wakubwa litalipuka bomu kubwa sana ambalo mabadiliko ya vyama vya siasa hayawezi kulituliza.

Viongozi wa caliber ya Nyerere tuliwapata kwa mchanganyiko wa malezi ya utamaduni wa Kiafrika pamoja na elimu ya magharibi, siku hizi tunakosa vyote viwili. Hili kwangu ni tatizo la msingi kuliko matatizo ya siasa za vyama sasa, kwa sababu haya ksho yataleta matatizo makubwa zaidi.

To be fair, sitaki ku minimize matatizo ya siasa za vyama sasa, kwa sababu katika nchi iliyo top down kama yetu, mtu wa juu akiamua kufanya reforms nzuri anaweza sana, tuna tabia ya ku idolize marais wetu kwa mfano.Lakini, my sense is, rais anahalalisha kumomonyoka maadili, na anatengeneza vi Magufuli vingine huko kwa kina Makonda, Jerry Muro, Gambo etc

Katika nchi yenye matatizo ya kiutamaduni kama yetu, hata wazee wa CCM kama marais wastaafu wanaonekana kushindwa kumuasa Magufuli aache kauli zisizo na staha za kirais, kwa sababu hiyo ni distraction hata kama anataka kufanya mageuzi, hatuna a coherent direction.

Sasa katika nchi ambayo hatuwezi kuwa na common decorum tu, habari za political ideology ni kumfundisha calculus sisimizi.

My main concern kwa sasa si kwamba siasa za vyama zinaendaje.

I am more concerned kuona rais anasema atawapiga shangazi wa wapinzani wake wa kisiasa, vijana wanaokua sasa wanaona kumbe mwanamme kumpiga mwanamke ni kitu cha kawaida tu, regardless wanakuwa chama gani.

Rais anasema wazi kabisa kwamba vyombo vya dola vikipe upendeleo CCM katika chaguzi. Yani mambo ya aibu yanasemwa wazi kama kawaida tu, na hakuna anayesema sana, inazoeleka.

Common decorum imetoweka.

Hapo maana yake, atakayeshika madaraka baada ya huyu atakuwa anatoka katika mazingira mabaya na anaweza kutupeleka pabaya zaidi
Mkuu Kiranga

Nimejikuta naisoma na kuirudiarudia kila mara.

Shukrani sana kwa ujumbe huu mzito.
 
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
43,029
Likes
18,087
Points
280
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
43,029 18,087 280
Mkuu Kiranga

Nimejikuta naisoma na kuirudiarudia kila mara.

Shukrani sana kwa ujumbe huu mzito.
Ahsante sana.

Hata mwenyewe nimesoma tena hapa nikapata madini yangu mwenyewe tena kama sijayaandika mimi vile.

Na siku zinavyozidi kwenda tutaona umuhimu wa nasaha hizi zaidi kama hatutajirekebisha.
 
Mwalimu

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
1,492
Likes
285
Points
180
Mwalimu

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
1,492 285 180
Unajua tunaweza kuwa tunazungumzia tatizo la wananchi kukosa elimu ya uraia etc lakini tunafanya makosa kufikiri kwamba ni jukumu la serikali, vyama vya siasa na ngo peke yao... Tunasahau kwamba sisi pia kama wazazi kwenye ngazi ya familia na community tuna nafasi kubwa sana ya kuwajenga wanetu kwenye hili. Kwa kuwalea na kuwajengea wanetu values muhimu za integrity, ethics na kuziishi katika maisha yao ya kila siku huku na sisi wazazi tukiwa mfano kwa matendo yetu tayari tunakuwa tumetoa elimu ya uraia kwa kiasi fulani.
 
Forum statistics

Threads 1,250,901
Members 481,523
Posts 29,750,193