CCM Ipo Njia Panda - Haina Jinsi zaidi ya kuitumia Kete Ya Dr. Magufuli

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,361
2,000
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa umekiacha Chama Cha Mapinduzi kikiwa na makovu makubwa yakiongozana na maumivu makali. Kimepigwa ngumi na mateke ya kutosha.

Tumepata taarifa toka sehemu mbalimbali za nchi kwamba UKAWA wamejinyakulia viti lukuki kulinganisha na matokea ya miaka mitano iliyopita. UKAWA kupitia mshirika wake mkuu, CHADEMA, wamefanikiwa kusimamisha wagombea maeneo mengi kuliko ambavyo CHADEMA ilifanya miaka mitano iliyopita. Tumeshuhudia wagombea wa CCM waliopita bila kupingwa wakipungua sana. Kwa hali inavyoendelea, CCM inasubiri anguko lingine kabla ya uchaguzi Mkuu nalo ni kukataliwa kwa Katiba Pendekezwa!

Hii inaonyesha kwamba upinzani hapa nchini umeimarika na unazidi kuimarika kadri tunavyosogelea uchaguzi mkuu wa mwaka kesho. Kama UKAWA wataendelea kuwa pamoja na kuacha uroho ambao tumekuwa tukiushuhudia miaka kadhaa iliyopita, basi mwakani hali ni ya hatari kwa CCM. Kila kukicha watu wanapata confidence kwamba kumbe CCM inaweza kutoka na kisitokee chochote kama ambavyo waliaminishwa hapo zamani.

Kwa hiyo CCM inabidi ijipange kwa ajili ya uchaguzi mkuu kama inataka kubaki madarakani. Hali ya sasa ya makundi ndani ya CCM itaendelea kuitafuna hadi inaondoka madarakani na kuitafuna hata kama itakuwa upinzani na matokeo yake tunaweza kushuhudia chama kingine kikongwe hapa Afrika kikipotea kwenye ramani ya vyama kongwe kama ilivyotokea kwa KANU, UNIP, UPC, n.k

Katika hali kama hii ya tishio kubwa kutoka UKAWA, kwa sasa CCM watake wasitake wana turufu moja tu nayo ni Dr. John Pombe Magufuli. Inajulikana kwamba wahafidhina wengi ndani ya serikali wanaiogopa misimamo ya Dr. John Pombe Magufuli lakini kwa hili wataona ni afadhali zimwi likujualo na hivyo wakamsimamisha kuwaokoa. Wanaweza wakaamua Rais asiwe Mwenyekiti wa Chama ili kupunguza nguvu zake ndani ya chama.

Huyu ndiye compromising candidate ndani ya CCM na anauzika kwa Watanzania walio wengi.

Najua watu watakuja na hoja ya uuzaji nyumba za serikali. Waliuziwa watanzania.
 
mwimbule

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
569
500
Aliharibu kwa kugawa nyumba Za serikali. Hakuuza aligawa. Kuna maeneo nyumba ya billioni watu waligawiwa kwa millioni 20. Kwa kweli siamini kama atafaa. Pia kwenye samaki ametutia hasara sana. Barabara ya mtwara hadi sasa haijakamilika miaka yote huyo.
 
RockSpider

JF-Expert Member
Feb 16, 2014
6,866
1,500
Porojo nyingi kumbe mwisho wa siku unampigia debe Magufuli aka Political Entrepreneur firs class... Arudishe kwanza Nyumba za Serikali alizojigaia Arejeshe Trillions zetu kweye deals zake za kuwalipa wakandarasi na kuwatimua kimaigaombwe bila ya kazi kufanyika... CCM haina mwingine Zaidi ya Lowassa ambaye mnaogopa kuwa atawalipizia kisasi kwa mabaya yote mliyomtendea...

afwe

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
4,085
2,000
Aliharibu kwa kugawa nyumba Za serikali. Hakuuza aligawa. Kuna maeneo nyumba ya billioni watu waligawiwa kwa millioni 20. Kwa kweli siamini kama atafaa. Pia kwenye samaki ametutia hasara sana. Barabara ya mtwara hadi sasa haijakamilika miaka yote huyo.
Ile ilikuwa ni syndicate hawezi kufanya tu ati kwa vile ni waziri
 
murumbasi

Member
Dec 3, 2014
75
0
Magufuli hawezi kuwa Rais na hafai hata kidogo. Ni mtu mwenye jazba, matusi. Kumbuka alipokuwa waziri wa mifugo na Uvuvi aliwanyang'anya Wafilipino meli yao na baadaye wameshinda kesi na hivyo Taifa hili linadaiwa zaidi ya Tshs.300bn. Hii ni sababu ya majivuno yake akijifanya anajua kila kitu. Pili, mauzo ya nyumba za Serikali yeye ndiye aliyemdanganya Mhe. Mkapa ili wauziane nyumba za Serikali. Mpaka leo suala hili limekuwa na dosari kubwa na nina imani UKAWA ukiingia madarakani kesho yake nyumba zitarudishwa. Hata Chato hawezi kupata tena ubunge na ndiyo tuseme KWAHERI POMBE MAGUFULI.
 
mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,917
1,225
Maghufuri hawezi kuteuliwa urais, utakumbuka maneno yangu. Hata hivyo si kiongozi bora, hajui atoe maamzi gani wakati gani.
Unajidanganya sana kama mzee slaa pamoja na uzinzi wote,kuiba hela za watoto yatima kanisani na ukatili wa kutuma watu wa bavicha kumwagia tindikali watu lakini aliteuliwa na chama chake kugombea ije kuwa magufuli ambaye utumishi wake hauna chembe ya mashaka?
 
mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,917
1,225
Magufuli hawezi kuwa Rais na hafai hata kidogo. Ni mtu mwenye jazba, matusi. Kumbuka alipokuwa waziri wa mifugo na Uvuvi aliwanyang'anya Wafilipino meli yao na baadaye wameshinda kesi na hivyo Taifa hili linadaiwa zaidi ya Tshs.300bn. Hii ni sababu ya majivuno yake akijifanya anajua kila kitu. Pili, mauzo ya nyumba za Serikali yeye ndiye aliyemdanganya Mhe. Mkapa ili wauziane nyumba za Serikali. Mpaka leo suala hili limekuwa na dosari kubwa na nina imani UKAWA ukiingia madarakani kesho yake nyumba zitarudishwa. Hata Chato hawezi kupata tena ubunge na ndiyo tuseme KWAHERI POMBE MAGUFULI.
Kwani wewe mfilipino mbona unatetea weupe au unabwana mfilipino au mzungu.
 
mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,917
1,225
Porojo nyingi kumbe mwisho wa siku unampigia debe Magufuli aka Political Entrepreneur firs class... Arudishe kwanza Nyumba za Serikali alizojigaia Arejeshe Trillions zetu kweye deals zake za kuwalipa wakandarasi na kuwatimua kimaigaombwe bila ya kazi kufanyika... CCM haina mwingine Zaidi ya Lowassa ambaye mnaogopa kuwa atawalipizia kisasi kwa mabaya yote mliyomtendea...
Ndoto zako za mchana kweupe kabisa sidhani kama magufuli anaweza kushindwa kirahisi na mtu mwingine yoyote nadani na nje ya ccm.
 
Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,181
2,000
CCM mtungi ushatoboka... hautazibika kamwe na maji yakiwepo ndani
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom