CCM Ipo Njia Panda - Haina Jinsi zaidi ya kuitumia Kete Ya Dr. Magufuli

Watu hawataki tu lakini hakika nakuambia akisimama Magufuli CCM watakuwa wamemaliza uchaguzi wabaki kwenye kulumbana wenyewe kwa wenyewe.

CCM ina majembe!
LAKINI CHA MSINGI ZAIDI NI:
1) MAKUNDI KUFANYA KAMPENI ZAO KISTAARABU BILA KUCHAFUANA!

2) UONGOZI WA JUU KUWA 'NEUTRAL' NA KUTOA 'FULL DEMOCRACY' KWA WAGOMBEA WOTE NA BILA KUMUWEKEA YEYOTE VIKWAZO VYA KI'1947'!
3) WATARAJIWA WOTE KUMKUBALI ATAKAYEPITA NA KUMUUNGA MKONO 100% KWENYE KINYANGANYIRO KINACHOFUATA.

NB: MPAKA SASA ANANG'AA ZAIDI EDWARD LOWASSA , NA HILI PENDEKEZO LA JEMBE MAGUFULI NALO POA VILEVILE! LAKINI, 'MAGAMBA'
WENZANGU, CHA MSINGI NI CHAMA KWANZA NA MENGINE YATAFUATA!

TUSIJIDANGANYE, TANZANIA BILA CCM ITAYUMBA!
 
Mkuu najua alichoma nyavu kule Ziwa Victoria, akachoma nyavu nyumba ya Mungu na kwingineko. Hiii sasa ndiyo credit yake kwamba anaweza kusimamia sheria. Wavuvi wenyewe wapo wangapi? huku Lyakanyasi, kisiwani Juma na hata kule Bumbire tuko wachache na wengi waliopo huku ni wahalifu na wala hata kura hawawezi kupiga!

Chato inawezekana CHADEMA wakachukua vitongoji, sawa. Lakini ukija na ujumla wake ni kwamba Magufuli anakubalika na Watanzania wengi sana tena sana. Akitia timu hakuna wa kusimama naye hakika nakuambia.
Nadhani uko sahii,ata mimi akitia timu nampa kura yangu,wasiwasi wangu ni huo na pili kama yuko popular kiasi hich ndani ya chama chake.
 
CCM wanazo spare nyingi sana! Urais kusema kweli mtu akatae asikatae Magufuli ni mtu anayekubalika kwa makundi na maeneo makubwa ya nchi hii. Hatuwezi kuchukua muda mwingi kumnadi kwa watanzania:
  • Akiwa wizara ya uvuvi na mifugo - alitoa takwimu mpaka za vifaranga vya samaki, alikamata meli zinazoendesha uvuvi kwenye eneo la Tanzania n.k
  • Akiwa wizara ya ujenzi - tumeshuhudia barabara kibao za lami, vivuko na alisimamia kauli ya kuvunja sheli zilizojengwa kwenye hifadhi ya barabara mwanza n.k
  • Akiwa wizara ya ujenzi - tulimshuhudia akifanya operesheni ya kuwanyang'anya viongozi magari na mashine za serikali zilizokuwa zinafanya kazi binafsi badala ya kuhudumia watanzania,

Kusema kweli, Magufuli ni kiongozi ila tu huwa hatumuelewi kwa nini hataki kujitokeza kugombea urais katika nchi. Akijitokeza mapenzi yangu yatahama kutoka kwa baadhi ya waliojitokeza na nitamuunga mkono.

magufuli ni aina ya viongozi wanaohitajika kwa sasa...mwenye uwezo wa kutoa maamuzi magumu..ni moja ya mawaziri wachache waliodumu kwenye nyadhfa zao kwa muda mrefu tangu awamu ya tatu...
 
Aliharibu kwa kugawa nyumba Za serikali. Hakuuza aligawa. Kuna maeneo nyumba ya billioni watu waligawiwa kwa millioni 20. Kwa kweli siamini kama atafaa. Pia kwenye samaki ametutia hasara sana. Barabara ya mtwara hadi sasa haijakamilika miaka yote huyo.

Hajawatia hasara maana mlijihusisha na uvuvi haramu kenge wewe.
 
Unajidanganya sana kama mzee slaa pamoja na uzinzi wote,kuiba hela za watoto yatima kanisani na ukatili wa kutuma watu wa bavicha kumwagia tindikali watu lakini aliteuliwa na chama chake kugombea ije kuwa magufuli ambaye utumishi wake hauna chembe ya mashaka?

Magufuli ndio mzinzi namba moja na kuhonga nyumba za serikali, kuna dada mmoja geologist alimpa nyumba ya serikali maeneo ya ubungo, kwa sasa kamjengea mbweni nyumba ya kifahari😳CCM hakuna mtu msafi hata mmoja
 
Aliharibu kwa kugawa nyumba Za serikali. Hakuuza aligawa. Kuna maeneo nyumba ya billioni watu waligawiwa kwa millioni 20. Kwa kweli siamini kama atafaa. Pia kwenye samaki ametutia hasara sana. Barabara ya mtwara hadi sasa haijakamilika miaka yote huyo.

Ndugu yangu Mwimbule na mwenzio Kaguta muelewe nafasi yake ni ya uwaziri na aliepo juu yake ndie mwenye maamuzi ya mwisho. Huu naamini ulikuwa ushawishi wa raisi wake Mkapa na ukumbuke alijibinafsishia na mgodi wa kiwira na hata baraza la mawaziri lilillopitisha maamuzi hayo nalo ni la kifisadi tu.
 
Magufuli kama aliuza nyumba za serikali, akiwa Rais si atauza na wanach wake! Serikali inapata hasara kwa kulaza viongozi wengi hotel kwa kukosa nyumba.
 
Ccm wote wameoza,si pinda,si lowasa,si wassira,si makamba Jr,si magufuli,si membe,si nchimbi,si sitta(mbabe) nk. Wote vi.nye.si wananuka rushwa
 
sema ana nafuu kuliko wengine, lakini usiseme akisimamishwa atakubalika kirahisi nchi nzima. Wavuvi wa Lyakanyasi hawakutoka kuzimu wengi wana ndugu, rafiki huko ukerewe, sengerema, musoma, bukoba n.k. ambao wana maamuzi katika kura za urais. Bahati mbaya sana ni kuchagua sheria za kufuata na kuziacha zingine ambazo zinawaumiza wananchi. Maamuzi mengi pia yanayoumiza nchi ni tatizo lingine ingawa hayasemwi, ingawa atakapoingia Ikulu yanaweza kutumiwa kuumiza nchi zaidi. Yawezekana pia hana makundi, lakini je anaweza kuwaunganisha haya makundi na kuweza kuunda serikali imara?

Umenena vizuri.

Kwa kuwa hana makundi nina imani atayaunganisha makundi na kuwa na serikali imara inayofuata utawala wa sheria.
 
Kimbunga,

Naomba unifafanulie tofauti za kiutendaji kati ya Magufuli na Werema....!!

.........

Sijui unataka tofauti zipi kwa kuwa Werema ni Mwanasheria na Magufuli si mwanasheria ila anafpenda kufuata sheria na kuzitekeleza

WE NEED COMMENTS KAMA HIZI NA SI YALE MAB-WEGE YA PALE LUMUMBA YANAYOARISHA KWA KUTUMIA MDOMo..
Magufuli ndio mzinzi namba moja na kuhonga nyumba za serikali, kuna dada mmoja geologist alimpa nyumba ya serikali maeneo ya ubungo, kwa sasa kamjengea mbweni nyumba ya kifahariCCM hakuna mtu msafi hata mmoja
 
Umenena vizuri.

Kwa kuwa hana makundi nina imani atayaunganisha makundi na kuwa na serikali imara inayofuata utawala wa sheria.
Hapo ndipo unapokosea. Kuunganisha watu na kuwaongoza pia ni kipaji anachokuwa nacho mtu au kujaliwa na mwenyezi Mungu. Siyo kwa sababu huna makundi basi una uwezo wa kuwaunganisha. Narejea tena sijui kama anao huo uwezo. Is he a team player?
 
Nakumbuka Mwanza wakati ule wa mkapa akiwa waziri wa ujenzi. Alivunja petro station ya mansoor pale Mwanza kuelekea airport maeneo ya njia panda ya kirumba. Aliivunja kwa mbwembwe sana. Aliambiwa mwanzo na wizara ya ardhi kwamba lile ni eneo LA man so or kihalali lakini wapi, alionyweshwa hadi hati ya eneo Lakini wapi sikio LA kufa??!?. Alivunja jamaa akaenda mahakamani Mahakama kuu ya Tanzania Mwanza. Kesi ilikuwa Kwaiyo jaji mchome. Serikali ikaambiwa imlipe Jamaa billioni tatu. Kwaiyo si kiongozi mzuri. Lingine serikali na wizara yake wameongeza ukubwa wa barabara kwa kubadilisha au kuammend sheria ya Barabara. Lakini cha ajabu pamoja na kuweka upya alama za mipaka ya Barabara nchini kote, yeye na tanroad yake hawajafanya tathmini ya Mali za watu kwa àjili ya kuwalipa. Ukumbuke hawaruhusiwi kupaendeleza kabisa. Je hii ni haki? Kama anajisifu anafuata sheria mbona hataki kufuata sheria Kwaiyo kuwafanyia tathmini hawa wananchi maskini ambao tayari sheria imewakuta. Mbona anakuwa double standard. Hafai kabisa anawaonea watu.

Last edited by a moderator:
Unajidanganya sana kama mzee slaa pamoja na uzinzi wote,kuiba hela za watoto yatima kanisani na ukatili wa kutuma watu wa bavicha kumwagia tindikali watu lakini aliteuliwa na chama chake kugombea ije kuwa magufuli ambaye utumishi wake hauna chembe ya mashaka?
hata wewe bila uzinzi ungezaliwa kuwa na heshima DR slaa unatakiwa kumuheshimu kama baba yako sawa dada
 
Nakumbuka Mwanza wakati ule wa mkapa akiwa waziri wa ujenzi. Alivunja petro station ya mansoor pale Mwanza kuelekea airport maeneo ya njia panda ya kirumba. Aliivunja kwa mbwembwe sana. Aliambiwa mwanzo na wizara ya ardhi kwamba lile ni eneo LA man so or kihalali lakini wapi, alionyweshwa hadi hati ya eneo Lakini wapi sikio LA kufa??!?. Alivunja jamaa akaenda mahakamani Mahakama kuu ya Tanzania Mwanza. Kesi ilikuwa Kwaiyo jaji mchome. Serikali ikaambiwa imlipe Jamaa billioni tatu. Kwaiyo si kiongozi mzuri. Lingine serikali na wizara yake wameongeza ukubwa wa barabara kwa kubadilisha au kuammend sheria ya Barabara. Lakini cha ajabu pamoja na kuweka upya alama za mipaka ya Barabara nchini kote, yeye na tanroad yake hawajafanya tathmini ya Mali za watu kwa àjili ya kuwalipa. Ukumbuke hawaruhusiwi kupaendeleza kabisa. Je hii ni haki? Kama anajisifu anafuata sheria mbona hataki kufuata sheria Kwaiyo kuwafanyia tathmini hawa wananchi maskini ambao tayari sheria imewakuta. Mbona anakuwa double standard. Hafai kabisa anawaonea watu.

Last edited by a moderator:
Ccm wote wameoza,si pinda,si lowasa,si wassira,si makamba Jr,si magufuli,si membe,si nchimbi,si sitta(mbabe) nk. Wote vi.nye.si wananuka rushwa
ukoo wa panya wote hawafai ndani ya ccm hakuna aliye msafi bora upande wa UKAWA DR Slaa ndo tegemeo jipya kwa wananchi wote
 
Back
Top Bottom