CCM inaogopa kivuli cha Maalim Seif

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,790
"Kama ilivyo kawaida kwa viongozi mbalimbali kutembelea wenzao wanapokuwa hospitali, jana ilikuwa tofauti kwa Maalim Seif baada ya klutoonekana kwa kiongozi yeyote kutoka Serikali ya Zanzibar wala ya muun gano" ( Gazeti Mwananchi la leo limeripoti)

Kisa hiki kinanikumbusha kisa kilicho shabihiana cha Firauni(Pharoh) na Nabii Mussa (Moses). Wakati Moses ilipogundulika kuwa ni myahudi na si mwana familia ya Firauni, na kwamba anatyarisha mipango ya kuwakomboa wana waisrel kutoka utumwani( out of bondage), Firauni ilimlazimu kutowa fatwa ya kupiga marufuku kusikika, kutajwa au hata kukumbukwa jina la Moses katika himaya yake

Tukiangalia uhasama huu wa kijinga na kishenzi umetokana na nini hasa? ni kutokana na siasa, kugombania ulwa au kujishuku tu? Ni ujinga hasa kwa sisi wazanzibari ambao mara zote tunapenda kujitofautisha na wengine kwa kujifanya ni waungwana, wastaarabu na wenye kuhurumiana.

Kama Firauni ilimlazimu kutowa fatwa ya kupiga marufuku kusikika, kutajwa au hata kukumbukwa jina la Moses ndivyo vyombo vya habari vya taifa( hasa Zanzibar), ZBC na gazeti la Zanzibar Leo vyote kwa pamoja vimelemazwa kuwa na ububu, uziwi na upofu kwa kufuata fatwa hiyo dhidi ya Maalim Seif.

Kipi hapa kinachotisha ni nini hasa; ni Maalim Seif au kivuli chake?
 
Vivuli hatari kwa Maccm ni cha Seif,Lowassa na Freeman,Hawa ni watu wamewageuza Ccm kuwa watumwa ndani ya nchi yao.Huku wausika wakiendelea kula raha
sema LOWASSA na wamlambao miguu maana wote aliwanunua ili habari zake za ufisadi zifutike kabisa masikioni mwa Watanzania.
 
katika maisha yangu sijawahi kusikia mtu anaomba kutembelewa hospitalini, hii ni mara yangu ya kwanza.
NI KWELI KWA SABABU WEWE HUTOKANI NA JAMII ILIOSTAARABIKA NA KIUNGWANA HUWEZI KUJUA WALA KUSIKIA WEWE UMEZOWEA KUSIKIA NA KUFURAHIA KAMA MTU KACHUNWA NGOZI, ALBINO KAKATWA MKONO
 
Screenshot_2016-03-09-13-10-18.png

swissme
 
Baraghash umewahi tu kupost! Magufuli alikua na ratiba ya kumtembelea mgonjwa! tizama swissme kaleta latest update! Hakuna adui au rafiki wa kudumu ktk siasa! Hao hao watoto wao wakipata/kuolewa wote utawakuta pamoja meza moja! Hao hao wakipatwa msiba hali kadhalika! Hivyo be cool! Siasa is a game
 
Nimekubali na ndio nimetoa tano kwenye post inayohusu ziara ya JPM; ila na wewe umewahi kuisoma post yangu haraka haraka

Jikumbushe "vyombo vya habari vya taifa( hasa Zanzibar), ZBC na gazeti la Zanzibar Leo vyote kwa pamoja vimelemazwa kuwa na ububu, uziwi na upofu kwa kufuata fatwa hiyo dhidi ya Maalim Seif."

Viongozi wetu wengine ni kama wametiwa shemere, cha kufanya na kutenda kinaamriwa na alishika hatamu. Subiri kesho utasikia na kusoma kwenye vyombo vya habari misururu mirefu ya viongozi kwenda kumjuulia hali, utafikiri ya kukata tiketi mechi ya Simba na Yanga.
 
katika maisha yangu sijawahi kusikia mtu anaomba kutembelewa hospitalini, hii ni mara yangu ya kwanza.
Hakuna maana hiyo na akili yako fupi kama kimba la mwisho.tunachomaanisha ni kwamba kwenye maradhi hakuna haja ya kuendeleza siasa za chuki bali kutembeleana kuonesha umoja na kukomaa kwa democrasia.
 
magufuli anaenda kumtembelea kwa sababu amesha sema suala la zanzibar halimuhusu, kwa akili ya haraka haraka kuna ambao ndio wamelianzisha, na wanaendelea kulisimamia hao ndio lina wahusu na hao hawathubutu kwenda kumjulia hali Maalimu Seif nao ni JK, na Mkapa.
 
NI KWELI KWA SABABU WEWE HUTOKANI NA JAMII ILIOSTAARABIKA NA KIUNGWANA HUWEZI KUJUA WALA KUSIKIA WEWE UMEZOWEA KUSIKIA NA KUFURAHIA KAMA MTU KACHUNWA NGOZI, ALBINO KAKATWA MKONO
Ndiyo mkuu.majitu kama haya yana roho mbaya hadi kwa majirani na ndugu.umeshindwa kuficha hata maovu yako?
 
Hakuna maana hiyo na akili yako fupi kama kimba la mwisho.tunachomaanisha ni kwamba kwenye maradhi hakuna haja ya kuendeleza siasa za chuki bali kutembeleana kuonesha umoja na kukomaa kwa democrasia.
Hivi kiswahili lugha yako ya ngapi. Nani mwalimu wako wa kike wa mwisho aliokusomesha.
 
magufuli anaenda kumtembelea kwa sababu amesha sema suala la zanzibar halimuhusu, kwa akili ya haraka haraka kuna ambao ndio wamelianzisha, na wanaendelea kulisimamia hao ndio lina wahusu na hao hawathubutu kwenda kumjulia hali Maalimu Seif nao ni JK, na Mkapa.

Jk alipofiwa na Kaka yake hatukuziona hata kwato zenu!
 
Back
Top Bottom