Mukuru
Member
- Apr 14, 2009
- 40
- 0
MWANASIASA mkongwe nchini, Musobi Mgeni ameibuka na kukishambulia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa madai ya kuwafanya wasomi kuwa ni watumwa.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili, jana mkoani hapa, mwanasiasa huyo alisema kuwa CCM imewapumbaza hata wasomi kiasi cha kuwafanya hata wasithaminike kwa elimu yao.
Niwaulize wasomi wa madigrii yao, wewe mwandishi wa habari na wenzio ndio mjiulize, mimi sina shida yoyote na sijawahi kuwa mtumwa, lakini sasa hivi wasomi wote ni watumwa, mmekuwa watumwa katika nchi yenu, alilalamika.
Alieleza moja ya athari za hali hiyo ni watu kuthamini fedha kuliko utu wala haki za wanyonge.
Kama huna pesa hutakiwi wala kusikika, alisema Mgeni katika mahojiano yaliyofanyika Kijijini kwake, Ndugu Wilaya ya Kwimba.
Mgeni ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CUF mwaka 1995, alisema umaskini na njaa iliyopo nchini sasa hivi, haikuletwa na Mungu na badala yake imeletwa na utawala usiojali unaofanywa na CCM.
Alisema umaskini umewafanya Watanzania kuwa wajinga na kwamba hayo ndiyo matunda ya mauaji ya albino.
Alifananisha CCM na nyoka akasema mtoto atakayezaliwa na nyoka hawezi kutofanana na nyoka akiwa na maana kwamba kiongozi yeyote kutoka CCM atakuwa na mtazamo sawa na wenzake waliomtangulia.
Najua humu JF kuna wasomi wengi tu...je, ni kweli tumefanywa watumwa na CCM kama anavyodai huyu jamaa? Au ni mtazamo finyu?

-----------------------------------------