"CCM imevaa nepi halafu inajisifia"- Mzee wa Upako-Lusekelo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"CCM imevaa nepi halafu inajisifia"- Mzee wa Upako-Lusekelo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KALABASH, Oct 30, 2011.

 1. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 453
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Akihojiwa huhusu mafanikio ya CCM katika miaka 50 iliyopita Mchungaji Lusekelo Mzee wa Upako amesema:"Yaani ni sawa na mtu mzima kuvaa nepi; ndiyo nepi ni nguo lakini mtu mzima akivaa nepi anakuwa kichekesho. Haya wanayodai kwamba ni maendeleo ni sawa na mtu mzima kuvaa nepi halafu akaanza kujisifia" mwisho wa nukuu Gazeti la NYAKATI jumapili Octoba 30- Novemba 5 -2011. Pamoja na kwamba mimi si mshabiki au mojawapo wa kondoo wa Mzee wa Upako naona angalizo lake hili kuhusu miaka 50 ya CCM ni chakula cha vichwa(food for thought?) vya wachambuzi hapa JF. Karibuni!
   
 2. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,523
  Likes Received: 2,440
  Trophy Points: 280
  Yeye aendelee na wizi wake kwa kutumia jina la mungu.
   
 3. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,291
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  mi sielewi tunasherehekea nini wakati tumepiga hatua kinyumenyume
   
 4. O

  OSCAR ELIA Member

  #4
  Oct 30, 2011
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mzee wa upako aache kutumia lugha ya uchochezi,maana waumini wake wanaweza kugawanyika ndani ya kanisa.hata kama viongozi wa dini watakiwa kuikosoa serikali yetu wanapaswa kutumia lugha ya staha ingawa itakuwa ina uma kwa viongozi walioko madarakani.
   
 5. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,032
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  labda kwa vile hapati ruzuku serikalini kama ilivo kwa makanisa mengine
  angekuwa anapata asingebwabwaja kihivo.
   
 6. M

  Makupa JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,741
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Ni makanisa yapi yanapata ruzuku
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,474
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Angesema tu kwamba wanatembea uchi tungemwelewa.
   
 8. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2011
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,025
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  mbona ccm haijafikisha miaka 50?au anamaanisha miaka 50 ya uhuru wa tanganyika?sijaelewa mkuu.
   
 9. Aggrey86

  Aggrey86 JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 856
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mmmm!! haya mzeeee wa upako bwana!!
   
 10. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2011
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Una maana gani unaposema watumie lugha ya staha? Mbona jambo hili liko wazi sana? Ukuaji wa uchumi wa nchi yetu hauwiani na utajiri wa rasilimali tulizonazo. Hivi majuzi Lukuvi amedai pato la taifa limepanda kufikia Tsh. 770,000 kwa mwaka kutoka Tsh 770 wakati wa uhuru. Hajatuambia wakati ule thamani ya pesa yetu ilikuwa na uwiano gani na dola ya marekani. Anajua kuwa thamani ya pato la mwananchi wakati wa uhuru ni kubwa kuliko sasa!

  Hakuna lugha mbadala ya kumuita fisadi, mwizi nk. Serikali yetu ni legelege, hakuna lugha ya staha zaidi ya hiyo.
   
 11. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2011
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kuna makanisa yanapata ruzuku???? Tutajie tafadhali.
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,153
  Likes Received: 843
  Trophy Points: 280
  wanakwambia wamesthubutu wameweza wana songambele.....sijui wamethubutu nini? wameweza nini? wanasonga kwenda wapi?....wapumbavu kweli
   
 13. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,799
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hivi mzee wa upako ni mzaramo?
   
 14. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,740
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hawa mabwege lazima waambiwe ukweli. Lugha za staha na kuambiana "huyu ni mwenzetu" ndizo zimetufikisha hapa tulipo. Lazima tudai mabadiliko kwa hali na njia yoyote ile.
   
 15. gimmy's

  gimmy's JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2011
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 2,319
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Siwezi kushangaa kwa hawa wachungaji wa sasa ambao dini leo imekua pazia ili nyuma yake warahisishe maslah yao kwa siri,leo wachungaji ndio wauza unga wakubwa,wachungaji leo wanawania nyazifa mbalimbali ktk siasa,kiukweli jamaa hana jipya!
   
 16. mchuziwanyoka

  mchuziwanyoka JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 374
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mzee wa upako wewe endelea kufuga ngombe ukamue maziwa mambo ya siasa kwako ngumu mzee wa upako au nauku umetuma namba ya A/C
   
 17. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #17
  Oct 31, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wameweza kunvalisha mtu mzima nepi, nakushusha akili yake ikawa ya kichanga.
   
 18. Pelekaroho

  Pelekaroho JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  saafi!
   
 19. T

  Thesi JF-Expert Member

  #19
  Oct 31, 2011
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Uko sawa kabisa kuhusu kulinganisha mapato ya miaka tofauti.
  hapa viongozi wa serikali huwa wananitia kichefuchefu wanapolinganisha uchumi, ukusanyaji wa kodi au maendeleo fulani katika miaka tofauti.
  utakuta wanakuambia kodi imepanda kutoka bilioni 200 hadi bilioni 700 katika kipindi cha miaka 10. yaani huu ni usanii mkubwa. hawakuambii pesa imeshuka thamani kwa kiasi gani hvo bil 700 zina thamani gani ssa hivi. utakuta fedha imeshuka mara 3 au nne hvo bil 700 ni sawa tu na bil 200 ya wakati huo ila unapigwa changa la macho kuwa wanafanya kazi nzuri.
   
 20. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #20
  Oct 31, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,222
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Nadhani wakumbuka enzi za Mikingamoooo!!! walikuwa wana itwa wahujumu uchumi nadhani hilo ndilo walitaka au?
   
Loading...