CCM imepigwa kitu kizito kisogoni

CCM imepigwa kitu kizito kisogoni

Mbona vya vipo vingi, mbona chadema tu?
Hawezi kukujibu. Watu wa aina hii hawajitambui. Wanasubiri wafanyiwe kila kitu. Subiri kuna siku akili zitawakaa sawa tu. Kwa haya ilivyo sasa CCM haiwezi kurekebisha chochote bali inaendelea kuididimiza nchi. Acha watu wakipata shida ndiyo watapata akili.
 
Ni Suala la muda mfupi ujao, haya niyasemayo yatadhihirika huko site.

CCM ya wanyonge imepigwa kitu kizito na CCM ya mtandao. Hili sio la kuogopa kusema,labda Moderators wanifanyie yao kwa kuuondoa uzi huu.

Ila ukweli utabaki kuwa ukweli.

Kwa hii safu yenu mpya,
mmeingizwa chaka na walewale walioshindwa kulivua gamba.

Walewale walioiacha hadi ikaingia ICU.

Hakuna kipindi CCM itaishi kwa unafiki baina ya wanachama wenyewe kwa wenyewe kama sasa.

Ni vigumu kusema CCM haitagawanyika kuelekea 2025.

Mnaweza kubaki na raisi asiye dhibiti bunge la jamhuri.
Maana wabunge 75% ni ngumu kurudi bungeni.

Wapinzani mngekuwa makini,hiki ndio kipindi muhimu mrudi site kujijenga.

Tokeni huko mijini mje kuongea lugha ya wapiga kura na kero zao.

CCM hii ya mama na Kinana kwa mtindo huu wa majibu ya jazba kwa wananchi.

Kama tume itasimamia haki...CCM 2025 ni ngumu sana kutoboa.

View attachment 2170598View attachment 2170601
Yaani hao ndio wahuni wenyewe.
 
Kwa hiyo pole pole kupelekwa ubarozini ilikuwa ni kupisha hili?

Hapana alikuwa ni mmoja wa mbunge wa vimemo ambaye ni kigogo wao na ametafutiwa njia nzuri ya kumuondoa. Ingekuwa vizuri tuwasaidie wabunge wengine wa vimemo wajijue.

Waliotoka upinzani wote hasa wale wa CDM mjipange hata kama uko kwenye nafasi nyingine serikalini. CCM hawawezi kukukubalini wanawaona mmechukua nafasi zao.
 
Hatimaye watoto wa mjini vs sukuma gang matokeo ni..... Born town ndiyo washindi!!!, Polepole ndiyo huyo katupwa nje ya siasa huko Malawi!!!.

Vijana wa CCM naamini mtatusaidia kudai katiba mpya...... Au bado itakuwa haina tija kwenu....😀. @crime
 
Sukuma Gang/Chawa na Mataga yamebaki yanatumbua macho yanaiaangalia CCM ya WANYONGE inavyoenda kuzikwa Chato.
 
Gang limepigwa za uso mnahahaaa...😀
CDM badilikeni acheni Uanaharakati....!

FANYENI SIASA, tambueni mahitaji halisi ya mlala hoi na jinsi gani ya kusolve..!

2025 ni Kama Kumsukuma Mlevi ...!
Iwe kwa Katiba mpya au hii hii...iwe Kwa Tume mpya au hii hii ...

Muuza mihogo ukimwambia andamana Dai KATIBA Mpya haielewi.

Lakini ukimwambia bei ya mafuta Kukaangia mihogo itashuka ukinichagua ujue umempata..!

Mtu wa Kawaida Ukimwambia 'tozo la miamala' hatuambiwi tena Zimekusanywa shin ngapi ? Na Zinaenda Wapi? Anaelewa. Amkeni Amkeni!

Lile Genge la 'Wahuni' limesusiwa Chama. Mnataka nini tena?
 
CCM ndio chama pekee ambacho kimetawala nchi hii tangu enzi. Kwanini uviingize vyama vingine?. Acha unafiki, kura mnaipa CCM halafu lawama mnataka kuvipa vyama vingine.

Fuatilia kauli za viongozi wa vyama vingi TZ, hata maandishi ya wanachama tofauti wa vyama vilivyopo sasa Tanzania hapa JF.

Utagundua ukweli, uhalisia wa hivi vyama vyote vilivyopo sasa.

Niambie kwa maoni yako chama gani kitaleta positive changes, kinasimamia maslahi mapana ya Taifa?

Chama gani kati ya hivi kitaweza / kinaweza kuwaunganisha Watanzania wote wa dini zote, kanda zote,makabila yote, vijana, wazee, wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara, matajiri, maskini, wasio na vyama na kuwavuta wa vyama vingine kwa sera, itikadi na ushawishi wao?
 
imerudi ccm iliyoingiza magufuli 2015 inayoiba kura ikabakiza maeneo ya upinzani sio ya magufuli inaibaa kooooote nakujinasibu inapendwa akati haipendwi.....yawatoto wa town imerudi kumsaidia mama bilahivo pengine pangekua pagumu
 
Walewale waliowekwa kitimoto kwa utovu wa nidhamu na Bashiru na Mangula leo ndio viongozi wa CCM top top.
 
imerudi ccm iliyoingiza magufuli 2015 inayoiba kura ikabakiza maeneo ya upinzani sio ya magufuli inaibaa kooooote nakujinasibu inapendwa akati haipendwi.....yawatoto wa town imerudi kumsaidia mama bilahivo pengine pangekua pagumu
Uko sahih kbsa wamerudishwa kimkatat San hawa
 
Nakubaliana na wewe kwamba walioifanya CCM kwenda ICU ndiyo wameeudi Chini ya upole wa mama SSH.
Ccm inaenda kuwa dhaifu lakini si dhaifu kufikia udhaifu wa upinzani.

Wapinzani bado hawajaweza kushawishi wapiga kura.
Wanacheza ngoma ya watawala. Wamekuwa ni kikundi cha kusubiri ccm kafanya nini na ndiyo watoke kusema.

Wapiga kura wanataka kusikia vitu tofauti kutoka kwa wapinzani.
Wapiga kura gani unaongelea wewe.labda unaongelea Tume ya uchaguzi na vyombo vya dola.maana kwa hali ya kawaida kamwe haiwezekani kile kilichofanyika mwaka 2020 ukakiita uchaguzi.Sasa hao Ccm wao walishawishi nini wapiga kura hadi nchi nzima ikachagua Ccm.hebu toka kwenye huo usingizi.
 
Back
Top Bottom