CCM imepigwa kitu kizito kisogoni

CCM imepigwa kitu kizito kisogoni

CDM badilikeni acheni Uanaharakati....!

FANYENI SIASA, tambueni mahitaji halisi ya mlala hoi na jinsi gani ya kusolve..!

2025 ni Kama Kumsukuma Mlevi ...!
Iwe kwa Katiba mpya au hii hii...iwe Kwa Tume mpya au hii hii ...

Muuza mihogo ukimwambia andamana Dai KATIBA Mpya haielewi.

Lakini ukimwambia bei ya mafuta Kukaangia mihogo itashuka ukinichagua ujue umempata..!

Mtu wa Kawaida Ukimwambia 'tozo la miamala' hatuambiwi tena Zimekusanywa shin ngapi ? Na Zinaenda Wapi? Anaelewa. Amkeni Amkeni!

Lile Genge la 'Wahuni' limesusiwa Chama. Mnataka nini tena?
Yaani serikali ikuambie kila inachofanya wewe kama nani hasa?

Mbona mipango ya serikali iko clear kwenye bajeti na Halmashauri zenu,usifanye kila mtu zoba kama wewe.
 
Wewe Ni Mungu hadi ujue kesho?. Nani alijua Kinana atakuwa Makamu Mwenyekiti kutoka kupewa adhabu?. Leo Membe kasamehewa. Waliomtukana Magufuli kwenye simu ndio mawaziri leo. Usijipe nafasi ya umungu.
Mi sio nyumbu wa fisiemu kiongozi

Tatizo kila anaewambia ukweli unadhani ametoka kwenye huo mchama wa ajabu ajabu

Na huo ndio ukweli hakuna upinzani hii nchi
 
Kuna familia ambazo inabidi tukubaliane kama Taifa zipigwe marufuku kugombea nafasi yoyote ile ya uongozi maana tumeshaona namna walivyo na uchu wa madaraka na kutaka kujibinafsishia hii nchi kama mali binafsi.
Mojawapo ni ya wajinga kama wewe
 
CCM ni kipimo.cha ujinga wa watanzania. CCM inapokaa madarakani, usifikiri kuwa itaondolewa na CHADEMA. CCM itaondolewa na watanzania waliofuta ujinga vichwani mwao.

Kama wewe ni mwanaCCM, amini nakuambia unatembea kwenye nyota ya ujinga.
 
Nakubaliana na wewe kwamba walioifanya CCM kwenda ICU ndiyo wameeudi Chini ya upole wa mama SSH.
Ccm inaenda kuwa dhaifu lakini si dhaifu kufikia udhaifu wa upinzani.

Wapinzani bado hawajaweza kushawishi wapiga kura.
Wanacheza ngoma ya watawala. Wamekuwa ni kikundi cha kusubiri ccm kafanya nini na ndiyo watoke kusema.

Wapiga kura wanataka kusikia vitu tofauti kutoka kwa wapinzani.
Ni kweli..wao hawatumii sera badala yake wamekuwa wadandia matukio.
Mfano leo woote wamekodolea Mkutano mkuu wa ccm Dodoma.
Na kwa kiasi kikubwa wao ndio wapashaji na wachangiaji au washabikiaji wa yanayotokea huko.
 
Bahati mbaya hata chadema baada ya mbowe kutoka ni kama wamezubaa
 
Kwa hiyo pole pole kupelekwa ubarozini ilikuwa ni kupisha hili?
 
Tanzania inahitaji chama kipya. Chenye maslahi ya dhati, mikakati na dhamira thabiti kwa Watanzania wote.

Chama kitachowaunganisha Watanzania wote wa vyama vyote, makabila, dini, kanda, maskini, matajiri wafanyakazi, wafanyabiashara, wakulima na wamachinga, mama ntilie nyuma ya maslahi ya wengi, maslahi ya Taifa.

Kwa sasa hatuna chama kama hicho. Vyama vyote kwa sasa vipo kwa ajili ya maslahi yao, (Narrow interest) na sio kuipigania Tanzania na Watanzania kwa ujumla wao.
Nakubaliana na wewe ruaharuaha.
 
Ni Suala la muda mfupi ujao, haya niyasemayo yatadhihirika huko site.

CCM ya wanyonge imepigwa kitu kizito na CCM ya mtandao. Hili sio la kuogopa kusema,labda Moderators wanifanyie yao kwa kuuondoa uzi huu.

Ila ukweli utabaki kuwa ukweli.

Kwa hii safu yenu mpya,
mmeingizwa chaka na walewale walioshindwa kulivua gamba.

Walewale walioiacha hadi ikaingia ICU.

Hakuna kipindi CCM itaishi kwa unafiki baina ya wanachama wenyewe kwa wenyewe kama sasa.

Ni vigumu kusema CCM haitagawanyika kuelekea 2025.

Mnaweza kubaki na raisi asiye dhibiti bunge la jamhuri.
Maana wabunge 75% ni ngumu kurudi bungeni.

Wapinzani mngekuwa makini,hiki ndio kipindi muhimu mrudi site kujijenga.

Tokeni huko mijini mje kuongea lugha ya wapiga kura na kero zao.

CCM hii ya mama na Kinana kwa mtindo huu wa majibu ya jazba kwa wananchi.

Kama tume itasimamia haki...CCM 2025 ni ngumu sana kutoboa.

View attachment 2170598View attachment 2170601
Mbona hueleweki. Kwa hiyo unapenda pale jpm kaiba kura zote na kuwapa ccm na kuwatangaza kwa nguvu? Mbona kipindi Cha jpm ndo ccm iliporomoka ikabaki Ni ubabe tu kwamba umchague usimchague atatangazwa tu.
 
Hapo ndio kuna yule mzee wa goli la mkono, yule wa kuchakachua matokeo kule Masaki, na wazazi wao.

Hao wakikutana na msaada wa tume feki ya uchaguzi, na polisi, ndio wanarudi madarakani kila siku, wale kina crimea na idugunde ni wapiga soga tu mitandaoni.

Halafu sikujua kumbe hilo kundi lina member wanawake Samia na wengine, ila yeye alikuwa kimya sana, hapa ndipo mtego uliposetiwa ukawanasa wale jamaa zangu kina Bashiru na Polepole.
Mkuu Magufuli na kundi lake walilewa madaraka mpaka wakawa hawaoni mbele zaidi ya futi moja. Nakuapia Magufuli inaonekana alishajipachika umungu mtu na akadhani hakuna kitakachogusa tena. Ilikuwa siyi siri kuwa Magufuli alikuwa hapendwi kabisa na kina Kinana na mpaka mama alikuwa upande wao. Hata habari nyingi zilizokuwa zinavuja mama alikuwa anahusika kwa asilimia kubwa. Unaona yule mama kichaa Mange anavyotamba sasa? Wanalipa fadhila za kumtumia kum-attack Magufuli. Wakati wa uchaguzi ''uchafuzi'' wa 2020 nilikuwa nazungumza na rafiki yangu nikamwambia hili suala la Magufuli kuendelea kumfanya Samia awe makamu wake litakakuja kumgharimu sana. Hii ni kwa sababu nilikuwa najua ushirika wao ulikuwa na paka na panya na hawakuendana kabisa kimtazamo.
 
Ni Suala la muda mfupi ujao, haya niyasemayo yatadhihirika huko site.

CCM ya wanyonge imepigwa kitu kizito na CCM ya mtandao. Hili sio la kuogopa kusema,labda Moderators wanifanyie yao kwa kuuondoa uzi huu.

Ila ukweli utabaki kuwa ukweli.

Kwa hii safu yenu mpya,
mmeingizwa chaka na walewale walioshindwa kulivua gamba.

Walewale walioiacha hadi ikaingia ICU.

Hakuna kipindi CCM itaishi kwa unafiki baina ya wanachama wenyewe kwa wenyewe kama sasa.

Ni vigumu kusema CCM haitagawanyika kuelekea 2025.

Mnaweza kubaki na raisi asiye dhibiti bunge la jamhuri.
Maana wabunge 75% ni ngumu kurudi bungeni.

Wapinzani mngekuwa makini,hiki ndio kipindi muhimu mrudi site kujijenga.

Tokeni huko mijini mje kuongea lugha ya wapiga kura na kero zao.

CCM hii ya mama na Kinana kwa mtindo huu wa majibu ya jazba kwa wananchi.

Kama tume itasimamia haki...CCM 2025 ni ngumu sana kutoboa.

View attachment 2170598View attachment 2170601
Hatimaye chama kimerudi kwa 'wenyewe', wale walugaluga kwishnei.
Ngoma mbuchuchu
 
Nakubaliana na wewe kwamba walioifanya CCM kwenda ICU ndiyo wameeudi Chini ya upole wa mama SSH.
Ccm inaenda kuwa dhaifu lakini si dhaifu kufikia udhaifu wa upinzani.

Wapinzani bado hawajaweza kushawishi wapiga kura.
Wanacheza ngoma ya watawala. Wamekuwa ni kikundi cha kusubiri ccm kafanya nini na ndiyo watoke kusema.

Wapiga kura wanataka kusikia vitu tofauti kutoka kwa wapinzani.
Upinzani Tanzania hauna shida yoyote. Tatizo hasa la Tanzania ni watu kama wewe wanaosubiri washawishiwe na upinzani! Kama shida zote zilizo Tanzania kama ukosefu wa ajira, maisha magumu, kunyimwa haki nk hakujakushawishi kutaka mabadiliko hata hao wapinzani wafanye nini utashawishika? Wewe subiri ukidhani kuna siku utafanyiwa kila kitu uende mezani tu kula uone hasara itakuwa ya nani. Ule ''uchafuzi'' wa 2020 ulivyofanywa kibabe na watu wakawa kama makondoo unadhani mabadiliko yangekuja yenyewe!
 
Wakuu oneni hili jinga. Ndo nini hiki sasa limeandika? Eti lenyewe ndo lipo serious
..... Ni bora mimi nilio serious kuliko wewe, ambae hujui unachokitaka na chama chako... Uwe Sisiem au chadema...
 
Back
Top Bottom