Ni Suala la muda mfupi ujao, haya niyasemayo yatadhihirika huko site.
CCM ya wanyonge imepigwa kitu kizito na CCM ya mtandao. Hili sio la kuogopa kusema,labda Moderators wanifanyie yao kwa kuuondoa uzi huu.
Ila ukweli utabaki kuwa ukweli.
Kwa hii safu yenu mpya,
mmeingizwa chaka na walewale walioshindwa kulivua gamba.
Walewale walioiacha hadi ikaingia ICU.
Hakuna kipindi CCM itaishi kwa unafiki baina ya wanachama wenyewe kwa wenyewe kama sasa.
Ni vigumu kusema CCM haitagawanyika kuelekea 2025.
Mnaweza kubaki na raisi asiye dhibiti bunge la jamhuri.
Maana wabunge 75% ni ngumu kurudi bungeni.
Wapinzani mngekuwa makini,hiki ndio kipindi muhimu mrudi site kujijenga.
Tokeni huko mijini mje kuongea lugha ya wapiga kura na kero zao.
CCM hii ya mama na Kinana kwa mtindo huu wa majibu ya jazba kwa wananchi.
Kama tume itasimamia haki...CCM 2025 ni ngumu sana kutoboa.
View attachment 2170598View attachment 2170601