CCM imegawanyika; CHADEMA wajifunze kutoka Zambia. Mbowe ampishe Tundu Lissu Uenyekiti

Mgombea wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema anaongoza katika matokeo ya kura za awali katika uchaguzi mkuu.

Hakainde alionyesha kuongoza siku ya jana huku chama chake cha UPND kikikusanya kura katika majimbo mengi nchini humo.

Raisi alieko madarakani Edgar Lungu mwenye umri wa miaka 64 tayari amelalamika kwamba uchaguzi huo hauko huru na wa haki.

Mgombea Hichilema amewaambia wazambia kuwa wapuuze kauli hizo za raisi Lungu na kwamba huu ndo wakati mwafaka kwa wazambia kuungana na kuimarisha umoja.

Lakini moja ya sababu kubwa ya kura nyingi kwenda kwa bwana Hichilema ni ukosefu wa ajira nchini humo miongoni mwa vijana ambao ndo nguvukazi ambayo serikali imeshindwa kuitumia katika kuijenga Zambia kiuchumi.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka tume ya Uchaguzi ya Zambia vijana wengi walojiandikisha kupira kura wana umri wa miaka 34 kwenda chini.

Katika uchaguzi wa mwaka 2016 bwana Hichilema alishindwa na hata baadae kutumiwa vikosi vya usalama nyumbani kwake baada ya kutangaza kuwa matokeo ya uchaguzi ule yalichakachuliwa.

Safari hii wapiga kura wamejitokeza kwa wingi kupita maelezo na wote wameazimia kumpa kura bwana Hichilema mwenye umri wa miaka 59.

Hichilema anajielezea katika video zake Youtube kuwa ni mtoto wa maskini, na amekwenda shule bila viatu hadi kufikia chuo kikuu.

Kitaaluma bwana Hichilema ni mhasibu na alikuwa afisa mtendaji mkuu katika kampuni yake mwenyewe ya uhasibu kabla ya kufikria kuingia kwenye ulingo wa siasa.

Sera za bwana Hichilema ni kutaka kuimarisha uchumi wa nchi hiyo na kuimarisha soko la ajira ambalo limeathiri vijana wengi.

Matatizo yanayoikabili Zambia yanafanana kwa kiasi kikubwa na matatizo ya Tanzania, vitendo vya rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya fedha, maendeleo duni mijini, mazingira mabovu ya biashara na uwekezaji, deni la taifa na mengine lukuki.

CCM ndicho chama kinachoongoza serikali na mpaka sasa kila ishara iko wazi kuwa CCM imegawanyika katika makundi zaidi ya moja.

Miaka mitano imepita tumesikia kuwa CCM iligawanyika kati ya kundi linalojiita CCM asili na CCM mpya, na sasa tunasikia kauli tofautitofauti na zinazokinzana kutoka kwa wanachama waandamizi wa chama hicho.

Pia hata gazeti maarufu linalomilikiwa na chama hicho gazeti la UHURU nalo limetumika katika malumbano yanoendela ndani ya chama hicho na kwa kuandika vichwa vya habari kumhusu mwenyekiti wake na kuzusha fataki ndani ya chama hicho.

Kama si umakini wa wazee wa chama hichi kikongwe kuingilia kati na kumtuma katibu mkuu wake bwana Daniel Songoro kwenda kuzawazisha mambo, basi hali ingeendelea kuwa tete hadi leo hii.

Songoro bado hajajibu masuali makuu mawili kwanza, je CCM imegawanyika au la, na pili je CCM ina msimamo upi wa pamoja kama chama kuhusiana na chanjo ya UVUKO-19 kwa,mba ni lazima watanzania wachanjwe au chanjo hiyo ni hiari?

Mgawanyiko huu ndo ilikuwa nafasi ya pekee kwa chama kikuu cha upinzani cha Chadema kujitengenezea mazingira mazuri ya ushindi katika uchaguzi ujao wa 2025.

Badala yake si viongozi wake wakuu katibu mkuu, wala uenezi ambae amejitokeza kuonyesha angalau Chadema imeanza kujenga stratejia ya ushindi.

Chadema kinahitaji kujindaa kwelikweli na kama kweli chama hiki kina dhamira ya kweli ya kushika dola, basi kina wajibu wa kuachana na siasa za matukio na kujikita katika kujenga hoja zenye tija ili kujijengea imani kwa wapiga kura.

Suala la mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kuwa na kesi ya ugaidi inayoendelea mahakamani lisiwe sababu ya Chadema kama chama ambacho kina miaka 29 sasa kwenye ulingo wa siasa za vyama vingi kukosa mwelelekeo na kuonekana hakina mikakati.

Huu ndo ulikuwa wakati wa makamu mwenyekiti Tundu Lissu kuwa mastari wa mbele kukiongoza chama hicho na pengine kupewa nafasi ya uenyekiti wa chama hicho ili akiandane uzuri chama kwa uchaguzi ujao.

Ni maoni yangu binafsi kuwa Tundu Lissu kwa sasa amejifunza kuwa mwanasiasa badala ya mwanaharakati na kwa uwezo wake, ujasiri wake na kauli zake ambazo atakuwa sasa amefahamu namna ya kuzipanga uzuri, anafaa kabisa kuwa mwenyekiti wa Chadema.

Ni wakti sasa kwa Tundu Lissu kurudi nyumbani Tanzania na kuanza kazi ambayo nadhani bado hajaimaliza.

Vyombo vyote vya ulinzi na usalama havina budi sasa kujifunza kutoka Zambia na Malawi kuwa kuna wakati wananchi wanaamua kuwa chama kilichopo madarakani kimefikia tamati na wanataka chama mbadala.

Serikali ina wajibu wa kuhakikisha maisha ya Tundu Lissu yanalindwa na wale wote wasio na nia njema kwake na anasimama kwa uhuru katika jukwaa la kisiasa.

Tundu Lissu akiwa mwenyekiti wa Chadema taifa atakipanga chama atakavyoona yeye inafaa, kuteua timu yake ambayo ina watu makini na kutengeneza sera na ilani mpya ya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi wa 2025.

Kama raisi wa Malawi Chikwera na mgombea wa sasa wa uraisi Zambia bwana Hakainde Hichilema waliweza, sioni tatizo Chadema washindwe uchaguzi wa 2025.

Mgombea wa chama cha upinzani akipata kura za kutosha na watu wakijitokeza kwa wingi kama walivyofanya Zambia kiasi cha tume ya Uchaguzi ya Zambia kutia akili kuwa Hichilema anashinda kwa kura za kutosha.
Mkuu nikupongeze tu mawazo mazuri kama kweli uliyoyaandika yanatoka chini ya sakafu ya moyo wako. Mkuu mbona suala la ushindi kwa vyama vya Upinzani unaeleweka sana. Hata chama kinachotawala kinalijua hilo. Toka 2015 hawa majamaa hawajashinda kwenye box uwanjani bali kwenye box gizani.
 
Back
Top Bottom