Uchaguzi 2020 CCM imechokwa na Watanzania tuache utani kabisa

Kuna mijitu inakuja hapa inaandika" vijana fanyeni kazi achana na siasa" ukiona hivyo ujue ni kutoka CCM, wanavunja moyo vijana. . Sasa mwakani vijana wote wanapiga kura .
 
Ningekuwa na nafasi Kama ya Siro, haki ya Mungu CCM wangenikoma. Yaani ingekuwa nipe nikupe, ningehakikish Mimi na jamaa wa jamaa zangu na mpaka vitukuu tunakuwa matajiri. Maana Siro akiamua hata kesho CCM ifutike inafutika.no way

Ifutike kwani hana bosi wake aliemteua?
Anaanzaje kuifuta wakat kuna mkuu anaempa order?
 
Kuna mijitu inakuja hapa inaandika" vijana fanyeni kazi achana na siasa" ukiona hivyo ujue ni kutoka CCM, wanavunja moyo vijana. . Sasa mwakani vijana wote wanapiga kura .
Hayo ndiyo maajabu, CCM hawana tofauti na shetani, kwa Sababu huwa hawapendi kuwa wakweli na hawajawahi kushirikiana na mtu mkweli. Sasa Kama vijana waachane na siasa, kwanza waulize swali moja tu, Baba wa hili Taifa alianza kufanya siasa Akiwa na umri gani?.
 
2020 hivi vyama vya Siasa vikishindwa kuondoa huyu Jinamizi wa Nchi hii CCM, Sisi tusio na Vyama Tutatafuta njia mbadala ya kuwapumzisha. Tumechoka. Nchi zote za Africa mashariki zinasonga mbele kiuchumi ati sisi tunarudi kinyumenyume.

Hatutakubali, hii Nchi Siyo Mali ya CCM wala CHADEMA wala ICT Wala Chama Chochote cha Siasa, hii Nchi ni Mali yetu Sisi Wananchi., Mungu ametupa kila kitu, lakini kila Siku tunazidi kuporomoka. Ati Kisa, CCM. Waondoke zao kabisa.
 
Kama siyo mbinu ya JPM Kupiga Marufuku mikutano ya kisiasa tangu Alipoingia Madarakani, sasa hivi tungekuwa tunaongea mengine kabisa, Nina Imani hata kitendo cha kuvunja katiba ya Nchi makusudi ni baada ya Kuona CCM ilivyozidiwa ktk Kampeni za Uraisi, 2015. Binafsi Mimi siyo mfuasi wa Chama chochote cha siasa, ila Mmi ni Mtanzania ninayependa sana Nchi yangu...
Umeongea utumbo mtupu jombaa...kwanza sijui unawasemea watanzania asilimia ngapi..kwa sababu asilimia 90 ya watanzania wapo nyuma ya Magufuli na serikali yake.. unasikia kila kukicha wananchi wakipongeza juhudi znazofanywa na serikali hii..hili halina doubt kabisa.

Lengo la andiko lako ni kutaka kupewa uhuru wa kufanya siasa tuu..huko kwingine koote ni blabla za utumbo wa mbuzi..kwani nani kakukataza kufanya mikutano kwenye majimbo yenu..mmeelekezwa fuateni sheria na taratibu..tatizo lenu nyinyi wanaharakati mnataka kujiamulia tu chochote kinachokuja kichwani mfanye..hivi hamjifunzi hata kwa wenzenu.
 
Kama tu kipindi cha JK ilitaka kumfia Hali ilikuwa Co mbaya watu kila siku ulikuwa sherehe Leo kwa Hali hii utasemaje ccm inapendwa?
 
Kama unaakili timamu co shabiki tu kwa yaliyowapata wakulima, wafanyabiashara na watumishi na haya ndo makundi ktk nchi hii na hata uweje lazima uwepo ktk moja ya haya lazima umeguswa na uongozi WA ccm hvyo huwezi itetea
 
Kwa tume huru ya uchaguzi 2020 hawa sisiemu hata kura asilimia 7(7%) hawapati.I'm telling you
 
Viatu vyangu vya kazini vimechoka kweli, hata ukipiga rangi vinakuwa visafi tu ila mikunjo mikunjo ya uzee inabaki. Inabidi tu nivivae tena na kesho sababu mbadala wake ni ndala za kuogea na siwezi kwenda nazo kazini. Nikitoka kazini nikivivua navaa ndala angalau kidogo miguu ipate hewa lakini siwezi kwenda na ndala kazini.

CCM bado haina chama mbadala cha kukabidhi nchi zaidi ya sisi kupata ahueni kupitia wabunge. Chagueni wabunge wengi ili Utlist viatu vya uongozi wa juu vinapokuwa vimetubana siku nzima, basi jioni tuvae kandambili za upinzani kupitia bunge. (ila bado sijui kama wakiwa wengi tutaufaika au itakuwa tatizo, nasahauri kujaribu tu)
 
2020 hivi vyama vya Siasa vikishindwa kuondoa huyu Jinamizi wa Nchi hii CCM, Sisi tusio na Vyama Tutatafuta njia mbadala ya kuwapumzisha. Tumechoka. Nchi zote za Africa mashariki zinasonga mbele kiuchumi ati sisi tunarudi kinyumenyume. Hatutakubali, hii Nchi Siyo Mali ya CCM wala CHADEMA wala ICT Wala Chama Chochote cha Siasa, hii Nchi ni Mali yetu Sisi Wananchi., Mungu ametupa kila kitu, lakini kila Siku tunazidi kuporomoka. Ati Kisa, CCM. Waondoke zao kabisa.
Ukiona maisha yanakushinda hama nenda kwingine jombaa
 
Umeongea utumbo mtupu jombaa...kwanza sijui unawasemea watanzania asilimia ngapi..kwa sababu asilimia 90 ya watanzania wapo nyuma ya Magufuli na serikali yake.. unasikia kila kukicha wananchi wakipongeza juhudi znazofanywa na serikali hii..hili halina doubt kabisa...
Ukiona mtu yeyote Leo anaitetea CCM basi jua huyo ni kula kulala, labda baba, mama, shangazi au mjomba anafanya kazi CCM na yeye ni kijana wa nyumbani. Hakuna mtu yeyote Tanzania hii Leo mwenye akili timamu asiyejua kuwa CCM ni ya Wazee kwa hiyo imechoka na haina mbinu mpya tena.
 
Chama cha mashetani ccm kimechokwa vibaya sana ,sasa Jiwe anahasira sana maana yeye alijua anapendwa sana na watanzania ,sasa kilichomwacha hoi ni Kule kushindwa uchaguzi vibaya sana ile 2015 ,pamoja na kupindua matokeo lakini ilimuuma sana ,ili kulipiza kisasi Jiwe akaanza kuwakomoa wananchi ,Mara vunjia nyumba ,Mara vyeti feki ,Mara tumbua tumbua ,Mara fungia biashara ,hiyo yote ilikuwa ni visasi na hasira za kukataluwa na watanzania .
Mmefilisika sera kichwani sasa hivi mnatapatapa hamna pa kushika...biashara zenu za madili na utapeli zimefilisika..maisha yamekuwa magumu kilichobaki ndio mnaharahara humu mitandaoni..hahahaha..
 
Ukiona maisha yanakushinda hama nenda kwingine jombaa
Yaani nihame Nchi yangu kwa Sababu ya CCM, Haitawahi kutokea, kwanza hawa watu sasa hivi wako mwisho mwisho tu wa uhai wao, I believe , withing 10 years from now, hakuna kitu kitaitwa CCM Nchi hii,
 
Ukiona mtu yeyote Leo anaitetea CCM basi jua huyo ni kula kulala, labda baba, mama, shangazi au mjomba anafanya kazi CCM na yeye ni kijana wa nyumbani. Hakuna mtu yeyote Tanzania hii Leo mwenye akili timamu asiyejua kuwa CCM ni ya Wazee kwa hiyo imechoka na haina mbinu mpya tena.
Viongozi wenu vijana shupavu wote wameenda ccm kumssupport Magufuli na serikali yake..sikuelewi hoja yako inajikita kwenye utafiti upi...endeleeni kutapatapa kwa sababu hamna sera kwa sasa..hata kiongozi wenu wa safari ya matumaini karudi nyumbani kumenoga...mmebaki na Mr Zero tu..mnatia aibu sana
 
Yaani nihame Nchi yangu kwa Sababu ya CCM, Haitawahi kutokea, kwanza hawa watu sasa hivi wako mwisho mwisho tu wa uhai wao, I believe , withing 10 years from now, hakuna kitu kitaitwa CCM Nchi hii,
Hama sio sababu ya ccm..sababu maisha yamekushinda..dili zenu zote zimefungwa huna pa kuhemea...nakushauri basi nenda hata ukaanzishe kilimo, kule utapata mbogamboga na mazao ya chakula chako na watoto jombaa..unalolisubiri la kupiga hela halitakuja tena..fanya biashara halali lipa na kodi forodhani..fullstop
 
Mmefilisika sera kichwani sasa hivi mnatapatapa hamna pa kushika...biashara zenu za madili na utapeli zimefilisika..maisha yamekuwa magumu kilichobaki ndio mnaharahara humu mitandaoni..hahahaha..
Mkalipe kwanza korosho za watu mliowatia umasikini kwa upumbavu wenu huko mtwara ndiyo uje na upupu wako hapa, mmechukua korosho za watu tangu mwezi wa Saba mwaka Jana na mpaka sasa hamjawalipa, halafu bado mna mishipa ya kuja kuandika upuuzi hapa JF , hamna aibu, Mawakala wa Shetani Nyie.
 
Viongozi wenu vijana shupavu wote wameenda ccm kumssupport Magufuli na serikali yake..sikuelewi hoja yako inajikita kwenye utafiti upi...endeleeni kutapatapa kwa sababu hamna sera kwa sasa..hata kiongozi wenu wa safari ya matumaini karudi nyumbani kumenoga...mmebaki na Mr Zero tu..mnatia aibu sana
Wale wavaa milegezo , kula kulala na wanaowekwa vinyumba na vibibi vizee tena vinavyoumwa Kama akina nyie ndio watakaoungaa Mkono juhudi za ujinga na za kudhulumu watu. Mkalipe kwanza korosho za wakulima masikini mnaowapiga danadana mwaka sasa. Majambazi wakubwa
 
Back
Top Bottom