CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!

CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!

sio ccm tu bali vyama vyote tawala vya africa vishapitwa na wakati. Hata wao wanajuo hivo ndio maana jambo dogo tu wanajaza polisi. vyama vingi africa vinajivunia , KATIBA MBOVU, jeshi na tume zisizokua huru
 
Paschal kama ni kweli wamechokwa ni bora kuendelea nao pamoja na uchome wao kuliko kuwakubali hawa unaosema hawajajiandaa ?
 
Wanabodi,

Kutokana na majukumu yangu kama Mshauri wa Siasa wa Ubalozi fulani, nawajibika kuwapo Dodoma kwa muda fulani kwa kazi fulani inayowahusu wabunge.

Sasa nikiwa hapa Dododo kwenye Bunge jipya, nimebahatika kukutana baadhi ya wabunge wapya wa CCM na wa kambi ya upinzani, kujaribu kufahamiana nao, sio siri, baadhi yao hawana hata substance ya ni nini kilichowafanya washinde, na kwa viti maalum ndio kabisa usiseme!, sikuona ni kipi kilichowafanya wateuliwe na vyama vyao!, wengi wao japo wameteuliwa kutimiza hitaji la usawa wa kijinsia, sababu za uteuzi wa baadhi yao ni ile jinsia yao kwa matumizi ya kutoa zile huduma muhimu za kibinaadamu kama vidumu vya waheshimiwa sana na sio kuchangia mijadala na hoja nzito za bungeni, na hili litathibitishwa na michango yao kikao cha Januari.

Nilipoongea na baadhi ya wale makamanda waliokata magogo kule Kanda ya Ziwa, kiukweli nimewaona baadhi yao ni watu wa kawaida tuu with nothing special kilichowafanya wachaguliwe na kuibwaga CCM, hivyo nimefikia jibu moja tuu la uhakika, kuwa CCM katika baadhi ya maeneo, imechokwa mpaka basi!, upinzani hata ungesimamisha jiwe, lingechaguliwa!, nadhani hii ni moja ya sababu kuu iliyopelekea wengi wa waliojiandikisha, hawakujitokeza kupiga kura, waliona kujitokeza kupiga kura ni kujisumbua tuu!.

Nasisitiza CCM imechokwa, na ule ushindi wa kishindo wa toka Asilimia 80% niliyohakikishiwa na mwana CCM mwandamizi mpaka asilimia 60% ni uthibitisho tosha, Watanzania sasa wameichoka CCM ila pia hawakuwachagua wapinzani kwa wingi zaidi, kwa sababu wapinzani bado hawajaonyesha kukomaa vya kutosha na utayari kukamata dola na kutawala.

Najua kwa dhati, japo JK anafurahia ushindi kwa furaha, ni furaha ya machoni tuu, lazima moyoni ana lia kwa huzuni ya kukataliwa toka ushindi wa kishindo wa asilimia 80% ya 2005 hadi ushindi kiduchu wa asilimia 60 za 2010, na hiyo asilimia 20% kukataliwa ni kukataliwa tuu, kunauma.

Hivyo chama makini chochote lazima kikae chini na kujiuliza, hivyo CCM lazima watakaa na kujiuliza kulikoni, huenda wakajipanga upya na kuja kwa mbinu mpya, ila kwa vile CCM imechokwa, hata ijipange upya vipi, safari ya kwaheri ndio imeanza, there is nothing to stop it from failing down unless ibadilike kwa revamping.

Dawa pekee ya kuitibu CCM, ni kuirevamp CCM completely, task nambari moja ni Makamba should go first with his old guards team. Msisubiri mpaka uchaguzi mkuu wa chama chenu, miaka miwili ijayo (2012), itakuwa too little too late. If you are to do anything, do it now and fast!. Leteni fresh blood kina January type, Kippi, Nape type and the like ambao wanaweza siasa za kisasa za dot com type.

Hakuna ubishi, Chadema imenyanyuka, toka wabunge 5 mpaka 22 wa kuchaguliwa tena majimbo ya haja, huku sio kukua bali ni kupaa, tatizo kubwa la Chadema, bado hawajipanga.

Kichama, wanachadema mkubali msikubali, chama chenu japo kipo juu, lakini bado hamjakomaa kufikia kiwango cha kukabidhiwa nchi, bado mko kiuana harakati zaidi na hamjajipanga kwa sura ya kitaifa na utayari wa kutawala nchi.

Kwa vile CCM imekaa mkao wa kifo, hii ndio opportunity yenu Chadema kujipanga kimkakati ili muwe na sura ya kitaifa, Watanzania wawamini wawakabidhi nchi mwaka 2015. Sehemu muhimu kabisa to keep watch kuhakikisha hamuiachii ni hiyo Kanda ya Ziwa ambayo imeipokonya CCM na kuishika, hii ndio Kanda determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii. Aliyeishika Kanda ya Ziwa ndio rais wa Tanzania. Hivyo CCM wataelekeza all it might powers to reclaim what it has lost.

Kwa upande wa Chadema, first and foremost, anzeni na Mwenyekiti wenu Freeman Mbowe, he shouli go!. Ajiuzulu uenyekiti, ampishe Dr. Slaa kwenye usukani wa chama, Katibu Mkuu mpeni Zitto, hii itaifuta ile dhana ya nepotisim kwenye chama chenu, na kulivua lile koti la ukanda na ukabila ili walioichoka CCM wawafungulie mikono kwa kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura 2015.

Kupumzishwa kwa Freeman Mbowe sio kuwa hafai no, anafaa sana lakini kwa background yake na nature ya kazi zake, hapo alipoifikisha Chadema amaishafanya kazi kubwa na kufikia mwisho wa uwezo wake. Kwa background yake ya a former DJ na sasa ni mfanya biashara, focus ya wafanyabiashara kote dunia nzima ni maximisation of profits, hivyo Mbowe atahitaji ruzuku ya Chadema itumike kuivest kwenye assets, kwenye vitu.

Ili Chadema kiweze kushika nchi 2015, it has to invest on people na sio kwenye vitu na kuivest kwenye mass mobilisation na sio kutegemea mikutano ya hadhara na maandamano. Chadema needs to have able people kuiwezesha kushika dola five years to come na reaching out mechanism kuwafikia the mases kwa kumiliki media yake yenyewe. Mbowe hawezi kukubali ruzuku ya Chadema itumike to invest on people, it's a loss kwa mfanyabiashara na kuivest kwenye mass media sio profitable investment kwa business man ambaye ni for profit making. Dr.Slaa na Zitto sio wafanyabiashara hawa ni ma techcrats. Chama kishikwe na wanasiasa sio wafanyabiashara.

Kitendo cha Chadema kuihodhi kambi rasmi ya upinzani Bungeni, huu ni udhaifu mkubwa ambao hautawafikisha mbali. Pamoja na kanuni za Bunge kuruhusu Chadema kuunda kambi rasmi ya upinzani peke yake, Chadema peke yenu hamuwezi!. Lazima muwashirikishe wapinzani wengine wote hata kama hawastahili. You have to unite and work as one against a common enemy.

Kama CCM hii iko ICU na Chadema haijajipanga, spika ndio huyo mama ma over confidence na over reaction, 2015 tutegemee nini?.

Angalizo: Paskali wa Jamii Forums ni political commentator ambaye yuko objective, bila kuegemea chama chochote, upande wowote na hufanya kazi kwa wote, ila ni muumini wa demokrasia ya kweli ndani ya bunge for the balance of power, hivyo nashangilia sana kambi ya upinzani kuingiza vichwa 100 bungeni, ni matumaini yangu, 2015 kazi itakamilishwa!.

Paskali
Kwamba mbowe should go? Mbowe wanaenda wapi anamuachia nani,

Kaja
Mwinyi mbowe YUPo
Mkapa mbowe YUPO
Kikwete mbowe YUPO
MAGUFULI mbowe YUPO TU

ANAENDA WAPI ANAMUACHIA NANI, YEYE MSAMIATI WA KUNG'ATUKA HAJUI
 
Nafanya tuu rejea ya bandiko hili, kwa kulihusianisha na hiki kinachoendelea sasa, nilisema CCM imechokwa, sasa, hii ya viongozi wa upinzani kujiunga CCM, jee ni kiashiria sasa CCM, imepunguzwa kuchokwa, na sasa inapendwa, au ni tafsiri kuwa Chadema bado haijajipanga, hivyo sasa ndio Chadema inachokwa, CCM inajipanga?.

Na hawa wanaojiunga CCM sasa, jee wanajiunga CCM kwa sababu sasa CCM ni chama kizuri, au wanajiunga CCM kumfuata Magufuli?.

Paskali
 
Nafanya tuu rejea ya bandiko hili, kwa kulihusianisha na hiki kinachoendelea sasa, nilisema CCM imechokwa, sasa, hii ya viongozi wa upinzani kujiunga CCM, jee ni kiashiria sasa CCM, imepunguzwa kuchokwa, na sasa inapendwa, au ni tafsiri kuwa Chadema bado haijajipanga, hivyo sasa ndio Chadema inachokwa, CCM inajipanga?.

Na hawa wanaojiunga CCM sasa, jee wanajiunga CCM kwa sababu sasa CCM ni chama kizuri, au wanajiunga CCM kumfuata Magufuli?.

Paskali


Maslahi na njaa tuu zinawasumbua. NJAA KITU HATARI
 
PASCO,

Mwanajamvi nimefurahi sana kujitambulisha kama Political analyst. Ningelifurahi sana kusaidia Taifa lako kama analist kama ungelitusaidia yafuatayo:

i) Utafuti unaonyesha nini duniani kuhusu Leader of the Opposition katika mifumo ya mabunge yaliyoko Duniani. Kwa mtu yeyote anayefanya analysis angelitegemea kuona American Model na WestMinster Model zinaeleza nini. Analysis yako ime base kwa personalities badala ya Model na analysis ya aina hii kwa maoni yangu ni ya hatari sana kwa kuwa inakosa misingi ya kisayansi. Politics is science and should never be reduced to anything less than empirical analysis to be scientific.

ii) Analysis yako imetoa Conclusions kabla ya kujenga plausible major and minor. Scientific and logical conclusion can only be based on a well founded "major and minor". Ili tunaofuatilia tuweze kunufaika na analysis yako ningelitegemea a properly constitued logical arugement inayofuata clasical logical construction ambayo ndio msingi wa analysis yoyote ambayo ni credible.

iii) Analysis yako inaonekana kukosa basic and simple facts. Kwa mfano unapoeleza muundo wa Kambi ya Upinzani tungelitegemea misingi ya hoja yako, analysis ya kwanini tuko hapa tulipo ambapo Chadema wameunda Kambi bila kuwashirikisha CUF and reasons leading to the same, kama kulikuwa na majadiliano yeyote yalikuwapo kwanini yalishindikana, Political Statusquo ya CUF ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inayoongozwa na CCM kama ambavyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano inaongozwa pia na CCM hiyo hiyo na Thesis na Antithesis inayotokana na hali hiyo na matokeo yake au conclusions zinazotokana na situation hiyo kutokana na empirical analysis. Vinginevyo analysis unayojenga inaweza kuwa flawed na ikawa msingi mkubwa sana wa political fallacy ambayo ni ya hatari sana katika analysis ya kisayansi, na athari yake ni mbaya kwa kuwa wako wengi ambao watatumia analysis hiyo bila kuifanyia uchambuzi independent wakiamini umetolewa kwa msingi wa kisayansi. Athari za Fallacies katika historia inajulikana sana kwa historical philosophers pamoja na political philosophers.

iv) Maneno "Kuhodhi", "ubinafsi", "umimi", bila kuwa qualified ni manifestation ya "emotion", na kwa kiwango kikubwa ya "ego". Bila vigezo sahihi ya kisayansi maneno hayo ni manifestation kuwa ya kuwa subjective ambayo kimsingi ni kinyume na dhana ya "objective Political analyist unayoijenga. Hivyo ili tunufaike na matumizi ya maneno haya ningelitamani sana kuona qualification ya maneno hayo ili yaweze kulisaidia Taifa letu, kuliko kuyatumbukiza kwa mfumo unaoweza kutafsiriwa kwa sura mbalimbali. Na kwa bahati mbaya hoja hizi zimekwisha kujitokeza mara nyingi kwenye jamvi letu. Kwa vile nia na lengo la jamvi ni kusaida Taifa letu, na Taifa linajengwa na watu wenye uchungu wenye sifa na ujuzi mbalimbali, na hasa kwa kuwa umejitokeza hadharani kama Political Analist ambaye ni "objective" basi nilikuwa nimefurahi sana kupata analysis ambayo inatumia objective criteteria katika hoja zote ulizokuwa unajenga.

Natanguliza shukrani za dhati, na ninategemea kupata objective political analysis ya mapendekezo yako.

Mungu Ibariki Tanzania.
Mzee nikiona mabandiko yako kama haya najiuliza hivi wakati anateuliwa Mashinji watu walijipa muda kupitia kazi zako hizi zenye kuonesha wazi fikra zako na angalau wamezikusanya maktaba wazitumie kama rejea wakati wanapanga mikakati yao ya kukiendeleza chama?

Nimesoma mara mbilimbili nikajiridhisha kweli wewe ni daktari wa falsafa unaetumia vizuri elimu yako ktk kutatua changamoto mbalimbali zinazo kuzunguka ktk majukumu yako ya kila siku.

Mzee tupo tutakao kukumbuka sana. Sikufanya kosa kukupa kura yangu 2010.
 
Kadri siku zinavyokwenda, naona kama kibao kinaanza kugeuka, sasa ni kama Chadema inachokwa, CCM Inajipanga!.

Ushauri kwa Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe, auzingatie ushauri wa bandiko hili before its too late, kisije kumfia mkononi.

Paskali
 
Kadri siku zinavyokwenda, naona kama kibao kinaanza kugeuka, sasa ni kama Chadema inachokwa, CCM Inajipanga!.

Ushauri kwa Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe, auzingatie ushauri wa bandiko hili before its too late, kisije kumfia mkononi.

Paskali
Mkuu ulichokisema hapa kina shabihiana na maneno yangu haya kwenye ule uzi wa vijana wengi wa UDSM wajiunga CCM.
Mimi nilisema maneno yafuatayo hapo chini.

Zamani ilikuwa aibu kwa kijana wa chuo kikuu hasa UDSM kujiunga CCM.

Labda kidogo kule UDOM walikuwa wanasikika UVCCM na walikuwa wanazomewa na kuitwa vilaza wanachuo wa kata kisa walijiunga CCM.

UDSM, IFM na vyuo vingi vya dar hadi paka waokota makombo cafteria walikuwa CHADEMA.
 
Kadri siku zinavyokwenda, naona kama kibao kinaanza kugeuka, sasa ni kama Chadema inachokwa, CCM Inajipanga!.

Ushauri kwa Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe, auzingatie ushauri wa bandiko hili before its too late, kisije kumfia mkononi.

Paskali
Mkuu naongezea kwenye hii hoja yako niliyosema kuhusu hali ya sasa ktk uzi fulani wa wanafunzi 400 wa UDSM kujiunga CCM.

Mkuu hata akina Mnyika, Mtatiro, Silinde, Ally Happy, Makonda, na wengine wengi walionzia siasa zao tangu vyuoni walitumwa kusoma.

Kweli sasa wapinzani wamekuwa kama CCM ya enzi za JK Kikwete na CCM imekuwa kama Upinzani wa enzi hizo hasa wamekuwa kama CHADEMA ya Dr. Slaa.

Miaka mitatu tu iliyopita wakati wimbi la vijana wanakimbilia CHADEMA kila kona ya nchi hasa UDSM, tukawasikia viongozi wa serikali na wana CCM wanasema kauli kama yako kwamba vijana wametumwa kusoma. Waache siasa vyuoni.

Kweli hii dalili mbaya kwa upinzani.
Natumaini hao vijana hawajatishiwa bunduki, au kunyang'anywa mali zao au kufilisiwa na TRA kama anavyojaribu kutuaminisha Yericko Nyerere na baadhi ya wanachadema humu mitandaoni n.k.

USHAURI kwa chadema wakubali mambo sio mazuri na tatizo lipo ndani ya chama chao. Wajisahihishe vinginevyo wanaifuata njia ya NCCR Mageuzi na CUF.
 
Kadri siku zinavyokwenda, naona kama kibao kinaanza kugeuka, sasa ni kama Chadema inachokwa, CCM Inajipanga!.

Ushauri kwa Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe, auzingatie ushauri wa bandiko hili before its too late, kisije kumfia mkononi.

Paskali
Mimi inanipa shida sana nikiona waasisi wa vyama wanawapa vyama mtu mwenye uhusiano naye,ina fanya aliopewa chama aogope kuitoa kwa watu wa mbali,ni kama prince arudishe madaraka kwa wananchi inakuwa ngumu sana,nadhani ni wakati wa kuitisha uchaguzi wa huru ndani ya vyama vya upinzani ili tupate upinzani wenye nguvu na kuaminika,Chadema ikiendelea na hii system ya wakina Mbatia,mrema,lipumba haifiki mahali,nchi zetu za kiafrika dola zinatumika kwa nguvu au kwa fedha kuidhoofisha upinzani,wanachama wasipopewa fursa ya kuchagua ndani ya vyama na kuhisi chama ni chao huwa chama kinageuka ufalme au ya jamii fulani tu kama kenya.
 
Wanabodi,

Kutokana na majukumu yangu kama Mshauri wa Siasa wa Ubalozi fulani, moja ya kazi zangu ni kufanya kitu kinaitwa "stakeholders mapping", hii hufanyika kwa kitu kinachoitwa "interactions" hivyo from time to time, huwa nawajibika kuwapo Dodoma kwa interactions na waheshimiwa wabunge.

Sasa nikiwa hapa Dodoma kwenye hili Bunge jipya, nimebahatika kukutana baadhi ya wabunge wapya wa CCM na wa kambi ya upinzani, kujaribu kufahamiana nao, sio siri, baadhi yao. kwa kuwaangalia tuu na kuzungumza nao, hawana kabisa any substance ya ni nini kilichowafanya washinde, na kwa wabunge wa viti maalum ndio kabisa usiseme!, kwa baadhi ya wabunge hawa wa viti maalum, sikuona ni kipi kilichowafanya wateuliwe na vyama vyao kuwa wabunge wa viti maalum!, wengi wao japo wameteuliwa kutimiza hitaji la usawa wa kijinsia, sababu za uteuzi wa baadhi yao ni ile jinsia yao kwa matumizi ya kutoa zile huduma muhimu za kibinaadamu kama vidumu vya waheshimiwa sana na sio kwa ajili ya kuchangia mijadala na hoja nzito za bungeni, na hili litathibitishwa na michango yao bungeni katika mijadala mbalimbali, kuna baadhi mtawashuhudia kazi yao itakuwa ni kuonyesha umaridadi wa mavazi, kuonyeshea shapes na kuuza tuu sura kule mjengoni!.

Nilipoongea na baadhi ya wale makamanda waliokata magogo kule Kanda ya Ziwa, kiukweli nimewaona baadhi yao ni watu wa kawaida sana tuu with nothing special kilichowafanya wachaguliwe na kuibwaga CCM na vigogo wake wenye nguvu, influence na pesa, iliyoota mizizi kwenye kanda hivyo , hivyo nimefikia jibu moja tuu la uhakika, kuwa CCM katika baadhi ya maeneo, imechokwa mpaka basi!, upinzani hata ungesimamisha jiwe, jiwe lingechaguliwa!, nadhani hii ni moja ya sababu kuu iliyopelekea wengi wa waliojiandikisha kupiga kura, hawakujitokeza kupiga kura, waliona kujitokeza kupiga kura ni wastage of their valuable time, ni kujisumbua tuu!.

Nasisitiza CCM imechokwa, na ule ushindi wa kishindo wa Kikwete toka asilimia Zaidi ya 80% mwaka 2005 hadi asilimia 60% 2010, ni uthibitisho tosha, Watanzania sasa wameichoka CCM ila pia hawakuwachagua wapinzani kwa wingi zaidi, kwa sababu wapinzani bado hawajaonyesha kukomaa vya kutosha kuweza kukabidhiwa nchi kwa kushindwa kuonyesha utayari kukamata dola na kutawala.

Najua kwa dhati, japo CCM na JK wanafurahia ushindi huu kiduchu kwa furaha, ni furaha ya machoni tuu, lakini moyoni ni maumivu na vilio kwa huzuni ya kukataliwa toka ushindi wa kishindo wa asilimia 80% ya 2005 hadi ushindi kiduchu wa asilimia 60 za 2010, na hiyo asilimia 20% ya kukataliwa, kukataliwa ni kukataliwa tuu kunauma!.

Hivyo chama makini chochote lazima kikae chini na kujiuliza, hivyo CCM lazima watakaa chini na kujiuliza kulikoni, ni katika kujiuliza huko, huenda wakajipanga upya na kuja kwa mbinu mpya, kwa nguvu zaidi na kasi zaidi, ila kwa vile CCM imechokwa, hata ijipange upya vipi, kama Chadema itajipanga, then kwa CCM, safari ya kwaheri ndio imeanza, there is nothing to stop it from failing down unless ibadilike kwa revamping.

Dawa pekee ya kuitibu CCM chovu iliyochokwa, ni kuirevamp CCM completely, task nambari moja ni Makamba and his old guards pale Lumumba, should go, kupisha new blood. Tena CCM msisubiri mpaka uchaguzi mkuu wa chama chenu, miaka miwili ijayo (2012), itakuwa too little too late. If you are to do anything, just do it now and fast!. Leteni fresh blood kina January type, Kippi, Nape type and the like ambao wanaziweza siasa za kisasa za .dot com type.

Hakuna ubishi, Chadema imenyanyuka, toka wabunge 5 mpaka 22 wa kuchaguliwa tena majimbo ya haja yenye impact ikiwemo kuyashika majiji makubwa katika mikoa the big five!, huku sio kukua bali ni kupaa, tatizo kubwa la Chadema, bado hawajipanga mkao wa kichama tawala, ili kikabidhiwe nchi, kitawale, Chadema bado kimekaa kichama harakati, hivyo kuna wengi wanakiona kama bado hakijakomaa kiasi cha kukabidhiwa ikulu yetu!.

Kichama, wanachadema mkubali msikubali, chama chenu kwa sasa japo kipo juu, lakini bado hamjakomaa kufikia kiwango cha kukabidhiwa nchi, bado mko kiuana harakati zaidi kuliko ki chama tawala, na hamjajipanga kwa sura ya kitaifa na utayari wa kutawala nchi.

Kwa vile CCM imechokwa na imekaa mkao wa kifo, hii ndio opportunity yenu Chadema kuongeza offensive ili kuisindikiza CCM kaburini, kwa kujipanga kimkakati ili muwe na sura ya kitaifa, kwa kuonyesha Watanzania kuwa mmekomaa na mko tayari kutawala, hivyo Watanzania watawamini watawakabidhi nchi mwaka 2015.

Sehemu muhimu kabisa kwa Chadema to keep watch kuhakikisha hamuiachii ni hiyo Kanda ya Ziwa ambayo imeipokonya CCM na kuishika, hii ndio Kanda determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii. Aliyeishika Kanda ya Ziwa ndio rais wa Tanzania. Hivyo CCM imeumia sana kupoteza Kanda ya Ziwa na wataelekeza all it might powers to reclaim what it has lost, hivyo Chadema itumie uwezo wake wote kulinda what it has!.

Kwa upande wa Chadema, lazima kibadilike, first and foremost, anzeni na Mwenyekiti wenu Freeman Mbowe, he should go!. Ajiuzulu uenyekiti, ampishe more able person kama Dr. Slaa kwenye usukani wa chama, Katibu Mkuu mpeni Zitto strategically, hii itaifuta ile dhana ya nepotisim kwenye chama chenu, na kulivua lile koti la ukanda na ukabila ili walioichoka CCM wawafungulie mikono kwa kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura 2015 kwa kujionyesha Chadema ni chama cha wote, dini zote na kanda zote.

Kupumzishwa kwa Freeman Mbowe sio kuwa hafai no, anafaa sana lakini kwa background yake na nature ya kazi zake, as a businessman, hapo alipoifikisha Chadema amaishafanya kazi kubwa na kufikia mwisho wa uwezo wake. Kwa background yake ya a former DJ na sasa ni mfanyabiashara, focus ya wafanyabiashara kote dunia nzima ni maximisation of profits, hivyo Mbowe atahitaji ruzuku ya Chadema itumike kuivest kwenye assets, kwenye vitu vya kuonekanika yaani assets kama magari, mavazi, etc

Ili Chadema kiweze kushika nchi 2015, it has to invest on people na sio ku invest kwenye vitu. Chadema must invest kwenye mass mobilisation na sio kutegemea mikutano ya hadhara na maandamano. Chadema needs to have able people kuiwezesha kushika dola five years to come kwa kutumia reaching out mechanism kuwafikia the mases kwa kumiliki media yake yenyewe. Chadema lazima ifanye recruitment ya able people, watakaokuja kuendesha serikali ya Chadema. Mbowe hawezi kukubali ruzuku ya Chadema itumike to invest on people, it's a loss making venture kwa mfanyabiashara na kuivest kwenye mass media sio profitable investment kwa business man ambaye ni in for profit making. Dr.Slaa na Zitto sio wafanyabiashara hawa ni ma technocrats. Chama kishikwe na wanasiasa watendaji sio wanasiasa wafanyabiashara. Chadema iwekeze kwenye watu na kupanua mtandao wake hadi vijijini, ili kwenda kuiongoa CCM kuanzia kule chini kabisa kwenye mizizi yake ambako ni kule kwenye mashina. Chadema imiliki media yake yenyeshe for mass mobilization na sio kutegemea mikutano na maandamano, huko ni kuendeleza uanaharakati, Chadema inatakiwa kukaa mkao wa kutawala, ikitangaza kitu, kinafika Tanzania nzima!.

Chadema ina tatizo la umimi. Kitendo cha Chadema kuihodhi kambi rasmi ya upinzani Bungeni, huu ni udhaifu mkubwa ambao hautawafikisha mbali. Pamoja na kanuni za Bunge kuruhusu Chadema kuunda kambi rasmi ya upinzani peke yake, Chadema peke yenu hamuwezi!. Lazima muwashirikishe wapinzani wengine wote hata kama hawastahili. You have to unite and work as one against a common enemy. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.

Kama CCM ndio hii iko ICU na Chadema haijajipanga, spika ndio huyo mama ma over confidence na over reaction, 2015 tutegemee nini?. Kama Chadema haitabadilika, then 2015, japo imechokwa, japo chovu, ni CCM tena!.

Angalizo: Paskali wa Jamii Forums ni political commentator ambaye yuko objective, bila kuegemea chama chochote, upande wowote na hufanya kazi kwa wote, ila ni muumini wa demokrasia ya kweli ndani ya bunge for the balance of power, hivyo nashangilia sana kambi ya upinzani kuingiza vichwa 100 bungeni, ni matumaini yangu, 2015 kazi itakamilishwa!.

Paskali
Hii ni ya lini? Au ni ndoto?
 
Mkono mtupu hau lambwi wapiga kura wengi ni masikini kusema tu 'peoples power' halafu ushinde? Kuna takiwa Sayansi ya kutosha kukabiliana na hili wengi tuna njaa zeti bana
 
Back
Top Bottom