CCM imechanganyikiwa?

Tanzania ya viwanda Inawezekana kwani ni sera ya marudio tu japo haikuwahi kutumika kama slogan ya taifa na aliyeitekeleza sera hii kwa kiasi kikubwa ni Nyerere kwani ametuachia viwanda vingi vikubwa sana vilivyoongoza kwa ukubwa afrika kwa mfano spm mgololo Iringa ni kiwanda kikubwa afrika nzima na vingine vingi lkn vikafa kwa sab mbali mbali za kizembe wizi ubadhirifu ufisadi rushwa upendeleo siasa n.k,kwa kuangalia makosa ya nyuma na kujifunza Kenya ambao recently wameingia kwenye uchumi wa kati,tunaweza kwa sababu tuna resources zote muhimu kama watu, Ardhi,vyanzo vya umeme japo havijatumika vizuri na miundo mbinu ya kuridhisha inatakiwa dhamira tu ya kweli, na hii vita ya ufisadi na rushwa aliyoitangaza kwa nguvu mpya ina sweep the way. This is the Superb president.
 

Sawa, ili tusiharibu mudhui ya uzi huu nenda kwenye ule uzi useme kwa sasa tunafikaje huko. Hapa ulichoongea ni historia, kwa sasa kaseme tunafikaje kwenye Tanzania ya viwanda na wala kusema tuna superb president peke yake hakutoshi. Nenda kwenye huo uzi utoe maelezo yako ya kina. Kule ni facts tu na sio ushabiki.
 
Sina ushabiki na wala sio mwanaccm bali ni mfuatiliaji wa siasa ya upande wowote na kuichambua kadri niwezavyo nimekuwa nawaponda ccm kwa muda mrefu kutokana na ufisadi na kuleana kwao kuna wabunge wa wapinzani nawapenda kwa uwezo wao binafsi hali kadhalika ninampenda magufuli kutokana na nia yake ya kuwageuka wanaccm wenzake majambazi lkn nimepiga kampeni mtaani kwetu ya nyumba kwa nyumba 2015 ya kuwashawishi watu wasiwape kura wagombea wa udiwani na ubunge wa ccm lkn wampe magufuli kuliko lowassa ambaye ni fisadi aliyethibitishwa na bunge, kampeni yangu ilifanikiwa mpk leo nachukiwa na diwani aliyeshindwa kutoka ccm na amenitamkia,eneo ninaloishi diwani na mbunge ni kutoka upinzani na mama yangu mzazi ni mwanachadema mkereketwa mwenyewe huwa nampeleka kwenye mikutano na huwa nahudhuria, Kwahiyo mimi sio kada wa ccm you rather call me kada wa maendeleo.
 

Sawa kada wa maendeleo, samahani kwa kukuita kada wa ccm. Twende kule kwenye mada ya Tanzania ya viwanda, hapa tutaharibu maudhui na uzi huo upo. Nimeshakuona una akili, sasa twende ukaitumie akili yako kwa faida ya watanzania.
 
Thats why hatutakiwi kuwapa nchi wapinzani, Noy yet.
Unlike you, I blame hao wapinzani,
Mwanaume ananunuliwaje?
Mwanaume wa kweli husimamia Kile anachokiamini,
Sasa kama watu inafika kipindi wanakubali kununuliwa its obvious wako Brainwashed, Not fit enough to rule,
 
Mwanaume mpumbavu wa Mwisho ndio atakubali kununuliwa, na hatuwezi kuwapa nchi watu cheap namna hii, kama wananululiwa na Kina Bashite unadhani tukiwapa nchi wakakutana na wale wazungu wa makinikia atatoka mtu hapo??
Pasitokee mtu bila aibu akazungumza hili mbele ya Umma, its shame, (Very shame indeed)
Yaani kama una watu kwenye Chama wananunulika basi hakuna watu hapo, ni Watu wenyewe Akili za Kuku, ama Chama kimejaa Vikaragosi.
Halafu kiongozi mzima anakuja na kusema watu wake wananunuliwa? Haoni kama inatia kinyaa?
 
Kutokua mzalendo ni kusema ukweli mabaya yote wanayofanya watawala ,so we mshana jr sio mzalendo kabisa.ila ngoja ni wai kuchukua nyavu maana muda umefika wa kwenda kuvua .Ila naskia Paka wetu siku hizi hukamata panya kimya kimya
 
Nani aliyekuumiza?? Mbona vijana mnapenda sana kuyakuza mambo na kuyafanya kishabiki??? Acheni siasa majitaka
 
Hata hapa kwetu kuna ma kabila makubwa mawili yaani ccm na chadema ukipenda mwangaluka na shimboni shafo. CCM hoyeeeee
Kwani mwenyekiti msukuma ??si mzinza...vikabila vidogo vinakuwaga vya wahamiaji kama wazanaki
 
Nani aliyekuumiza?? Mbona vijana mnapenda sana kuyakuza mambo na kuyafanya kishabiki??? Acheni siasa majitaka
Mbona jina lako linaleta kichefuchefu sana, aliye ku Mark hilo jina medula oblangata yake haikuwa sawa, Mawazo yako na jina lako yanaendana kwani hata uandikacho ni takataka
 
None sense
 
Hata uwe mzuri kiasi gani, ukiwa na marafiki wezi na wahalifu, hakika nawe utakuwa mchafu tu. Haya yanayoendelea sasa yanaratibiwa na watu wenye nia ovu wakiongozwa na wanaojiita wana mapinduzi na wafufuaji WA ccm mpya, hawa ni wabaya kuliko tandu, ccm asili wako vinywa wazi , ni adui yupi wanae pambana nae? Upinzani? Huu ni zaidi ya wendawazimu, Mzee wetu hawa jamaa wanampeleka jau maskini ya Mungu hajui, ni muda tu utasema, hakuna jiwe litakaloachwa kufukuliwa hata kama itachukua karne .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…