Ni wajinga pekee ambao wangeweza kununulika kwa thamani ya kuikana imani yake na itikadi wanazoziamini na kuzisimamia, wajinga kama hao siamini kama wangeweza kupatikana kwenye chama kinachojinathibisha kuwa ni "chama makini". Msihangaike kumtafuta mchawi bali mjitathimini wenyewe kwanza.
Sote tunaishi mitaani na tunayaona yanayoendelea kwa sasa, tunaingia kwenye vikao, tunasikiliza maoni ya wana mitaa wenzetu, Kuhusu kununulika kwa mazingira ya huku sijasikia, ila kuna uwezekano madiwani wengi wa Cdm 2020 eidha wakaacha kugombea ama wakagombea kupitia Ccm ingawa nalo ni gumu. Ukiondoa vita dhidi ya ufisadi, umeiondoa Cdm kwenye ramani, kosa lilianzia hapo tu.