CCM imechanganyikiwa?

CCM imechanganyikiwa?

Rais alivyompandisha cheo mtu mwenye tuhuma za rushwa hapo ndio alimaliza mchezo. Na boss wa Takukuru angefanya lolote yangemkuta yaliyomkuta Nape kwenye sakata la Makonda na clouds.

Ukitaka kujua ni siasa zinachezwa , wote tunakubaliana kuna rushwa kubwa na ndogo na ni tatizo nchi hii, nani kafikishwa mahakamani na kufungwa mpaka leo? Akina Shaka ns Gulamali juzi lilifanyika igizo la kupambana rushwa, umeona hatua? Walipokamatwa mbona hakukuwa na waliokuwa wanawagaia rushwa? Za kuambiawa changanya na zako.
Kutokufungwa mla rushwa mpk sasa haimaanishi hawatafungwa bado utawala una miaka miwili tu stay tuned.
 
Mkuu wame pagawa siyo wamechanganyikiwa kuchanganyikiwa wangetakiwa waokote makopo ajira ya jk kuchanganyikiwa ni hali ya mtu kuto kujuwa afanye nini ndio maana wana nunuwa wana siasa ndio kuchanganyikiwa huko ni sawa na wafa mfa maji haachi kutapa tapa !! atajishika ata na jani wakati halina uwezo wa kumsaidia kujiokoa!
 
Kama kuna ushahidi wa ccm kuhusika ni kweli inapaswa kukemewa kwa nguvu zote, lkn wasi wasi wangu makamanda jahazi linatoboka baada ya kujadili nini tatizo mnakuja na visingizio lukuki. Wanachama wanakimbia eti oohh wanahongwa sababu nyepesi kweli kweli.

Kwa sasa mmekosa mtu kama slaa mnabaki kulia lia tu mitandaoni. Ukweli ni kuwa mmewaangusha wananchí hata kabla ya kupewa dola, mlichobakisha kwa sasa kila anaekuambieni ukweli eti ccm. Edo na wengine kadhaa wapo njiani nyie katafteni flash mseme wanahongwa.
Rudia kusoma ulichoandika then kanusha kuwa think tank wako siyo Bashite, hata kupanga hoja hujui????
 
Prove beyond reasonable doubt kuwa wananunuliwa toa porojo hapa za kuja na flash disk

Toeni boriti ndio mpambane na Magu otherwise mwafwaa
 
Akina Zitto, Kitila, Mwigamba, Kafulila, Msando nk wote walihama enzi za Slaa. Sasa sijui unamaanisha nini kwamba watu wanahama kwakuwa Slaa hayupo. Ni hivi, sasa hivi ccm imeamua kununua wapinzani ili ijenge taswira inakubalika kitu ambacho sio kweli.
KUMBE WAPINZANI MNANUNULIKA!!!
Kwa hiyo mkiiongoza nchi na mkapewa pesa ya kutosha mtaiuza nchi!!!

Mengine ni aibu kuyasema. Kama mnanunulika ni aibu hivyo ficheni hiyo aibu kwa kutosema.
 
Mnajidhalilisha watu gani mnanunilika kama Karanga? Tukiwapa nchi mtauza nyie siyo bure.
 
Prove beyond reasonable doubt kuwa wananunuliwa toa porojo hapa za kuja na flash disk

Toeni boriti ndio mpambane na Magu otherwise mwafwaa
Naona mmeitwa kujibu hoja... Jibuni kwa weledi basi sio mipasho... Kumbukeni anasoma
 
Angalien Tbc Mjadala Ulioko Rais Aongezewe Miaka Iwe 20 Au 28 , Tuombe Kwa Ajiri Ya Nchi Yetu
 
Tuhuma ni zile zilizothibitishwa na kufikishwa mahakamani pekee hizo za vijiweni sio tuhuma rasmi kifupi mnyeti hana tuhuma official zaidi ya tetesi na fununu ambazo wanasiasa wengi wanazo akiwemo magufuli mwenyewe.

Kwa haya maelezo yako ndio maana nakuambia hakuna vita vya rushwa nchi hii.
 
Kutokufungwa mla rushwa mpk sasa haimaanishi hawatafungwa bado utawala una miaka miwili tu stay tuned.

Hilo hutokaa ulione, ikifika 2020 mwezi marchi watapandishwa watu kizimbani kisha ikifika wakati wa kampeni itumike kama kick kwamba kuna kupambana na rushwa. Lakini wenye mtazamo wa mbali tunajua ni kiini macho.
 
KUMBE WAPINZANI MNANUNULIKA!!!
Kwa hiyo mkiiongoza nchi na mkapewa pesa ya kutosha mtaiuza nchi!!!

Mengine ni aibu kuyasema. Kama mnanunulika ni aibu hivyo ficheni hiyo aibu kwa kutosema.

Huna hoja wewe, nchi iuzwe mara ngapi? Kuna mikataba 16 aliingia JK na wachina muda mfupi kabla ya kutoka madarakani. Unajua mikataba ile ilisema nini?
 
Kwa haya maelezo yako ndio maana nakuambia hakuna vita vya rushwa nchi hii.
Hamna kwa mtazamo wako lkn takwimu zinaonyesha rushwa imepungua na watumishi wengi wa kada za chini wanafungwa kila kukicha lkn kesi nyingi ziko mahakamani katika stages tofauti.
 
Hilo hutokaa ulione, ikifika 2020 mwezi marchi watapandishwa watu kizimbani kisha ikifika wakati wa kampeni itumike kama kick kwamba kuna kupambana na rushwa. Lakini wenye mtazamo wa mbali tunajua ni kiini macho.
Endelea kutabiri kazi inachapwa na wengi wamefungwa.
 
Hamna kwa mtazamo wako lkn takwimu zinaonyesha rushwa imepungua na watumishi wengi wa kada za chini wanafungwa kila kukicha lkn kesi nyingi ziko mahakamani katika stages tofauti.

Hizo takwimu za kuonyesha rushwa zinapungua ziko toka enzi na enzi, na hao watumishi wa kada za chini wamekuwa wakifungwa kwa rushwa mara zote. Angalia taarifa za enzi za JK utaona kupungua kwa rushwa na watu kufungwa. Simply hakuna jipya. Narudia tena huu utetezi wako unaotoa hapa ni kama unachekesha walionuna.
 
Huu ni zaidi ya utoto na ulemavu wa kukosa tafakuri... Haya yanayoendelea nchini nikiri wazi kuwa pamoja na kwamba kuna matukio ya kutisha ya kuwashambulia wapinzani kwa silaha za moto na silaha nyingine zenye kujeruhi na kusababisha ulemavu....

Lakini hili la kutumia ushawishi wa ahadi za mali pesa vyeo na ulinzi kwenye bishana ili watu warejee ccm ni uhuni na michezo ya kitoto kabisa

Tusijaribu kuwaiga Rwanda.... Ukubwa wa ile nchi ni sawa na mkoa mmoja wa Tanzania... Tusiige zile siasa kuna kuna mvutano wa makabila mawili... Siasa za pale zinahusika sana na ukabila
Tumeshashuhudia yaliyotokea kwenye uchaguzi wa madiwani hivi karibuni, watu wameumizwa sana.. Watu wamejeruhiwa sana, watu wamebambikiwa kesi sana... Hii ni ishara gani kwenye uchaguzi 2020?(kama utakuwepo lakini) tofauti ya hoja ndio tuumizane kiasi hiki? Vyombo vyetu vya usalama na tume ya uchaguzi vimevaa miwani ya mbao

Kama hii haitoshi pamoja na kufanya yale yote kwenye uchaguzi ule sasa ni mwendo wa kununua wapinzani... Naamini kuna kundi kubwa sana ndani ya ccm wanashangazwa na haya lakini hawana pa kusemea.. Hawa wanaonunuliwa wanaenda kutupwa huko... Ni uchoyo na ulafi wa aina yake... Ni sawa na kuwa na makabati ya nguo lakini bado unataka na za jirani....

Hawa wanaonunuliwa hawaendi kuonyesha vipawa vyao huko, wanaenda kuminywa na kufichwa ili mradi tu kukomoa kaliba fulani ya watu...

Hivi kipaumbele ni kuua upinzani? Ingekuwa mashindano yako hivyo kusingekuwa na kushindana basi... Tunapoteza muda mwingi kwenye siasa za kipuuzi kabisa.. Mwisho wa siku morali wa kujenga taifa unashuka kabisa.... ccm halisi wanabaki na kinyongo, ccm makinikia wanakuwa na hofu na kutojiamini.... Mwendo mpya wa kuwindana kusimangana na kuchomeana unaaza.... Ni aina gani hii ya siasa mnafanya?

Mtanunua wangapi? Mtawabana wangapi ili waombe Po na kujiunga nanyi? Kumbukeni kuna kura million 6 +, tena hizi mmezitamka nyie... Uhalisia ni kwamba zipo zaidi ya hapo tena kwa mbali sana....

Tunawakemea kwa sauti ya uzalendo hamjengi bali mnabomoa, hamtengenezi bali mnaharibu.. Hamuunganishi bali mnatenaganisha.... Huu ni uwendawazimu na kukosa tafakuri... Hivi mmesahau kuwa WAKATI SI MILELE?!?!??
Ww sio mzalendo kabisa
 
Hizo takwimu za kuonyesha rushwa zinapungua ziko toka enzi na enzi, na hao watumishi wa kada za chini wamekuwa wakifungwa kwa rushwa mara zote. Angalia taarifa za enzi za JK utaona kupungua kwa rushwa na watu kufungwa. Simply hakuna jipya. Narudia tena huu utetezi wako unaotoa hapa ni kama unachekesha walionuna.
Unataka iishe kabisa? Inawezekana lkn ni ngumu sana kwa sab mpk sasa hakuna nchi iliyoweza kumaliza rushwa duniani tunapishana viwango tu. Wewe subiri mnyeti akamatwe kwani ndio kipimo chako pekee cha kupambana na rushwa nchini.
 
Back
Top Bottom