CCM ilivyo sasa haiokoleki wala haibebeki hata kwa Machela!

CCM ilivyo sasa haiokoleki wala haibebeki hata kwa Machela!

Na si lazima vijana tukubaliane na mawazo yako Kuntakinte. Hatuwezi kupigana kuiokoa CCM kwa nini unatutaka tuiokoe CCM ambayo haijawahi kutujali katika uhai wake na inatutaka tuiokoe ikiwa mfu. inaweza kurudi vibaya zaidi ikatumaliza kabisa.

Mkuu MpigaFilimbi heshima mbele,

nimekusoma mkuu na napenda kusema kwamba sijamlazimisha mtu akubaliane na yale ninayoyasema au mawazo yangu ila cha msingi ili kuimarisha mapambano haya lazima kuwe na hoja mbalimbali na zitakazotupa dira ya nini kifanyike na sio kukaa tuu kusema hewala kwa kila kinachosemwa lazima tuwe na mchango wa mawazo na sio mtu mmoja ndio atawale fikra za watu wote na kumpongeza kiunafki, tusiwe wavivu hata kwenye kufikiri au kuchangia (kuchangia sio lazima kuwe positive na mada husika)
 
Mageuzi yanaletwa na wananchi, tusitegemee CCM itajibadilisha yenyewe hapo ilipofikia inahitajika outside force kuibadilisha.

CCM imegeuka daraja linalotumiwa na watu wasiokuwa na nia njema na nchi yetu kupata nafasi za uongozi. Mageuzi ya uhakika yataanzia kwenye root cause, kuweka vigezo ambavyo vitazuia watu wa aina ya Rostam Azizi, Kigoda, Sumaye, Mkapa, Lowasa and the rest kuqualify kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama na serikali.
 
Nimekupata sana mkuu. Naomba nijibu kama ifuatavyo;

1. Kwenye hoja namba moja kama ilivyokwenye bold sikumaanisha kila mtu agombee ila nilichokuwa namaanisha moja ya njia katika mapambano ya katika vita hii ni kuingia kwenye hizo nafasi ambazo wanatumia mafisadi kwa maana kwa kukaa nje na kubwabwaja tuu hakusaidi inakuwa kama kelele za Mbu nje ya Chandarua kuna msemo "unasema kama huwezi kushindana nao basi jiunge nao" lakini kichwani unajua unafanya nini

Ukishindwa na watu wanaofanya uovu na wewe utakuwa mwovu ukijiunga nao katika uovu wao huku "kichwani unajua unafanya nini". Kuna mambo ya kujiunga nao na mambo ya kuwapinga. CCM sasa hivi kimesimama kama adui wa demokrasia na jamhuri yetu; kujiunga nao ni usaliti wa taifa.

2. Bold ya pili, ni kweli ninaweza ninaweza nikawa na mtizamo finyu ila lazima hapa tukubaliane kwamba vita hii lazima watu tujiamini ndani ya mioyo yetu na sio kuongea ongea tuu, utashi na kuthubutu ndio nafikiri jambo la msingi zaidi kwa Tanzania yetu ya sasa.

wengine tumethubutu na kujiamini katika vita hii; wale wasiothubutu au kujiamini wamebakia kujiumauma meno. Hii ni vita ya uhai wetu kama taifa; we can not afford to lose.

3. CCM kiukweli inaokeleka na napenda kurudia hapa CCM INAOKOLEKA na kwa yeyote anayefikiri haiokoleki alete mbadala wake napenda ni nukuu "Kupigia kelele Ufisadi na hata kuiombea CCM ianguke na kumeguka, hakutaleta mabadiliko ya maendeleo Tanzania" by Rev Kishoka

condition inasema " ilivyo sasa" na ninakuhakikishia kwa jinsi ilivyo sasa haiokoleki.

4. Kuhusu hao mafisadi wanne ambao unasema wanatikisa Taifa je unawajua na kama unawajua ni wakina nani? Na je unaushahidi wa kupelekea wao kupelekwa mbele za haki kujibu tuhuma maaana nafikiri utakuwa umesaidia kwa njia moja ama nyingine kurahisisha mapambano ya vita hii na pengine tukashinda jumla?

Siyo mimi niliyetaja idadi ya mafisadi; mimi nimerudia tu. Ninachojua kwa uhakika kuwa ufisadi katika taifa letu umepandwa, kupaliliwa na utawala na mfumo ulioundwa na CCM. Na hivyo, ufisadi ni mtoto wa damu wa utawala wa CCM, na CCM haiwezi kumkana ati kwa vile mtoto kageuka ameanza kuiba hadi vya nyumbani!

5.Mimi naogelea vijana sisi na sio wale wa TANU ukiachilia mbali hawa wazushi wa chahche waliopo sasa

Vijana ni vijana tu; wakiwa wazushi au vinginevyo. Kama kinachoangaliwa ni "ujana" tu basi wapo wengi na CCM inayo hadi Jumuiya yake kama vile vyama vingine navyo.

6.Kuhusu issue ya fikra mimi hapa kweli tupo pamoja kabisa na wala sina pingamizi juu ya hili ila sasa tukubaliane sio kila mwenye fikra anaweza kuiweka kwenye matendo hasa kwa watanzania kwahiyo mbali na fikra lazima tukubaliane kwamba lazima kuwe na mapinduzi ndani ya mioyo yetu binafsi kama ulivyofanya ripoti ya meremeta nafikiri kwa upande mwingine itakuwa imeiokoa sasa CCM kwa kujua wapi panaa udhaifu na wapi wajipange vizuri ili upuuzi ule usijetokea tena.


no comment

CCM INAOKOLEKA KWA SASA KAMA KUTAKUWA NA MAPINDUZI BINAFSI YA MIOYO KWA KILA MWANANCHI NA FIKRA

Labda unamaanisha mapinduzi ndani ya wana CCM; na unasema inaokoleka na unaweka condition kuwa "kama kutakuwa"; Mimi nimesema ilivyo sasa "sasa" yaani kama hakuna mabadiliko yoyote haikoleki; unakubali?
 
Ni kwanini Ccm wajadili mambo yanayotokea bungeni na wasijadili sera zao? hii inaonesha kwamba hata haya matawi ya kijiweni yanafunguliwa huku ulaya na kwingineko ni moja ya mkakati wa kuwanyamazisha watanzania maana kila atakeye jiunga na matawi haya ya nje inabidi akaubaliane na masharti ya uanachama ikiwemo kukubali maamuzi ya kamati kuu inayotaka kunyamazisha makamanda wa kupanda na ufisadi...
 
Katika TAASISI na ASASI za UMMA zenye nguvu kabisa NCHI hii CCM ni mojawapo. Inazidiwa kidogo na asasi za kidini na taasisi nyingine ambazo zipo kwa nguvu za kisheria na KATIBA yetu.
Dhana kwamba CCM haiokoleki hainikai vizuri akilini kwa sababu sioni inahitaji kuokolewa kwa LIPI HASA? Ninachofahamu mimi ni kuwa baadhi ya VIONGOZI wake ndio ambao hawaokoleki hata wafanyeje. Mmoja wao ni EL ambaye nadhani alipaswa kuelewa tokea mwanzo kuwa hakustahili kuwa WM wetu. Akajisahau. Akaangalia yule tu aliyemteua. JK alituduwaza sana baadhi yetu kwa kumteua huyu bwana kwenye nafasi ile nyeti. Hivyo ndivyo ilivyotokea hata kwa uteuzi wa Makamba. Uteuzi ambao nadhani ulitokana na "UTIIFU" wake kwa wanaomteua. Huyu mzee naye ni wa kuondoka tu aidha kwa kujiondoa mwenyewe kwa visingizio vyovyote vile au kama alivyoondolewa Gama.
CCM ina MIZIZI mizito kwa Watanzania hata kwa tusio wanachama wake.
 
Anayelala usimuamshe maana utalala wewe. Hakuna kitu kibaya kama kulewa madaraka. Ubaya wake unatokana na sababu kuwa mara nyingi inawezekana facts zikawa overlooked.
Nilipokua na kua USSR na Eastern block zilikuwa na nguvu sana. Niliwaona watu wema na sikuwahi kujiuliza mambo yao ya ndani yalikuwaje. Kama ilivyo kawaida ya mficha maradhi, hawa jamaa walikuwa busy kuonyesha dunia kuwa mambo yao yalikuwa safi. Ila taratibu internally, weakness zao ziliwafanya wakasambaratika. Walikuwa na maguvu..nani hakumjua raisi wa Romania? Au uwezo wa KGB? Ila KGB haikuweza kuzuia kusambaratika kwa USSR.
Kama leo chama tawala kitasahau kipo madarakani kwa ajiri ya wananchi wote, basi kitakuwa kimefanya kosa kubwa. Wapenzi na wanachama wanataka kuona mabadiliko na haya yanayoendelea sasa naona kama yanalenga kuwalinda wahalifu wachache tu. Itakuwaje watu wakichoka kwa ajiri ya umasikini na ugumu wa maisha kila kukicha huku wachache wakila na kuvuna wasichopanda, huku wakilindwa na watawala wetu?
Mwenye macho haambiwi ona. Mambo yanabadilika na hili halihitaji baraka za NEC au CC. Ni watu watakaoamua. Watu wana nguvu kubwa!!! Ni watu waliobomoa ukuta wa Berlin...ni watu waliosambaratisha USSR...na ni haohao watu watakaoibadili Tanzania bila kujali anayeongoza anatetea nini kama ikibidi.Tusitoe huo mwanya maana inaweza tokea
 
Sio kila anachosema MKKJ na gazeti la Mwana Halisi tukubaliane nacho.

Hapa lazima tukubaliane kwamba CCM inaweza kuokoleka pale vijana tutakapoamua kwa pamoja na wananchi wote kwenye ngazi mpk za vitongoji kuubadili utawala huu uliopo sasa.

Tatizo vijana tumekuwa waoga na wengi wetu ni wanafki tunabwabwaja tuu bila vitendo natoa pongezi sana kwa Mwakalinga aliyeamua kwenda kupambana ameonyesha jinsi gani kakomaa na mapinduzi yanawezekana sasa ule ndio mfano na sio kusema HAIKOLEKI hizi ni lugha za kibwanyenye hao mafisadi ni binadamu kama sisi sasa kwanini wasibadilike ikiwa ni sisi hao hao ndio tunawapigia kura tena bahati nzuri mwakani tena tunayo nafasi.

Tusiwe na Mawazo mgando, muda wa Mapinduzi na Uhuru umewadia (refer to MKJJ's thread https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/36225-2010-ni-mwaka-wa-uhuru-wetu.html) na vijana na wananchi kwa ujumla sasa hivi ndio tunatakiwa kuonyesha kwamba tumechoka kwa maneno na sasa ni vitendo.

Seems rafiki yangu hoja ya MJJ hujaielewa,naomba uisome ndo ukosoe,hata wewe pia una hoja muhimu hapo,MJ anonyesha CCM ilipo kwa sasa haiokoleki, na kuwangoa hawa jamaaa ngumu,vijana wenyewe wamewekwa huko na hao mafisadi,kagombee hata ujumbe then uwe tofauti nao uone km unapata chance.Hapa ni kwamba bora CCM ifariki,iibuke upya na watu wenye kuthubutu,lakini taifa libaki limesimama na liendelee!!!MKJ tunawakilisha mzee
 
Sio kila anachosema MKKJ na gazeti la Mwana Halisi tukubaliane nacho.

Hapa lazima tukubaliane kwamba CCM inaweza kuokoleka pale vijana tutakapoamua kwa pamoja na wananchi wote kwenye ngazi mpk za vitongoji kuubadili utawala huu uliopo sasa.

Mzee Mwanakijiji hongera kwa uchambuzi wako makini. Aluta Continua.

Mkuu Kuntakinte siwezi kulaumu msingi wa imani yako lakini ni vizuri iwapo utajua machache tu kuhusu kasoro ya imani yako kuwa Vijana wa kibongo wanaweza kuiokoa CCM na kuleta mabadiliko. Hebu fikiria:

Je ni vijana hawahawa wanaotafuta A's za wizi kwa kuiba mitihani?

Je ni vijana hawahawa wanaoamini kuwa huwezi kufanikiwa bila ya kuiba?

Je ni vijana hawahawa waliozaliwa na mafisadi?

Je ni vijana hawahawa wanaowaza nyimbo za bongofleva all the time?

Je vijana hawahawa waliofundishwa na walimu wasiojua maana ya uzalendo?

TAFADHALI HEBU FIKIRIA UPYA.
 
Ukimpenda mtoto wako kwa kiwango nachokiona hapa, naamini hata kama ni mwizi utaendelea kumtetea tu. Kuna watu hapa hawataki kusikia kuwa CCM haiokoleki, mimi sijui kwa nini? Tawala zote zilizokuwa na nguvu nyingi duniani zilipoanza kutenda kinyume na mapenzi ya mungu huo nio ulikuwa mwanzo wa kuanguka kwake. Kuna dalili za wazi kuwa mamlaka zote za juu za CCM zimeamua kutenda kinyume na mapenzi ya mungu.

Kwa muda wa miaka minne sasa hakuna maamuzi yoyote mazito yamefanywa na hivi vikao vikuu vya chama na hata raisi mwenyew hajafanya maamuzi yoyote mazito, mambo ya kufanyia maamuzi wote tunajua yako mengi sana. Taifa linaonekan kulegalega kwa sababu ya kutokufanya maamuzi hayo.

Katika hali ya namna hii, hata mwananchi wa kawida kabisa ameshaanza kuona mapungufu haya. Hizo ni dalili mbaya kwao, wanahitaji watu wenye hekima na busara nyingi kuwasaidia.

Miaka hamsini, pengine ni umri wako wewe unayeitetea CCM, hakuna kitu. kwa nini tusiijaribu CUF kwa miaka Mitano? Kwanini Tusiijaribu Chadema kwa Miaka mitano?

Kuna wana CCM wengine wamegundua hili na tayari wamejipanga kuwa na mwelekeo tofaouti, wamekubali kuwa kama wamarekani KWANZA TAIFA HALAFU CHAMA BAADAE. Nawashauri wale wanaoonyesha msimamo mkali hapa juu ya kuitetea CCM waliangalie hili linaweza kuwa wazo mbadala.
 
Ni maiti iliyowazi, imekaa porini kuda mrefu, inanuka, kweli machela haifai hapa, maana njia nzima itanuka na kusababisha magonjwa, inahitaji special equipments kuibeba na kuizika, wakati wa kuzika itazikwa shimo refu zaidi kama vile una dispose nuclear waste, maana hatutaki athari zake ziendelee katika jamii!
 
Wazee wakiwapa fedha ndogo tu za kuzibulia mademu vijana mnafyata kama kwamba mmeahidiwa nusu pepo.
Sijui ni kijana gani ndani ya CCM ambaye hajakumbwa na upepo mbaya wa jini Mahaba Ngawila.
Vijana wa CCM ni misukule wa kujitolea.
Unakatwa ulimi wako ili uchicheme tena kwa kuahidiwa fedha na madaraka. Hayo mapinduzi mtayaanzisha na kuyaendeleza kwa ndoto zenu na uroho wenu????

Kwanza umoja wenu wa vijana wa CCM umeingiliwa kwa nyuma na Mizee yenye misuli minene ya kiCCM. Hakuna anyefurukuta ndani ya umoja huo bila kuwa kipenzi cha minunda ya CCM.

Jinasueni kwanza kutoka katika makucha ya Mafisadi wenye kuungwa mkono na CCM ndipo mtatangaza mapinduzi ya kweli.

Wa-Madilu taratibu basi! moderators can kick your....b#*t, ila umenifurahisha kwa lugha fasaha na pallatable one
 
Hoja ina nguvu sana, CCM iko kwenye wakati mgumu sana, na uongozi wa juu ndio tatizo kubwa, uongozi umekuwa dhaifu sana, hauwezi kukemea, hauwezi kutoa tamko lolote dhidi ya uovu wa viongozi wake, ni kulindana tuuuuu na kila mtu kuangalia maslahi yake;
kuna vitu vya kukufanya mtu ufukilie kwamba hili analosema MMJJ lina ukweli:
1. tazama uongozi wa juu wa CCM...nani msafi?? nani wakumuuliza mwenzie..mkapa?? chenge??? JK??
2. angalia maamuzi yasiokuwa na msingi, kwanini leo hii Spika awekwe kitimoto kwa makosa ambayo walifanya wanachama wa CCM?
3. lini CCM iliwakemea mafisadi..EL,RA,AC...si bado wapo kwenye nafasi zao??? na bado wanaendelea kuwasafisha...na hao ndio wenye sauti kwenye chama.

lazima tukumbuke samaki mmoja akioza....CCM sasa inanuka uozo kwakuwafuga viongozi waozo na njia pekee ya kukiokoa chama hiki ni kukiua tu na kuanzisha chama kingine..tuangalie wenzetu wakenya?? na njia ya kukiua ni kwa wale wasafi kuthubutu kutoka ndani ya chama kile na kujiunga kwingine na kuwaacha wale ving'ang'anizi humo tuone kama hakijabaki kuwa kana KANU....
wakati kama huu ndio ungekuwa muafaka kwa Spika Sita kujitoa CCM, namuhakikishia lazima tumpe uraisi popote atakapo kwenda...tunafanya jitihada za kumshawishi...umejitahdi kuonyesha uongozi mzuri.

"ripoti ya meremeta bungeni november"...
 
Mwanakijiji sina tatizo kabisa na makala zako zote za JF na zingine zote, isipokuwa mara chache nitakuwa nikitofautiana nawe pale nitakapo ona dhamira yangu yanituma hivyo. kitendo cha CCM kuona kwamba kuna mchwa wanaotaka kukibungua na kuamua kuitana /kukalishana/kuonyana ni kitendo cha kijasiri kwa chama/ taasisi au kikundi chochote kile vinginevyo utakuwa ni wehu uliotukuka kuona kuwa taasisi inakaribia kuparaganyika kwa kusababishwa na mmoja wenu au wenzenu nanyi mkaamua kukaa kimya bila bila kufanya tafakuri jadidi. walichofanya CCM ndicho kinacho stahili personal nawapongeza sana japo yawezekana walichokifanya wewe na wengine wengi msifurahishwe.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
 
Ndani ya CCM kuna watu wanaipenda Tanzania kwa dhati na wana uchungu wa kweli na nchi. Nina amini hawa watu watamegeka ama wataiacha CCM na kujiunga na wanaharakati wanaopinga uchafu unaofanywa na CCM. Vyombo vyote vya ulinzi Tanzania ni mali ya CCM na wala si mali ya watanzania ingawa vinaendeshwa kwa gharama za watanzania. Na katika vyombo hivi vya ulinzi bado kuna watu wana uchungu na nchi yao na bila shaka wangependa kabisa kujiunga na wanaharakati katika kupinga uchafu unaofanywa na CCM lakini kwa namna moja ama nyingine wamepigwa mkwara. Ila kuna siku kila kitu kitabadilika kwani huwezi kushindana na nguvu ya ukweli na haki.

Wabunge ndani ya CCM mnaopinga ufisadi eleweni kwamba hamkuzaliwa na CCM, kuicha CCM haitakuwa mwisho wa uhai wenu bali itakuwa ni mwanzo wa kukubalika kwa wananchi wenye uchungu na nchi hii, ni mwanzo mzuri wa kuanza mapambano ya kweli ya kuelekea kutafuta uhuru wa kweli wa nchi yetu. Iacheni CCM mara moja bila ya kujali mapesa mnayoyapata huko bali jalini uzalendo na haki.
 
Na si lazima vijana tukubaliane na mawazo yako Kuntakinte. Hatuwezi kupigana kuiokoa CCM kwa nini unatutaka tuiokoe CCM ambayo haijawahi kutujali katika uhai wake na inatutaka tuiokoe ikiwa mfu. inaweza kurudi vibaya zaidi ikatumaliza kabisa.
Tunahitaji kuwa majasiri ndiyo, lakini si kwa kuiokoa CCM ni kuipigania nchi yetu na uhuru wetu uliopokwa na wakoloni CCM na genge lake. Kwenda kujiunga huko si hatua ya mapambano hata kidogo.

Ahsante sana kwa mawazo yaliyojaa hekima na busara. Hakuna umuhimu wowote wa kuiokoa CCM chama kilichojaa mafisadi. Watanzania waweke jitihada za kuiokoa CCM kwa lipi hasa ambalo CCM imelifanya hata kustahili kuiokoa. Hata Muasisi wa CCM Mwalimu kama angekuwa hai asingepoteza muda wake kutaka kuiokoa CCM chama ambacho hakina dira na kukosa mwelekeo.. Sasa hivi wako radhi kuwakumbatia mafisadi kwa nguvu zote bila kujali maslahi ya nchi.
 
Ndani ya CCM kuna watu wanaipenda Tanzania kwa dhati na wana uchungu wa kweli na nchi. Nina amini hawa watu watamegeka ama wataiacha CCM na kujiunga na wanaharakati wanaopinga uchafu unaofanywa na CCM. Vyombo vyote vya ulinzi Tanzania ni mali ya CCM na wala si mali ya watanzania ingawa vinaendeshwa kwa gharama za watanzania. Na katika vyombo hivi vya ulinzi bado kuna watu wana uchungu na nchi yao na bila shaka wangependa kabisa kujiunga na wanaharakati katika kupinga uchafu unaofanywa na CCM lakini kwa namna moja ama nyingine wamepigwa mkwara. Ila kuna siku kila kitu kitabadilika kwani huwezi kushindana na nguvu ya ukweli na haki.

Wabunge ndani ya CCM mnaopinga ufisadi eleweni kwamba hamkuzaliwa na CCM, kuicha CCM haitakuwa mwisho wa uhai wenu bali itakuwa ni mwanzo wa kukubalika kwa wananchi wenye uchungu na nchi hii, ni mwanzo mzuri wa kuanza mapambano ya kweli ya kuelekea kutafuta uhuru wa kweli wa nchi yetu. Iacheni CCM mara moja bila ya kujali mapesa mnayoyapata huko bali jalini uzalendo na haki.

Hapa mkuu naungana na wewe kwa kiasi kikubwa umesema kweli kabisa.
 
Samweli Sita & co simameni imara na hakuna sababu ya kuyumba wala kuomba msamaha. Kuwaomba msamaha mafisadi & co ina maana mmeamua kukubaliana nao na kuungana nao katika machafu yao. Rudisheni kadi zao na waachieni CCM yao ambayo inatumbukia shimoni.
Jiungeni na vyama pinzani ili kuongeza nguvu na bila shaka mtarudi bungeni kwani wananchi tulio wengi tumeona na kuridhika na kazi zenu, na ni sisi ndiyo tunapiga kura na kuchagua.
Kubaki kwenu ndani ya CCM kunatupa hofu na mashaka juu yenu, imani yetu kwenu imepungua kwa maana tumeelewa kwamba mmeamua kujiunga na mafisadi ili kutumaliza.

CCM si mzazi wenu, bali ni chama cha siasa kama Chadema, CUF nk.

Hiki ni kipimo cha kweli kuona kama mna uzalendo wa kweli ama kelele mlizokuwa mnapiga kuhusu ufisadi ni za kweli ama mlikuwa mnatuzuga.

Chagueni kweli na haki ama mapesa ya CCM na kushibisha matumbo yenu.
 
What i can say is that MMKJJ is in the right path!Keep it up
 
Hapo ndugu yangu mwankijiji nakukubali kabisa

Hayo ndio mawazo tunayo yahitaji
 
Back
Top Bottom