CCM ilivyo sasa haiokoleki wala haibebeki hata kwa Machela!

Mwanakijiji sina tatizo kabisa na makala zako zote za JF na zingine zote, isipokuwa mara chache nitakuwa nikitofautiana nawe pale nitakapo ona dhamira yangu yanituma hivyo. kitendo cha CCM kuona kwamba kuna mchwa wanaotaka kukibungua na kuamua kuitana /kukalishana/kuonyana ni kitendo cha kijasiri kwa chama/ taasisi au kikundi chochote kile vinginevyo utakuwa ni wehu uliotukuka kuona kuwa taasisi inakaribia kuparaganyika kwa kusababishwa na mmoja wenu au wenzenu nanyi mkaamua kukaa kimya bila bila kufanya tafakuri jadidi. walichofanya CCM ndicho kinacho stahili personal nawapongeza sana japo yawezekana walichokifanya wewe na wengine wengi msifurahishwe.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!

Hakitadumu tena kamwe Mzee usijidanganye labda ujifariji kwa kuwa wewe ni sehemu ya tatizo ndani y'a Chama chenu poleni...! Chama chenu hakiokoleki kabisa,,,,!
 
Kabla mkutano kuanza rasmi, mtangazaji wa
kituo cha television cha TBC1 (kituo
kilichojigeuza kuwa cha CCM huku kikichukua
ruzuku ya serikali ya Watanzania wote), kilikuwa
kikiwahoji wajumbe mbalimbali wa mkutano
huo.
Wote waliohojiwa walionekana wanaipenda
sana CCM na kwa siku ya jana walidai kuwa na
furaha na matumaini makubwa. Walitumia
nafasi hiyo kuwaalika watanzania mbalimbali
hasa waliowahi kuwa wanachama wa chama
hicho waliohamia upinzani warudi.
Maelezo yao ni kwamba hakuna chama kingine
mbadala wa CCM katika kuliongoza taifa hili.
Mmoja alimgusia Mbunge wa Maswa Mashariki,
John Shibuda (CHADEMA) akisema yeye kaona
na kasema kweli kuwa huko alikohamia hakuna
lolote.
Lakini kilinichofanya niandike makala hii ni
sababu walizozieleza wanachama hao wa CCM
kama chanzo cha matumaini yao makubwa na
furaha mioyoni mwao.
Katika hali ya kushangaza, wote walisema
wamefurahishwa sana na hotuba ya Mwenyekiti
wao ambayo walisema ilikuwa nzuri sana na
imehitimisha makundi ndani ya chama.
Wakasema kilichowafurahisha zaidi ni
kupendekezwa kwa Philip Mangula kuwa
Makamu wa Mwenyekiti Taifa kwa upande wa
Tanzania Bara.
Wana CCM bwana! Kuna wakati niliwahi
kupendekeza kwamba pengine siku nchi hii
itakapopata ukombozi wa pili ambao sote
tunaulilia kuwe na haja ya kuwachukua baadhi
ya viongozi wakuu wa CCM wa enzi hizi na
baadhi ya makada na wanachama wao
waliobobea kujaribu kupima akili zao kama ziko
sawa.
Maana kuna uwezekano wa kuwa tunawapigia
kelele na kuwarushia tuhuma kila siku kumbe
wenzetu wanafikiria kwa kutumia ‘masaburi’
badala ya vichwa! Ama kule vichwani sehemu
za ubongo zinazohusika na mahesabu na
utambuzi (kwa kiingereza ndo naifahamu vizuri
kama Arithmetic and Logic), ziliondolewa
wakiwa kwenye hospitali za wazungu nje ya
nchi wakabakiziwa sehemu za ubongo
zinazohusika na kuimba na kucheka tu.
Hakuna Mtanzania asiyejua kwamba
Mwenyekiti wa Taifa wa CCM ambaye pia ni Rais
wa nchi huwa anaongea asichomaanisha. Wengi
tuna uzoefu wa hotuba zake alizowahi kuzitoa
akiwa ‘serious’mpaka tukadhani rais ni huyu
kumbe alikuwa atulisha upepo.
 
Kwa hakika adui yako muombee Njaa.

Hongera Mwanakijiji. Wasi wasi wangu usiwe ule wa Fisi kumfuata mwan'Adam kwa kufikiri kuwa ipo siku mikono yake itadondoka nae apate kitoweo.

Pole sana.
 
Nnapoikumbuka ccm ya zamani iliyokua na waadilifu kama hayati baba wa taifa Mwl. JKN, E.Sokoine, R.Kawawa, J.Warioba, J.Butiku and the likes.

Sijamgusia Mh. K.Mwiru kwanza amechelewa kupumzika na na siasa kama niliowataja hapo juu matokeo yake amekutana na ccm digitali mwishowe kajikuta mpaka anapewa uwakilishi wa witch doctors ndani ya BMK.

Nikiiangalia ccm ya sasa yenye mmomonyoko mkubwa wa maadili najikuta naona giza tu mbele. Yaani najua nitokako, ila sijui nilipo wala niendako. Ccm hii ina vichwa kama Nape, A.Kinana, Le Captain J. Komba, Masatu W, D. Sanga & the likes. Hii ya sasa imejaa wapotofu wa maadili, wapiga dili wachumia tumbo. Humu uadilifu ni sifuri kabisa, hawa hata kwenye chaguzi zao ziwe za ndani ya chama nyinginezo hawashindi bila rushwa baadaya hopo ni kupiga dili mwanzo mwisho.
 
Bila kumsahau mjumbe wa baraza la wazee Le Mutuz System , yaani hiki chama magumashi matupu !
 
Loh Mwanakijiji maneno ya miaka mitano iliyopita yanaishi hadi leo kweli ulichokisema
 
Nikisoma post hii nakumbuka ile hadithi ya fisi anayetembea sambamba na mwanajeshi anayekwenda mwendo wa "shoto kulia shoto kulia" akidhani kwamba mikono ya mwanajeshi inakaribia kudondoka ili apate mlo.

Ndo walewaleee!
 
Kwa hakika adui yako muombee Njaa.

Hongera Mwanakijiji. Wasi wasi wangu usiwe ule wa Fisi kumfuata mwan'Adam kwa kufikiri kuwa ipo siku mikono yake itadondoka nae apate kitoweo.

Pole sana.

Kwa hiyo na wewe unaamini ccm itatawala milele! It's naturaly impossible. You should've know this already unless you never went to school. No hard feelings lakini budy
 
Kwa hiyo na wewe unaamini ccm itatawala milele! It's naturaly impossible. You should've know this already unless you never went to school. No hard feelings lakini budy

kama mkiendeleza unafiki kama mlivyofanya katika bunge lenu la Katiba la Mh Sitta basi mjue mtatawaliwa milele.

Kumbukeni kukingoa chama tawala kunahitaji utayari na umakini wa upinzani na kujipanga kwa lolote na kukabiliana nalo kwa nia ya kujikomboa.

pole sana
 
Back
Top Bottom