CCM ilivyo sasa haiokoleki wala haibebeki hata kwa Machela! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM ilivyo sasa haiokoleki wala haibebeki hata kwa Machela!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 19, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 19, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  CCM ILIVYO SASA HAIOKOLEKI (MwanaHalisi)
  Na. M. M. Mwanakijiji

  Kuna watu ambao kwa makosa ya fikra zao na kiburi cha utamu wa madaraka na hasa wale waliopigwa ganzi ya ufisadi wanaamini katika mioyo yao kuwa CCM itadumu milele. Hawa pamoja na vikaragosi wengine wa ufisadi wamejiaminisha katika upotofu wao kuwa Chama hiki cha Mapinduzi kitatawala milele, kitadumu milele na kitaendelea kuwa kama kilivyo sasa milele. Hawa ni wa kuwekewa mikono na ikibidi kupepewa huku wanavutwa masikio.

  Leo niendelee kuwa mjumbe wa habari mbaya. CCM ni mazao ya binadamu; ni chombo kilichoundwa na wanadamu, kimeongozwa na kinaongozwa na binadamu na kutokana hilo tu peke yake CCM inakuwa ni chombo kinachoweza kuharibika, kuvunjika, kuporomoka na kwa hakika kabisa chaweza kuzama. Hakuna ustadi wa mwanadamu unaoweza kufanya kazi zake zisiwe na makosa milele. Katika uelewa wetu huu mdogo wa kibinadamu ni kazi za Mungu tu ambazo hazina makosa.

  Hivyo ninaposikia mtu anasema kwamba hakuna ufisadi ndani ya CCM ninamshangaa. Nikimsikia mtu anasema “CCM ni safi” ninamtumbulia macho kama mjusi aliyekoswakoswa na mlango. Na pale ninaposikia kuna wana propaganda wa CCM ambao wanaitetea CCM kuwa ni chama safi na kina “mafisadi wanne” tu ninafumba macho yangu kwa mshtuko na kama ningekuwa karibu ningemtundika konzi mtu huyo kumgutusha kutoka katika usingizi wake uliochanganyika na ulevi wa madaraka.

  Malumbano tunayoyasikia sasa na kugongana kunakoendelea hivi sasa ndani ya CCM na tutashuhudia zaidi miezi michache ijayo kunatoa ushahidi wa jambo moja kubwa kuwa CCM iko matatani na hakuna mtu wa kuiokoa. CCM haiokoleki.  Jipatie nakala yako hapa chini na isambazwe!!!


  Baadhi ya maoni niliyoyapokea tangu makala itoke leo:


   

  Attached Files:

 2. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2009
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimeufurahia uchambuzi wako mzuri....
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Ok....!
   
 4. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Uwii!!! sasa nianzishe chama changu au nijiunge na nini sijui
  Nimekaanganikiwa bado nikiwa KIJANA sasa anyways

  mie nimependa yanayojiri....
  "Nimekuja kuulizia kuhusu kampuni ya Triennex" - Kanzi:cool:

  "Triennex, what triennex?" Afisa:eek:

  "Triennex" A movie coming to the theatre near you!
   
 5. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sio kila anachosema MKKJ na gazeti la Mwana Halisi tukubaliane nacho.

  Hapa lazima tukubaliane kwamba CCM inaweza kuokoleka pale vijana tutakapoamua kwa pamoja na wananchi wote kwenye ngazi mpk za vitongoji kuubadili utawala huu uliopo sasa.

  Tatizo vijana tumekuwa waoga na wengi wetu ni wanafki tunabwabwaja tuu bila vitendo natoa pongezi sana kwa Mwakalinga aliyeamua kwenda kupambana ameonyesha jinsi gani kakomaa na mapinduzi yanawezekana sasa ule ndio mfano na sio kusema HAIKOLEKI hizi ni lugha za kibwanyenye hao mafisadi ni binadamu kama sisi sasa kwanini wasibadilike ikiwa ni sisi hao hao ndio tunawapigia kura tena bahati nzuri mwakani tena tunayo nafasi.

  Tusiwe na Mawazo mgando, muda wa Mapinduzi na Uhuru umewadia (refer to MKJJ's thread https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/36225-2010-ni-mwaka-wa-uhuru-wetu.html) na vijana na wananchi kwa ujumla sasa hivi ndio tunatakiwa kuonyesha kwamba tumechoka kwa maneno na sasa ni vitendo.
   
 6. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wewe Bwana jifunze Mambo ya CCM kabla hujaanza kuropoka. CCM inawakilisha jamii. sasa jamii gani ambayo haina makundi- kwa mujibu wa Interest zao. sasa kukaa na kujadili interests za makundi hayo ndiyo busara hizo za Chama Cha Mapinduzi. poa moto mwana kwetu.
   
  Last edited: Aug 19, 2009
 7. m

  mageuzi halisi Member

  #7
  Aug 19, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MZEE MWANAKIJIJI PAMOJA NA KUKUFAGILIA NAKUOMBA PIA UJUMUISHE NA HAYA MACHACHE YA KUONGEZEA "Uking'ang'ania umoja bandia na watu wasio na maadili, utaununua umoja huo kwa kupoteza itikadi yako na itakuwa kama gulio tu la kuwakusanya watu wa kila aina wanaotaka vyeo" KWA MTAZAMO WANGU HIVI NDIVYO ILIVYO CCM YA LEO. NINACHOSHINDWA KUELEWA NI KWANINI WAPINZANI WASIKAPILIZE ON THIS ONE? NADHANI WAPENDA MAGEUZI WOTE TUMESHAEARN OUR POLITICAL CAPITAL NA ILIYOBAKI TU NI KUENDELEZA MAPAMBANO HASA VIJIJINI.
   
 8. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  CCM sio haikoleki ,wandugu CCM ishakufa uliobaki ni ubabe wa kulazimisha vyombo vya dola wasizikwe tu,wawepo kwenye uongozi japo maiti.

  Yaani hawa ni sawa na yule nabii aliyekufa mpaka fimbo yake ilipomalizwa kuliwa na mchwa ndipo wananchi majini na mashetani walipotanabahi kumbe alikwisha kufa zamani.Tofauti yao yule alikuwa nabii na hawa ni machinjachinja.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Aug 19, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hili ni kweli.
  Ni "lazima" tukubaliane na hili? Kuwa ndio njia pekee? Hilo litakuwa lengo la kuiokoa CCM au Tanzania?

  Kwanini unafikiri njia pekee ya "kupambana" ni kugombea? Kuna nafasi ngapi za kugombea? Wangapi ambao wamegombea na hawapambani? Mtu hapongezwi kwa kuamua kugombea! anapongezwa kwa kupambana na katika kupambana si lazima mtu agombee. Mtu anayetaka watu wote wagombee ili waoneshe kupambana haelewi maana ya vita! Si wote wanaopigana ni lazima wawe mstari wa mbele au waendeshe vifaru!

  Ni mtazamo finyu.

  Kama kitu hakiokoleki utakuwa ni unafiki kutumia neno jingine ambalo halimaanishi unachotaka kusema. Kama unataka tuamini kuwa inaokoleka sema "CCM inaokoleka". Mtazamo wangu ni kuwa "ilivyo sasa" sasa ni lazima ujifunze kutumia lugha vizuri ninaposema "ilivyo sasa" nina maana ya condition. Kwamba ilivyo sasa haikoleki; wewe unachozungumzia ni kubadilisha "ilivyo sasa".

  Ndiyo sababu hiyo; mafisadi hao "wanne" walioko CCM ndio wanalipelekesha taifa hivi wakifikia watano itakuwaje?

  Kwanini unafikiri vijana wanaweza kubadilisha nchi; wengine si wako humo humo madarakani na wengine waliingia tangu wakiwa vijana? Ujana siyo hoja ya mabadiliko wala uzee siyo kizuizi cha mabadiliko; tatizo ni fikra. Leo hii tunashuhudia "vijana" wakijiunga na CCM kutoka kila kona ya dunia na kuanzisha matawi yake ughaibuni; leo hii tunawaona "vijana" wakibeba mabango kushangilia CCM nambari wani; na ni vijana hao hao ambao hawachelei kuwa wa kwanza kuandamana kuunga mkono msimamo wa chama (usishangae siku chache zijazo zikianza kutokea pongezi toka UVCCM na wengine juu ya msimamo wa chama wa Dodoma na hata maandamano!)

  Ujana siyo hoja kama vile uzee usivyo; hoja ni fikra, msimamo, mwelekeo na mtazamo wa mabadiliko. Ni bora niwe na mzee mwenye fikra za mabadiliko kuliko kijana mwenye mawazo ya kifisadi!
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Aug 19, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Bahati nzuri ninaijua CCM kuliko baadhi ya watu humu, nimekulia na kujifunza katika darasa la chama. Kati ya mimi na wewe mropokaji yu dhahiri.

  kama ingekuwa rahisi hivyo kwanini wakae na kujadili makundi hayo? ni mara ngapi jamii imekaa kujadili makundi yaliyomo ndani yake?
   
 11. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Nadhani Mzee wa kijijini endelea kufanya yake unayo amini itakuwa legacy kwa Nchi yako.Mtu akitaka kukutuna atatukana tu .Wanao kupinga na mawazo yako kwa jinsi unavyo mambo yalivyo ni vijana amba wana himiza kuingia CCM na si kutafuta njia mbadala .Mawazo yanatoka kwa wao wanao kupinga maana you are hitting them so hard .Ndiyo mkono unao walisha lazima waje kwa wingi hapa namadai yao .
   
 12. Kifaru Kajeruhi

  Kifaru Kajeruhi Member

  #12
  Aug 19, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi bwana nakufagilia sana mwanakijiji hebu endelea kutufumbua macho......maana sasa waelewa hasa sisi wasomi tunahamasika sana...ila bado ninaona kuna watu humu bongo lala. big up mwanakijiji.................big up MZEE SIX
   
 13. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Nikisoma post hii nakumbuka ile hadithi ya fisi anayetembea sambamba na mwanajeshi anayekwenda mwendo wa "shoto kulia shoto kulia" akidhani kwamba mikono ya mwanajeshi inakaribia kudondoka ili apate mlo.
   
 14. S

  Shamu JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ushahidi unaonesha CCM itatawala kwa muda mwingi. Kuna mbinu nyingi ambazo CCM wanatumia in order kutawala milele. CCM na Serikali yake walipokubali kuanzisha vyama vingi, kitu cha kwanza walichofanya ambacho bado kinawasadia ni kupandikiza watu wao ndani ya upinzani. Ukiangalia viongozi wengi wa vyama vya upinzani ni "former" CCM. Hii ndiyo mbinu inayowasaida mpaka sasa hivi. Wapinzani waliotaka kuhama bila ya maridhaa ya CCM tayari tumeshawazika, kama Kolimba, Malima nk. Njia iliyobakia ya kuiondoa CCM, ni kuweka viongozi bora ndani ya CCM.
   
 15. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #15
  Aug 20, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Wafuasi wengi wa CCM pamoja na viongozi wao bado hawajatokana na kasumba na ukilitimba wa CHAMA KIMOJA; na ndio maana viongozi wa ccm wanatoa maelekezo kama vile wadanganyika wote ni wanachama wao!! Hata Pakacha hapo juu anasema "CCM INAWAKILISHA JAMII" anasahau kuwa uwakilishi wa CCM ni kwa wanachama wake TU ambao ni percent ndogo sana ya jumuiya ya wadanganyika!Consequently, NEC ya ccm inapotoa maazimio hayo yanakuwa relevant na binding kwa wafuasi wao tu; kwahiyo azimio lao kwamba tumuache Mkapa apumzike kwa amani akila hela zetu alizotuibia, linawahusu mafisadi wenzie wa CCM na sio wananchi tunaotabika na maisha yakizidi kuwa magumu kila leo!!Ninawahamasisha wananchi wazidi kumzomea yeye pamoja na mafisadi wenzie popote anapoonekana kwenye hadhara.
   
 16. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Na si lazima vijana tukubaliane na mawazo yako Kuntakinte. Hatuwezi kupigana kuiokoa CCM kwa nini unatutaka tuiokoe CCM ambayo haijawahi kutujali katika uhai wake na inatutaka tuiokoe ikiwa mfu. inaweza kurudi vibaya zaidi ikatumaliza kabisa.
  Tunahitaji kuwa majasiri ndiyo, lakini si kwa kuiokoa CCM ni kuipigania nchi yetu na uhuru wetu uliopokwa na wakoloni CCM na genge lake. Kwenda kujiunga huko si hatua ya mapambano hata kidogo.
   
 17. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2009
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Asante Mwanakijiji. Umesahau kugusa jambo moja muhimu kuhusu viongozi wa juu wa CCM. Uwezo wao wa kuona na kuchambua mambo ni mdogo sana. Sijui inakuwaje viongozi wa juu kabisa wa nchi tunaowategemea kutoa dira ya maendeleo ya taifa letu wanakuwa na uelewa mdogo kiasi hicho. Jamani!!

  Pili ni kwamba nina wasiwasi sana hii sumu ndani ya CCM imepandikizwa na Rostam. Huyu bwana nimegundua ni mtu hatari na asiyekubali kushindwa kamwe. Amezunguka kila mahali serikalini kurudisha "nafasi yake" na aliposhindwa basi jamaa kahamishia majeshi yake ndani ya chama. Na kwa hakika sasa amem-bana JK kwenye kona. Walau kwa sasa.

  Muanguko CCM ni dhahiri sana kwa sasa kuliko wakati mwingine wowote ule; kwa sababu message hii ya uongozi wa CCM sio kwa Sitta wala kwa wale wabunge mahiri bali ni kwa JK mwenyewe.

  Tujiulize swali; ni kwa nini siku zote za nyuma Mkapa hakudhubutu kamwe kutia mguu ndani ya vikao vya juu vya CCM isipokuwa hiki cha mwisho? Kikwete lazima anajua amewahiwa na amepoteza nguvu zake kama mwenyekiti. Ni heri akubali ushauri wako na kuamua: Liwalo na liwe! Otherwise he is gone!
   
 18. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #18
  Aug 20, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nimekupata sana mkuu. Naomba nijibu kama ifuatavyo;

  1. Kwenye hoja namba moja kama ilivyokwenye bold sikumaanisha kila mtu agombee ila nilichokuwa namaanisha moja ya njia katika mapambano ya katika vita hii ni kuingia kwenye hizo nafasi ambazo wanatumia mafisadi kwa maana kwa kukaa nje na kubwabwaja tuu hakusaidi inakuwa kama kelele za Mbu nje ya Chandarua kuna msemo "unasema kama huwezi kushindana nao basi jiunge nao" lakini kichwani unajua unafanya nini

  2. Bold ya pili, ni kweli ninaweza ninaweza nikawa na mtizamo finyu ila lazima hapa tukubaliane kwamba vita hii lazima watu tujiamini ndani ya mioyo yetu na sio kuongea ongea tuu, utashi na kuthubutu ndio nafikiri jambo la msingi zaidi kwa Tanzania yetu ya sasa.

  3. CCM kiukweli inaokeleka na napenda kurudia hapa CCM INAOKOLEKA na kwa yeyote anayefikiri haiokoleki alete mbadala wake napenda ni nukuu "Kupigia kelele Ufisadi na hata kuiombea CCM ianguke na kumeguka, hakutaleta mabadiliko ya maendeleo Tanzania" by Rev Kishoka

  4. Kuhusu hao mafisadi wanne ambao unasema wanatikisa Taifa je unawajua na kama unawajua ni wakina nani? Na je unaushahidi wa kupelekea wao kupelekwa mbele za haki kujibu tuhuma maaana nafikiri utakuwa umesaidia kwa njia moja ama nyingine kurahisisha mapambano ya vita hii na pengine tukashinda jumla?

  5.Mimi naogelea vijana sisi na sio wale wa TANU ukiachilia mbali hawa wazushi wa chahche waliopo sasa

  6.Kuhusu issue ya fikra mimi hapa kweli tupo pamoja kabisa na wala sina pingamizi juu ya hili ila sasa tukubaliane sio kila mwenye fikra anaweza kuiweka kwenye matendo hasa kwa watanzania kwahiyo mbali na fikra lazima tukubaliane kwamba lazima kuwe na mapinduzi ndani ya mioyo yetu binafsi kama ulivyofanya ripoti ya meremeta nafikiri kwa upande mwingine itakuwa imeiokoa sasa CCM kwa kujua wapi panaa udhaifu na wapi wajipange vizuri ili upuuzi ule usijetokea tena.

  CCM INAOKOLEKA KWA SASA KAMA KUTAKUWA NA MAPINDUZI BINAFSI YA MIOYO KWA KILA MWANANCHI NA FIKRA


   
 19. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #19
  Aug 20, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu Lunyungu heshima mbele,

  1. umeongelea issue ya kutukanwa, naomba niweke sawa mimi nimemuelewa MKJJ vizuri sana ila yale yalikuwa mawazo yangu na sio kwamba nilimtusi na isitoshe nimefurahi ameweza kunijibu vizuri ni katika kuwekana sawa na sio kila unachopewa basi wewe ukawa unameza tuuu.....ni katika kuwekana sawa kuimarisha mapambano dhidi ya vita hii.

  2. haha... kuhusu hitting them, i suppose hukunimaanisha na mimi kwasababu i ve been a fan of Mzee Mwanakijiji since nimejiunga na Jambo Forum kwa hiyo kama ulinimaanisha na mimi hapa nafikiri unaweza ukawa umekosea.
   
 20. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #20
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Wazee wakiwapa fedha ndogo tu za kuzibulia mademu vijana mnafyata kama kwamba mmeahidiwa nusu pepo.
  Sijui ni kijana gani ndani ya CCM ambaye hajakumbwa na upepo mbaya wa jini Mahaba Ngawila.
  Vijana wa CCM ni misukule wa kujitolea.
  Unakatwa ulimi wako ili uchicheme tena kwa kuahidiwa fedha na madaraka. Hayo mapinduzi mtayaanzisha na kuyaendeleza kwa ndoto zenu na uroho wenu????

  Kwanza umoja wenu wa vijana wa CCM umeingiliwa kwa nyuma na Mizee yenye misuli minene ya kiCCM. Hakuna anyefurukuta ndani ya umoja huo bila kuwa kipenzi cha minunda ya CCM.

  Jinasueni kwanza kutoka katika makucha ya Mafisadi wenye kuungwa mkono na CCM ndipo mtatangaza mapinduzi ya kweli.
   
Loading...