CCM iko Mahututi Igunga, inalazimisha Kukohoa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM iko Mahututi Igunga, inalazimisha Kukohoa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by spencer, Sep 21, 2011.

 1. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  GreatThinkers,

  Mapema kabla ya kuanza kampeni niliwaletea thread niliyoipa jina la Kauli toka Igunga' Tope katika maji halisafishwi kwa grisi, Kwa maana contamination huongezeka.

  Watu wanajiuliza, Hivi wanaompigia kampeni Dr. Kafumu ni CCM ipi? Iwapo hata Rostam Fisadi naye kashiriki kumnadi????

  Nimeshuhudia Kampeni za CDM zinajaaa watu makini, vijana na watu wanaotaka kupata msimamizi na mwakilishi wao Bungeni, hawataki mtu wa kwenda kupiga mabenchi na kupitisha hoja, wanamta Kashindye wa CDM

  CCM.A inapata pata vikongwe na watoto wadogo wadogo walio kati ya miaka 4-12 hakika wala si wapiga kura

  CCM.B inapata watu rika la kati wachache ambao hata hivyo hawajaamua kwa wabaki au wapigie CDM, CCM.B imechanganyikiwa inashindwa kujenga hoja Inaogopa kuishupalia CCM.A kwa sababu ni mwambata, inashindwa kuishambulia CDM kwa sababu nguvu ya Umma itawaona kweli wao CCM.B

  CCM Iko hoi Igunga, ni kama Mgonjwa anayepumua kwa mashine halafu anajaribu kukohoa, Wameshakufa kimebaki kivuli. CCM hawapo hai namaanisha kishneeeeey.
   
 2. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #2
  Sep 21, 2011
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Maandishi yako yanawatia moyo wanaotaka mageuzi.
   
 3. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Maneno yake yaonesha anatapatapa.
  OTIS.
   
 4. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Maandishi yake yanaonesha jinsi gani alivyo mtaalamu wa siasa za vichochoroni za kueneza uongo.
   
 5. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Igunga ccm wasipotumia mbinu yao B waandike maumivu
   
 6. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Mimi yangu macho, hivi inawezekana kushinda igunga? kama Mkuu wa polisi wa wilaya kapelekwa na wana-CCM, Polisi wenyewe ndiyo hao, Msimamizi wa uchaguzi wa Wilaya ukimkagua utamkuta ni mkereketwa wa CCM, Tume ya Taifa ya uchaguzi yenyewe imewekwa na CCM kwa maslahi ya chama. CCM hushindwa pale ambapo hata kuiba kura imeshindikana. Mimi msimamo wangu nasubiri chaguzi zitakazo fanywa pindi tutakapokuwa na katiba mpya. Kwasasa katiba iliyopo haifai kwa uchaguzi wa vyama vingi ni katiba ya CCM kwa maslahi ya CCM
   
 7. k

  kinyongarangi Member

  #7
  Sep 21, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tarime walishindwa mbele ya makamba.inawezekana
   
 8. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  WANAZUONI wa Kiislamu nchini wameipa siku tatu Chadema Taifa kulaani kitendo cha wafuasi na viongozi wake kulidhalilisha vazi tukufu la hijab na kumwomba radhi Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario, kwa kumvua sitara yake.

  Wamesema iwapo chama hicho kitapuuza kufanya hivyo na kupita muda huo wanazuoni hao na Waislamu wataiona Chadema kama chama chenye sera na madhumuni ya kuhujumu Uislamu na Waislamu wa Tanzania na kuhimiza Waislamu kukiepuka kama ukoma.

  Kauli hiyo iko kwenye tamko la Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania (HAY-AT) lililosomwa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti Kuu ya Umoja huo, Shehe Sherali Hussein Sherali na kusema siku tatu hizo zilianza jana.

  Wanazuoni hao zaidi ya 10 wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Shehe Suleimani Kilemile, walitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari na kusema baada ya hapo umoja huo utakaa na kutafakari hatua stahiki za kukabiliana na dharau hizo na kuelekeza Waislamu cha kufanya.

  Sherali alisema ifahamike, kwamba shambulio lolote dhidi ya hijab ni dhidi ya Uislamu na Waislamu wote, haliwezi kuvumilika na watakabiliana na yeyote anayetaka kuidhalilisha amri ya hijab iliyo katika Quran sura ya 33:59.

  "Tunataka ifahamike, kwamba yeyote atakayelidharau vazi la hijab kwa kauli au vitendo, atakuwa amewachokoza Waislamu na sisi kamwe hatukubali hilo liendelee na kukaa kimya, tutachukua hatua stahiki na ikibidi tutalazimika kuondoa munkari kwa mikono yetu wenyewe, kama dini yetu inavyotuelekeza," alisema.

  Aliongeza kuwa wanalaani na kupinga kitendo kilichofanywa na wanaodaiwa kuwa wafuasi na viongozi wa Chadema kumvua nguo Mkuu huyo wa Wilaya na kumwacha bila sitara.

  Alisema Kimario ni Mwislamu anayefuata mafundisho ya Uislamu yanayomtaka kila
  mwanamke ajisitiri kwa vazi la hijab, hivyo kumvua ni kumdhalilisha kwa wanajamii kama mwanamke wa Kiislamu, mama mwenye watoto na kiongozi wa Serikali.

  Tumetafakari tukio hili kwa undani na tunalichukulia kama shambulio la wazi na la makusudi dhidi ya mafundisho yetu na dini ya Kiislamu, yanayomtaka kila mwanamke aliyevunja ungo, kujisitiri kwa kuvaa vazi la hijab," alisema Sherali.

  Aliwaomba Watanzania wote, wanaharakati wa asasi za kijamii na wa haki za binadamu, viongozi wa vyama vya siasa na wa dini zote, kulaani na kupinga unyanyasaji huo wa kijinsia na kidini unaokwenda kinyume na Katiba ya nchi na utamaduni wa Watanzania wa kuheshimiana.

  "Tumesikitishwa na ukimya wa asasi za kijamii zinazodai kutetea haki za binadamu na za wanawake, kutolaani kitendo hiki cha mwenzao kudhalilishwa kijinsia, kuendelea kukaa kimya kunatulazimisha kuwaona wanafiki na ndumilakuwili juu ya madai yao ya kutetea wanawake," alisisitiza.

  Alisema wanaitaka Serikali ilitafakari kwa kina tukio hili la kudhalilishwa mwanamke Mwislamu, akilitumikia Taifa kama mmoja wa viongozi wake, kukaa kimya kutatoa tafsiri hasi juu ya jinsi inavyolichukulia tukio hilo na kuitaka kuwachukulia hatua kali wahusika.

  Wanawake Waislamu Katika hatua nyingine, kikao cha wanawake Waislamu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee Jumapili, wanawake walilaani tukio hilo.

  Kikao hicho chini ya Mwenyekiti wake Fatma Juma, kiliwataka wanawake na wapenda amani wote kulaani kitendo hicho cha udhalilishaji wanawake.

  Walisema kitendo hicho kimeonesha dharau, si tu kwa Uislamu, bali hata kwa madhehebu mengine na kinaweza kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini hivi sasa.

  Tamko la kikao hicho, lilisema litaanza kusambazwa katika misikiti yote Ijumaa, ili Waislamu waelewe namna walivyoguswa na kusononeshwa na tukio hilo.

  Shura ya Maimamu
  Habari zaidi zilizopatikana zilisema Shura ya Maimamu nayo itakutana hivi karibuni kujadili tukio hilo la mwanamke wa Kiislamu kuvuliwa hijab.

  Mbali ya kukutana huko, Shura hiyo itaandaa maandamano ya kupinga kitendo hicho ambacho wamekitafsiri kuwa ni matusi dhidi ya Uislamu.

  Katibu wa Shura ya Maimam, Shehe Ponda Issa Ponda, jana alithibitisha kuwapo kwa ajenda hiyo.

  Akizungumza na gazeti hili jana alisema kitendo kilichofanywa na wafuasi wa Chadema kimekosa utu, ustaarabu, uungwana na maadili mema na kinapaswa kukemewa na wapenda amani wote nchini, bila kujali itikadi zao, kwani kikiachwa kitazidi kukomaa na kuonekana ni
  jambo la kawaida katika jamii.

  Akizungumzia kadhia hiyo, Katibu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini (Baraza Kuu), Shehe Ramadhan Sanze, naye alisema taasisi yake inaungana na wanaolaani tukio hilo .
   
 9. H

  HAKI bin AMANI Senior Member

  #9
  Sep 21, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aliye juu mngoje chini = (Dalili ya kukata tamaa). Aliye juu mpandie huko huko = (Dalili ya mafanikio).
  Well done CDM keep it up.

   
 10. wijei

  wijei JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Hao nao ni CCM C
   
 11. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2011
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  kweli ccm iko mahututi .Chadema wakimaliza kazi kuifanya Igunga kuwa jimbo la upinzani naomba wafanye operation Tanzania sehemu zote za vijijini ambapo huko bado kunashida ya wananhci kulewa somo la kuitosa ccm daima katika chaguzi zijazo.Hakika Mungu akifungua ufahamu wa watu wote tutasifa jina lake maana tutakuwa tumejikomboa kutoka kongwa la mtumwa wa shetani ccm
   
 12. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ni shura ya maimamamu au shura ya maamuma? Naomba cv za hao masheikh kwa sababu mtume muhamad aliagiza elimu itafutwe hata uchina sasa kwa taarifa zilizopo hakuna shehe hata mmoja hapo aliyesoma hata vyuo vilivyopo nchini achilia mbali vya uchina ndio maana wanayumbishwa na ccm kama itakavyo.
  Maaskofu sidhani kama wanaweza kupelekwapelekwa na ccm ya kina nape kwa sababu elimu ya nape hata padri kamzidi.
  Tunawaomba waislamu waliosoma ambao hawapati nafasi za kuwa viongozi kwenye taasisi za kiislamu wawaelimishe wenzao kwamba bakwata,uvccm na uwt ni taasisi za ccm na malengo yao ni kudhoofisha makundi lengwa vijana wameshaishtukia,uwt imehashtukiwa na kinamama bado bakwata waislamu mpaka washtuke 2050.
  Mchana mwema.
   
 13. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Mbona hawakusema kitu wakati Mbunge wa viti maalumu wa CUF alipolazwa mahabusi moja na wanaume? Laana ya udini itawatafuna nyie!
   
 14. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2011
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Simama...siteteee...mbele yaa Igunga..na Igunga ..isikie hiiyo sauti yakooo.....Kama kweli Umetenda mema kwa taifa hili watakutetea wanaigunga..together we can and we will.
   
 15. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 4,016
  Trophy Points: 280
  Katika kuonyesha hali ya ukomavu kisiasa na kufuta historia chafu nawashauri CUF wamuondoe mgombea wao na watoe support wa CHADEMA kama muhafaka huku bara!
   
 16. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #16
  Sep 21, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  c angalau ipo mbali na A
   
 17. Naibili

  Naibili JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,681
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Igunga bila ccm inawezekana!
   
 18. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Tanzania bila CCM inawezekana?
   
 19. C

  Capitani Member

  #19
  Sep 21, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu, tusikimbile kutafsiri ,ama kutaka haki za binaadamu haraka haraka bila kutafakali, mbona visa vya akina mama kudhalilishwa na vyombo vya dola ni vingi sana, kwavile ni vya chama tawala, vyama vingine vikifanyiwa sawa , wao hata jambo moja tu hukuuzwa kuwa kubwa na kelele vilio vingi, tuweni wenye hekima , tutafakali, kwanza na kuwa makini kabla ya kukurupuka kwa matendo., (KUMBE KWELI KWELI NYANI HAONI K.............. zake.
   
 20. zululima

  zululima Member

  #20
  Sep 21, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  inakuwakilisha jinsi usivyomzalendo. magamba tatizo sana bana...
   
Loading...