CCM ijibu hoja za CHADEMA - Sumaye

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,213
Anasema Isiiachie serikali peke yake...

Akizungumza na Mwananchi bila kujua kwamca CCM wangekuwa wanazungumzia suala hilo, Sumaye alisema, CCM inatakiwa kukabiliana kisiasa na hoja za
CHADEMA na si kuiacha serikali ipambane nao.

Kwa mujibu wa Sumaye, kazi ya siasa ni ya chama na si seikali, hivyo CCM wanapaswa kuwa msatari wa mbele kupambana na
CHADEMA kwa sera na kujibu hoja zao zote ili kuongeza imani ya wananchi kwa chama hicho.

"Wale CHADEMA wanafanya kazi ya siasa na hawa CCM wamekaa kimya, wanaiacha serikali ndio inatoa majibyu, hali hiyo si nzuri, chama kinapaswa kujibu hoja zote na kama hakina majibu, kiyaombe kwa serikali" alisema Sumaye.


Sumaye alisema CCM inahitaji viongozi waadilifu, wachapakazi, na wasio waoga kumshauri rais juu ya masuala mbalimbali ili kuuwa na mabadiliko ya kiutendaji yanayoendana na joto la kisiasa lililopo.


Source: Mwananchi

Maoni yangu:
Ni Kweli Wanahitaji kujibu hoja, So far si Kikwete, si Pinda, si Chiligati, Si Wassira alojibu hoja, wote waliishia kulalama tu na kuwatisha chadema, wanatakiwa kujibu hoja.

Lakini Jamaa naye anajiandaa nini 2015.
 
pongezi kwake ... kwakuwa ametambua kuna hoja ...! sisiem itakufa na sintofahamu
 
Kuna haja ya kujibu hoja coz wakati wa Ben, mfumuko wa bei haukuwa hivi, mtokeo ya shule, njaa, umeme. Watu kwa kiasi flani walikuwa na matumaini ambayo kwa sasa hayapo.
 
Huyu ni mmoja ya wale waliokubwa na Rungu la fitina la Mkwere 2015, alipigwa kijembe kuwa anamilik 25 bil. Lakin alichokisema huyu bwana ni chamsingi, km chadema wametoa hoja, wanapaswa kujibiwa kwa hoja, sio kulaumu, kunung'unika na kulalama pasipo sababu za msingi! Vitisho havitaweza kamwe kufuta hoja za CDM kwa wananchi bt zitakiua chama chao.
 
Simple,ahitaji akili nyingi kufikili nini CDM wanasema,sasa wanaccm wanakurupuka baadaya kujibu hoja wana wanaazisha hoja ya kujinjika kwa amani.AMANI HAKUNA WATU WANALALA NA NJAA,
 
CCM kwa nini waitumie serikali kujibu hoja za Chadema, kama alivyosema Sumaye hoja za Chadema ni za Kisiasa zijibiwe na Chama cha siasa na si serikali, Chiligati Jibu hoja na sio kutishia Chadema, sumaye amewashauri kama hamna hoja za kujibu kwa vile ninyi ni vilaza, ombeni majibu kwa watu wenye akili.
 
Hivi TENDWA alitoa ule mkwara kiserikali ama kichama. Mimi niliona ilikuwa kiCCM zaidi. Bahati mbaya hawa jamaa hawawezi tofautisha CCM na serikali including dola, hivyo itakuwa ngumu sana kwao kuweza kununua wazo la Mh. Sumaye.
 
Atleast Sumaye ameonyesha kuelewa somo, cdm wamefanya kazi kubwa mno; ni zamu ya ccm kujibu hoja nzito kwa hoja nzito, na sio zile hoja zao nyepesi nyepesi za kisiasa!

Ila mtashangaa watakavokurupuka...
 
Mimi najiuliza kitu kimoja kwamba hawa CCM huwa wanajiandaa kutoa matamko yao au huwa kila mtu anajisemea? Je wanajua kuwa kuna utofauti kati ya CCM na SERIKALI? Au wanafanya makusudi?
 
Hakuna hoja itakayojibiwa Pinda kashaonyesha nini serikali watafanya subirini!!!
 
Subiri watakavyomjibu sumaye badala hoja za chadema ndio uje ccm ya mipasho badala hoja na sera
 
Mi naona ukimya wao unasababishwa na hoja nzito za CDM, ambazo nyingi majibu yake hayajibiki kirahisi. Sisiem kumebaki walalamikaji tu, wakiongozwa na mwenyekiti wao.
 
Point taken! Well said sumaye! Hakuna haja ya kutishana na nashangaa hawa wanaoendelea kuwatisha watu oh aman itatoweka oh chadema wana vurugu huu ni ujinga na ukosefu wa hoja. Cdm wana hoja nzito zinazowashinda ccm kujibu so wanaishia kutoa vitisho kupitia serikali na tendwa badala ya ccm km chama kujibu hizo hoja. Nadhani nao waendeshe mikutano kwa wananchi kuweza kutoa majibu ya hoja za chadema. Token dar nendeni mikoan mkajibu tuhuma na sio vitisho!
 
Alichoongea SUMAYE ni cha msingi: hii inadhihirisha ni namna gani CCM haina uwezo wa kuwajibika kwa Wananchi, uwezo wa kujibu hoja za msingi CCM haina zaidi ya kukingiwa kifua na Nguvu ya dola. Itafika wakati na dola yenyewe itashindwa kuvumilia na hatimaye tuwe kama Nchi za kiarabu.
 
Hakuna la maana watakalojibu maana hoja zote zinazotolewa dhidi yao ni nzito, ndio maana wamebaki kutoa vitisho!
 
They have nothing to say coz everything is in mess.
what will they say and convince the netizens and rest?
 
Alichoongea SUMAYE ni cha msingi: hii inadhihirisha ni namna gani CCM haina uwezo wa kuwajibika kwa Wananchi, uwezo wa kujibu hoja za msingi CCM haina zaidi ya kukingiwa kifua na Nguvu ya dola. Itafika wakati na dola yenyewe itashindwa kuvumilia na hatimaye tuwe kama Nchi za kiarabu.
haata dola walishawachoka ila wanatimiza tu wajibu, kwani unadhani wenyewe hawana ndugu,jamaa na marafiki??
kwani unadhani wenyewe hawayaoni maisha yalivyo??
 
Back
Top Bottom