Kwani Hoja zenyewe zinazotakiwa Kujibiwa na CCM kwenye Majukwaa ni zipi basi? Kama ni Dowans Suala hilo liko Mahakamani, ni Makosa kulijadili nje yake kabla hukumu haijatoka, Kama ni Kupanda bei ya Umeme na Mgao Tanesco imeshatoa Maelezo, Kama ni Mabomu ya Mbagala Serikali imeshatoa Tamko na Tunasubiri matokeo ya Uchunguzi ili ijulikane Hatua za Kuchukua na Watakao wajibishwa (ingawa CDM wameshatoa Hukuma kabla hata Mabomu yenyewe hajamalizika Kulipuka!) Wakati wa Kampeni, kila Chama kiliwasilisha hoja zake kwa Wananchi, CDM kiliwasilisha hoja zake (Wenyewe wakiziita "MABOMU") kwa Wananchi, CCM ilizijibu kwa Nguvu zote katika ngazi zote, Aidha CCM ilionesha ilichokifanya katika kila Kijiji, Kata, Mkoa na Taifa ndani ya Miaka 5 iliyopita na Mapungufu yake na Kile ambacho CCM itafanya kwa Miaka 5 ijayo endapo itapewa Ridhaa na Wananchi kuongoza tena, Kule ilikofanya Makosa ilipoteza Wabunge na Madiwani, kule ilikofanya Vizuri ilishinda (Kama Ina Uwezo mkubwa wa Kuiba kura si Ingeiba kote) Matokeo ya Jumla CCM ilishinda Urais, Wabunge na Madiwani Wengi
sana. Kazi ya CCM hivi sasa ni Kuisimamia Vizuri Serkali yake itekeleze Yale yaliyoahidiwa Kipindi cha Kampeni (ilani yake ya Uchaguzi) imepewa Kikatiba Miaka 5 kuyatekeleza. Sasa cha Ajabu hata miezi mingapi Haijapita, tayari CDM Inapanda Majukwaani na Mabarabarani na kutaka hoja zilezile za Wakati wa Kampeni zijibiwe tena, Kwa hiyo CCM isifanye kazi zake na Kujipanga upya Bali na yenyewe iingie Barabarani na kuanza Malumbano na CDM kwa Sababu tu CDM inataka hivyo, kwani wao ni Nani? Ikumbukwe CDM kutoka na Hoja na Sera zake wakati wa Kampeni ilipata Walioikubali kwenye Urais wapatao 2.2millioni ambao ni Watu wengi na Wengi wao ndio hao Tunaowaona Kwenye Maandamano yao, Lakini jiulizeni CCM nayo ilipata Wangapi? 5.2 Millioni, hata ingechakachua Vipi, isingeweza kuiba Kura nyingi kiasi hicho, Je, CCM nayo ikiwaingiza hao Barabarani Hali itakuwaje? Jamani msione Simba kalowa Mkadhania ni Paka! Mmesahau Sumaye huyuhuyu na Bosi wake Mkapa alivyowafanya Wapinzani walipoandamana kule Pemba Unguja na Buguruni walipoandamana Kupinga Matokeo? Au hamumuelewi anapodai Hoja za CDM zijibiwe? Hamjui kwamba anamuona Kikwete na Pinda wamekuwa wapole sana kwa Wapinzani na anataka Wajibu Mapigo Kama Alivyofanya Yeye na Mkapa? Mnataka Hivyo?