CCM ijibu hoja za CHADEMA - Sumaye

Mkuu,
Umeongea kimafumbo zaidi, na inahitaji zaidi ya common-sense ku'decode message hii.
Embu jaribu kuileta kwa engo ingine ili akina yakhe waambue!


Hii ni food for thoughts kwa wakubwa na ambao wako matured tuu ambao tayari wana meno 32 watoto wanapewaga maziwa ili tumbo liweze kudigest...
 
KipimaPembe, unachotaka kutuambia ni Kuwa CDM ikishinda na Kuunda Serikali, Slaa akiwa Rais basi wenzake wote, kina Freema, Zitto, Lisu, Mnyika, Mdee wote atawaacha Kwenye Chama wafanye Siasa, Kisha yeye atatafuta Wataalamu nje ya Wigo wa CDM aunde Serikali na kuwaacha wapiganaji wake Waendelee kujitolea kupiga Siasa kwenye Chama, Si ndio unavyomaananisha? It's Very Unrealistic! Hoja za CDM za sasa Karibu zote zimelenga Serikali, Kwanini Serikali yenyewe Isijibu? Si ndiyo yenye Takwimu zote? Hivi Gari likiendeshwa vibaya Barabarani anashikwa Dereva au mmiliki wa gari?
 
Yeye ajibu minong'ono huko Hanang' kwamba wafanya biashara wanaoshikilia biashara kwa bunduki hasa ya usafiri na hata kufikia kuchoma magari ya watu kwamba yeye ndio anayewakingia kifua ndio maana wanaishi kama wako kwenye jamhuri yao!
 
Bahati nzuri cdm hawana propaganda katika hili. Ccm ni wazuri sana kwa prop na wakizidiwa wanarusha ngumi. Sumaye wape vidonge vyao hao
 
Wakti mwingine CCM kuna watu wanao-think deep! Sumaye have spoken. I support the former PM.He is correct to the dot.

Hata hivyo namshauri Sumaye atumie utaratibu wao wa ki-CCM kupitia vikao vyao or whatever means AMSHAURI M/kiti wake KIWETE wazo hilo ili aweze kujibu hoja za CDM na aache vitisho.

Vitisho havitawasaidia CCM sana sana vitazidi kuwadhalilisha na kuwapunguzia heshima kwa Watz!!!
 
yeah its true man, hawa jamaa hawajui hata responsibility zao, ccm should be responsible and wajibu hoja za chadema na sasa wamekuja na sera et watakifutia chama chetu usajili, let me won them dont even think of it now coz ur too late, vinginevyo amani hakuna tena hapa.
 
KipimaPembe, unachotaka kutuambia ni Kuwa CDM ikishinda na Kuunda Serikali, Slaa akiwa Rais basi wenzake wote, kina Freema, Zitto, Lisu, Mnyika, Mdee wote atawaacha Kwenye Chama wafanye Siasa, Kisha yeye atatafuta Wataalamu nje ya Wigo wa CDM aunde Serikali na kuwaacha wapiganaji wake Waendelee kujitolea kupiga Siasa kwenye Chama, Si ndio unavyomaananisha? It's Very Unrealistic! Hoja za CDM za sasa Karibu zote zimelenga Serikali, Kwanini Serikali yenyewe Isijibu? Si ndiyo yenye Takwimu zote? Hivi Gari likiendeshwa vibaya Barabarani anashikwa Dereva au mmiliki wa gari?

Inawezekana wewe ndivyo ulivyoelewa! Lakini Chadema wakifanya kama CCM ilivyofanya, yaani wanaharakati wote wa Chadema tunaowaona leo, wote wahamie serikalini, basi Chadema hakiwezi kuwa tofauti na CCM na fate yao itakuwa ile ile ya CCM.

Mwenendo na taratibu za kibepari zinataka kutenganishwa kwa shughuli za chama na serikali. Chama kinatakiwa kibaki kikiwa kimesimama chenyewe na chama kiwe na uwezo wa kutoa jicho la pili kwa viongozi walio serikalini. Ikiwa chama na serikali itakuwa kitu kimoja, hilo jicho la pili linakosekana na chama na serikali huwa kitu kimoja.

Mwenendo wa nchi zote za kiafrika zilizotoka katika mfumo wa chama kimoja cha siasa umekuwa ni huu wa kuchanganya chama na serikali (kama ilivyokuwa tu wakati wa chama kimoja) na wengi mnaamini kuwa ndo sawa. Ukweli ni kuwa huo mfumo si sawa. Angalia yanayoendelea Kenya. Baada ya kuingia vyama vingi, vimeendelea na mfumo ule ule wa chama kimoja; yaani chama na serikali havitenganishiki. Matokeo yake, Chama kikitoka serikalini ni marehemu. Angalia Zambia, Angalia malawi, n.k. Mfumo wa South Africa ndo sahihi, pengine kwa sababu ya historia ndefu ya mapambano kule; ukiangalia ANC kama taasisi bado inabaki imesimama na ina watu wengi wenye nguvu ambao hawapo serikalini.

Angalia nchi zote ambazo zimeusimika mfumo wa ubepari ukasimama uone tofauti yake. Inawezekana CCM inao watu wa hivyo walio nje ya serikali, lakini mfumo hauruhusu watu hao kuwepo kama jicho la pili la kukisaidia chama. Wakati mwalimu alipokuwa hai, alikuwa hiyo sauti. Lakini baada ya yeye kutoka, chama kimebaki hakina nguvu ya kuiambia serikali chochote kwani chama chote kipo serikalini. Tatizo ni kuwa mwalimu alikuwa akifanya mwenyewe kutokana na mapenzi yake tu kwa nchi, ila hakuweka mfumo ambao ungeweka checks and ballances za kukiwezesha chama kuikosoa serikali au kuwawezesha wale waliomo kwenye chama kuwakemea walioko serikalini wanapofanya kinyume na malengo na matakwa ya chama. Chama inatakiwa kiwe na uwezo wa kuwaambia viongozi wa serikali kuwa hayo mnayoyafanya si sera ya chama. Na kiwe na uwezo wa kuwashughulikia wanaoshindwa kujirekebisha. Na hili iwe ni kimfumo, si kimtu binafsi.

Kwa kifupi ni kuwa, ikiwa Chadema itashinda, lazima wabakie watu makini ndani ya Chama ambao hawataingia serikalini. Yes wabaki nje wakifanya kazi ya evaluation na kutoa au kufanya kitu kinaitwa Quality Asurance. Hawa watu inabidi wawe nje ya serikali na inabidi wawe watu wenye nguvu ambao wale waliomo serikalini hawawezi kuwa-ignore. Na hawa ndo wanahakikisha kuwa always serikali iko kwenye mstari.

Vinginevyo, Ikiwa Chadema itaingia madarakani halafu hii timu yoote tunayoiona ikazama yote serikalini, ujue chama kimekufa. Uchaguzi utakaofuata inabidi viwe vinazuka vyama na alliances za uchaguzi zenye lengo la kuwafikisha watu fulani fulani madarakani, wakishaingia madarakani alliance hizo zinakufa! Kama unavyoona Kenya. Ndo maana unaona ufisadi serikalini kule Kenya hauwezi kuondoka kamwe, kwani hakuna vyama! Kuna makundi maslahi tu.

Vyama vya kudumu, vinabaki pembeni na kuzisimamia serikali zake na kuhakikisha serikali siku zote inakuwa kwenye mstari.

Kwa ujumla vyama inatakiwa vitoe uongozi, wakati serikali ikitenda. Chama ambacho viongozi wote ni sehemu ya serikali kimfumo hawawezi kuirekebisha serikali inapokosea. Wanakuwa wao ndo chama na wao ndo serikali, kama ilivyo sasa hivi hapa bongo.
 
KipimaPembe, unachosema ni Sahihi kabisa, lakini Je, huoni kuwa it's Contradictory kudai CCM ambayo inapaswa iwe nje ya Serikali ijibu hoja zinazohusu Serikali? Nifahamuvyo, ndani ya CCM kuna Wanasiasa Mahiri wengi sana Ambao hawamo Serikalini lakini wana Uzoefu mkubwa wa Mambo ya Serikali, K.m. Ndani ya Kamati Kuu ya Taifa ya Chama, kuna kina Mzee Mwinyi, Mkapa, Karume, Malechela, Kinana nk ni Wengi mno ambao hawamo Serkalini lakini wanajua Masuala ya Kiserikali na Kisiasa Kinyumenyume, Ukishuka kidogo kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa ndo kabisa, utakumbana na kina Salim Ahmed Salim, Sumaye nk Mikoani kuna Kamati za Siasa za Mikoa yote ya Tz Wamejaa tele design za kona Pancras Ndejembi, Mfumo huo upo mpaka Kwenye Level ya Vijiji ambavyo Serikali inaongozwa na WanaCCM basi Viongozi hao wanapaswa Kuwajibika kwa kuwasilisha Taarifa za Utekelezaji wa ilani Kwenye Vikao vya kamati za Siasa za Matawi husika, kule hakuna viongozi wa Serkali Bali ni wa Chama tu! Kwa hiyo sio Kweli kuwa Chama hakina wana Siasa ila Wote wako Serkalini, hata hao mnaowasema kila saa kina Chiligati, Makamba, Tambwe nk hawamo Serikalini. Ni sahihi kwa Chama kuielekeza Serkali yake namna ya Kukabiliana na CDM kisheria, Kwani chenyewe hivi sasa Kina Jukumu kubwa la kuisimamia Serkali kutekeleza ahadi zilizotolewa wakati wa Uchaguzi na pia Kujipanga upya kulingana na Hali ilivyo sasa, na Kwa Uchaguzi Mkuu wa Chama hicho Mwakani. Kosa liko wapi?
 
Sumaye: CCM ijibu hoja za Chadema Send to a friend Sunday, 06 March 2011 09:21 0diggsdigg

tluwaysumaye_thumb.jpg
Claud Mshana
WAKATI CCM ikitaka dola ikidhibiti Chadema, Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya tatu, Fredrick Sumaye, amekitaka chama hicho tawala kukabiliana na hoja za Chadema kisiasa badala ya kuiachia Serikali ipambane nao.Juzi CCM kilisema nyendo za Chadema zina agenda ya siri ya kuking’oa madarakani kwa kutumia nguvu kinyume cha katiba hivyo kiliitaka Serikali na vyombo vya dola kuchukua hatua za kisheria haraka.

“CCM inaviomba vyombo vya dola viwe imara kuchukua hatua za kisheria… Wanachofanya Chadema ni kutuchonganisha na wananchi, kutoa kauli hatari za kujaribu kughilibu akili za watu ili kuchochea machafuko, umwagaji wa damu na uasi. “Wanachochea wananchi wakisema, ‘peoples’ na hujibu ‘power’! (nguvu ya umma), Je mpo tayari kufanya kama Tunisia, Misri? (ambako serikali zilipinduliwa kwa nguvu ya umma)” alisema Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM, Itikadi na Uenezi, John Chiligati kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika juzi, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili bila kujua kwamba CCM wangekuwa wanazungumzia suala hilo, Sumaye alisema CCM inatakiwa kukabiliana kisiasa na hoja za Chadema na si kuiachia Serikali ipambane nao.

Kwa mujibu wa Sumaye, kazi ya siasa ni ya chama na si serikali, hivyo CCM wanapaswa kuwa mstari wa mbele kupambana na Chadema kwa sera na kujibu hoja zao zote ili kuongeza imani ya wananchi kwa chama hicho.Sumaye alisema si ishara nzuri kwa CCM kukaa kimya wakati wapinzani wanaendelea kukishtaki kwa wananchi kuwa kimeshindwa kufanya kazi.

Sumaye ambaye Mwananchi Jumapili ilimtafuta kusikia maoni yake kuhusu mfululizo wa mikutano ya Chadema na mustakabali wa CCM, alisema chama hicho tawala kinapaswa kujibu hoja zote za Chadema kisiasa na kama hakina majibu kiiombe Serikali majibu hayo na iyatoe kwa wananchi.

“Wale (Chadema) wanafanya kazi za siasa na hawa (CCM) wamekaa kimya, wanaiachia Serikali ndio inatoa majibu, hali hiyo si nzuri, chama kinapaswa kujibu hoja zote na kama hakina majibu, kiombe kwa serikali,” alisema Sumaye.Mjadala wa uhalali wa mikutano na maandamano ya Chadema uliibuliwa na Rais Jakaya Kikwete alipolihutubia taifa kupitia radio na televisheni Februari 28, mwaka huu na kuwaleza wananchi kuwa chama hicho cha upinzani kina lengo la kuleta machafuko nchini.

Rais Kikwete alisema hayo alipokuwa akilihutubia taifa mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.Kauli hiyo ya Rais Kikwete ambaye Chadema waliipuuza, ilisisitizwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Steven Wassira, aliyesema kuwa Chadema wasije kuilaumu serikali ikikosa uvumulivu na kuanza kutumia dola kukishughulikia.

Akihojiwa na gazeti hili Sumaye hakuishia kuishauri CCM kuja na hoja za kisiasa kujibu mapigo ya Chadema, bali pia alieleza aina ya watu wanaofaa kukiongoza chama hicho tawala wakati huu wa mabadiliko makubwa ya kisiasa.Sumaye alisema CCM inahitaji viongozi waadilifu, wachapakazi na wasio waoga kumshauri rais ili kuwa na mabadiliko ya kiutendaji yanayoendana na joto la kisiasa lililopo. “Tunahitaji viongozi wasioogopa kumshauri rais juu ya masuala mbalimbali, kama utakuwa na viongozi waoga, lazima kutakuwa na matatizo,” alisema Sumaye.

Kuhusu mabadiliko ndani ya CCM ambayo Rais Kikwete alisema ni lazima yafanyike, Sumaye alisema anakubaliana msimamo huo na anampongeza Rais kwa kutambua kuwa chama kinahitaji mabadiliko makubwa ya kiutendaji.“Kwanza nampongeza Mwenyekiti, maana ameona hilo. Watu wengi wanaona kuna umuhimu chama kurekebishwa na eneo muhimu ni utendaji wa viongozi wa ngazi mbalimbali ndani ya chama,” alisema Sumaye.

Sumaye alieleza kuwa CCM kitaendelea kushika dola, lakini kama kinataka hayo yatimie, mabadiliko ndani ya chama ni muhimu.Alisema umuhimu wa CCM kujifanyia tathmini ya utendaji ulianza kujionyesha katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, ambapo ikilinganishwa na chaguzi nyingine, chama kilipata upinzani mkali."Sasa ni dhahiri kunahitajika mikakati madhubuti ili kuhakikisha mwaka 2015 unakuwa mrahisi kwa CCM," alisema Sumaye.

Ndejembio atabiri anguko
Habel Chidawali anaripoti kutoka Dodoma kuwa, Kada maarufu wa CCM, Pancras Ndejembi amekitabiria chama hicho kikongwe kuzama.Kada huyo ambaye ni Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Dodoma alisema jana kuwa hali ilipofikia kwa sasa, CCM inaonekana kupoteza mwelekeo na kutia shaka mustakbali wa chama hicho siku za usoni.

Ndejembi ambaye aliwahi kutumikia nyadhifa mbalimbali ndani ya serikali na chama katika utawala wa Serikali ya awamu ya kwanza, alisema CCM bado haijaingia shimoni ila inaelekea huko.“Ni kweli chama hakifuati utaratibu uliokuwepo ndio maana nasema kuwa kinaelekea kuzama tofauti kabisa na enzi zetu ambapo Mwalimu Julius Nyerere alikuwa anasisitiza kuwa turudi kwa wanachama tukae nao na kuzungumza, jambo ambalo sasa hilo halipo na viongozi wamebaki huko juu,” alisema Ndejembi.

Alisema viongozi wa ngazi ya taifa wamebaki katika maofisi yao na kushindwa kurudi katika ngazi za chini kuimarisha chama na matokeo yake wanaishia kupiga kelele bila ya kuwa na uhakika wanachama ngazi ya chini wanataka nini.Ndejembi hivi alisema hakuna mshikamano wa dhati ndani ya chama jambo linalowafanya wanachama kumuachia mzigo wote Mwenyekiti wa Taifa.

“Watu wanaishia kulaumiana kila kona kwamba chama kimefanya nini, mara wanasema bado kimesimama wengine wanasema kuwa kinayumba, ila ukweli utabaki palepale kuwa CCM tunazama sasa,” alisisitiza.Kuhusu nguvu ya wazee ndani ya Chama Ndejembi alisema: “Sisi tumestaafu hivyo tupo tupo na kama hawataki kutuita unadhani tutakwenda ? Lakini, wakisema tuende tuko tayari kukaa pamoja nao kutengeneza utaratibu wa kukinusuru chama kisizame kabisa katika tope”.Ushauri

Kuhusu nini kifanye ili kukinusufu CCM, alisema unahitajika mshikamano wa dhati kati ya viongozi na wanachama: “viongozi wanahitaji kutambua kwa dhati kuwa chama kiko ngazi ya chini kuanzia kwa wajumbe wa nyumba kumi sio ngazi ya mikoa”.Alishauri kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa anatakiwa abaki kama kiongozi wa kutoa ushauri kwa juu, lakini awe na watu wanaochukua mawazo kutoka kwa wanachama wa ngazi ya chini.

Hata hivyo, alisema viongozi wa taifa bado wana mfumo mbovu wa mawasiliano, kwani kila mtu katika nafasi ya juu ni msemaji, jambo linalofanya wajichanganye katika taarifa zao.


Source: Mwananchi
 
Je hali kama hii aiwezi kuigawa CCM kutokana na maneno yanayotolewa na makada wao?
 
linalohusu CCM kujibu hoja nasio kutoa shutuma kwa CHADEMA,Napia ukisoma gazeti la Tanzania daima la leo kuna maelezo ya kina,cz kukikosoa chama juu ya tarati buzake za kisiasa uwon waweza leta mgawanyiko kati ya wanachama wazalendo na wale ambao wapo kwa maslai yao binafsi?
 
kwa wenye akili matamko kama hayo niyakufanyia kaz na ndio yanayokijenga chama mana ukweli unawekwa mezani watu wanafanyia kaz ila kwa wenye upeo hafifu watatoa maneno yakushutumiana
 
Sumaye amshangaa Tambwe
Na Mwandishi wetu,
NIPASHE

Chama Cha Mapinduzi(CCM) kinaathiriwa na viongozi maslahi wasio na upeo wa kujua yale wanayosema yanakisaidia au kukuangamiza chama hicho katika siasa za ushindani wa vyama.
Kauli hiyo ilitolewa Dar es salaam jana na Waziri Mkuu Mstaafu,Bwa Frederic Sumaye katika mahojiano maalum na gazeti hili kuhusu kauli zilizotolewa dhidi yake na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda wa CCM Bw Hizza Tambwe.
Bw Sumaye ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM( NEC) alisema baadhi ya viongozi waliopewa madaraka HAWANA historia na chama hicho na hawaelewinamna kauli zao zinavyokiathiri chama jambao ambalo sasa ni kero kwa wanachama na watu wenye uchungu wa kweli na CCM.

Maoni yangu: wagosi hawa wanasubiri nini kuanza kusaga lami
 
Tambwe Hizza kiboko, huyu alisema ni bora amlale mama yake kuliko kurudi CCM sasa sijui ameshalifanya hilooo

Hawa mawaziri wakuu nao wakishaondoka ndio kwanza akili zinawakaa sawa,HATA PINDA=mtu wakujiliza,mvivu,pro-ufisadi,asiyejua dhamana ya cheo chake, asiye jasiri ATATOA MATAMKO MAKINI AKIONDOKA.

Tatizo la hii nchi kwa sasa ni JAKAYA KHALFAN MRISHO KIKWETE na siyo TAMBWE
 
Yeah! Naungana na mh. Waziri mkuu mstaafu na kada wa ccm kwa hilo, yeye kabaini bt wenzie bado ving'ang'anizi, na siajabu wakampinga. Viongoz km Tambwe kamwe msitegemee mawazo chanya toka kwao, then nawalaumu ccm kwa kukumbatia idara ya propaganda kuendeshea chama! Nakumbuka siku ile ya kipima joto mada ikiwa Suala la katiba Kada TAMBWE ALIONGEA UPUUZI SANA, HANA HOJA THEN ANAMIJAZBA LUKUKI, Polen ccm!
 
Je umemsikia Mh.Samwel Sitta leo asubuhi kwenye Tv. Kwa ufupi kawaambia tuache kumshutumu mh.dr slaa. Dr.Slaa yuko sahihi,ccm tuwe makini na matamshi yetu. Mwanzo wa mafanikio ya cdm unaanza kutimia!
 
Back
Top Bottom