CCM Igunga wafyekana mapanga kugombea pesa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Igunga wafyekana mapanga kugombea pesa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Sep 15, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  • Kada wa CCM ajeruhiwa kwa panga, bintiye abakwa

  KADA wa CCM, Francisco Msalika amejeruhiwa kwa panga kichwani na binti yake kubakwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Mtaa wa Benki ya zamani mjini Igunga na watu ambao walimtaka atoe pesa za kampeni. Akizungumza akiwa kitandani katika wodi ya majeruhi katika hospitali hiyo, kada huyo alisema tukio hilo lilitokea juzi kuamkia jana majira ya saa nane za usiku. Alisema alisikia kishindo ambacho kiliuvunja mlango wake wa chumbani na kisha watu hao kummulika kwa tochi kali usoni.

  Alisema wakati akijaribu kuchukua panga lake ambalo alilihifadhi chini ya kitanda ili akabiliane na mhalifu huyo, alikatwa panga la kichwa ambalo lilimfanya aanguke chini na kishindo hicho kilimwamsha mkewe na mwanaye wa kike ambao nao walijikuta wakikabiliana na mvamizi huyo.

  "Alininyang'anya panga nililokuwa nataka kuchukua na kusisitiza kuwa anataka simu na pesa nilizopewa za kampeni," alisema na kuongeza kuwa alimruhusu achukue suruali ambayo alikuwa ameining'iniza katika msumari ukutani ambayo ndiyo iliyokuwa na fedha.Msalika alisema mhalifu huyo alimtwanga panga jingine kichwani ambalo lilimfanya apoteze fahamu kwa muda na kisha kumshika mkono mtoto wake wa kike na kuondoka naye.

  "Nilizinduka na kujikokota nikisaidiwa na mke wangu hadi kwa jirani zetu ambao wana pikipiki ili waniwahishe polisi na baadaye hospitali, lakini kabla hatujaondoka binti yangu akarudi," alisema Msalika. Alisema kuwa walimwuliza alipokuwa amemuachia akajibu kuwa ni jirani na mtoni. Msalika alisema kwa kuwa binti huyo hakuwa katika hali nzuri, hakuendelea kumhoji zaidi na badala yake alipelekwa polisi na kupewa PF 3 na kisha kupelekwa hospitali ya wilaya.

  Msalika alisema kesho yake asubuhi alikuja mkewe na makada wengine wa chama hicho akiwamo mwanamke aliyemtaja kwa jina moja la mama Kashi walikuja kumletea chai ndipo mama wa mtoto alipomueleza kuwa binti yao katika kadhia ile alibakwa. "Mimi nashangaa huyo mtu kuja kutaka pesa kutoka kwangu wakati kampeni za safari hii sikushiriki kabisa tofauti na inavyokuwa miaka ya nyuma," alisema na kuongeza kuwa CCM huwa wanamtumia kutumbuiza kwa kwaya katika hafla tofauti.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Anthony Ruta alithibitisha kutokea kwa tukio hilo: "Ni kweli tukio hilo lipo na mtoto amethibitika hospitalini kuwa alibakwa na hali yake inaendelea vizuri na jeshi la polisi limefungua faili kuhusiana na tukio hilo la ubakaji na hakuna mtu ambaye ameshatiwa mbaroni kuhusiana na tukio hilo."

  Hilo litakuwa ni tukio la pili ambalo linahusiana na masuala ya kampeni za kisiasa zinazoendelea mjini Igunga za kuwania kiti cha ubunge katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2, mwaka huu. Katika tukio la kwanza, mtu mmoja, Mussa Tesha alimwagiwa tindikali na jeshi la polisi linamshikilia mtu mmoja kuhusiana na tukio hilo.

  Mwananchi
   
 2. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Waacheni wafu wazike wafu wao!
   
 3. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Soon yaja mengi Polisi, UWT na CCM watajibu.
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Na hili ni hawa Chadema wanaochochea?
   
 5. K

  Kalila JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2011
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wana waonea sana chadema check yule jamaa anavyohojiwa kwenye chadematv kupitia youtube na haya yote ipo siku watayajibu kwa ocampo
   
 6. Vmark.

  Vmark. JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2011
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  There is every indicator that now worms are feasting in CCM genitals!
   
 7. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Tatizo ninaloliona ni kuuhusisha uhalifu na siasa. Hili ni tatizo kubwa sana na tukiendelea hivi, nchi itakuwa kama somalia.

  Alimwagiwa mtu tindikali, wakasema eti ni wafuasi wa chadema. Juzi Mwigulu amesema kuna magaidi wameletwa na cdm Igunga, ikaachwa ikapita sababu za kisiasa, leo mwingine kavamiwa na mwanae kabakwa, tunasema ni wana ccm wanauana!

  Ndugu zangu, tukifanya hivi tutawafanya polisi na usalama wa taifa kuacha kufanya kazi yao na mwisho uhalifu utakuwa ni siasa. Tunaiharibu nchi yetu wenyewe!

  Tuwalazimishe polisi wafanye kazi yao na kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa na kushtakiwa bila kujali ni wa chama gani. Na mwigulu akamatwe ahojiwe aseme hao magaidi walipo ili hatua zichukuliwe bila kujali chama chake.

  Tukiendelea kushangilia kwasababu ni ccm ni kuliangamiza taifa tunalisema kila siku tunalipenda kwa moyo wote!
   
 8. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Wachinjane kabisa
   
 9. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,142
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  zote hizo ni taarifa. kwa vyombo vya ulinzi na usalama, wanatakiwa kuwa makini. mtu ana taarifa, halafu unamwacha aendelee kuitangaza bila kumakamata na kumhoji anazitoa wapi taarifa. huu ni uzembe kwa polisi, uhamiaji na usalama wa taifa.
   
 10. m

  mpigilie JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hata kama kitashinda chama gani ikiwa ushindi utapatikana kwa njia hizi basi hakuna sababu ya kusheherekea huo ushindi. Lengo la uchaguzi ni kupata mwakilishi bora wa igunga atakae tetea maslahi ya wana igunga na sio kuleta maafa igunga.
  Yeyote anayehusika kati ya magamba,girlfriend wa magamba au magwanda....basi na alaaniwe
   
 11. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Siasa za bongo bana juzi tumesikia mtu kamwagiwa tindikali, leo tena mtu kakatwa mapanga! Hilo Jimbo la Igunga litamaliza watu
   
 12. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,555
  Likes Received: 4,683
  Trophy Points: 280
  Mwisho wa ubaya ni aibu, CCM wamezidi umafia, na watachinjana sana mwaka huu.ILAANIWE CCM NA WOTE WANOIUNGA MKONO
   
 13. k

  kiloni JF-Expert Member

  #13
  Sep 15, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Utawala uliofitinika ndio huu. Mene mene tekeli na peresi. Polisi wanasubiri waone ni CDM ndiyo waakti poleni watz.
   
 14. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #14
  Sep 15, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,857
  Trophy Points: 280
  Uwepo wa CCMni janga la kitaifa.
   
 15. B

  BENITOO Member

  #15
  Sep 15, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  acha hizo..we ni mtanzania??
   
 16. M

  MgungaMiba JF-Expert Member

  #16
  Sep 15, 2011
  Joined: Aug 28, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 80
  Yeah! Sure, Very Sure Indeed!
   
 17. J

  JERRY JF-Expert Member

  #17
  Sep 15, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kada wa CCM ajeruhiwa kwa panga, bintiye abakwa Send to a friend
  Wednesday, 14 September 2011 20:35
  0digg
  Joseph Zablon, Igunga
  KADA wa CCM, Francisco Msalika amejeruhiwa kwa panga kichwani na binti yake kubakwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Mtaa wa Benki ya zamani mjini Igunga na watu ambao walimtaka atoe pesa za kampeni.

  Akizungumza akiwa kitandani katika wodi ya majeruhi katika hospitali hiyo, kada huyo alisema tukio hilo lilitokea juzi kuamkia jana majira ya saa nane za usiku. Alisema alisikia kishindo ambacho kiliuvunja mlango wake wa chumbani na kisha watu hao kummulika kwa tochi kali usoni.

  Alisema wakati akijaribu kuchukua panga lake ambalo alilihifadhi chini ya kitanda ili akabiliane na mhalifu huyo, alikatwa panga la kichwa ambalo lilimfanya aanguke chini na kishindo hicho kilimwamsha mkewe na mwanaye wa kike ambao nao walijikuta wakikabiliana na mvamizi huyo.

  “Alininyang'anya panga nililokuwa nataka kuchukua na kusisitiza kuwa anataka simu na pesa nilizopewa za kampeni,” alisema na kuongeza kuwa alimruhusu achukue suruali ambayo alikuwa ameining’iniza katika msumari ukutani ambayo ndiyo iliyokuwa na fedha.

  Msalika alisema mhalifu huyo alimtwanga panga jingine kichwani ambalo lilimfanya apoteze fahamu kwa muda na kisha kumshika mkono mtoto wake wa kike na kuondoka naye.

  “Nilizinduka na kujikokota nikisaidiwa na mke wangu hadi kwa jirani zetu ambao wana pikipiki ili waniwahishe polisi na baadaye hospitali, lakini kabla hatujaondoka binti yangu akarudi,” alisema Msalika.

  Alisema kuwa walimwuliza alipokuwa amemuachia akajibu kuwa ni jirani na mtoni. Msalika alisema kwa kuwa binti huyo hakuwa katika hali nzuri, hakuendelea kumhoji zaidi na badala yake alipelekwa polisi na kupewa PF 3 na kisha kupelekwa hospitali ya wilaya.

  Msalika alisema kesho yake asubuhi alikuja mkewe na makada wengine wa chama hicho akiwamo mwanamke aliyemtaja kwa jina moja la mama Kashi walikuja kumletea chai ndipo mama wa mtoto alipomueleza kuwa binti yao katika kadhia ile alibakwa.

  “Mimi nashangaa huyo mtu kuja kutaka pesa kutoka kwangu wakati kampeni za safari hii sikushiriki kabisa tofauti na inavyokuwa miaka ya nyuma,” alisema na kuongeza kuwa CCM huwa wanamtumia kutumbuiza kwa kwaya katika hafla tofauti.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Anthony Ruta alithibitisha kutokea kwa tukio hilo: “Ni kweli tukio hilo lipo na mtoto amethibitika hospitalini kuwa alibakwa na hali yake inaendelea vizuri na jeshi la polisi limefungua faili kuhusiana na tukio hilo la ubakaji na hakuna mtu ambaye ameshatiwa mbaroni kuhusiana na tukio hilo.”

  Hilo litakuwa ni tukio la pili ambalo linahusiana na masuala ya kampeni za kisiasa zinazoendelea mjini Igunga za kuwania kiti cha ubunge katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2, mwaka huu. Katika tukio la kwanza, mtu mmoja, Mussa Tesha alimwagiwa tindikali na jeshi la polisi linamshikilia mtu mmoja kuhusiana na tukio hilo.

  Sirro awashukia Chadema na CCM

  Naibu Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Isaya Mngullu amevionya vyama vya CCM na Chadema kwa kushindwa kutoa ushirikiano kuhusiana na tuhuma mbalimbali za kushindwa kuwajibika kwa jeshi hilo katika matukio tofauti yaliyojitokeza Igunga kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Igunga.

  Akizungumza ofisini kwake jana, Kamishna huyo alisema viongozi wa vyama hivyo katika mkutano wa pamoja na Msajili Msaidizi wa Uchaguzi Igunga, Jumatatu iliyopita walidai kuwa wana ushahidi wa matukio tofauti ya kushindwa kuwajibika kwa jeshi hilo na wangetoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili hatua zichukuliwe.

  “Pale katika mkutano walililaumu jeshi letu kwa nyakati tofauti na sisi tuliwataka wafike kituoni ili watupe ushirikiano, lakini cha ajabu hadi sasa si Chadema wala CCM ambao wamefanya hivyo jambo ambalo linachafua sura ya jeshi," alisema Mngullu.

  Chadema katika mkutano huo kupitia Mratibu wa Kampeni za uchaguzi huo, Mwita Waitara kilidai kuwa kina ushahidi wa makundi ya vijana ambayo yameandaliwa kwa kupewa mafunzo ya kutumia tindikali, mapanga na silaha nyingine zikiwamo sumu na dawa za kulevya kuwakabili wapinzani wao kisiasa.

  Waitara alidai katika mkutano huo kuwa vijana hao wamesambazwa katika kata mbalimbali za Mji wa Igunga kwa ajili ya kutekeleza mpango huo na makambi hayo ya mafunzo yalikuwa katika maeneo tofauti nje ya mji huo na ushahidi wanao.

  CCM kupitia Mkurugenzi wake wa Uchaguzi, Matson Chizii kilidai kuwa katika tukio la Tesha kumwagiwa tindikali, kulikuwa na ucheleweshwaji walipomfikisha majeruhi katika kituo cha polisi akisema askari aliyekuwa zamu aliwabeza kwa kuwaambia kuwa suala hilo ni la kisiasa.

  Chizii alikiri kuwa hajafanya kile alichoahidi katika kutoa ushirikiano kwa polisi lakini akasema vijana wao wa Green Guard wanalifanyia kazi suala hilo.

  "Mambo yalinitinga kidogo lakini nawasiliana na vijana wangu ili tuone kama wataweza kunipa maelezo ya kutosha na pia kama wataweza kumtambua askari ambaye aliwajibu hivyo," alisema Chizii na kuongeza kuwa atawasiliana na jeshi hilo kwa hatua zaidi.
   
 18. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #18
  Sep 15, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Polisi wako wapi?? Huu uhalifu wanautazama tu, au wanasubiri kupiga watu tu wakati wa maandamano??
   
 19. delabuta

  delabuta Senior Member

  #19
  Sep 15, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wamezoea kugawa pesa na ndio maana watu wanajua kuna pesa za mgao sasa kama hajawapa wenzake lazima wamlambe mapanga, dhamba ya kula nyama ya mtu hiyo huwwezi kuacha,ccm hoyeeeeeeee kidumu chama cha majambazi
   
 20. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #20
  Sep 15, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  siasa wachezazo ccm ipo siku itawatokea puani! wanafanya siasa za uchochezi!
   
Loading...