CCM Igunga wafyekana mapanga kugombea pesa

Hakuna haja ya kuifurahia na kuishabikia habari hii. Mtu muungwana angeanza kwa kutoa pole kwa majeruhi kabla ya kushangilia watu kukatana mapanga. Uzalendo wetu uko wapi sasa kama tunafikia hatua ya kushangilia watu kuuana?
<br />
<br />
kumbe huwa unahoja nzuri safi sana, pole sana kwa bint na pia babaye.
 
Hakika Mwigulu anazo sifa zote za mtu FISADI kwa jinsi anavyoendelea kupayuka payuka ovyo huku na kule Igunga.

Kidogo alianza na RUSHWA la pishi la ubwabwa, akaja nalo tindikali kwa kijana wake mngoa mabango ya CHADEMA na hivi sasa anakoelea ni wa kukamatwa na wanakijiji endapo kweli PCCB itachagua kutii amri ya Mzee Benjamin Mkapa kule CCM kutembeza rushwa nyingine ya KUGAWA MAHINDI kushawishi nayo waapiga kura.

Katika hilo PCCB watapata kuelekezwa na wana-Igunga juu yaa kitu gani kinatakiwa kifanyike pindi RUSHWA inapotembezwa wazi wazi kununua kura sawa na jinsi hali ilivyo Igunga hivi sasa.
 
Siasa za fedha na siasa za dhuluma sio nzuri, hata hivyo kuwa na mambo kwa kiasi ni wajibu wa kila mmoja, hakuna sababu ya mtu kuumia katika siasa ila labda iwe kwa hoja
 
Back
Top Bottom