Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,226
- 48,672
Kitendo cha kuwa na wanasiasa wanaoiongoza Serikali lakini kiongozi wa chama cha siasa kinachoiongoza hiyo serikali kuanza kutoa maelekezo kwa watendaji wa serikali, ni dalili kwamba chama kilichoko madarakani hakijiheshimu.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania, hakuna mahali popote panapotoa fursa kwa chama Kilichoko madarakani kuisimamia serikali nje ya mfumo rasmi. Mambo ya Viongozi wa CCM kujifanya wanaikagua serikali kama inatekeleza mambo yao, ni uvunjivu wa Katiba na ishara kwamba CCM haijiheshimu.
Ziara za Kinana ni kama zinaonesha kwamba Msimamizi Mkuu wa Serikali kashindwa kuisimamia serikali hivyo Kinana sasa anafanya kazi hiyo. Kinana anatoa maagizo kwa serikali kwa mamlaka gani aliyo nayo?
Kama CCM ingekuwa inajiheshimu ingemzuia Kinana kufanya anachofanya kwani kinaidhalilisha serikali wanayoiongoza na kitendo hicho pia kinaonesha Msimamizi wake Mkuu ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania anayetokana na chama chao, hatimizi majukumu yake ipasavyo.