CCM Arusha kuwafukuza madiwani wake wanne leo

Naima Ernest

Member
Joined
Apr 5, 2013
Posts
41
Reaction score
22
Nimepata habari kutoka kwenye kamati ya siasa ya wilaya ya CCM inayoendelea sasa katika ofisi zao kuwa madiwani wanne watafukuzwa leo.

Mtonyaji anadai kuwa ni ktendo cha madiwani hao kuungana na wale wa CHADEMA, pia inaaminika kuwa hao madiwani ni marafiki wakubwa na mwenyekiti wa CHADEMA wilaya, anayeaminika kuwarubuni.

Juzi ijumaa madiwani wa CCM waliendelea na kikao pamoja na wale wa CHADEMA hata baada ya meya wao kutoka na kususa
 
CCM arusha ilishafutika yamebaki majengo ambayo baadae yatabadilishwa kuwa ofisi za umma na ule uwanja wa sheh Abeidi.
pipoooooz
 
Ni kitu kisichowezekana. Thubutuu! Si Nape Jeetu Patel atakodi hata Ungo apae kuwazuia wasilete balaa hilo! Wanajua wazi wakifanya hivyo, Chadema wanaviokota viti hivyo, ki-ulaiini!!!!
 
Nimepata habari kutoka kwenye kamati ya siasa ya wilaya ya CCM inayoendelea sasa katika ofisi zao kuwa madiwani wanne watafukuzwa leo.

Mtonyaji anadai kuwa ni ktendo cha madiwani hao kuungana na wale wa CHADEMA, pia inaaminika kuwa hao madiwani ni marafiki wakubwa na mwenyekiti wa CHADEMA wilaya, anayeaminika kuwarubuni.

Juzi ijumaa madiwani wa CCM waliendelea na kikao pamoja na wale wa CHADEMA hata baada ya meya wao kutoka na kususa

THUBUTU!!!!! Kwani wamesahau 4 - 0? Kama wana ubavu huo wawafukuze uone kama hawajahamia CHADEMA na kurudia udiwani wao.

Nimekumbuka kale kamkwara ka Kagera ka kukwafukuza madiwani kisha kubatilisha uamuzi..

Chezea wananchi wakielimika wewe!!!!
 
CCM wilaya au Mkoa haina mamlaka ya kuwafukuza madiwani waliochaguliwa na wananchi bila baraka za kamati kuu.

Lakini tuchangie as an entertainment.
 
Nimepata habari kutoka kwenye kamati ya siasa ya wilaya ya CCM inayoendelea sasa katika ofisi zao kuwa madiwani wanne watafukuzwa leo.

Mtonyaji anadai kuwa ni ktendo cha madiwani hao kuungana na wale wa CHADEMA, pia inaaminika kuwa hao madiwani ni marafiki wakubwa na mwenyekiti wa CHADEMA wilaya, anayeaminika kuwarubuni.

Juzi ijumaa madiwani wa CCM waliendelea na kikao pamoja na wale wa CHADEMA hata baada ya meya wao kutoka na kususa

Uwongo mwingine bana haujatulia kabisa,CCM hawawezi na hawako tayari kufanya hivyo,kapate habari za uhakika zaid
 
Mengine tuongee jamani, lakini hili la ccm kumfukuza diwani yeyote wa Arachuga haliwezi tokea, ng'o!.
 
Back
Top Bottom