CCM acheni utapeli kupitia TV, inatia kinyaa

CCM acheni utapeli kupitia TV, inatia kinyaa

Usizungumzie kushindanishwa, hoja unayotakiwa uijibu na utuambie ni lini magufuli alichukua fomu ya kugombea nafasi hiyo ya uenyekiti na kuirudisha? hao wote unaotaka kuringanisha na hicho mnachokifanya huwa wanachukua fomu na kuzirudisha na pia matangazo ya uchaguzi utolewa kwa watu kutakiwa kuchukua fomu, sasa kwa CCM hayo ufanyika?
Katiba ya ccm inasemaje?
 
Tangu lini ccm wakapenda uchaguzi ni magumashi tu
 
Chama Cha Mafisiem
Hakuna Ubishi Ccm Ni Genge La Wasaka Tonge
Ambao Kamwe Wanataka Kufanya Tanzania Ni Yao
 
Mleta mada, kwani CCM wameenda kinyume na katiba yao?

107. (1) Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itakuwa
na wajumbe wafuatao:-
(a) Mwenyekiti wa CCM.
(b) Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wanaotokana na
CCM.

(c) Makamu wawili wa Mwenyekiti wa
CCM.
(d) Rais wa Zanzibar anayetokana na CCM
(e) Katibu Mkuu wa CCM.
(f) Manaibu Katibu Mkuu wa CCM
(g) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa
Organaizesheni.
(h) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa
Itikadi na Uenezi.
(i) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa
Mambo ya Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa.
(j) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa
Uchumi na Fedha.
(k) Wenyeviti wote wa CCM wa Mikoa.
(l) Makatibu wote wa CCM wa Mikoa.
(m) Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Makamu
Mwenyekiti kutoka kila Jumuiya ya
wananchi inayoongozwa au
inayojishirikisha na CCM.
(n) Wajumbe wengine wote wa
Halmashauri Kuu ya Taifa
wanaopatikana kwa mujibu wa vifungu:
92(4)(b); 105(10); 105(15); 106(5)(c) na
108(13)(e).
114

(13) Unapofika wakati wa Uchaguzi,
Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa
itashughulikia mambo yafuatayo:-
(a) Kuteua jina la Mwanachama
atakayesimama
katika uchaguzi wa
Mwenyekiti wa CCM, na majina mawili
ya Wanachama watakaosimama katika
uchaguzi wa Makamu wa Mwenyekiti
wa CCM.

(b) Kupendekeza kwa Mkutano Mkuu wa
CCM wa Taifa majina yasiyozidi matatu
ya Wanachama wanaogombea nafasi
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na kuyawasilisha mbele ya
Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa.
(c) Kuchagua jina moja la Mwanachama
atakayesimama katika uchaguzi wa
Rais wa Zanzibar.
(d) Kuwachagua Katibu Mkuu wa CCM,
Manaibu Katibu Mkuu wa CCM, Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa
Organaizesheni, Katibu wa
Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi na
Uenezi, Katibu wa Halmashauri Kuu ya
Taifa wa Mambo ya Siasa na Uhusiano
wa Kimataifa na Katibu wa Halmashauri
Kuu ya Taifa wa Uchumi na Fedha.
(e) Kuwachagua Wanachama wasiozidi
kumi kuwa Wajumbe wa Halmashauri
Kuu ya CCM ya Taifa kutokana na
mapendekezo ya Mwenyekiti wa CCM.

Duh!! huo ni uchaguzi gani? wakati kinachoonyesha kwenye Katiba ya CCM ni jina moja tu linateuliwa kwa ajili ya kupigiwa kura ikiwa na maana hakuna ushindani wa wagombea zaidi ya mmoja na hakuna uchukaji wala urejeshaji wa fomu za kugombea.
 
mbowe ni mwenyekiti wa maisha wa chadema mtu yeyote ambaye hataki challenge ni mtu wa kumwogopa sana
Mbowe alikuwa katibu mkuu wa Chadema na mwenyekiti aikuwa Bob Makani, nadhani dogo tatizo ni umri huwezi kuyajuwa haya.

Tuanze kumuogopa Magufuli kwanza maana hamna wa kumchallenge kwenye uenyekiti anakwenda kurithishwa kama Usultan.
Mleta mada, kwani CCM wameenda kinyume na katiba yao?
Ndio ni kinyume cha katiba ya ccm, inaikitisha sana mashabiki wengi humu wa ccm hawaijui hata katiba yao inasemaje.

Kingunge alisimama kwenye katiba mkapuuza kwa kifupi ccm haina katiba kwa sasa.
 
Kazi kwenu wafia vyama. Lakini nakumbuka kuna mwenyekiti mmoja alisema waacheni wafu wazike wafu wao. Nyie hamtaki kuwaacha kwanini?
 
unapozungumzia democracy ina maana pana sana democracy si kupiga kura tu ni hata makubaliano ya wengi pia ni democracy vilevile sasa wanachoenda kufanya ccm dodoma ni democracy ya makubaliano au utamaduni wao kama walivyofanya chadema mlimani city kumchagua lowassa ile ni democracy japo kwenye katiba ya chama hakuna kitu kama kile hata ww kuanzisha thread hapa pia ni democracy kuna mfano leo england inaongozwa na wazir mkuu ambae HAJAPIGIWA KURA BALI KATEULIWA HYO NAYO NI DEMOCRACY
Unajuwa ndugu usiandike vitu usivyo na upeo navyo, kwa unwritten constitution ya Uingereza wanachaguwa chama na siyo mtu, wewe kwa sababu IQ yako iko below zero huwezi kulijuwa hili.

Hata South Africa wanachuguwa chama siyo mtu ndio maana Thabo Mbeki alipojiuzuru Urais nafasi ya Urais ilichukuliwa na Montlante wa ANC kwa sababu chama cha ANC ndio kilikuwa na haki ya kutowa Rais kwa miaka mitano ile.

Na hata huko UK hii si mara ya kwanza Tony Blair pia alipoachia madaraka chama chake cha Labour kilimteuwa Gordon Brown kushika madaraka kwa sababu muda wa Labour kuunda serikali ulikuwa haujaisha.

Tanzania tunachaguwa mtu na siyo chama kama wengi mnavyodanganywa na kuaminishwa na hii ndio sababu kuu ya ccm kuvunja katiba yao kulazimisha mtu wao anayechaguliwa ndio awe chama.

Kama una nia ya kujifunza nimekupa elimu ya bure hapo na ndio msingi wa ccm kukataa na wala hawataki mgombea binafsi.

Magufuli ana sifa zote za kusimama kama mgombea binafsi na akaongoza serikali bia majungu ya vyama kwa kutumia sapoti ya umma.
 
Bora ya sisi tunoajiita CCM.......vipi kuhusu nyie mnaojiita DEMOKRASIA....ILI HALI HIYO DEMOKRASIA utekelezaji wake ni SIFURI.....
 
Unajuwa ndugu usiandike vitu usivyo na upeo navyo, kwa unwritten constitution ya Uingereza wanachaguwa chama na siyo mtu, wewe kwa sababu IQ yako iko below zero huwezi kulijuwa hili.

Hata South Africa wanachuguwa chama siyo mtu ndio maana Thabo Mbeki alipojiuzuru Urais nafasi ya Urais ilichukuliwa na Montlante wa ANC kwa sababu chama cha ANC ndio kilikuwa na haki ya kutowa Rais kwa miaka mitano ile.

Na hata huko UK hii si mara ya kwanza Tony Blair pia alipoachia madaraka chama chake cha Labour kilimteuwa Gordon Brown kushika madaraka kwa sababu muda wa Labour kuunda serikali ulikuwa haujaisha.

Tanzania tunachaguwa mtu na siyo chama kama wengi mnavyodanganywa na kuaminishwa na hii ndio sababu kuu ya ccm kuvunja katiba yao kulazimisha mtu wao anayechaguliwa ndio awe chama.

Kama una nia ya kujifunza nimekupa elimu ya bure hapo na ndio msingi wa ccm kukataa na wala hawataki mgombea binafsi.

Magufuli ana sifa zote za kusimama kama mgombea binafsi na akaongoza serikali bia majungu ya vyama kwa kutumia sapoti ya umma.
cdhani kama leo ikitokea mm na ww tukaenda kupima IQ unaweza kunizidi kwanza jambo moja tu ambalo ufahamu wako unaweza ukawa mdogo kama mbegu za mchicha ni mada inazungumzia democracy si constitution na mm nimejikita kwenye democracy si constitution sasa ukitaka kuleta mambo ya katiba inasemaje anzisha thread inayozungumzia katiba kama imevunjwa au aijavunjwa pia nakushauri kuwa unasoma kwanza na kutafakari si kusoma na kukimbilia kujibu unaweza onekana mjinga kumbe ukuelewa swali je milivyo mchagua lowassa pale mlimani city ndo katiba ya chadema inasema vile ??? ukiniuliza mm nitakwambia mlivunja katiba ila mlifanya democracy pia unatakiwa kujua kuna tofauti kati ya constitution na democracy pia unaweza kufanya democracy bila ya kufata katiba ila huwezi kufata katiba bila ya kuapply democracy kama una hoja nyingine leta mezani tujadili hapa ni jukwaa huru na tunatumia democracy yetu kwa kuelimishana na kupeana taarifa
 
hakuna mgombea mwenza,yeye kosa lake lipi,
hajasema kosa ni la JPM, bali mfumo mzima wa chaguzi ndani ya C.C.M.

JPM kama ana kosa ni kule kula maneno yake kwamba hapendi mtu kuwa na vyeo vingi. Lakini yeye mwenyewe cha Rais hakimtoshi.

Ole Sendeka amesema kusimikwa kwa JPM kuwa Mwenyekiti hakufuati Katiba ya C.C.M. bali utamaduni.

Waulizwe wajibu, kwa nini utamaduni na sio Katiba ya C.C.M.?
 
Kama unazungumzia demokrasia ungeanza na mbowe na maalim seif kwanza !
 
Ni vema wakajifunza kusema "NO" where possible sio kila kitu zidumu fikra za mwenyekiti.
 
Kama Katiba ya nchi hupigiwa kura ya ndio au hapana sioni kama kuna tatizo la Mhesh. Magufuli kupigiwa kura ya namna hiyo kutoka kwa wanachama wake. Lengo ni kuona kama wanachama angalau nusu wanamkubali hiyo inatosha maana sio rahisi wananchama wote wakamkubali Ni ukweli usiopingika kuwa haiwezi kutokea wanachama wote kumpigia kura ya ndio labda huyo malaika naye pengine angepingwa hasa na kizazi hiki cha vijana wengi wasomi na wenye miono tofauti na bunifu.
 
NIMESHINDWA kuelewa,wanatumia bl3 na zaidi kwenda kukabidhi chama..kweli ccm mbele kwa mbeke
 
Povu la nini! Mbona upande wa pili lini mara ya mwisho mmefanya uchaguzi? Kwa katiba ipi iliyompa nafasi MR NYEUPE kuwa KIONGOZI MKUU WA GENGE LENU? Sasa hivi Mzee wa kubadilishia GIA ANGANI anahaha! anajuta kumfahamu NYEUPE!
Mr nyeupe kawashika [emoji1]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom