CCM acheni kulialia, hizi ndizo siasa chafu mlizochagua

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Siasa chafu za ubaguzi mlizochagua kuitana wale si wenzetu wale wasaliti, wale si wazalendo ni mbegu mbaya mnayopanda, mnajenga jamii yenye mgawanyiko, mnaligawa taifa kwa matendo yenu.

Lissu alipopigwa risasi serikali ilizuia watu kumfanyia maombi waliojaribu walikamatwa, wabunge wa CCM walizuiwa kwenda kumjulia hali waliopanga walionywa, vijana wa CCM walitoa kejeli pasipo kuzuiwa walisema kajipiga mwenyewe, Ndugai alizuia mshahara wake baadae akamvua ubunge, serikali haikugharamia matibabu yake na vitimbi vingi.

Msidhani nyie kwa vile ni chama tawala mtabaki salama siku zote, niwaambie tu kuna siku na sio mbali wana CCM itakuwa zamu yenu kulia, mtaomba tuwe wazalendo na tuonyeshe utu kwa viongozi wenu.

Dunia ni duara ipo siku itakuwa zamu ya CCM kujeruhiwa tutawakumbusha matendo waliyowafanyia wengine na kuwaomba nao wavumilie.
 
Naweka sawa: nchi haichafuki ila ni wahuni wote waliopanga na kumshambulia Lissu kwa risasi na wale wote wanaohangaika kumnyima haki zake za matibabu na ubunge na wale wote wanaoshangilia madhira aliyoyapata Lissu. Hao wote ni wahuni tu wanaoelezwa ukweli.

Kama ni kuchafuka walishajichafua wenyewe anachofanya Lissu ni kuieleza dunia juu ya wahuni hawa na uhuni wao. Nchi ipo itabaki isipokuwa wahuni watapita kama walivyopita wahuni wengine waliovuruga katiba mpya
 
CCM inatumia mbinu chafu kuendelea kubaki madarakani, bila kuangalia athari zake kitaifa. Chuki kubwa wananchi(wanao jitambua)walio nayo dhidi ya CCM na serikali yake, ni matokeo ya siasa hizo chafu. Inawataka watu kuwa wazalendo huku ikiendesha siasa za ukandamizaji.
 
2183704_IMG_1183.jpg
 
Back
Top Bottom