CCJ yasogeza muda mbele kumjibu Tendwa; "Ni kuhusu timing"..

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Chanzo: Tanzania Daima
na Irene Mark

CHAMA Cha Jamii (CCJ), kimejiandaa kujibu kauli ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, ya kuwa hana pesa za kufanya uhakiki wa majina ya wanachama wao kabla ya kuwapa usajili wa kudumu.

Taarifa za ndani kutoka kwenye chama hicho ambacho kimekutana kwa dharura na kujifungia kwa siku tatu kujadili kauli hiyo, inasema imeshtushwa na kauli za msajili, hivyo kimejipanga kutoa tamko kwa maandishi leo.

Tendwa alikaririwa na vyombo vya habari hivi karibuni akisema kwa sasa ofisi yake haina fedha kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa majina ya wanachama wa CCJ, badala yake fungu lililopo ni kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu sheria mpya ya uchaguzi iliyosainiwa kwa mbwembwe na Rais Jakaya Kikwete Machi 17, mwaka huu.

Aidha, msajili huyo alisema majibu ya kuwa na fedha ama kutokuwa nazo kwa ajili ya kuzunguka mikoani kufanya ukaguzi wa majina hayo, atayatoa Agosti 19 mwaka huu, muda ambao ni vigumu kwa CCJ kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31.

“Ukweli viongozi na wanachama wa CCJ wameshtushwa sana na hii inaonekana ni mbinu ya kutuzuia kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu ujao, hivi ninavyoongea na wewe tangu juzi wanakutana wanajifungia wakijadili suala hilo hilo.

“Kesho watazungumza na waandishi wa habari kuwaeleza nini wamekubaliana kama chama na kuona namna nyingine inayofaa kupitia ofisi ya msajili itakayotuwezesha kupata usajili wa kudumu ikiwezekana kabla ya Juni,” kilisema chanzo hicho cha uhakika kutoka CCJ na kubainisha kwamba tamko hilo kali litatolewa kwa maandishi.

Aidha, chanzo hicho kilihoji kuwa: “Kila mwaka serikali inatenga fungu kwa ajili ya usajili wa vyama vipya, tangu kuanza kwa mwaka huu hakuna chama kilichosajiliwa ni vipi Tendwa anakosa fedha?”

NB:
Majibu hayo yanatarajiwa kutolewa leo saa tano asubuhi kwenye Ofisi za Maelezo. MM
 
Tunaisubiri hiyo saa 5 asubuhi kusikilizia hilo tamko kali!

Kwa maoni yangu, kwa serikali hii kiziwi, sijui hata kama hilo tamko kali litasikika, litasaidia. Dawa ya kiziwi ni hearing aid, ila kwa ukiziwi unaotokana na kuziba masikio kwa wax, dawa yake ni kuyazibua tuu, hivyo na tusubiri hili tamko litaandamana na hearing aid, au litayazibua hayo masikio.
 
JK ana wasiwasi wa kila kitu na wafuasi wake. Unajua yuko kwenye dilema hajui kipi kitamtesa, kifupi haelewi anataka nini.

Hiyo mi nimeiona ni ngwala tu kwa CCJ hakuna kuamka, lakini kujaribu si kushindwa endeleeni kupambana. Mimi mwana sisiem lakini nataka niwanyime watu kura zangu humo ndani harafu nahamia CCJ, nimejiandikisha nina familia ya watu saba wote tuna msimamo mmoja wa kuwanyima kura JK na Makongoro majirani nao wanasema hivi hivi ila nina uhakika wa zangu saba, ukichanganya na zile za wafanyakazi kokotoa mwenyewe.

Wengine niungeni mkono jamani hawa jamaa wasipate kura.
 
Mimi kwa ushauri wangu waende mahakamani. TENDWA na vibaraka wake anaowatumikia wameshaamua kuwa Chama hiki hakipati usajili wa kudumu, and they will stand for that. Ni vyema hawa jamaa wakawahi mahakamani ambapo haki inapatikana. Or else, they will be late and foudn themselves thrown out of teh game this year.
 
Lakini kwa mwenye kumbukumbu nzuri atakubaliana nami kuwa Tendwa alishaonesha nia ovu tangu awali aliposema kuwa CCJ hata ikikamilisha masharti, ni lazima usajili wake ufanyike baada ya miezi 6 iliyowekwa na sheria na sio chini ya hapo. Ushauri wangu ni kuwa CCJ ijiandae kwa lolote na ikibidi ijiandae kufanya shughuli zake bila kujali kuwa haitashiriki kwenye uchaguzi wa mwaka huu.
 
mi nauona mkono wa JK wazi wazi hapo, ofisi haina pesa namna gani?
na mbona haijafungwa? itaendesha vipi shughuli zake, inakuwa haina pesa
wakati wa kukishughulikia CCJ tu?

maana hata shule za bweni hufungwa zikikosa chakula,
 
wanza huyu tendwa alikuwa naongea kwa nyodo sana siku ile
yaani nikajua chama chetu hakitapata usajili mwaka huu

aliongea kwa majigambo sana huyu bwana, hana maana kabisa na kingereza chake cha uchochoroni
 
Ngoja tusubirie tamko la CCJ huenda likabadili sura ya SIASA za Bongo
 
wanza huyu tendwa alikuwa naongea kwa nyodo sana siku ile
yaani nikajua chama chetu hakitapata usajili mwaka huu

aliongea kwa majigambo sana huyu bwana, hana maana kabisa na kingereza chake cha uchochoroni

Alikuwa anatania tu wewe huujui utani wa Tendwa?
 
Vuta subira GS mbona unakuwa na Haraka ya Kusomea Barua ndani ya Bahasha! teh teh teh

Yani nina haraka kuliko upesi,nina muwasha washa wa kujua hilo tamko je litabadilisha hali ya hewa au ndio yale yale tu!.Na hivi leo niko free sibanduki humu,sichezi mbali unga wenyewe robo...
 
Yani nina haraka kuliko upesi,nina muwasha washa wa kujua hilo tamko je litabadilisha hali ya hewa au ndio yale yale tu!.Na hivi leo niko free sibanduki humu,sichezi mbali unga wenyewe robo...

Leo tuko hapa!

Sahihi yako: Jimbo gani huenda ukaanza kuhesabu kura yako leo hii
 
Daa,tuko wengi inatia raha...Mmh Mkuu kusema jimbo in public watu tayari watajua mimi ni nani,si unajau tena majina bandia na uhuru wa kuongea?NitakuPM..

Haina tatizo, kwa maana mimi nimeshatangaza waziwazi kura yangu kokote nitapokuwa Ubunge na Udiwani kwa CHADEMA
 
JK ana wasiwasi wa kila kitu na wafuasi wake. Unajua yuko kwenye dilema hajui kipi kitamtesa, kifupi haelewi anataka nini.

Hiyo mi nimeiona ni ngwala tu kwa CCJ hakuna kuamka, lakini kujaribu si kushindwa endeleeni kupambana. Mimi mwana sisiem lakini nataka niwanyime watu kura zangu humo ndani harafu nahamia CCJ, nimejiandikisha nina familia ya watu saba wote tuna msimamo mmoja wa kuwanyima kura JK na Makongoro majirani nao wanasema hivi hivi ila nina uhakika wa zangu saba, ukichanganya na zile za wafanyakazi kokotoa mwenyewe.

Wengine niungeni mkono jamani hawa jamaa wasipate kura.

Kwani kupiga kura mpaka uwe mwanachama? Kama wamekuchukiza sasa bado unasubiri nini humo? Unaongelea kuhama CCM au kutoipigia kura CCM?
 
Back
Top Bottom