Ccj watua chadema, baada ya kwata ya msajili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccj watua chadema, baada ya kwata ya msajili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kinepi_nepi, Jun 7, 2010.

 1. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  CCJ wamesema leo kwenye mkutano wa kukabidhi form ya kinyang'anyiro cha ubunge wa ubongo kuwa wanaungana na Chadema.
   
 2. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ni wazo zuri kama CCJ wakinyimwa uchaguzi wakaamua kuiunga mkono CHADEMA safi sana. Ndo tunataka mitazamo kama hiyo si tu kukimbilia kutaka uongozi. Na kwa sasa chama madhubuti cha upinzani ni CHADEMA!. Japo baadhi ya watu wasio makini wanatia shaka CAHDEMA! lakini mtu msomi na muadilifu na mtafiti atajua kuwa CHADEMA ndicho chama kwa sasa kinaonyesha nia...Mimi nashauri Wale vingunge waliotegemewa CCJ nao waiunge CHADEMA Mkono kwa dhati katika mchakato wa uchaguzi.....Vinginevyo nitaamini kuwa nia yao ilikuwa uchu wa madaraka tu. Kwa upande wa pili nashanga sana mkaguzi alisema hana bajeti ya kuhakiki CCJ! Je hiyo ya sasa kaipata wapi?
  Haya ndo mambo ya kifisadi tunayosema! iweje azungushezungushe zoezi leo aanze kuhakiki?!! Naongea hili kwani nimeenza kuona dalili za msajili kuinyima CCJ nafasi. Inawezekana kuna mkono wamtu hapo!
   
 3. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Du nimeiona hii kwenye gazeti la Mwananchi la tarehe 7 june 2010 Kurasa wa tatu. Any way kwanza ni mtu mmoja tu naye cheo chake ni Naibu Katibu Mkuu anaitwa Dickson Ng'hily ( ngoja mwanakijiji aamke atakavyo mkemea kwa nini anatangaza kusupport chama kisicho na itikadi si afadhali angeenda CCM ) . lakini hata hivyo inatia matumaini kuwa kumbe kuna wapiganaji wa kweli ndani ya CCJ. Hawa walioanza kutukana matusi na kudharau vyama vingine wakasahau hata mazuri ingawa ni machache yaliyofanywa na wapiganaji wetu halisi (sio hawa wanataka kuhama kisa mizengwe ya primaries)
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Maigizo at best. Mwanakijiji yupo wapi afanye clarufikesheni.
   
 5. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ha ha haaa , Mtego huo hapa wanagombanishwa watu, ha ha ha ili ionekane CHADEMA imeiwekea CCJ kauzibe isisajiliwe teh teh teh, hamna kitu hapo
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  He he..halafu ndio waje walete mabadiliko..THUBUTUUU..vyama vya siasa vyote ni usanii tu.
   
 7. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  CCJ sasa yatangaza ushirika na Chadema Monday, 07 June 2010 09:03
  Geofrey Nyang’oro

  UTATA uliogubika usajili wa Chama cha Jamii CCJ umekifanya kuamka na kutafuta washirika, baada ya jana kutangazia wafuasi wake wauunge mkono Chadema kama msajili huyo hatawapa kabisa usajili wa kushiriki uchaguzi wa Oktoba.

  Kauli hiyo ya kwanza ya CCJ kutangazia wafuasi wake kuunga mkono Chadema inakuja kipindi ambacho chama hicho kimetangaza kufungua kesi mahakamani kutaka uhakiki wa wanachama wake usitishwe kwa tuhuma za kukiukwa taratibu.

  Naibu Katiba Mkuu wa CCJ Dickson Ng'hily, alitangaza hilo kwa kutaka Watanzania kuunga mkono Chadema kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba kwani lengo la kuanzishwa chama hicho ni kuiondoa CCM madarakani.

  Ng'hily ambaye kiongozi ni msaidizi wa mtendaji mkuu wa chama, alitoa kauli hiyo wakati wa matembeza ya amani yaliyoandaliwa na Chadema, maalumu kwa ajili ya kurudisha fomu kwa wanachama wanaotaka kuwania nafasi za ubunge na udiwani kwa jimbo la Ubungo.

  “Wakati tunaanzisha CCJ tuliwaambia CCM kuwa watanzania wamechoka na wanataka mabadiliko, kwakuwa lengo kuu la CCJ ni kuleta mabadiliko niwaombe watanzania kuunga mkono Chadema kwani sera zake zimeonyesha dhamira ya kweli ya kufikia huko,”alifafanua Ng'hily

  Aliongeza kwamba, kauli mbiu ya Chadema kwamba, ‘‘hakuna kulala hadi kieleweke inaonyesha wazi kuwa wanachama hao na viongozi wao wamejitoa mhanga kwa ajili ya kutetea rasilimali za watanzania.’’

  Katika hafla hiyo iliyoambatana na matembezi ya umbali wa kilomita nne kutoka uwanja wa mikutano Manzese hadi Kimara zilipo ofisi za Chadema, mkoa wa Kinondoni, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na uhusiano wa kimataifa wa Chadema John Mnyika, alirudisha fomu ya kuwania kiti cha ubunge wa jimbo hilo.

  Akizungumza mara baada ya kukabidhi fomu hiyo katika hafla hiyo iliyojaa shamrashamra za aina yake, alisema Tanzania inahitaji mabadiliko ya uongozi ya uongozi ili iweze kuendelea.

  “Tunaingia kwenye uchaguzi mkuu huku tukijua kuwa nchi inakabikliwa na matatizo lukuki yanayotokana na utawala wa Mfumu wa chama kimoja cha siasa, tunakabiliwa na tatizo la katiba yenye upungufu, tume isiyo huru na mzigo wa viongozi mafisadi
  kutoka CCM wenye fedha za kununua uongozi,”alisema Mnyika.

  Source: Mwananchi

  Wanachama wa CCJ wana haki ya kushiriki uchaguzi, kama chama chao hakitapa usajili wa kudumu basi washiriki kama wagombea binafsi au kwa kujiunga na vyama vingine,
   
 8. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  dah!
  mwaka huu hapataenea!
   
 9. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Bad move for a CCJ kwasababu CCJ and Chadema wana ideology tofauti swali linakuja wataendana? Labda wameshakubaliana but nadhani it is a time bomb
   
 10. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ideology ya CHADEMA ni ipi na ya CCJ ni ipi, na CCJ ina Malengo gani na ya CHADEMA ina malengo gani?
   
 11. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hata Conservative wakati wanafanya kampeni hawakujua watakuja ungana na Liberal.
   
 12. 911

  911 Platinum Member

  #12
  Jun 7, 2010
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Its a very complicated task to model the African politics!
  Kuna tatizo kubwa sana la vyama vya siasa hapa Tanzania kukosa msemaji wa chama.Yani utakuta chama ni kimoja ila kila mtu na kauli yake kwenye media.Kibaya zaidi kauli hizo zinapokuwa zinapingana waziwazi.
   
 13. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #13
  Jun 7, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kama CCJ wamekwama kwenye usajili wasubiri hadi 2015 wakati wanajiandaa kupata usajili wa kudumu. Kujiunga na vyama vingine na watu wao kutimkia kwenye vyama vingine ili kugomea udiwani/ubunge ni kuangalia kwenye pua. Huwezi kumwambia mchumba wako kwamba unaenda ngambo kusoma, meanwhile, akakae na bwana mwingine mpaka utakapo rudi masomoni. Ukirudi utamkuta si wako!
   
 14. W

  WildCard JF-Expert Member

  #14
  Jun 7, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  CCJ haipo tena mwaka huu. Walikosea kuwatanguliza hawa ma-novice wa siasa zetu hapa. Wajipange upya tu.
   
 15. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #15
  Jun 7, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Demokrasia huwa haisubiri haiwezi kuacha gape lazima iji fix mahali, ikiacha gape linajazwa na aidha utawala wa kijeshi au wa kidikteta au wa kiimla, unapowaambia wanachama wasubiri hadi 2015 wakati huo watakuwa wanafanya nini.
   
 16. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #16
  Jun 7, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  This is a failed and abortive plan of CCM imewageuka walivyodhani(divide and rule) imekuja ndivyo sivyo, very sad my friends try another move.
   
 17. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #17
  Jun 7, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ahadi za JK hazijatekelezwa-Mnyika


  [​IMG]Monday, 07 June 2010 06:54
  Na Godfrida Jola
  MKURUGENZI wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. John Mnyika jana alirudisha fomu za kuomba kuwania ubunge katika Jimbo la Ubungo na kumshutumua Rais Jakaya Kikwete kuwa ameshindwa kutekeleza ahadi alizotoa kwa Watanzania, likiwamo la kuleta maji Dar es Salaam.
  Akizungumza katika mkutano wa hadhara kabla ya kurejesha fomu hizo, Bw. Mnyika alisema pamoja na ahadi hiyo ya maji kutotekelezwa na Rais Kikwete kuwatupia mzifo Dawasa na Dawasco, pia ameendelea kutoa 'ahadi hewa' zinazoongeza ugumu wa maisha kinyume na alivyoahidi maisha bora kwa kila Mtanzania wakati anaomba kuchaguliwa.

  Akihutubia mkutano huo uliojaa mashabiki wake na wasikilizaji wengine katika eneo la Manzese, Bw. Mnyika alisema baada ya kuingia madarakani serikali ya awamu ya nne kumekuwa na kero nyingi kutokana na viongozi wengi kuwa wabinafsi na hivyo kutumia fedha za umma kujilimbikizia mali.
  "Tulitegemea serikali kufufua viwanda vilivyokufa ili kuwapatia ajira wamachinga na mamalishe wanaohangaika katika viwanda hivyo, lakini mambo yamekuwa kinyume na matarajio," alisema Bw. Mnyika.
  Alisema mabadiliko ya kweli yatapatikana kwa wananchi kupiga kura kuwachagua viongozi wanaopenda maendeleo.
  Bw. Mnyika alikosoa kauli aliyoitoa Rais Kikwete wakati wa ziara yake jijini Dar es Salaam hivi karibuni kuwa anawafahamu kwa majina madiwani wanaouza viwanja na kuwaonya, kuwa ina nia ya kuwalinda wezi.
  "Kama Kikwete hatachukua hatua dhidi ya madiwani na meya, suala la kuuza viwanja vya wazi na vya umma, litafikishwa kwa wananchi kuamua," alisema Bw. Mnyika
  Alisema mfumo wa sasa umekuwa wa wananchi kutumikishwa na viongozi kwa maslahi yao badala ya viongozi kuwatumikia wananchi kama inavyotakiwa.
  Mkutano huo ulisindikizwa na maandamano yalioanzia Manzese hadi Ofisi za CHADEMA Jimbo la Ubungo kurudisha fomu.
  Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Jamii (CCJ), Bw. Dickson Ng'hily aliyesema demokrasia haiwezi kuwepo kama nchi itaongozwa na chama kimoja kwa muda mrefu.
  "Tumeungana na CHADEMA ili kuwatia moyo Watanzania kuwa hatutakiwi kulala mpaka kieleweke, tunatakiwa kupigana imara hadi tupate maisha bora kwa kuchagua viongozi bora," alisema Bw. Ng'hily.

  Source: Majira

  MyTake: Jamaa ameonesha Mwanzo Mzuri sana na CHADEMA wafanye hivyo katika yale maeneo yanayoonekana CCJ, CUF, TLP nk vina Nguvu. Tunahitaji Bunge lenye nguvu liweze kutindua Mifumo mibaya ambayo imekuwa ikizalishwa na kulelewa na bunge lenye wingi wa Wabunge kutoka chama kimoja tena kilicho madarakani
   
 18. W

  WildCard JF-Expert Member

  #18
  Jun 7, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mnyika,
  Wewe haujawahi kuahidiwa U-Minister kama mwenzako Zitto?
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Jun 8, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Naam haya ndio maneno..Sasa naupamba mjadala huu kwa kuamsha munkari za watu...

  Kila kitu kina mwanzo wake na napenda sana kumshukuru Mwanakijiji ambaye amekuwa hapa kijiweni akikusanya mawazo mbali mbali ya watu, hivyo kuweza kufikisha ujumbe huu kunakohusika. Binafsi nilijua Mzee Mwanakijiji kuuliza maswali mengi na yenye utata mkubwa alikuwa na lengo kubwa zaidi ya kudadisi, hivyo natanguliza shukran maanake Katibu wa CCJ amezungumza kama tulivyotumia muda mrefu kumshauri Mwanakijiji...

  Kinachofuata CCJ na Chadema ni kukaa meza moja na kuanza kuwachuja wagombea. Wale ambao walioko vyama vingine ambao wako tayari kujiunga na nguvu hii mpya na wameonyesha nia kubwa ya kufanya mageuzi ya Utawala kulingana na agenda zitakazo pangwa, wapewe pia support kupitia vyama vyao..

  Maadam Imeshindikana kabisa vyama hivi kuunda chama kimoja basi mshikamano wa aina hii unaweza kuwa hatua ya kwanza muhimu sana isipokuwa mnahitaji kuepuka makosa yaliyofanyika huko nyuma ktk mshikamano ulokuwa baina ya CUF na TLP na Chadema. Nina hakika Mapandikizi wanajulikana na huu ndio wakati wa kuwaacha solemba.

  Muhimu mchague wagombea ambao kwanza wana uwezo ikiwa ni pamoja na kuzungumza, Elimu ya kutosha na bila kusahau maarufu (popular)... Hili la mwisho mnaweza kulidharau lakini ni muhimu sana kulizingatia kwani toka Uhuru ni asilimia zaidi ya 80 hushinda kwa sababu ya Umaarufu wao..Na ndio maana hawa wabunge wa CCM waliendelea kuchaguliwa kila uchaguzi hata kama hawakufanya vizuri..Yapo majimbo ambayo CV ya mtu ni muhimu zaidi kuliko Umaarufu hilo litumike pia ktk kampeni zenu..Tunarudi palepale - WATU na MAZINGIRA..
  Sii kazi rahisi lakini nina hakika maadam wananchi wametangaziwa Mshikamano huu tayari matumbo yanaanza kuloloma hadi kwapa kuwawasha CCM, kwa sababu hawajui hatma ya Mshikamano kama huu dakika za mwisho.

  Bado nguvu kubwa inatakiwa kuunganisha wanachama wa vyama vingine...Nitarudia kusema ni nguvu ya watu wananchama na sio Chama kama chama inayoweza kutupa Ushindi. Hivyo ni kazi ya viongozi wa vyama hivi kuweka wazi support zao ktk majimbo ambayo yamegombewa na chama cha ushirika huu. Lengo ni kumng'oa CCM madarakani, kwa sababu ameshindwa kutimiza wajibu wake..Wajibu ambao tunaelezwa na wazee wetu kama Salim A. Salim aliposema haya:-

  The struggle for freedom was not merely that of regime change. It was intended to ensure larger freedoms including the right to decide how we are governed, by whom and for what period. It was to remove injustice and ensure that the country's resources are utilized for the betterment of our peoples. It was to fight disease, ignorance and abject poverty.
   
 20. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #20
  Jun 8, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  kumbe wana akili zao timamu.
   
Loading...