CCJ kuwasilisha wanachama wa mikoa 10 Jumatatu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCJ kuwasilisha wanachama wa mikoa 10 Jumatatu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Luteni, Mar 16, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Chama Cha Jamii (CCJ), Jumatatu ijayo kitakwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, kuomba usajili wa kudumu baada ya kutimiza sharti la kupata wanachama 2,000 katika mikoa 10.

  Chama hicho kimevuka kiwango cha idadi ya wanachama wanaotakiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa kwa ajili ya kupatiwa usajili wa kudumu, baada ya kufanikiwa kupata wanachama 7,000 badala ya wanachama 2,000 waliotakiwa kupatikana katika mikoa 10 ya Tanzania Bara na Zanzibar.

  CCJ kimepata mafanikio hayo katika kipindi cha siku 15 tangu kipatiwe cheti cha usajili wa muda Machi 2, mwaka huu.

  Kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, chama chenye usajili wa muda kinatakiwa ndani ya siku 180 kiwe kimepata wanachama 200 kwa kila mkoa kwa walau mikoa 10 ya Tanzania Bara na Zanzibar, ambapo CCJ ilipewa muda iwe imekamilisha suala hilo hadi Novemba, mwaka huu.

  Kutokana na mafanikio hayo, chama hicho kimesema kinatarajia kuwasilisha kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini orodha ya wanachama kilichowapata katika mikoa hiyo, Jumatatu kuomba kupatiwa usajili wa kudumu.

  Katibu Mkuu wa CCJ, Renatus Muabhi, aliitaja mikoa ambayo chama hicho kimefanikiwa kuvuna wanachama hao kuwa ni Mwanza, Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya, Shinyanga, Tabora, Pwani, Dar es Salaam na Unguja na Pemba.

  Alisema katika mikoa hiyo waliteua watu kwenda katika mikoa hiyo kuandikisha wanachama na kwamba, katika kila mkoa walipeleka kadi 700 na hadi kufikia jana taarifa walizozipata kutoka vyanzo vyao katika uendelezaji wa uandikishaji wa wadhamini wanaowahitaji, zimethibitisha kwamba, kadi hizo zote zimeisha.

  “Kwa hiyo sasa hivi tume-stop tangu jana, ni kwamba, tunatengeneza hizo kadi sasa, kwa maana ya kuendelea tena kuzigawa,” alisema Muabhi katika mkutano na waandishi ulioandaliwa na chama hicho kwa mara ya kwanza, jijini Dar es Salaam jana tangu kipatiwe cheti cha usajili wa muda.

  Alisema mafanikio hayo yanaashiria jinsi gani Watanzania walivyoweza kukiunga mkono chama chao.

  “Kwa hiyo, tumeona kwamba itakapofika tarehe 22, mwezi huu, kama hakutatokea tatizo lingine, ambalo liko juu ya uwezo wetu, tutakwenda kuwasilisha kwa Msajili wa Vyama Siasa, John Tendwa idadi ya hao wadhamini, kwa maana ya wanachama 200 katika kila mkoa katika mikoa 10,” alisema Muabhi.

  Naye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCJ, Dickson Amos, alisema wakereketwa wa CCJ Morogoro waliwaomba kadi 3,000.

  Katibu Mkuu huyo alisema wanatarajia kufanya uzinduzi rasmi wa CCJ na shughuli zake Machi 21, mwaka huu.

  Alisema wameshakamilisha taratibu zote za kiofisi, hivyo wanataka sasa kukitambulisha chama hicho kwa Watanzania kwamba chama chao kiko imara na kiko tayari sasa kwa kazi.

  Aliwataka wananchi kujitolea kuiunga mkono CCJ, ikiwa ni pamoja na kujiandikisha kwa wingi, kujitolea ofisi sehemu mbalimbali kutokana na mahitaji yatakayojitokeza kwa sababu chama hicho ni cha wananchi.

  “Sababu ya kusema kwamba, wao inatakiwa waguswe moja kwa moja na ujio wa CCJ ikiwa ina malengo ya pekee kabisa na ya makusudi kabisa kwamba, imedhamiria kurudisha hadhi ya taifa la Tanzania, ambayo iliasisiwa na Baba yetu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,” alisema.

  Akitilia mkazo suala hilo, Amos, alisema katika uzinduzi huo, watapokea wanachama wapya, ambao baadhi yao wamewahi kushika madaraka makubwa ndani ya vyama vingi vya siasa.

  Alisema viongozi wa CCJ wanatarajia kufanya ziara kwenda kuzuru makazi ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, Butiama, wilaya ya Musoma Vijijini, mkoani Mara kesho.

  Alisema katika ziara hiyo, wanataka kwenda kuona kaburi la Mwalimu Nyerere na kufanya mazungumzo na familia yake, ikiwa ni sehemu ya kuthamini na kujali mchango wake katika taifa la Tanzania kama muasisi wake.

  Alisema wako viongozi wengi nchini, ambao ni waasisi wa taifa, wamekuwa na heshima kubwa, hivyo ilistahili nao wawape umuhimu wa hali ya juu kwa kuwafanyia ziara.

  Hata hivyo, alisema wameona kwa sasa wajaribu kuanzia kwa hayati Mwalimu Nyerere, ambaye tayari ana heshima ya pekee, kwa kuwa anatambuliwa rasmi kama Baba wa Taifa.

  “Kwa hiyo, hata wale waasisi wengine, napenda kutumia fursa hii kutoa shukrani za dhati kabisa kwamba, tuko nao na tunawathamini na tunathamini michango yao waliyoitoa katika taifa hili,” alisema Muabhi. Alisema watakapomaliza ziara ya Butiama kwa Mwalimu Nyerere, watakwenda kufanya mkutano katika eneo walikouawa kikatili watu 17 hivi karibuni, wilayani Musoma ambako watazungumza na wananchi wa eneo hilo pamoja na wazee. Muabhi alisema katika mazungumzo hayo watatoa usia wao kwa wazee hao pamoja na Watanzania wengine juu ya tukio lilitokea hapo kwamba, halikuwa la kawaida na halikustahili kuwapo katika misingi ya kibinadamu.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kila la heri CCJ..kweli nia mnayo na dhamira yenu ni ya dhati kabisa...Go CCJ GO!
   
 3. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Mbona faster hivi? watamchanganya Tendwa hawa, mzee kapewa kibarua cha kuhakikisha hakishiriki uchaguzi lakini...mmh...itakuwaje sasa!
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Mar 16, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Ngojeni tu kipate usajili wa kudumu kwanza..
   
 5. manenge

  manenge JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2010
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa kasi hii nadhani mtavunja rekodi ya kuwa na wanachama wengi kuliko vyama vingine hongereni sana
  Angalizo: muwe makini msije mkachukua mamluki watakiua chama mapema
   
 6. M

  Msharika JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Congrants ccj, that is enough alart for chama cha mafisadi
   
 7. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  CCM sasa jeneza linachongwa manzese, sijui kitazikwa wapi. Tendwa anayo kazi ya ziada kukitetea, labda naye atahamia CCJ hivi karibuni.

  Kuweni makini CCJ, mnakumbuka Mrema Lytonga alivyovuma kwanza halafu ikageuka nguvu ya soda? Msiruhusu ubinafsi na kupenda sifa ndani ya chama.
   
 8. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Mrema ana kazi yake maalum anayoitekeleza ktk upinzani.
   
 9. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Isije kuwa yale yale ya Mrema nakumbuka 1995 naye alihamia upinzanzani miezi kama hii karibu na uchaguzi na kuvuruga kila kitu
   
 10. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180

  Tuwe makini tusijeanza sukuma gari la mtu bure hapa.
   
 11. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Jamii (CCJ), Richard Kyabo (kulia), akiangua kilio baada ya yeye na Katibu Mkuu wake, Renatus Muhabhi, kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, katika kijiji cha Butiama mkoani Mara jana.
   
 12. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Duuuh kazi kweli kweli
   
 13. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mi hawa siwaelewi kabisa, ni kina nani tena hawa? mbona walivuma sana kabla hawajajitokeza? but mmh I cant read them!
   
 14. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kusema kweli na mm siwaelewi but something is behind this, akijitokeza mwenye nacho atapigwa rungu
   
 15. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Unashangaa nini katika kutafuta kura za kula sarakasi za kila aina lazima zitumike
   
 16. M

  MILKYWAY GALAXY JF-Expert Member

  #16
  Mar 19, 2010
  Joined: Dec 12, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mhh!
  Time will tell.
   
 17. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #17
  Mar 19, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  CCJ waibukia kwa Nyerere(Nipashe)

  [​IMG] Wabubujikwa machozi kaburini kwake
  [​IMG] Wahutubia hadhara, kadi kama njugu

  Viongozi wa Chama Cha Jamii (CCJ) jana walifanya ziara nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, na kufanya mazungumzo na wanafamilia hiyo.

  Viongozi hao walikutana na mkuu wa familia hiyo, Chifu wa Wazanaki, Japhet Wanzagi na mmoja wa watoto wa Mwalimu, Madaraka Nyerere.

  Viongozi wa CCJ waliotembelea familia hiyo ni Mwenyekiti, Richard Kyabo na Katibu Mkuu, Renatus Muabhi.

  Mbali na Chifu Wanzagi na Madaraka, mazungumzo hayo pia yaliwahusisha wazee mashuhuri wa kijiji cha Butiama.

  Katika mazungumzo hayo, Chifu Wanzagi alionekana kutoridishwa na jinsi sera ya ubinafsishaji ilivyoshindwa kuwaondoa Watanzania katika dimbwi kubwa la umaskini.

  Alisema kuwa ubinafsishaji huo ungefanyika wakati wa Mwalimu Nyerere, asingevumilia hali hiyo.

  Chifu Wanzagi alisema ingawa yeye ni mwana-CCM damu ambaye hawezi kukihama chama hicho kikongwe, lakini sera ya ubinafsishaji imeshindwa kabisa kuwasadia Watanzania kuondoka katika umaskini.

  "Mimi ni mwa-CCM, lakini kwa kweli sijui leo Mwalimu (Baba wa Taifa) angekuwepo angesema nini. Haiwezekani nchi ikatoa madini kwa watu wa nje, tena kwa bei poa huku wananchi wanaozunguka migodi hiyo wakikabiliwa na umaskini mkubwa, jambo hili linatusikitisha sana," alisema Wanzagi, ambaye pia ni msemaji wa familia hiyo.

  Alipongeza uanzishwaji wa chama hicho kwa kutambua kuwa kila Mtanzania ana haki ya kuchagua kujiunga na chama chochote cha siasa chenye lengo la kuleta mabadiliko katika nchi bila kuathiri umoja wa kitaifa.

  Naye Madaraka alisema Butiama ni eneo la kila Mtanzania kwa kuwa ndipo alipozikwa Baba wa Taifa, hivyo kila mtu au chama cha siasa kina haki ya kufika na kutoa heshima katika kaburi la kiongozi huyo.

  "Butiama ni ya Watanzania wote, hivyo kila chama au mtu ana haki ya kufika kwa lengo la kuona kazi mbalimbali zilizofanywa na Baba wa Taifa wakati wa uhai wake, ambazo zimehifadhiwa katika makumbusho yake na kuona sehemu alipozikwa," alisema na kuongeza:

  "Tena bila ya ubaguzi wowote, kama mwenyewe alivyokuwa akituasa Watanzania leo na kesho kuwa wamoja na kabila lao ni Tanzania."

  Kyabo alisisitiza kuwa lengo kuu la kuanzishwa kwa chama hicho ni kuhakikisha kinaenzi mema yote yalipiganiwa na Baba wa Taifa kwa maslahi ya Watanzania wote ingawa sasa yameonekana kusaulika.

  Alisema ndani ya CCJ, rushwa na ufisadi ni ajenda ya kwanza ambayo itasimamiwa kikamilifu.

  Alisema vitendo hivyo vilionekana wazi kumkera Baba wa Taifa kutokana na kusababisha kuwepo kwa baadhi ya watu wachache wanaonufaika na rasilimali za nchi huku idadi kubwa ya Watanzania ikiwa katika lindi kubwa la umasikini.

  "Leo tumekuja kuona mahali alipompumzishwa mwasisi wa Taifa la Tanzania ikiwa ni uzinduzi wa safari yetu ya nchi nzima kuelezea misingi yote iliyowekwa na Baba wa Taifa kwa nchi hii kwani CCJ inathamini kwa dhati michango hiyo, hiyo ndio sababu tumekuja kuwaeleza kuwa Mwalimu tutamtumia kila kona ya nchi yetu," alisema mwenyekiti Kyabo.

  Naye Muabhi alisema kushamiri kwa vitendo vya rushwa na ufisadi kunatokana na maamuzi ya viongozi wa CCM kukiuka misingi mizuri iliyoasisiwa na Baba wa Taifa kwa kuanzisha Azimio la Arusha ambalo walidiriki kuliua ili kupata mwanya wa kujineemesha.

  "Narudia kuwajulisha kuwa CCJ tunathamini sana misingi iliyowekwa na Baba wa Taifa katika uongozi wa nchi hii, ndio maana tutatumia nguvu zetu zote kuirejesha kupitia CCJ baada ya wao kuua Azimia la Arusha, baada ya kubaini linawaumbua," alisema.

  Hata hivyo, viongozi hao walionekana kububujikwa machozi wakati wakiweka mashada ya maua katika kaburi la Hayati Mwalimu Nyerere, hali ambayo iliamsha simanzi kubwa kwa baadhi ya wananchi na wazee wa kijiji cha Butiama waliofika kuonana na viongozi hao.

  Baadaye viongozi hao walifanya mkutano wa faragha ndani ya nyumba ya Baba wa Taifa kati yao na Madaraka na Chifu Wanzagi. Hata hivyo, baada ya kukutana, wote walikataa kueleza kilichozungumzwa kwa zaidi ya nusu saa.Baada ya kutoa kijijini Butiama, viongozi hao wa CCJ walikwenda katika mtaa wa Bugharanjabho, Kata ya Buhare katika Manispaa ya Musoma na kutoa pole kwa familia tatu zilizokumbwa na mauji ya ndugu zao 17 waliouawa kikatili kwa kukatwa mapanga usiku wa Februari 16, mwaka huu.

  Na katika hatua nyingine, umati wa wakazi wa mjini hapa na vitongoji vyake, jana walijitokeza kununua kadi za CCJ wakati wa mkutano wa uzinduzi wa chama hicho uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo.

  Mkutano huo uliohutubiwa na viongozi wa kitaifa wa chama hicho na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya vijana, wafanyabishara na baadhi ya wananchi wa kawaida.

  Wananchi walikuwa wakiimba kuwa sasa ni wakati wa ukombozi kutokana na kujinasua kutoka katika makucha ya wakoloni.

  Aidha, katika mkutano huo, wananchi hao walimchagua Mwenyekiti wa muda wa CCJ mkoani Mara, Sospiter Manumbu, ambaye atasimamia shughuli zote za chama hicho ikiwemo kutafuta ofisi rasmi ya mkoa na kufungua ofisi za wilaya mkoani Mara.

  Licha ya mkutano huo kumalizika saa 12:00 jioni, bado kulikuwa na mamia ya wananchi waliokuwa wamefoleni katika viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo wakisubiri kununua kadi za chama hicho kipya.
   
 18. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mkuu luteni sisi macho yetu mana hii style ya CCJ sijui....
   
Loading...