CC ya CCM haikuwa na jipya

CC ya CCM haikuwa na jipya

Wanatumia 'hekima na lugha ya staha' kuhakikisha kuwa chama chao hakipasuki na kuendekeza migogoro .Hivyo aliyeiba na asiye mwizi wote ktk kukijenga chama chao! Hii ni kwa Tanzania tu.
 
Kamati Kuu ya CCM iliyoketi leo Kisiwandui,Zanzibar ilitawaliwa na pongezi pamoja na maagizo ya hapa na pale ya kichama. Taarifa za kuaminika toka ndani ya kikao husika zinaonesha kuwa CC imepitisha karibu maazimio yote ya Kamati ya Komredi Mangula.

CC imepongeza ushindi kwenye Serikali za Mitaa. Pia CC imeipongeza Kamati Maalum ya Maadili chini ya Komredi Mangula kwa kuwabana na kuwarekebisha wagombea watarajiwa wa Urais.

"Hapo CC imesifu na kupongeza mwenendo wa wahusika kwasasa na kuwaona wanaofuata taratibu za chama. Hakukuwa na mjadala mkali kama ilivyotarajiwa" kilisema chanzo hicho toka Kisiwandui.

CC pia imempongeza na kumpa baraka Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa jinsi anavyoendelea kulishughulikia kwa weledi sakata la Escrow. Mwenyekiti ameahidi kuwa makini na mtenda haki katika hilo.

CC imeiagiza Sekretarieti ya CCM kufanya maandalizi kabambe ya Kura ya Maoni na uchaguzi mkuu kwa kutoa Ripoti mara kwa mara juu ya mikakati inayoendelea. Sekretarieti imeruhusiwa kuunda kamati mbalimbali za wataalamu ili kufanikisha maandalizi hayo.

CC imetambua na kupongeza ziara za kuimarisha chama na kukagua utekelezaji wa Ilani zilizofanywa na Sekretarieti chini ya Katibu Mkuu Kinana.

"Hayo ndiyo makubwa humo. Kikao hakikuwa na mjadala mkalí. Kilitawaliwa na busara" kimesema chanzo cha taarifa hii.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Asante mzee Throw-throw wa Lumumba, tulijua huko mambo mdebwedo tu.
 
Ningeshangaa kusikia mtu kafukuzwa..........CCM ninayoijua Mimi?
 
Kikao hicho kinathibitisha ule msemo unaosema ukishangaa ya Mussa utayaona ya Firauni!

Hivi watanzania wataielewaje CC ya CCM, wanapoisikia inaibuka na tamko la kumpongeza JK, wakati kiporo chake cha Muhongo, kuhusiana na Escrow account, ambacho aliahidi 'kukitafuna' baada ya siku 2. baada ya kile kikao chake na wazee wa Dar, hivi sasa inakatika wiki ya tatu, kiporo hicho JK ameshindwa 'kukitafuna' kwa kuwa 'kimechacha' ile mbaya?!
Imezoeleka kwamba ukizuga zuga baada ya muda fulani, wabongo wanasahau, mpaka liibuke issue jingine ndiyo watu kuhamaki kuhusu issue iliyosahaulika.
 
ImageUploadedByJamiiForums1421171106.758753.jpg

Basi sawa
 
Imezoeleka kwamba ukizuga zuga baada ya muda fulani, wabongo wanasahau, mpaka liibuke issue jingine ndiyo watu kuhamaki kuhusu issue iliyosahaulika.

uko sawa mkuu! unakumbuka kauli ya Mkapa kuhusu netgroup solution, alituhakikishia ghalama za umeme zitashuka na akawa ingiza methroup kwa msaada wa ffu! ghalama hazikushika zilapanda mala dufu na tumesahau!

Jk nae alituahidi maisha bora!! maisha yamekiwa mbinde yalichagizwa na kipindi kireefu cha mfumuko wa bei kiasi cha ku triple price in less than ten yrs, mfano unga toka sh 400 mpaka zaidi ya malatatu yake! tumesahau!!

Jk alisema shule bure haiwezekani hela zitatoka wapi, baada ya miaka michache huku serikali ikiwa dhogulkhali ameahusi elimu bure!! tumesahau!!

etc..!!!
 
hayo mapendekezo ya kamati ya mangula yaliyopokelewa na cc ni yapi mkuu ?
 
Sijawahi kutilia shaka habari zako Mzee Tupatupa aka throw throw. Ile nafasi ya mwenezi ingekuwa yako kama weledi ungezingatiwa
 
Do u expect any possiteve decision from CCM, CC? Keep on Waiting guys!
 
Hawa Jamaa wanashida sana, kwa sasa miji za town zote watakuwa wanapokelewa na CDM (Wabunge, Madiwani na wenyeviti) huenda wawe wanatua vijini!! Nadhani ndio maana kuzurura kwa JK Arusha town, Musoma mjini, Mwnza Kati (Nyamagana, Ilemela), Mbeya mjini, nk kumepungua kwa kasi sn!!
 
Kuna mtaa kule Boko, DSM unaitwa ... "Basi haya". Hiyo ndiyo comment yangu
 
WEZI WALIENDA KUPONGEZANA BAADA YAKUTAFUNA NCHI...ama kweli mtz laiti angeelewa adui wake mkubwa ni ccm asingechekanao
 
Pia CC imempongeza Chenge, Tibaijuka, Werema, Maswi, Prof. kwa kuwa wavumilivu hasa walipojitoa kuiokoa serikali pamoja na chama. Pia wameamua kwa kauli moja kuwa hawatamfukuza Prof. Muongo
 
Kama ni hivyo hawana tofauti na genge la wazee kule kwetu wakiwa kwenye vikao vyao vya dengerua na kwa furaha waliyonayo wanasifiana kwa kila kitu.
 
CCM inaanza kujitambuwa kuwa sakarati L mawti Imewadia,sasa wameanza kujenga urafiki wao kwa wao ,ufa ulikuwa mkubwa sana. Wanaponngezana kwa kupat angalau 60% kinyume na Matarajio yao.wimbi la mageuzi likuwa kubwa
 
Back
Top Bottom