CC ya CCM haikuwa na jipya

CC ya CCM haikuwa na jipya

Huyu jamaa mpuuzi na muongo wa kutupwa kazi yake kutunga uongo tu cc wanakaa leo hicho anachosema kimekaa jana labda aliitisha petro mselewa ila siyo jk

Mkuu Invisible husika hapa tafadhali

Mzee Tupatupa
 
Last edited by a moderator:
Nilipowasili tu jana usiku kutoka Arusha-kwa-Lema nikatamani kujua yaliyoendelea Kisiwandui, Zanzibar. Huko kulifanyika kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanya tathmini ya mambo kadha wa kadha yahusuyo chama.

Iliripotiwa kuwa ajenda ya wagombea urais ilikuwa moto na kumeafikiwa mambo magumu na mazito juu ya baadhi yao au wote. Nikataka kujua ukweli. Nikawasiliana na Mjumbe mmoja wa CC aliyekuwepo Kisiwandui.

Alichosema ni kuwa hakukuwa na jipya. Yamejadiliwa mambo ya kawaida sana ya kichama. Hata Ripoti ya Kamati ya Komredi Mangula iliwafagilia wagombea watarajiwa kwa kusema wamerekebishika na sasa wako safi.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na maandalizi ya uchaguzi ujao yaliteka sana kikao husika. Wakati wa kuwajadili wagombea mbalimbali chamani,wajumbe waligawanyika na kila mchangiaji alimfagilia wa kwake.

"Hakukuwa na jipya ndugu yangu. Nikirudi tutaongea vizuri"nikaambiwa na kuahidiwa na mjumbe huyo wa CC.

Mambo yanakaribia patamu!

Mzee Tupatupa wa Lumbumba,Dar es Salaam
Binafsi nashangaa sana nchi hii CCM hawana jipya na hakuna chochote,wanasukumwa na ukawa tu....ona elimu bure,bure!hakuna kitu hicho,mbina huku kwetu msingi ni bure je ni bure!...kauli za hovyo kwa watu hovyo
 
Najua usiyoyajua, sitaki kujua unayoyajua, yananitosha ninayoyajua, sitaki kujua kupitia unayoyajua, jua ya ufipa ya lumumba yatakufanya utoke jasho kwenye jua.

kijana kuwa makini , la sivyo utanyang'anywa hiyo id ya chama ulie na kusaga meno !
 
Unachanganya watu maana taarifa kwa mujibu wa Kubenea humu humu JF kikao ni leo 13/01/2015 hicho cha jana ni kipi wakati viongozi walikuwa kwenye sikukuu za Mapinduzi?

Mkuu Ndachuwa,Kubenea ni mwanaCC ya CCM? Yawezekana lakini nimedanganywa na aliyeko huko.

Mzee Tupatupa
 
Last edited by a moderator:
Huyu jamaa mpuuzi na muongo wa kutupwa kazi yake kutunga uongo tu cc wanakaa leo hicho anachosema kimekaa jana labda aliitisha petro mselewa ila siyo jk

Unanitaja nahusikaje hapa? Vijana wa CCM bure kabisa
 
mbona lugha yako inafanana na P.E.M?

Kijana,mwenzio nina bahati mbaya kufananishwa. Juzi niliulizwa kama nina undugu na Ndimara Tegambwage. Ni uandishi tu wa kushabihiana. Karibu Ofisini Lumumba.Ukifika niPM nikufuate

Mzee Tupatupa
 
…mwekiti anaendesha chama+nchi kama genge la mama lishe kazi anayojua ni kuweka na kupasha viporo…
 
Kijana,hujui ninayoyajua.Unayajua ninayoyajua. Tusubiri tuone

Mzee Tupatupa

Mzee Tupatupa nawe!Kwanini kugombana na hawa WATOTO?Ambao hata TANU YOUTH LEAGUE hawaijui.Usijibishane nao hawa,watakupa STRESS bureeeeeeeeeeee.

Waijui TWIST au Moro JAZZ ehhhhhhhhhhhhhh.Enzi zile twazikumbuka na ule wimbo wa Natizama dirishani ,naona mvua inanyesha ohhhhh.Sasa hawa mzee mwenzangu huko hawakujui,hata zile enzi za kuweka mawe kwenye FOLENI kusubiri SUKARI na MKATE WA SIHA,hawazijui,hawa ni wa kuwaonea huruma tuuuuuuuu
 
Nilipowasili tu jana usiku kutoka Arusha-kwa-Lema nikatamani kujua yaliyoendelea Kisiwandui, Zanzibar. Huko kulifanyika kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanya tathmini ya mambo kadha wa kadha yahusuyo chama.

Iliripotiwa kuwa ajenda ya wagombea urais ilikuwa moto na kumeafikiwa mambo magumu na mazito juu ya baadhi yao au wote. Nikataka kujua ukweli. Nikawasiliana na Mjumbe mmoja wa CC aliyekuwepo Kisiwandui.

Alichosema ni kuwa hakukuwa na jipya. Yamejadiliwa mambo ya kawaida sana ya kichama. Hata Ripoti ya Kamati ya Komredi Mangula iliwafagilia wagombea watarajiwa kwa kusema wamerekebishika na sasa wako safi.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na maandalizi ya uchaguzi ujao yaliteka sana kikao husika. Wakati wa kuwajadili wagombea mbalimbali chamani,wajumbe waligawanyika na kila mchangiaji alimfagilia wa kwake.

"Hakukuwa na jipya ndugu yangu. Nikirudi tutaongea vizuri"nikaambiwa na kuahidiwa na mjumbe huyo wa CC.

Mambo yanakaribia patamu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
ningeshangaa sana kama wangelikuja na jambo jipya. Wameendesha nchi kwa miaka 10 kwa kupiga soga kwenye mikutano bila ya kuwa na kitu kipya sababu hakuna mbunifu yeyote wa maendeleo ya nchi kati yao zaidi ya kubuni namna ya kuiba hela ya umma. Creativity is zero.
 
Ukiwa muongo lazima kwanza kabla ya kuleta uongo wako uwe unajitahidi kuangalia ukweli wa suala unalotaka kulitengenezea uwongo

Eti Kamati Kuu ya CCM ilikaa na kuwaongelea wagombea wa Urai na uchaguzi wa serikali za mitaa.

Tatizo lenu vijana wa BAVICHA mnadhani mnafamu wakati hamfahamu lolote. Hata wanaokubaliana na uwongo wako ni kundi lenye fikra kama zako.

Kwa taarifa yako kikao kilichofanyika juzi ni Kamati Kuu Maalum ya NEC.

Inayofafanya kikao leo ni Kamati Kuu.

Hivi ni vikao viwili tofauti ambavyo vina wajumbe tofauti na majukumu tofauti.

Kwa mwanaCCM hai yoyote anafahamu tofauti yake achilia mbali mfanyakazi wa CCM.

Huyu eti ndiyo anawadanganya ni mfanyakazi wa CCM na wao wanakubali.

Wajinga ndiyo waliwao
 
Back
Top Bottom