CBE Mwanza yahitaji mamilioni kulipa fidia


Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
634,713
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 634,713 280
CBE Mwanza yahitaji mamilioni kulipa fidia


Na Wilhelm Mulinda, Mwanza

CHUO cha Elimu ya Biashara nchini (CBE) kinahitaji Sh. milioni 243,264,846 ili kulipia fidia ya ardhi katika eneo la Kiseke jijini hapa kwa ajili ya kupanua chuo hicho katika Kampasi ya Mwanza.Hayo yalisemwa juzi na Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Wycliffe
Lugoe katika sherehe za mahafali ya 45 ya chuo hicho, Kampasi ya Mwanza.


Alifafanua kuwa baada ya kulipa fidia hiyo ndipo Halmashauri ya Jiji la Mwanza itatoa hati miliki ya ardhi hiyo kwa chuo hicho.

Dkt. Lugoe alisema kuwa pamoja na mambo memgine, ardhi hiyo itatumika kwa ajili ya ujenzi wa kampasi mpya, nyumba za wafanykazi, kumbi za mihadhara, hosteli na Maktaba ya chuo.

Alisema kuwa kwa sasa kiasi cha fedha kilichobaki ni milioni 142,264,846 ili kukamilisha malipo hayo ya fidia ya sh. milioni 243 kwa vile Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko nayo tayari imesaidia kupunguza deni hilo.


Aidha chuo hicho kwa sasa kinakamilisha mazungumzo na Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Mwanza (NCU) ili kiweze kukodi ukumbi wake uliopo katikati ya jiji wenye uwezo wa kuchukua wanachuo 250 pamoja na kukarabati miundombinu iliyopo ili iweze kutumia teknolojia ya kisasa ikiwa ni pamoja na kuboresha maktaba.

Kampasi ya CBE ya Mwanza ambayo kwa sasa inatoa mafunzo ya elimu katika ngazi ya cheti, stashahada na stashahada ya uzamili, ilianzishwa mwaka 2007 ikiwa na wanafunzi 303 na hadi kufikia mwaka huu inawanafunzi 1,200.

Akizungumza katika mahafali hayo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Cyril Chami alisema kuwa serikali itaangalia uwezekano wa kupunguza tena deni hilo la fidia ya ardhi linalofikia Sh.milioni 142 au kulimaliza kabisa ili chuo hicho kiweze kuanza ujenzi katika eneo la Kiseke jijini Mwanza.

Dkt. Chami aliwaasa wahitimu hao kutambua kuwa elimu na stadi walizopata ni changamoto kwao kwa ajili ya kujiendeleza zaidi katika ngazi za juu za elimu na pia kutekeleza dhamira na malengo ya taifa.

Aidha aliwataka wanachuo ambao bado wanaendelea na masomo chuoni hapo kusoma kwa bidii na kuonya kuwa endapo watabweteka dunia haitawasubiri na matokeo yake ni kuishia kulalamika kutokana na kukosa fursa mbalimbali ili kuweza kukabili changamoto katika maisha.
 

Forum statistics

Threads 1,236,959
Members 475,327
Posts 29,274,766