Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na Uchumi wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Catherine Ruge (Msubhati) amesema ameamua kusimama na kugombea ubunge wa Jimbo la Serengeti Mkoani Mara, kwa lengo la kupigania haki za wananchi na kurejesha matumaini kwa jamii inayokabiliwa na changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
Leo Julai 22, 2025, mbele ya mamia ya wananchi waliojitokeza kumsindikiza wakati wa kurudisha fomu ya kugombea ubunge kupitia tiketi ya CHAUMMA, Msubhati amesema ameguswa na hali ngumu ya wananchi wa Serengeti na taifa kwa ujumla, hususan vijana, wanawake na wazee.
“Kama ninyi, nami nimeguswa na ukosefu wa haki. Nimeona vijana wakikatishwa tamaa, nimesikia vilio vya akina mama wanaopoteza watoto wao wakati wa kujifungua, na wazee wanaokosa dawa hospitalini. Nimeshuhudia familia zikifanya kazi kwa bidii bila kupata maendeleo,” amesema Msubhati
Ameongeza kuwa “Nimesikia sauti ya Mungu, nimeitika. Nimekuja kwenu watu wa Serengeti kuwaambia nipo tayari kwa mapambano. Si mapambano ya chuki bali ni mapambano ya matumaini, ya kuilinda haki ya kuishi kwa vijana wetu."
Catherine ameahidi kuwa iwapo wananchi wa Serengeti watampa ridhaa, atasimama mstari wa mbele kupigania mabadiliko yenye tija na ustawi kwa wote, bila kujali tofauti za vyama wala mitazamo ya kisiasa.