RMK Freelancers Agency
JF-Expert Member
- Jan 15, 2025
- 298
- 292
True case study!
“Nicas" (jina halisi limefichwa) alinitafuta mwezi uliopita kupitia JamiiForums baada ya kusoma baadhi ya threads zangu kuhusu personal finance na uwekezaji.
Aliniambia ana malengo mawili:
1.Kupunguza matumizi na kuweka akiba zaidi
2.Kujifunza kuwekeza kwenye hisa za Dar es Salaam Stock Exchange ndani ya miezi michache ijayo
Baada ya mazungumzo ya simu kwa mara ya kwanza, nilimuuliza maswali kadhaa ya msingi:
Hakukuwa na mfumo wa kufuatilia pesa zake.
Kwa hiyo hatua ya kwanza haikuwa investment wala savings, bali ushauri na knowledge kidogo ili kumpa financial awareness.
Tulianza na hatua kadhaa rahisi lakini zenye impact kubwa.
Kwanza, nilimshauri aanze kurecord mapato na matumizi yake yote ya kila siku kwenye application maalum ya personal finance and expenses management, nilimtajia application mbili za bure ambazo zinapatikana play/app store.
Nilimwambia bila data huwezi kujua pesa zako zinaenda wapi.
Pili, tulifanya kitu kinachoitwa money leak inspection. Hapa tulichambua matumizi madogo madogo ambayo mara nyingi watu hawayaoni lakini ndiyo yanayokula pesa nyingi kwa mwezi, Mfano:
kununua vitu vidogo kila siku badala ya kununua kwa bulk, costs ndogo ndogo zinazokwepeka, matumizi ya mara kwa mara yasiyo ya lazima, gharama za convenience, Nk.
Baada ya hilo nilimshauri mbinu mbinu kadhaa kama:
1.Kununua vitu muhimu kwa bulk
Badala ya kununua bidhaa ndogo ndogo kila siku, alinunua baadhi ya mahitaji ya msingi ya wiki au mwezi. Hii hupunguza gharama na pia hupunguza matumizi ya hisia kwenye manunuzi.
2. Mbinu ya “rounding up” kwenye saving
Kila mara anapobakiwa na kiasi kidogo kwenye matumizi yake ya siku, anakiweka moja kwa moja kwenye akiba. Ni mbinu ndogo lakini inaongeza saving bila mtu kuhisi pressure kubwa.
Na mbinu zingine!
Kwa wiki mbili zilizopita tumekuwa tukiongea mara kadhaa kwa wiki. Nimekuwa nikimpigia simu kumkumbusha:
- Mara kadhaa nimekuwa nikimfundisha hatua za msingi za kuwekeza kwenye hisa za Dar es Salaam Stock Exchange, ikiwemo jinsi ya kuchagua kampuni zenye fundamentals nzuri na umuhimu wa kuwekeza kwa muda mrefu badala ya kufanya maamuzi ya haraka.
Jana jioni alinitumia screenshot ya report kutoka kwenye app anayotumia kufuatilia matumizi.
Matokeo yalikuwa ya kushangaza.
Amepunguza matumizi kwa 58.1% ukilinganisha na wiki iliyopita.
Kwa maneno mengine, ametumia chini ya nusu ya pesa aliyokuwa anatumia kabla ya kuanza kuanza kuwasiliana na mimi!
Lakini pia ameanza kununua stocks kwenye kampuni akifata uchambuzi na maelezo ninayompatia.
Hii ni hatua kubwa sana.
Kama ataendelea na discipline hii:
ataweza kufikia lengo lake la kuweka kiasi fulani ndani ya miezi sita, atakuwa na emergency fund ya msingi, ataendelea kujenga portfolio ya uwekezaji.
Watu wengi wanadhani personal finance ni kitu kigumu sana. Ukweli ni kwamba mara nyingi ni mfumo wa tabia na maamuzi ya kila siku.
Nicas ameanza kuona tofauti kwa sababu ameanza kutumia logic badala ya emotions kwenye matumizi yake pesa.

- Mapato yake ya mwezi ni kiasi gani
- Matumizi yake makubwa ni yapi
- Anaweka akiba kiasi gani kwa sasa
- Anafuatilia matumizi yake au la

- kurecord matumizi yake
- kufuatilia lengo lake