Case study kuhusiana na mjadala wa Katiba Mpya

Katiba kutoka kwa mwanasiasa ni ile inayompa favour yeye kwanza

So ukimkaribisha mwanasiasa akutengenezee katiba, tegemea mivutano isiyo na maana(kila mtu atatetea kinachompa favour)
Katiba inatekelezwa na wanasiasa.

Kila kilichomo kwenye katiba kinalenga kutekeleza sera zitokanazo na siasa.

Huwezi kuondoa siasa kwenye mambo ya sheria na sera.

Mivutano hiyo ya kisiasa ndiyo huzaa mustakabali wa kesho ya taifa.

Kabla hujaendelea kuniquote jielimishe kidogo juu ya mifumo ya utawala na sheria.
 
Reactions: BAK
Lengo na madhumuni ya chama cha siasa ni kuikosoa serikali sio ku deal na Raisi. Chadema hawajawahi kujenga shule, zahanati au hospitali toka chama kianzishwe. Watu wanataka chadema wafanye kazi yao kuisimamia serikali. Hakuna ufisadi wowote uliovumbuliwa na chadema watu tuna maswali kuhusiana na ulinzi wa rasilimali za taifa kama ujenzi wa bandari ya bagamoyo mpaka sa hivi chadema hawana nakala ya mkataba. Kama mkiangalia naona mamlaka ya raisi juu ya sheria ya ardhi ni makubwa kuliko hata katiba. Nilitegemea chadema kutoa msimamo wao lakini ukimya wao kwa mtazamo wa wengi wameweka mkazo sana kutawala sio shida za wananchi. Wakiendelea na tamaa ya madaraka watakosa vyote. Nawashauri waweke nguvu kubwa sana kwenye kuisimamia serikali kuliko kudai katiba hiyo inawafanya waonekane wana tamaa ya madaraka. Waanze kuchukua ruzuku kwanza wqsipo chukua ruzuku chama chao kitqhusishwa na ufadhili wa wazungu.
 
Mleta mada unachanganya baina ya vitu vitatu; Katiba mpya, katiba bora na kuheshimu katiba. Vyote hivyo ni vitu vitatu tofauti na tusilazimishe kuwa kitu kimoja, wala tusilazimishe kimoja kuwa mbadala wa kingine. Mtawala wa sasa akiheshimu katiba iliyopo sasa hiyo haina maana hii katiba itakuwa bora au kuwa mbadala wa kuwepo katiba mpya.

Swali, Je, Tanzania ya leo inahitaji katiba mpya? Na huo ndio mjadala unaopaswa kujadiliwa.

Kwa maoni yangu, kwa kuzingatia haya, kwanini ni lazima tudai Katiba mpya sasa;

1. Tanzania kama taifa hatujawahi kutunga katiba yetu sisi wenyewe toka kuumbwa kwa ulimwengu (Katiba iliyopo sasa ni urithi wa katiba ya kikoloni ya serikali ya Tanganyika tuliyoifanyia mabadiliko mengi mnoo, mara kwa mara tangu tunapata uhuru mpaka leo hii kiasi cha katiba yenyewe kupoteza taswira yake halisi ya mwanzo)

2. Mabadiliko ya kisiasa, kijamii na kiuchumi yaliyofanyika miaka 1990s hususani kuruhusu mfumo wa vyama vingi vya kisiasa, uchumi huria na uhuru wa kijamii, hayawezi kuhimilika kwa katiba iliyopo sasa hata tuifanyie mabadiliko kiasi gani.

3. Mabadiliko makubwa yaliyofanyika kwenye katiba ya Zanzibar hayawezi kubebwa na katiba iliyopo sasa hata kama tutaifanyia mabadiliko makubwa.

4. Udhaifu mwingi na nyufa nyingi zilizomo kwenye katiba hii ya sasa (jambo ambalo wanasiasa wa pande zote wanakiri hivyo) kiasi ambacho sote tunajiuliza na kushangaa zilikuwaje zikawepo kwenye katiba yetu, ni kielelezo tosha cha kudai kuwepo kwa katiba mpya.

5. Kelele na fukuto la kijamii na kisiasa la kutaka kuwepo kwa katiba mpya itakayokidhi mahitaji ya kizazi cha sasa limekuwepo kwa zaidi ya miaka 30 sasa bila kunyamaza wala kuchoka, hakuna namna tunaweza kulikwepa, kulipuuzia au kulifuta. Dawa ni kulifanyia kazi.

NOTE
Katiba yoyote ikifanyiwa mabadiliko mengi, makubwa au mara kwa mara inapoteza sura, muundo na mantiki ya kuendelea kuwa katiba iliyotungwa na walengwa. Katika ya Tanzania iliyopo sasa, haijarishi ni nzuri au mbaya, imepoteza uhalali wa kuendelea kuwa katiba iliyotungwa na walengwa (watanzania!) kwa sababu ya utitiri wa viraka vya mabadiliko uliofanywa na serikali kupitia bunge.
 
Na wanaoweka msimamo kuwa katiba siyo kipaumbele chao ilihali wameshindwa kutatua hayo matatizo unayoyasema lengo lao siyo kutawala ?
 
Reactions: BAK
Katiba sio kipaumbele cha wanannchi walio wengi wa Tanzania .

Kama wao wanataka katiba mpya waunde ya kwao na waitumie wao kama wao .

..ndugu yangu Tz ni yetu sote.

..kwa hiyo katiba yetu inapaswa kutatua mahitaji ya makundi mbalimbali ambayo ni sehemu ya Watz.

..kwa mfano, hatuwezi kukataa kusikiliza maombi ya wafanyakazi ambao ni percent ndogo ktk nchi yetu, kwasababu wakulima, wafugaji, na wavuvi, ambao wako wengi zaidi ktk jamii yetu, hawajatoa maombi yoyote kuhusu katiba.
 
Reactions: BAK
Kama unakubaliana na utengenezwaji wa katiba kupitia wanasiasa hupaswi kuwa mmoja wa wanaoipinga katiba tuliyonayo,

Wewe ndio ulianza kuniquote, so unaweza nipuuza.
 
mada nzuri sana hii

wachangiaji tusiharibu huu mjadala

maoni yangu
katiba ya sasa haitufai tena kwasababu imeshindwa kwenda sambamba na mabadiliko ya kiuchumi,kiteknologia,kimazingira na kiutawala.
 
Je una uhakika gani hiyo katiba mpya haitakanyangwa iwapo unadai iliyopo imekanyagwa!
 
Unategemeo gani ukipata hiyo katiba mpya?
Katiba mpya itapatikana haijalishi ni leo au kesho.

Lengo kubwa la katiba mpya ni kurejesha madaraka kwa wananchi ili waweze kujiamulia mambo yao wenyewe badala ya watawala wezi.

Huwezi kuvipata ulivyovitaja hapo bila kwanza kuwarejeshea madaraka wananchi wenyewe kutoka kwa watawala na hilo itawezekana tu kupitia katiba mpya
 

Power to the people ndo malengo yako. Nimazuri kwa kweli lakini kila kizuri hakikosi kasoro. Katiba za mrengo wa power to the people zinamapungufu yake. Je unayajua??
 
Power to the people ndo malengo yako. Nimazuri kwa kweli lakini kila kizuri hakikosi kasoro. Katiba za mrengo wa power to the people zinamapungufu yake. Je unayajua??
Yataje wewe unayeyajua mimi nitakuambia suluhisho la hayo mapungufu.
 
Reactions: BAK
Huathiri hata uchumi ,Sera ambazo hazina muelekeo (ineffective policies)
 
Je una uhakika gani hiyo katiba mpya haitakanyangwa iwapo unadai iliyopo imekanyagwa!
Haitakanyagwa kwasababu itaweka mipaka kati ya mhimili mmoja na mwingine, na zaidi, itaainisha ni yapi majukumu ya kila ofisi ya serikali, na kipi kitatokea kwa atakae kwenda kinyume na taratibu za ofisi yake, hii ni kianzia kwa Rais mpaka wabunge, mahakimu na majaji.

Iliyopo inakanyagwa kwasababu watawala wameigeuza kichaka cha kujifichia wakifanya maovu yao.

Mfano, Rais akishaingia madarakani kwa kuiba kura, matokeo yake hayaruhusiwi kupingwa popote, na Tume ya uchaguzi imepewa mamlaka ya kuwa chombo pekee cha kutangaza washindi wa uchaguzi wakati wajumbe na mwenyekiti wake ni wanateuliwa na mwenyekiti wa CCM..
 
Yaani nilikua nakuona una akili,kumbe amuna kitu.
 
Katiba ni nini?nani anahitaji katiba mpya??katiba ni ya nani??kwa nini tinahitaji katiba mpya??ukijibu haya maswali kwa ufasaha utapata kujua kwa nn ccm wanasema mbowe dikteta
 
Ukisema katiba mpya,

Tutajiuliza nani anayeidai,

Kwa interest zipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…