1.kwenye ndoa si mahala pa kubadili tabia za msingi labda mchumba awe below 20 yrs
2.tabia ndogo ndogo zaweza badilishwa,kama kuwa msafi...unaweza mbadili.
3.zile tabia zake mbaya,idadi yake zidisha kwa mbili ndizo jumla ya tabia zake zote usizozitaka......nina maana zipo tabia zingine mbaya kabisa hutazijua kamwe hadi uolewe.....usitishike ni mambo ya kawaida.huyo jamaa yako sie yeye wa baadae.
4.hakuna mtu anaeoa/kuolewa na malaika, kila mtu ana kasoro nyingi tu ,hata wewe unazokasoro zako dawa nikuvumiliana
5.akikupenda sana sana,i mean sana...yaani kuzidi maelezo(na sijui utafanyaje hadi awe hivyo)basi aweza kuwa vile upendavyo kwa muda....penzi likichuja anarudia tabia yake ya awali.
6.kwenye uchumba kila mtu ni kondoo,mpole mwema,anajali....kila utakachomweleza ni ndio,yaani hapo nidhamu ni mia.baada ya ndoa nidhamu ni sifuri........
Inapungua hadi siku itafika sifuri.
Hata hivyo usijali sana....ni mawazo yangu tu. Mng'ang'anie sana huyo jamaa hadi kieleweke....si unajua tena?achana na mambo ya kumpekua pekua kuku,utashindwa kumla.