Campain John Magufuli let pregnant student complete their educatin

Campain John Magufuli let pregnant student complete their educatin

Hizo asasi ziwasaidie kuwalipia ada wakasome shule binafsi sio kutafuta kiki mitandaoni...wanatufanya sisi wajinga ...wanaopigia debe haki za binadamu ndio wanyonyaji wakubwa wa uhai wa mataifa yetu changa kiuchumi.....waende zao huko...

Wanaoinyonya na kuiuza Tanzania ni Viongozi wetu. Tusiwasingizie watu wa nje. Ni ubinafsi wa Viongozi wetu na uongozi wao wa dhuluma ndiyo umetutesa na kuleta changamoto na shida nyingi Tanzania ikiwa pamoja na za hawa watoto. Hakuna mtu wa nje anaweza kutufanya sisi wajinga, ni viongozi wetu wanajuwa hatuna elimu ya kutosha ya kuelewa ndiyo maana tunawalaumu hawa watoto. Pesa zinazoibiwa na Viongozi wetu, mabillioni, zingeweza kuwapa watoto wote elimu bila kujadili. Zingeweza kuondowa shida nyingi za hawa watoto, wasingepata mimba kwaajili ya kupewa mfuko wa chips na watu wazima wengine wenye vyao serikalini. Hawa watoto hawawashiki wanaume kwa nguvu wawaoe mimba . Hawa ni watoto, Uongozi wa nchi ukiwa mbaya kila kitu kinaenda vibaya, na watu wana kosa heshima. Elimu yetu mbovu kila wanachosema Viongozi hata kwa watoto wetu tunaitikia tu, ni kwasababu hatujui faida ya elimu ni nini. Utawezaje kusema watu wa nje waje wawaelimishe watoto wetu kama kweli tuna elimu sawa sawa? Jukumu la kuwaelimisha watoto wetu ni sisi wenyewe walipa kodi.
 
Mkubwa alivyo jaa kiburi, hii patition hata iwekewe signature na dunia nzima haitosaidia kitu.
Naona wat hamjamuelewa maharage, akisema kitu amesema, huwa harudi nyuma kurekebisha.

He is too arrogant, anajihisi kua na nguvu moja kubwa sana na anahisi ndiye mwenye akili na uchungu kuliko watanzania wengine, kwa hiyo kila anachofikiria na kuamua ndiyo sahihi.

Mtu wa namna hiyo ogopa sana, msubiri muda wake uishe asepe tu, ila kumpangia vitu ashasema hapangiwi. Sio mara ya kwanza watu mnakuja pamoja kusema afanye kitu flani, kumbuka kwa kila mtu moja anayempiga, kuna kilaza mwingine asiyejua hata kuandika anam~support.

Najuta kutoa nauli kusafiri hadi bongo na kumpigia kura huyu jamaa. Simpendi Lowassa ila huyu jamaa alivyogeuka sasa hivi simpendi mara mbili zaidi.

Ana bahati amepata madaraka Wakati viongozi wenye kupenda haki duniani hawako madarakani. Trump ana historia ya kudharau wanawake, Uingereza bado wanaunda serikali yao. Lakini lazima atasikia maoni ya dunia, hiki ni kijiji, huwezi kuishi peke yako. Investors wengine hawatapenda kufanya business na Tanzania kwa uonevu wa wanawake, NDOTO yetu ya viwanda itaishia njiani. Ubaya Pamoja na nia nzuri ya kupigana na ufisadi, lazima aiongoze Tanzania kwa haki, na sio kwa mawazo yake ya kizamani. Rais Magufuli hana exposure hiyo ndiyo shida tunayo.Bado ana mawazo ya kutuongoza kwa amri na siyo kwa sheria atashindwa. Wengi tuliyokuwa tunamsifu kwa kazi yake tutamchukia.
 
Serikali haisomeshi wazazi bure. Wanafunzi waliopata hadhi ya uzazi wakakope Bodi ya mikopo wajisomeshe.
Au wakasome elimu ya uzazi na malezi ya familia ktk madarasa ya clinic za wazazi maana huko nako serikali imeisha walipia
ruzuku 'ADA' sababu hiyo nayo bado ni elimu muafaka kwao.
 
Unaweza kuzini peke yako? JE wanaonabakwa na Ndiyo wengi. Tanzania ina record mbaya ya kubaka Watoto. Watoto wanabakwa mpaka na baba zao, lakini mnaona haya kujilaumu, mnalaumu watoto. Wanaume wakiweka heshima zao kibindoni watoto hawatapata ujauzito. Mnaunaviki sana.
Kwa hiyo wakishabakwa na wakizaa na kuruhusiwa kuendelea na masomo ndio wanaondoka ktk risk ya kubakwa tena au?
 
Tanzania haswa ya Kikwete Mwenye pesa anafungwa? Tangu lini? Mtoto mwenye wazazi masikini polisi gani atamsikiliza, mahakamani gani inamfunga Mwenye pesa, kushindana na aliyemubaka Mwenye pesa. Chunguza wangapi waliofungwa miaka 30? Utakuta ni masikini. Kuna Wakati Tanzania unauwa, ukiwa na pesa kesi anageuziwa maiti. Amekufa hawezi kujitetea. Sasa Viongozi waneshindwa kuwakinga hawa watoto wamewageuzia kesi. Haya ndiyo maisha ya masikini wengi wanapambana nayo. Viongozi hawana habari, wenyewe wanalindwa na watoto wao. Magufuli tuliokuwa tunamtegenea kusaidia haki za masikini ameungana na Manma Kikwete tajiri mme wake aliyesaidia kuwaletea hawa watoto ufukara na ukosefu wa sheria ya kuwatetea hawa watoto.
Mtoto wa kike akipata ujauzito hata kama alitongozwa au alijipeeleka mwenyewe kukidhi matamanio ya mwili kingono husingizia alibakwa ili kukwepesha kuwajibika moja kwa moja na tatizo, ndio maana wewe ktk utetezi wako unatoa takwimu utafikiri kweli wote walibakwa, au ni wapi uliona baada ya ujauzito binti anakiri kuwa alitongozwa?
 
Hizi ndizo changamoto zinazowapata watoto wa kike tizama video. Hii ni mojawapo tu, mambo haya ni Mengi Tanzania. Kuzaliwa nwaamke, ama zeruzeru ama uzee ni mateso makubwa Tanzania

Kwa hiyo wakishabakwa na wakizaa na kuruhusiwa kuendelea na masomo ndio wanaondoka ktk risk ya kubakwa tena au?

Mtu akiwa na elimu itamuwezesha kupata kazi na kuibadilisha maisha yake na ya mtoto wake. Ukimunyima fulsa ya kuendelea na masomo, basi huo ndiyo unakuwa mwisho wa maisha yake Pamoja na mtoto wake. Kuna watoto wengi sana wanapatikana na Hii mikata ya ujauzito, kwa sababu mbali mbali, tusitowe adhabu kwa wote hayo ni makosa. Tutizame pia na makosa yanayofanywa na Viongozi wetu ambayo yameleta changamoto nyingi kwenye familia hizi, tusiwalaumu watoto tu.

Au wakasome elimu ya uzazi na malezi ya familia ktk madarasa ya clinic za wazazi maana huko nako serikali imeisha walipia
ruzuku 'ADA' sababu hiyo nayo bado ni elimu muafaka kwao.

Acheni kutembea na Mabinti zenu. Tabia hii ipo Tanzania sana, mnajikinga kwa kuwaadhibu hawa watoto na ni nyinyi ndiyo mnawaharibu hawa watoto Kisha munawaadhibu, dhambi kubwa acheni. Na HUYU ameshikwa tu kwaajili anaonekana hana chochote. Angekuwa ni mkubwa serikalini ingepita tu. Acheni unafiki.
 
Kwani elimu ni lazima secondary education?

Kwa nini kuwa one watoto ikiwa mababa mpaka waheshiwa wanatembea na watoto . Na hawa ni wengi , na wengine hawashishikiki. Ukiwa mtiti wa kike, ama, zeruzeru ama mzee Kuishi Tanzania ni mateso. Hata haya Rais kuwaadhibu watoto na siyo makosa yao.

Back
Top Bottom