Campain John Magufuli let pregnant student complete their educatin

Campain John Magufuli let pregnant student complete their educatin

Tayari nimetia saini yangu

Asante baba. Elimu ni Kufukuza umasikini, na ni kupigana na uonevu. Ingekuwa ni Rais wa Kenya, ama wa Uingereza, akatamka maneno aliyoyatamka Rais Magufuli kwa watoto hawa, watoto wetu, moto ungewaka, maprofessor na mawakili, na Viongozi wa dini wasingenyamza kama tulivyonyamaza, na hii nikwasabu elimu yao iko juu ya ujuzi na sio ya vyeti wanajuwa haki zao.
 
Hii itapelekea watoto wengi wahanga wa huu mkasa kuhatarisha maisha yao kwa kujaribu kutoa mimba hali inayoweza kuchangia wengine kupoteza maisha.

Elimu ni haki ya msingi ya kila mtu na swala la mimba haifai kutumiwa kama kisingizio na baadhi ya watu kuwanyima wengine haki yao hiyo muhimu.

Pia sio rais anayesomesha watu ktk nchi hii bali ni pesa za watanzania wote walipa kodi, wakiwemo wazazi wa hao wahanga wa mimba.

Umefika muda sasa rais aache kuingilia kila kitu na kujiamulia tu anavyoona yeye inafaa, taasisi zipo nyingi tu, ziachwe na zenyewe zifanye kazi, hii hali tunayoendelea nayo haiakisi misingi kamili ya demokrasia.

Maamuzi mengine kabla hayajafikiwa inahitajika "wide consultation" ili kupata "consensus". Mwenendo huu wa sasa unazalisha wanafiki wengi wanaounga mkono hoja kama hii kiwaziwazi lakini kwa dhamira ya ndani wanakiri wanaburuzwa. Hii haifai kabisa waache watoto wa watu wasome kwani pesa ni zao sii za mtu yeyote.

Umesema kweli, Watanzania tumechoka kuongozwa kama ng'ombe. Rais Magufuli amewahujumu hawa watoto bila ya kuwasikiliza wamepataje ujauzito. Kesi nyingi za ubakaji Tanzania, na shida nyingi zinazowakabili hawa WATOTO Rais hazijui, anaishi Ikulu watoto wake hawatembei mile 10 bila kula kuchota maji. kuna wizara mbali mbali zinaweza kushughulika na kusikiliza shida za hawa watoto, kwa nini wengi wanaoata ujauzito. Hakuna mtoto anazaliwa na ngono mikononi. Watoto wote wana akiwa innocent, hali ya maisha inawabadilisha. Sio wote wamepata mimba kwa kupenda, wote wamehukumiwa kifungo kimoja, na Rais Magufuli, mtu gani mwenye elimu sawa sawa gani anaweza kuamua hivyo?
 
Wewe ni mtu wa namna gani? Bila shaka ulipatikana kwa sela za Cameron

Vyovyote nilivyopatikana Mimi sina makosa. Ni kama hawa watoto wanaozaliwa na watoto wenzao, hawana makosa. Wenye makosa ni society, watu wenye ukosefu wa mawazo ya elimu kama nyinyi, Hamuoni mbali, na wewe sio makosa yako, ni elimu mbovu nchi yeti inayotupa. Serikali baada ya serikali, wametuongoza kama Ngo'ombe na hatujui kwa elimu yetu mbovu na Ndiyo tuko wengi. Ni rahisi sana kuongoza wajinga, you will get away with murder unchallenged.
 
we mama obama kwani siku hizi wanaobaka wanaachwa Huru???? nilidhani wanafungwa 30yrs

umequote sheria za nchi gani

cheki vzr na obama akufafanulie

Sheria tunazo, hata za kuwalinda hawa watoto wetu zipo, lakini hazifuatwi, zingekuwa zinafuatwa Rais Magufuli asingeamua kuwaachisha hawa watoto masomo na kuwadhurumu haki zao.

Bunge limeamua kwa wingi, watoto waendelee na masomo, na bunge ni sauti ya Watanzania, watunga sheria na wapitisha sheria, na wawakilishi wa Watanzania, Raisi ameamua kupinga, amevunja sheria ya katiba na haki za hawa watoto. . Rais, aliyechaguliwa na wananchi, amepinga, na kwa kuwa tuna wajinga wengi kuliko walio na elimu, tu namuunga mkono kwa woga ingawaje amevunja sheria aliayoapa akichukuwa uongozi ataiheshimu, bila ya kujali sauti za watu waliomuweka kwenye madaraka.

Mtu mmoja sauti yake anaunguruma kama Simba utafikili Kumuchaguwa Watanzania wamemuuzia nchi na haki zao. Sheria zipo, nieleze nani Mwenye pesa anafuata sheria, chanzo cha shida za watoto hawa ni nini? Kama sio uongozi mbaya na uvunjaji wa sheria. Wewe umeishamshitaki mtu mwenye pesa Tanzania haswa Wakati wa utawala uliyopita ukashinda Kesi? Shule zetu kukosa fedha za kuwalipa waalimu vizuri na kuziweka kwenye mazingila mazuri, kama sio wizi wa Viongozi wetu, watoto wetu wangepata sio tu elimu bure hata vyakula mashuleni vingepatikana. Watoto wasingepata ujauzito kwaajili ya mfuko wa chips kwa kuwa wana njaa.

Shule zenyewe zipo kwenye hali mbaya, watoto hata vyoo vya kujisadia ni shida, shule hazina vifaa, jamani waliimu mko wapi mnaojuwa changamoto zinazowakabili watoto wetu? Viongozi wetu waliojirundikia mali za wengi, mama Kikwete ni mtu wa kusema kweli? Kuna makosa makubwa watoto hawa wamefanya kuliko Kikwete, mmewe ? Mbona bado Watanzania wanaendelea kumlipa pesheni na Rais Magufuli ameapa kumukinga wakati anatuonyesha wazi uwozo wa uongozi wa Kikwete na kuoanguwa kila kitu alichokiacha. Rais ashugulike na watafunaji wa nchi hii. Ni hivi Sasa tunaona, kesi za zamani watu waliowatendea Watanzania maovu na wakachwa huru Wakati wa uongozi wa Kikwete. Hiyo ndiyo vita Rais Magufuli angepambana nayo, kuleta maisha bora kwa watoto wetu na sio kupambana na watoto wetu.
 
Hii itapelekea watoto wengi wahanga wa huu mkasa kuhatarisha maisha yao kwa kujaribu kutoa mimba hali inayoweza kuchangia wengine kupoteza maisha.

Elimu ni haki ya msingi ya kila mtu na swala la mimba haifai kutumiwa kama kisingizio na baadhi ya watu kuwanyima wengine haki yao hiyo muhimu.

Pia sio rais anayesomesha watu ktk nchi hii bali ni pesa za watanzania wote walipa kodi, wakiwemo wazazi wa hao wahanga wa mimba.

Umefika muda sasa rais aache kuingilia kila kitu na kujiamulia tu anavyoona yeye inafaa, taasisi zipo nyingi tu, ziachwe na zenyewe zifanye kazi, hii hali tunayoendelea nayo haiakisi misingi kamili ya demokrasia.

Maamuzi mengine kabla hayajafikiwa inahitajika "wide consultation" ili kupata "consensus". Mwenendo huu wa sasa unazalisha wanafiki wengi wanaounga mkono hoja kama hii kiwaziwazi lakini kwa dhamira ya ndani wanakiri wanaburuzwa. Hii haifai kabisa waache watoto wa watu wasome kwani pesa ni zao sii za mtu yeyote.


Maamuzi haya ta Rais Magufuli ni kweli yatauwa watoto wengi, lakini hajali, nashindwa kumuelewa, uongozi wake unatetea wanyonge kweli ama ni kujivisha sifa.
 
Serikali haisomeshi wazazi bure. Wanafunzi waliopata hadhi ya uzazi wakakope Bodi ya mikopo wajisomeshe.


HUYU Bwana serikali yuko wapi, na ni nani. Serikali ni watu, watu ndiyo Serikali. Rais Magufuli amechaguliwa na watu, na hao Watu wengi wao wanataka watoto wa some sauti zao kupitia kwa wakikilidhi wao Wabunge . Ni Mama Kikwete Mke wa Rais, ambaye Rais Magufuli anaoanguluwa uongozi wake uliojaa ufisadi uliosababisha shida nyingi za hawa watoto. Wawili wameungana pamoja kuwadhurumu hawa watoto haki zao, kwa kuwa maishani mwao hawajui shida ya mtoto wa Tanzania ni nini.
 
Anazini peke yake kumbe!
Madam T. Wanapoziniana huwa hatuwaoni. Kinachotambulisha uzinifu ni mimba. Mimba IPO kwa mwanamke ( ke)
Tunamuuliza," pichu ulimvulia nani?" Hasemi. Akitutajia aliyemuingizia dude ( aliyevunja hygene) tutamshitaki kwa kumpa mimba mwanafunzi .
Akikaa kimya anabeba msalaba.
 
Madarasa yatakuwa kama Guest house hivi maana wanafunz watakuwa wamepewa ruksa
 
Tanzania haswa ya Kikwete Mwenye pesa anafungwa? Tangu lini? Mtoto mwenye wazazi masikini polisi gani atamsikiliza, mahakamani gani inamfunga Mwenye pesa, kushindana na aliyemubaka Mwenye pesa. Chunguza wangapi waliofungwa miaka 30? Utakuta ni masikini. Kuna Wakati Tanzania unauwa, ukiwa na pesa kesi anageuziwa maiti. Amekufa hawezi kujitetea. Sasa Viongozi waneshindwa kuwakinga hawa watoto wamewageuzia kesi. Haya ndiyo maisha ya masikini wengi wanapambana nayo. Viongozi hawana habari, wenyewe wanalindwa na watoto wao. Magufuli tuliokuwa tunamtegenea kusaidia haki za masikini ameungana na Manma Kikwete tajiri mme wake aliyesaidia kuwaletea hawa watoto ufukara na ukosefu wa sheria ya kuwatetea hawa watoto.
Sheria zipo atakayebaka anahukumiwa na wanaharakati wameweka madawati ya jinsia kwenye vituo vya polisi. So agenda hapa sio ubakaji agenda ni Mwanafunzi kuzaa na kuendelea na shule kwa pesa ya serikali.
 
Wewe unaujinga mkubwa. Sasa usipowaruhusu hawa watoto wasiendelee na masomo, na ni wengi sana watakwenda wapi na watoto wao? Kama wewe una watoto mala ya mwisho ni lini ulikaa na watoto wako ukasikiliza matatizo wanayowakabili? Ama wewe katika maisha yako una kumbuka lini ulikaa na mzazi wako ukafunguka na kumuekezea baba ama mama yako changamoto zinazokukabili? Hiyo siyo kacha yetu, na matokeo yake mtoto akibakwa hasemi kwa woga. Tafuteni sababu ni kitu gani haswa na kwa nini kuna idadi kubwa ya watoto Tanzania wanapata ujauzito kuliko jirani zetu. Jawabu elimu, wazazi wengi, na watu kama nyinyi elimu yetu ya kufikilia ni ndogo sana. Mmanachukuwa njia ya mkato kuwafukuza watoto hawa shule kuongeza ujinga Tanzania. Elimu gani unayo wewe bila ya kupiga hesabu. Kila watoto 100, Tanzania 30 wanapata ujauzito, kutowaruhusu waendelee na elimu. Wajinga wangapi unaongezea Tanzania watoto hawa na watoto wao.
Hivi mnawaza kwa kutumia nini? Unaposema ni wengi je, ni wengi kuliko wale wanaokosa nafasi ya kuendelea mara wamalizapo darasa la saba??

Anayesema wasiendelee ni nani? Shida ni kuendelea kupata incentives za serikali, cha kufanya wao wasome ODL (open distance learning) nje ya formal education.

Watanzania jamani siyo lazima tufanye wafanyayo wazungu ili kufikia maendeleo na kufanya hivyo tutakuwa ni kukopi tutashindwa kufikiri na kubakia kuishi kwa maigizo.
 
Sheria zipo atakayebaka anahukumiwa na wanaharakati wameweka madawati ya jinsia kwenye vituo vya polisi. So agenda hapa sio ubakaji agenda ni Mwanafunzi kuzaa na kuendelea na shule kwa pesa ya serikali.

Serikali ni watu, na bunge limepitisha kwa wingi watoto kuendelea na shule. Utawezaje kutomruhusu mtoto aliyepata mimba kwa kubakwa kwa kumuwekea jinsia vituo vya polisi? Akienda polisi ndiyo amepata haki? Watoto wengi hawafiki hata polisi kwa kutishwa na wengine hawaaminiwi. Kaka yangu mkubwa akiyekuwa inspector wa polisi alitaka kumbaka dada yangu mkubwa, dada akalalamika kwa wazee matokeo yake huyu bwana, Kwani tangu siku hiyo sikumuiti kaka tena mpaka leo, akampiga dada yangu na kusema amemsingizia. Dada akaenda polisi, Polisi wakasema lakini hakukubaka. Hii ilikuwa mwaka 1972. HUYU jamaa aliendelea kubaka watoto wa jamaa na nduguwengine, na wengine akawapa mimba , na wengine matokeo yake waliopoteza maisha yao. Polisi ingemuchukulia hatuwa, wangeokiwa maisha ya watoto aliowabaka. Kwa sasa amestaafu na anakula pensheni yake. Na wako wengi Tanzania, tena wana vyao wanabaka watoto. Lakini ni watoto wa kike ndiyo wanalaumiwa, hawana sauti. Ingekuwa anaishi kwenye nchi zinazojali watoto HUYU bwana angefia jela, lakini Tanzania ni kitu cha kawaida.

HOTUBA ya Rais imenisikisha, Pamoja na heshima zote kwakwe, haswa ya kupigana na ufisadi ambao umewaumiza Watanzania wengi haswa wanawake na watoto. lakini kwa hili ameonyesha hathamini wakina mama kabisa. Wako wa namuunga mkono kama wewe, na Hii ni kwa kuwa Watanzania wengi hatuna elimu ya kimawazo, ni kujifanya tumna high moral standard na Huu ni uwongo mkubwa. Hotuba yake imeonyesha Rais haijui dunia vizuri na maendeleo ya wakinamama. Unaweza kuwa na elimu, lakini ukawa hujaelimika kimawazo, na shida kubwa ya Viongozi wetu wengi, na wanafanikiwa kutuongoza kwa kuwa hatuelewi Serikali ni nina, na bunge Lina kazi gani, tunajuwa mtu akiwa Rais basi anajuwa ndiye mwenye nchi na watu wake. Hawezi kuendelea kutawala kama anatawala ng'ombe. Serikali ni watu, yeye ametruliwa kuongoza tu sio kuwadhulumu watoto. Rsis anafanya kazi nzuri sana haswa yakuchunga asilimali zetu, lakini kuvunja sheria hivi bila ya kujali, uongozi wake hautaheshimiwa duniani kite. Tanzania ni kijiji kimojawapo hapa duniani, hawezi kufanya anavyotaka kama anataka kuheshimiwa, Wakati Mwenye pesa ndiye mwenye sheria. Tanzania haitaki wajinga, tuna wajinga wa kutosha. Ni haki ya watoto wote Tanzania wapate elimu na hawamuombi Mtu mmoja. Tanzania ni yetu wote, na pesa ni za walipa kodi, ikiwa pamoja na wazazi wa hawa watoto.
 
Hivi mnawaza kwa kutumia nini? Unaposema ni wengi je, ni wengi kuliko wale wanaokosa nafasi ya kuendelea mara wamalizapo darasa la saba??

Anayesema wasiendelee ni nani? Shida ni kuendelea kupata incentives za serikali, cha kufanya wao wasome ODL (open distance learning) nje ya formal education.

Watanzania jamani siyo lazima tufanye wafanyayo wazungu ili kufikia maendeleo na kufanya hivyo tutakuwa ni kukopi tutashindwa kufikiri na kubakia kuishi kwa maigizo.

Nchi za Kiafrika tumebaki nyuma kwa kutoheshimu haki za binadamu na ubinafsi wetu. Dhuluma ya wengi, Mtu anaingia madarakani anaindesha nchi kama yake binafsi.

Tanzania tumekuwa piece full siyo kwa uongozi mzuri, ni kwa uvumilivu wa Watanzania. Tabu za wanyonge mala nyingi watu walio serikalini hawazijui. Watoto wetu wanasoma kwa shida kubwa, shule zenyewe zipo kwenye hali mbaya. Waalimu hata nyumba za kuishi hawana. Sheria za kumukinga mtoto na uhalifu, hakuna, hata kama zipo hazifuatwi, ikiwa Rais mwenyewe hazifuati itakuwa watu wa jawauda. Amedharau sauti ya watu walio wengi kupitia bungeni, bunge lenye Wabunge wanaowawakilisha wananchi.

Watoto hawa wanapata ujauzito ni watoto kama watoto wengine, na changamoto wanazopata wanajuwa wenyewe, ikiwa hakuna wa kuzungumza nao, kwa kuwa kwa kifupi wanajulikana kama malaya. Culture ya Watanzania hawalalami. Rais mwenyewe alikuwa kwenye serikali ya nne, mambo mengi yakimuudhi lakini alikuwa kimya mpaka alipoingia madarakani ndiyo tunaona maudhi yaliyokuwa yakimusumbuwa.

Watoto wetu wana suffer in silence. Wazazi hatuzungumzi na watoto wetu, mawazo ya mbali wengi ni kama ya Rais wetu. Watoto hata wakibakwa hawasemi kwasababu kila mtu anasema walijitakia wenyewe, taifa limejaa watu ambao hatuna mawazonya mbali ya kujiuliza mbona inatokea zaidi kwa watoto Wetu? Hii ni kwasababu wengi wetu hatuna elimu ya kuona mbali. Badala ya serikali kuelimisha jamii, wazazi wazungumze na watoto, wawaelimishe lakini serikali inawakandamiza, wakati watu wenye ujuzi wa watoto wamefanya kazi kubwa kujadili na kuchunguza shida za hawa watoto na kutafuta sababu za kwa nini watoto wengi Tanzania wanapata ujauzito wakiwa wadogo, pamoja na bunge kupitisga sheria ya watoto waendelee na elimu. Mtu mmoja anakataa. Kuna haja kubwa ya katiba mpya kuiokowa inchi hii na watu wake. Maisha ya Watanzania million 50 kukabidhiwa mutu mumoja, ni hatari kubwa sana.
 
Unahakika wanafunzi wote wajawazito hubakwa. Kama ni hivyo Tz wanaume wengi wabakaji!

Tanzania ina record kubwa sana ya ubakaji kama hujui. Ingawaje sheria zipo, wanaofungwa ni wachache sana na wasiokuwa na pesa, waliombaka mtoto wa Mtu mwenye uwezo. kitu kingine, umasikini na ukosefu wa elimu kwa wazazi, ndiyo tuko wengi. Watoto wengi hawasemi kwa kuogopa kulaumiwa. Tanzania imekuwa na uongozi mbovu wa miaka mingi, sana. Hakuna mtu yeyote alikuwa akijali sheria. Unataka sheria unanunuwa, ukiwa huna pesa ole wako. Watoto wengi wameonewa, na wanaendelea kuonewa. HOTUBA ya Rais imepigilia msumali uonevu huu. Kila nikiisikiliza inaonyesha vile Tanzania tunaukosefu mkubwa wa elimu ya nawazo
 
Mkubwa alivyo jaa kiburi, hii patition hata iwekewe signature na dunia nzima haitosaidia kitu.
Naona wat hamjamuelewa maharage, akisema kitu amesema, huwa harudi nyuma kurekebisha.

He is too arrogant, anajihisi kua na nguvu moja kubwa sana na anahisi ndiye mwenye akili na uchungu kuliko watanzania wengine, kwa hiyo kila anachofikiria na kuamua ndiyo sahihi.

Mtu wa namna hiyo ogopa sana, msubiri muda wake uishe asepe tu, ila kumpangia vitu ashasema hapangiwi. Sio mara ya kwanza watu mnakuja pamoja kusema afanye kitu flani, kumbuka kwa kila mtu moja anayempiga, kuna kilaza mwingine asiyejua hata kuandika anam~support.

Najuta kutoa nauli kusafiri hadi bongo na kumpigia kura huyu jamaa. Simpendi Lowassa ila huyu jamaa alivyogeuka sasa hivi simpendi mara mbili zaidi.
 
Back
Top Bottom