CAG sio Muongo kwa vigezo hivi

CAG sio Muongo kwa vigezo hivi

Mkuu, huwa naamini sana katika busara zako ila hapa nadhani umepotoka au unataka kupotosha japo sidhani Kama una maslahi yoyote katika kufanya hivyo.

Unasema report ya CAG sio msahafu, hii ni kweli maana report inaweza kuwa na mapungufu kadha wa kadha. Ila ambacho sikubaliani na wewe ni hapo unapobariki manunuzi yasiyofuata kanuni, taratibu na sheria za fedha eti kwa kigezo kwamba manunuzi hayo yalifanyika kwa manufaa ya umma na umetolea mfano manunuzi ya ndege. Hii sio sawa mkuu.

Kama tuliweka taratibu/kanuni/sheria za manunuzi basi ni lazima zifuatwe na mtu akiacha kuzifuata anapaswa kuwajibishwa kwa maana kutofuata sheria halali zilizowekwa ni kosa kisheria na huwa tunasema no one is above the law, hata rais mwenyewe hayupo juu ya sheria.

Najua kuna ideology mbili katika kufanya maamuzi ambazo ni rule based na result based, wewe umebase kwenye result based, kwamba japo sheria hazikufuatwa ila results zimekuwa nzuri Sasa swali ni je vipi ingetokea result mbaya, mfano tungekuwa tumepigwa, ungekuwa na msimamo huo huo?

Halafu Kama unaongozwa na good will kwanini usifuate taratibu katika manunuzi? Watu wasio safi ndio mara nyingi huwa hawafuatwi sheria. Nahitimisha kwa kusema japo report ya CAG sio msahafu ila kwa kuwa nyaraka za manunuzi hazipo na taratibu zilisiginwa basi ni lazima watu wawajibishwe no matter results walizo deliver. Na hizo ndege naamini tumepigwa na ipo siku ukweli utaelezwa na inshaalah wote waliohusika watawekwa behind bars.
Mkuu Dawa Yenu, kwanza asante kwa hili, nimependa objectivity yako kwenye hoja ya kufuatwa kwa sheria taratibu na kanuni, za matumizi ya fedha za umma, lakini kama ulimsikia rais Magufuli akizungumzia mtindo wa manunuzi kwa kupiga tanchi, utakubaliana na mimi Magufuli did the right thing kununua ndege kwa cash kwa kupiga tanchi.

Kinachotakiwa ni uwepo tuu wa nia njema na ya dhati na kutanguliza mbele maslahi ya Taifa, kuhalalisha kukiukwa Sheria taratibu na kanuni.
P
 
CAG anapofanya ukaguzi anakagua nyaraka mbalimbali zinazothibitisha kuwa vitu vimenunuliwa na ni mali ya taasisi husika.

Lugola anapotosha umma kuwa Makontena yapo,hivi kama hayana nyaraka tutaaminije kama ni mali ya polisi Tanzania?

Nakumbuka enzi za utumishi,walikuja wakaguzi kukagua Rim za karatasi,kwakuwa wakubwa walikuwa wamekula pesa bila kununua rim hizo,wakaenda kuomba msaada kwa mfanya biashara mmoja kuwa awapatie rim za karatasi ili zitumike kuwaonesha wakaguzi,baada ya ukaguzi zitarudi kwa mwenye nazo.

Hata hivyo walipokuja wakaguzi,waliomba Store ledger ,quatation,Issue vocher na Delivery note.

Yaani tabu ikabaki palepale.
Maana hivyo vyote havikuwepo,bali wakubwa zangu walijiandaa kumuonesha rim wakidhani mchezo utakuwa umeisha.

Haya yamenikumbusha viroja vya Lugola Bungeni,kwamba Makontena yapo bila uwepo wa nyaraka?

Tutaaminije kuwa sii mchezo mchafu wa kutuonesha makontena yasiyomilikiwa na Polisi?

Lugola afanye tena Press conference akiwa na Store ledger mezani,Mkataba,delivery note na nyaraka zote zilizohojiwa na CAG.

Awaombe waandishi wazichapishe,hata hivyo atoe ufafanuzi kwanini kama hizo nyaraka zipo hazikuoneshwa mbele ya wakaguzi wa CAG?

Alikuwa anaficha nini hata alipopewa siku 21 kuwasilisha nyaraka lakini hakufanya hivyo mpaka ripoti ilipotoka?

Ujinga ni mzigo,Rais Magufuli ni Rais alijipambanua kupambana na ufisadi,manunuzi yoyote yasiyofuata sheria ni moja kati ya viashiria vya ufisadi ambao Rais hautaki,tunategemea kumsikia Rais wetu mpendwa akikemea kejeli za wateule wake kwa jicho lake ambao ni CAG.
 
Pascal
kwahiyo ni sawa hela za umma zitumike bila bunge kuhidhinisha hata kama tutaona matokeo ya kutumika fedha hizo?

wanaweza kusema ndege wamenunua kwa elfu moja kumbe wamenunua kwa mia tano...au walichukua elfu mbili wakatumia elfu moja,

hii serikali bado ina uongo uongo mwingi sana, sasa repoti ya CAG inawaumbua wanapaniki.
amesharusha jiwe gizani, siku hizi uandishi wake haunipi shida kuuelewa
 
Kwa yanayoendelea sasa ni dhihiri shahiri tunainyima nguvu/meno ili nafasi ambayo ipo kikatiba,
Watu wengine hawatakua waoga tena kuiba maana watetezi wapo wa kuwatetea, CAG nae atakosa nguvu ya kufanya kazi maana anayoyasema wengine hawataki kuyasikia
 
Sijasoma uzi, nmeishia kwa kichwahabar.

Nachoweza sema, Mpumbavu anaweza kujichanachana nakujigaragaza kwenye maji machafu ili mradi tu ajithibitishe kua yuko sahihi.

Usishangae, Waziri angesema "Kama Sare hazipo ,nitatembea barabaran uchi".

Wenye Hekima, Huficha aibu zao.
 
Paskal unasema ndege umezishuhudia, unajua bei zake? Tutajie
Mkuu Dyuteromaikota
huna haja ya kujua bei ya manunuzi ni siri ya kibiashara.

Ila mimi ni mtu ninayeongozwa na imani na uaminifu, Nina imani na Rais Magufuli, namuamini and I trust him rais anachotuambia ndio ukweli mtupu halisi hauna hata chembe ya uongo.

Rais wetu Magufuli ametueleza ndege zile ni mpya, kazinunua kwa cash kutoka kiwandani, kwa bei poa, hakuna middlemen hapo kati wa kuongeza cha juu. Mimi namuamini rais Magufuli ni rais mkweli, ndio maana Zitto alipoleta zile zake, nilishauri Zitto ashughulikiwe.

P.
 
kwahiyo ni sawa hela za umma zitumike bila bunge kuhidhinisha hata kama tutaona matokeo ya kutumika fedha hizo?

wanaweza kusema ndege wamenunua kwa elfu moja kumbe wamenunua kwa mia tano...au walichukua elfu mbili wakatumia elfu moja,

hii serikali bado ina uongo uongo mwingi sana, sasa repoti ya CAG inawaumbua wanapaniki.
Ni sawa. Kama unamwamini rais wako, akisema tumenunua ndege kwa bei poa, ni tumenunua kwa bei poa.
P
 
Mkuu Do, huna haja ya kujua bei ya manunuzi ni siri ya kibiashara.

Ila mimi ni mtu ninayeongozwa na imani na uaminifu, Nina imani na Rais Magufuli, namuamini and I trust him rais anachotuambia ndio ukweli mtupu halisi hauna hata chembe ya uongo.

Rais wetu Magufuli ametueleza ndege zile ni mpya, kazinunua kwa cash kutoka kiwandani, kwa bei poa, hakuna middlemen hapo kati wa kuongeza cha juu. Mimi namuamini rais Magufuli ni rais mkweli, ndio maana Zitto alipoleta zile zake, nilishauri Zitto ashughulikiwe.

P.
Kwa hiyo sasa hivi inabidi tuongozwe kwa trust na sio uwazi na uwajibikaji!!?
 
Hakuna aibu na adhabu kali km kumdhalilisha mwenzako bila ya sababu za msingi. Yaani matokeo na malipo ya udhalili ni udhalilifu mara dufu. Huyu kangi huyu kabla ya yeye kujivua nguo hiyo siku aliyoahidi, mimi nilimvua boxer siku aliyomfukuza yule officer wa magereza ktk kikao chake kwa kuchelewa. Sasa haya ndio malipo yake. Na si yeye tu pekee kuna bongolala mwingine hili Ndu Gay. Time will tell.
Kwanini Asaad kulidhalilisha bungu ughaibuni iwe sahihi lkn yeye akidhalilishwa isiwe sahihi? Mungu mwenye haki zote ANAWAONENI
 
Watanzania tunaumia kuona CAG anavyoshambuliwa bila sababu,CAG ndiye mkaguzi wa kodi zetu , watanzania tuna wajibu wa kusimama nae ili kuwe na usimamizi imara wa fedha zetu (effective finance management).

Haijawai kutokea duniani CAG kuitwa muongo isipokuwa Tanzania mbele ya umma na Bunge,tena kuitwa na waziri wa serikali inayopambana na rushwa na matumizi mabaya ya fedha.

Mchakato wa ukaguzi yaani "Audit process" ni mpana sana, kufahamu mchakato huu ndio unaweza jua uongo wa CAG au Ukweli wa CAG . Tutagusa gusa sehemu kadhaa .
Case study iwe *sare za Jeshi la polisi*

Ukisoma Ripoti ya CAG ya 2018 , kurasa 309 hadi 312 . Anasema ukaguzi juu ya sare za jeshi la polisi ni kufuatia ombi la Takukuru ,yaani Takukuru walipata taarifa wakampa CAG achunguze ,suala hili la sare ni la tangu 2015 Novemba hivyo kwa CAG huu ulikuwa ukaguzi maalumu, sheria ya ukaguzi wa umma Na 11 ya 2008 kifungu cha 29 na 36 kinampa nguvu hata kama ripoti yake hii ni ya 2018.

CAG anasema mkataba ulisainiwa tar 2/Nov/2015 Kati ya katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani na mzabuni "Daissy General Traders" kununua sare za polisi china mhasibu alipaswa awe ameingiza mzigo Kipindi kisichozidi siku 180 ,ila mzigo ulifika kwa siku mbili tangu call of order.

CAG anasema alitaka kujiridhisha kama kweli mzigo huo upo na umeingizwa kweli, CAG aliomba nyaraka kutoka kwa mzabuni (Daissy General Traders) kama mzigo uliingia kweli ,Hati ya kupokelea shehena,hati ya madai,orodha ya mali zilizo ktk meli,cheti cha ukaguzi.

CAG hakuishia hapo akaenda kuuliza Bohari kuu ya jeshi la polisi ambapo mzigo huo ulipaswa kufikia huko ,majibu yakawa hakuna mzigo wowote uliopokelewa.

CAG hakuishia hapo akaenda Bandarini katika Mfumo wa forodha TANCIS wa TRA yaani Tanzania Customer intergrated system) kupitia TANCIS katika mfumo(web-based) unaweza kuona mzigo wowote uliotoka au kushushwa na taarifa zake hubaki (discharged cargo and it's report). Soma "TANSCIS Bronchure of Jun 2016.Tancis makes cargo clear easy" bado CAG hakuona mzigo wowote.

CAG huwa haishii hapo ,huangalia pia mambo ya internal control system ya Ofisi inayokaguliwa, financial system, ledger na mambo ya sheria kwa utaalamu na taratibu itakuwa CAG alifanya hivyo pia.

CAG haishi hapo bado Kuna majadiliano mafupi huyafanya na wakaguzi wa ndani (internal auditors) au kamati ya ukaguzi (Audit committee) huitwa Exit meeting au Exit conference , wakaguzi wa ndani wananafasi ya kutoa utetezi wao juu ya findings za CAG.

CAG haishi hapo,ana andikia barua Ofisi iliyokaguliwa inaitwa "Audit management letter" akielezea kuhusu alichokigundua kama ni madudu ,rushwa ,ufisadi (Deficiencies in internal control) atajikita kushauri ,kutoa maoni na mapendekezo kwao waboreshe mifumo yao na utendaji (internal Control system ) Kama sheria inavyomtaka afanye hivyo kifungu cha 12 ,sheria ya ukaguzi wa Umma 2008.

CAG haishii hapo tuu ,kabla ya kutoa Ripoti yake ya ukaguzi (CAG Report) kwa Mh.Rais, na baadaye Bungeni .Ofisi zilizokaguliwa huwa zina nafasi ya kujibu kwa zinazopenda ,barua yao huitwa "Management representation letter au Management response" huwa wanaweza kukiri na kukubali kujirekebisha au wakaendelea kujitetea au pia waka kaa kimya ingawa kimya huonesha dharau.

Pia wengine huwa wanajibu kwa kuendelea kujitetea,
Ingawa kujitetea kwa hatua hii inahitaji facts zaidi ya alizonazo CAG ,na barua hii ya kujibu CAG pia huichukulia Kama ushahidi wa ukaguzi (Audit Evidence).

Sasa mchakato wote huu CAG anaitwa "MUONGO" ?

1.Mh.waziri anasema mzigo upo kwenye Kontena alienda kuona ,Mzigo uliagizwa 2015 leo 2019 huo mzigo upo kwenye makontena badala ya kuwa Bohari kuu ya jeshi la polisi au hata kuwa tayari kugawiwa kwa polisi , katika Kontena sare zinafanya nini ?

2.Je, anajua kilichojadiliwa katika Exit meeting ya CAG na wakaguzi wa ndani wa wizara?

3.Barua ya management response kwa CAG ,waliokaguliwa walikuwa na nafasi ya kuendelea kujitetea ,je walifanya hivyo ili waweke utetezi wa Mh.wazir ?

4.Fedha za umma zinapotumika kununua vitu ,lazima ziwe recorded katika ledger (Purchase ledger au costomer deposit) ,je CAG alipewa ledger ili aone transactions ya malipo kwa mzabuni?

5.Hizo sare katika Kontena zilifika lini ? ,Kama ni muda mrefu kwanini CAG aliangalia katika mfumo wa forodha (TANCIS-TRA) hakuona mzigo ulioingia ? ,kwanini alinyimwa nyaraka na mzabuni Daissy General Traders? ,Kwanini watu wa Bohari kuu walikataa hakuna mzigo ? ,Kama kulikuwa na taarifa yeyote kuhusu uwepo wa mzigo kwanini hakuambiwa kabla ya report yake kupelekwa kwa Rais ?

Tufahamu kuwa CAG hajitungii stori kuhusu ukaguzi,wala hafanyi yeye tuu bila kuhoji ,hitimisho la CAG linaundwa pia na majibu aliyojibiwa na wakaguliwa.Hivyo kauli ya kusema CAG ni muongo inapaswa ipingwe sababu itajenga Precedents kwa viongozi kadhaa wakitenda mskosa rushwa kwa kujua kabisa ,watabishia ukaguzi na kumuita CAG muongo,hii itakuwa ni hatari kwa ulinzi wa fedha zetu.

Hivyo tuhitimishe kwa kukubaliana pamoja kwa kusema CAG sio MUONGO,CAG anafanya kazi kwa nyaraka, utata ni pale nyaraka zinapokosekana.

Shukrani sana.

Abdul Nondo

abdulnondo10@gmail.com
Asaad siyo malaika au Mungu
 
kwahiyo ni sawa hela za umma zitumike bila bunge kuhidhinisha hata kama tutaona matokeo ya kutumika fedha hizo?

wanaweza kusema ndege wamenunua kwa elfu moja kumbe wamenunua kwa mia tano...au walichukua elfu mbili wakatumia elfu moja,

hii serikali bado ina uongo uongo mwingi sana, sasa repoti ya CAG inawaumbua wanapaniki.
br uko sawa tatizo la P huwa anajitoa ufahamu anapotumia K-VANTI
 
Lugola alimsafisha Lugumi kuwa hana tatizo lolote lakini CAG kaja tena kumkaanga Lugumi kuwa hakufanya kazi aliyopaswa kuifanya ipasavyo.
 
CAG anapofanya ukaguzi anakagua nyaraka mbalimbali zinazothibitisha kuwa vitu vimenunuliwa na ni mali ya taasisi husika.

Lugola anapotosha umma kuwa Makontena yapo,hivi kama hayana nyaraka tutaaminije kama ni mali ya polisi Tanzania?

Nakumbuka enzi za utumishi,walikuja wakaguzi kukagua Rim za karatasi,kwakuwa wakubwa walikuwa wamekula pesa bila kununua rim hizo,wakaenda kuomba msaada kwa mfanya biashara mmoja kuwa awapatie rim za karatasi ili zitumike kuwaonesha wakaguzi,baada ya ukaguzi zitarudi kwa mwenye nazo.

Hata hivyo walipokuja wakaguzi,waliomba Store ledger ,quatation,Issue vocher na Delivery note.

Yaani tabu ikabaki palepale.
Maana hivyo vyote havikuwepo,bali wakubwa zangu walijiandaa kumuonesha rim wakidhani mchezo utakuwa umeisha.

Haya yamenikumbusha viroja vya Lugola Bungeni,kwamba Makontena yapo bila uwepo wa nyaraka?

Tutaaminije kuwa sii mchezo mchafu wa kutuonesha makontena yasiyomilikiwa na Polisi?

Lugola afanye tena Press conference akiwa na Store ledger mezani,Mkataba,delivery note na nyaraka zote zilizohojiwa na CAG.

Awaombe waandishi wazichapishe,hata hivyo atoe ufafanuzi kwanini kama hizo nyaraka zipo hazikuoneshwa mbele ya wakaguzi wa CAG?

Alikuwa anaficha nini hata alipopewa siku 21 kuwasilisha nyaraka lakini hakufanya hivyo mpaka ripoti ilipotoka?

Ujinga ni mzigo,Rais Magufuli ni Rais alijipambanua kupambana na ufisadi,manunuzi yoyote yasiyofuata sheria ni moja kati ya viashiria vya ufisadi ambao Rais hautaki,tunategemea kumsikia Rais wetu mpendwa akikemea kejeli za wateule wake kwa jicho lake ambao ni CAG.
Hahahahah hio story ya rim imenichekesha sana
Sipatii picha walificha wapi sura zao dahhh
 
Mkuu Abdul Nondo, kwanza asante kwa nondo hii, sidhani kama mtu mzima mwenye akili timamu kichwani kwake anaweza kumuita CAG ni muongo, ujue tuna vichaa wengi kuliko tunavyojijua.

Kwa vile humu sio members wote wanaweza kusoma kila kitu, ni vema pia ungeweka ref ya aliyemuita CAG muongo kama hivi

Ila kwenye ripoti ya CAG, sio kila upotevu wa fedha za umma au matumizi makubwa ya fedha kwenye manunuzi bila kufuata taratibu ni matumizi mabaya ya fedha za umma au ni ufisadi.

CAG anakagua kufuatwa kwa sheria taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za umma. Hivyo kuna maeneo ni kweli sheria taratibu na kanuni zilikiukwa lakini fedha zikatumika vizuri kwa ajili ya manufaa ya taifa mfano mzuri ni fedha za kununua zile ndege mpya, hazikufuata mchakato wa manunuzi wala taratibu za matumizi ya fedha za umma, ikiwemo kupangiwa bajet, kuidhinishwa na Bunge, CAG kusaini etc, kwa vile tumefanya manunuzi kwa utaratibu mpya wa Rais Magufuli unaoitwa kupiga tanchi, hatimaye ndege zimekuja na tumezishuhudia.

Hata matumizi makubwa kwenye Vote 20, japo hayakuidhinishwa na Bunge, lakini ni matumizi mazuri tuu, sote tunashuhudia rais wetu katika ziara zake, anatembea na mabulungutu ya hard cash na kugawa kwa wananchi.

Pia kuna maeneo ya matumizi makubwa, sheria taratibu na kanuni zote zimefuatwa, lakini huko ndiko tunapigwa.

Ukaguzi huanza kwa Entrance Meeting na kumalizika kwa Exit Meeting, hivyo inawezekana hadi CAG anafanya exit meeting, hizi sare za Polisi zilikuwa hazijaingia, lakini baadae ziliingia na ni kweli ziko ndani ya makontena.

Japo Ripoti ya CAG sio Masahafu au Bible, ila kiukweli kabisa aliyemuita CAG muongo, sikuzote ni kama kituko fulani.
P

So you mean the end justify the means? je tutajuaje huyo mzee wa Chatto kama hajachukua 10% kwenye ndege? mambo mengine si ya kutetea. Hiyo mindege mbona haziingizi chochote zaidi ya sifa? We have to understand that matumizi mabaya ya raslimali ni ubadhirifu.
 
Huo mzigo wa sare lugola anaosema umeletwa juzi na c.a.g hela anayozungumzia ishapigwa ni ile ilomtumbia waziri aliemwachia mwigulu kijiti hivyo lugola aache kufanya watu hatuoni mbali
 
Mkuu Dawa Yenu, kwanza asante kwa hili, nimependa objectivity yako kwenye hoja ya kufuatwa kwa sheria taratibu na kanuni, za matumizi ya fedha za umma, lakini kama ulimsikia rais Magufuli akizungumzia mtindo wa manunuzi kwa kupiga tanchi, utakubaliana na mimi Magufuli did the right thing kununua ndege kwa cash kwa kupiga tanchi.

Kinachotakiwa ni uwepo tuu wa nia njema na ya dhati na kutanguliza mbele maslahi ya Taifa, kuhalalisha kukiukwa Sheria taratibu na kanuni.
P
Mkuu kwanini unakomaa kutetea hoja chakavu?inawezekaje mlango upo afu upite madirishani bila shaka unakuwa na nia ovu

Je tukisema na hao ambao hawajafuata sheria za manunuzi ya umma walikuwa na nia njema kwa taifa..

Nakuona unavyoweza kubalance pande zote mbili safi sana mkuuu
 
Report ya CAG itawaibua wote ndani ya Serikali ambao deals zao zimekuwa exposed. Imagine huo mpunga kina Lugola na wenzie walioutema baada ya mambo kuwekwa hadharani. Yaani sasa wanajikuta wanapayuka hovyo. Hasira zao sasa zimefunika uwezo wao wa kufikiri
Wewe nawe sijui nikuite Kilaza au nani!?!? Lugola kawa waziri wa mambo ya ndani tangu lini? Unabiwa ni issue ya 2015 November wakati hata serikali haijaanza kufanya kazi sawia. Muwe mnaficha ujinha wenu sometimes.
 
Accounting and Auditing are professionals. They have own ethics like other professionals. Kufanya ukaguzi wa mahesabu ni process ambayo inaanzia kwenye systems na procedures kama zimefuatwa hadi hatua za mwisho kama ni manunuzi kwa mfano hatua kwa hatua kama utaratibu wa uagizaji, ulipaji, usafirishaji, mapokezi ya bidhaa hadi utunzaji wake hatimae matumizi ya bidhaa husika kama imegawanywa kwa walengwa na kupokelewa kwa matumizi kwa waliokusudiwa. Nadhani tujifunze kuheshimu taaluma za watu tusizozijua ili tuepuke kuonekana tuna dharau kwani bila ya mgawanyo wa taaluma dunia isingeweza kufika ilipofika.
 
Back
Top Bottom