Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,498
- 113,604
Wanabodi,
Moja ya ugonjwa mkubwa na mbaya kuliko magonjwa yote yanayolikabili taifa letu, ni ugonjwa wa kukua kwa deni la taifa, ambalo linakuwa kwa kasi kubwa kuliko uchumi wetu. Ukuaji wa uchumi wetu wa taifa ni wastani wa asilimia 7% kwa mwaka, wakati ukuaji wa deni la taifa ni asilimia 20% kwa mwaka!. Rate hii ikiendelea, tutafikia kiwango ambacho deni litakuwa halihimiliki kwa kufikia kiwango cha mwisho cha uwezo wa kukopesheka, hivyo taifa letu kuwa halikopesheki.
Sababu kubwa ya kukua kwa deni la taifa ni kutokana na nchi yetu kupanga bajeti tegemezi ambayo ni bajeti kubwa kuliko makusanyo yetu, hivyo bajeti yetu ziku zote inategemea mikopo na misaada ya nchi wafadhili, inapotokea nchi wafadhili wamepunguza misaada, nchi yetu hujikuta inalazimika kukopa ili kutekeleza bajeti, both recurrent, na development.
CAG Prof. Mussa Assad ambaye kitaaluma ni mchumi, hapa anatoa dawa ya kutibu ugonjwa huo wa kutegemea budget tegemezi.
Msikilize.
Paskali.